Mwanzo 36:1-43, Mwanzo 37:1-36 NEN

Mwanzo 36:1-43

Wazao Wa Esau

(1 Nyakati 1:34-42)

36:1 Mwa 2:4; 25:30Hivi ndivyo vizazi vya Esau (yaani Edomu).

36:2 Mwa 26:34; 28:8-9Esau akaoa wake kutoka miongoni mwa wanawake wa Kanaani: Ada binti wa Eloni Mhiti, Oholibama binti wa Ana, mjukuu wa kike wa Sibeoni Mhivi, pia akaoa Basemathi binti wa Ishmaeli, dada yake Nebayothi.

36:4 1Nya 1:35Ada akamzalia Esau Elifazi, Basemathi akamzaa Reueli, 36:5 1Nya 1:35Oholibama akamzaa Yeushi, Yalamu na Kora. Hawa ndio wana wa Esau waliozaliwa kwake huko Kanaani.

36:6 Mwa 12:5; 1Nya 1:35Esau akawachukua wake zake, watoto wake wa kiume na wa kike na wote wa nyumbani mwake, mifugo yake pamoja na wanyama wake wengine wote na mali yake yote ambayo alikuwa ameipata akiwa Kanaani, akahamia katika nchi iliyo mbali na Yakobo ndugu yake. 36:7 Mwa 13:6; 27:39Mali zao zilikuwa nyingi sana kiasi kwamba haikuwa rahisi wao kuishi pamoja, nchi waliyokuwa wakiishi isingewatosha wote kwa ajili ya mifugo yao. 36:8 Kum 2:4Kwa hiyo Esau (ambaye ni Edomu) aliishi katika nchi ya kilima huko Seiri.

36:9 Mwa 2:4Hawa ndio wazao wa Esau, baba wa Waedomu, katika nchi ya kilima cha Seiri.

36:10 Mwa 36:3Haya ndiyo majina ya wana wa Esau:

Elifazi, mwana wa Esau ambaye mkewe Ada alimzalia; na Reueli, mwana wa Esau ambaye mkewe Basemathi alimzalia.

36:11 1Nya 1:45Wana wa Elifazi ni:

Temani, Omari, Sefo, Gatamu na Kenazi.

36:12 Kut 17:8, 16; 1Sam 15:2Elifazi mwana wa Esau alikuwa pia na suria aliyeitwa Timna, ambaye alimzalia Amaleki. Hawa ndio waliokuwa wajukuu wa Ada mke wa Esau.

36:13 Mwa 36:3Wana wa Reueli ni:

Nahathi, Zera, Shama na Miza. Hawa ndio waliokuwa wajukuu wa Basemathi mkewe Esau.

36:14 Mwa 36:2Wana wa Oholibama binti Ana, mkewe Esau, aliyekuwa mjukuu wa Sibeoni, aliomzalia Esau ni:

Yeushi, Yalamu na Kora.

36:15 Mwa 36:19-40; Kut 15:15Hawa ndio waliokuwa wakuu miongoni mwa wazao wa Esau:

Wakuu wa wana wa Elifazi, mzaliwa wa kwanza wa Esau ni:

Temani, Omari, Sefo, Kenazi, 36:16 Mwa 32:3Kora, Gatamu na Amaleki. Hawa ndio waliokuwa wakuu waliotoka kwa Elifazi huko Edomu, waliokuwa wajukuu wa kiume wa Ada.

36:17 1Nya 1:37Wakuu wa wana wa Reueli, mwana wa Esau ni:

Nahathi, Zera, Shama na Miza. Hawa ndio wakuu waliotoka kwa Reueli huko Edomu, waliokuwa wajukuu wa kiume wa Basemathi mkewe Esau.

36:18 Mwa 36:2Wakuu wa wana wa Esau ambao mkewe Oholibama alimzalia ni:

Yeushi, Yalamu na Kora. Hawa ndio wakuu waliotoka kwa mke wa Esau, Oholibama binti Ana.

36:19 1Nya 1:35Hawa ndio waliokuwa wana wa Esau (ndiye Edomu), na hawa ndio waliokuwa wakuu wao.

36:20 Mwa 14:6Hawa ndio walikuwa wana wa Seiri, Mhori, waliokuwa wakiishi katika nchi ile:

Lotani, Shobali, Sibeoni, Ana, 36:21 Mwa 36:30Dishoni, Eseri na Dishani. Hawa ndio wana wa Seiri huko Edomu waliokuwa wakuu kwa Wahori.

Wana wa Lotani walikuwa:

Hori na Homamu. Timna alikuwa dada yake Lotani.

Wana wa Shobali walikuwa:

Alvani, Manahathi, Ebali, Shefo na Onamu.

36:24 Mwa 36:2Wana wa Sibeoni walikuwa:

Aiya na Ana. Huyu Ana ndiye aligundua chemchemi ya maji moto jangwani alipokuwa akichunga punda za Sibeoni baba yake.

36:25 Mwa 36:2Watoto wa Ana walikuwa:

Dishoni na Oholibama binti wa Ana.

Wana wa Dishoni walikuwa:

Hemdani, Eshbani, Ithrani na Kerani.

Wana wa Eseri walikuwa:

Bilhani, Zaavani na Akani.

Wana wa Dishani walikuwa:

Usi na Arani.

36:29 Mwa 36:20Hawa ndio waliokuwa wakuu wa Wahori:

Lotani, Shobali, Sibeoni, Ana, 36:30 Mwa 36:21Dishoni, Eseri na Dishani. Hawa ndio walikuwa wakuu wa Wahori, kufuatana na makundi yao, katika nchi ya Seiri.

Watawala Wa Edomu

(1 Nyakati 1:43-54)

36:31 Mwa 17:6Wafuatao ni wafalme waliotawala Edomu kabla ya mfalme yeyote wa Israeli kutawala:

Bela mwana wa Beori alikuwa mfalme wa Edomu. Mji wake uliitwa Dinhaba.

36:33 Isa 34:6Bela alipofariki, Yobabu mwana wa Zera kutoka Bosra akawa mfalme baada yake.

36:34 Yer 49:7Yobabu alipofariki, Hushamu kutoka nchi ya Watemani akawa mfalme baada yake.

36:35 Rut 1:1, 6; Mwa 19:37Hushamu alipofariki, Hadadi mwana wa Bedadi, aliyeshinda Midiani katika nchi ya Moabu, akawa mfalme baada yake. Mji wake uliitwa Avithi.

Hadadi alipofariki, Samla kutoka Masreka akawa mfalme baada yake.

36:37 Mwa 26:22Samla alipofariki, Shauli kutoka Rehobothi ngʼambo ya Mto Frati akawa mfalme baada yake.

Shauli alipofariki, Baal-Hanani mwana wa Akbori akawa mfalme baada yake.

Baal-Hanani mwana wa Akbori alipofariki, Hadadi akawa mfalme baada yake. Mji wake uliitwa Pau, na mkewe aliitwa Mehetabeli binti Matredi, binti Me-Zahabu.

36:40 Mwa 36:15Hawa ndio wakuu waliotokana na Esau, kwa majina, kufuatana na koo zao na nchi zao:

Timna, Alva, Yethethi, Oholibama, Ela, Pinoni, Kenazi, Temani, Mibsari, 36:43 Mwa 36:9Magdieli na Iramu. Hawa ndio walikuwa wakuu wa Edomu, kufuatana na makazi yao katika nchi waliyoimiliki.

Huyu ndiye alikuwa Esau, baba wa Waedomu.

Read More of Mwanzo 36

Mwanzo 37:1-36

Ndoto Za Yosefu

37:1 Mwa 17:8; 10:19Yakobo akaishi Kanaani katika nchi ambayo baba yake alikuwa ameishi.

37:2 Za 78:71; 1Sam 2:24Zifuatazo ni habari za Yakobo.

Yosefu, kijana wa miaka kumi na saba, alikuwa akichunga makundi ya kondoo na mbuzi pamoja na ndugu zake wa mama wengine, yaani wana wa Bilha na wana wa Zilpa wake za baba yake, naye akawa akimletea baba yake taarifa mbaya kuhusu hao ndugu zake.

37:3 Mwa 44:20; 2Sam 13:18-19Basi, Israeli akampenda Yosefu kuliko yeyote miongoni mwa kaka zake, kwani ni mwanawe wa uzeeni, akamshonea joho lililorembwa vizuri sana. 37:4 Mwa 27:41; Mdo 7:9Ndugu zake walipoona kwamba baba yao anampenda Yosefu kuliko yeyote mwingine miongoni mwao, walimchukia na hawakusema naye neno lolote jema.

Yosefu akaota ndoto, naye alipowaeleza ndugu zake, wakamchukia zaidi. Akawaambia, “Sikilizeni ndoto niliyoota: 37:7 Mwa 42:6, 9; 43:26, 28Tulikuwa tukifunga miganda ya nafaka shambani, ghafula mganda wangu ukasimama wima, wakati miganda yenu ikiuzunguka na kuuinamia.”

37:8 Mwa 49:26; Kum 33:16Ndugu zake wakamwambia, “Wewe unakusudia kututawala? Hivi kweli wewe utatutawala sisi?” Wakaongeza kumchukia zaidi kwa sababu ya ndoto yake pamoja na yale aliyowaambia.

Kisha akaota ndoto nyingine, akawaambia ndugu zake akisema, “Sikilizeni, nimeota ndoto nyingine, wakati huu jua, mwezi na nyota kumi na moja zilikuwa zinanisujudia.”

37:10 Rut 2:16Alipomwambia baba yake pamoja na ndugu zake, baba yake akamkemea akisema, “Ni ndoto gani hii uliyoota? Hivi kweli mama yako na mimi na ndugu zako tutakuja kukusujudia wewe hadi nchi?” 37:11 Mdo 7:9; Lk 2:19, 51Ndugu zake wakamwonea wivu, lakini baba yake akaliweka jambo hilo moyoni.

Yosefu Auzwa Na Ndugu Zake

37:12 Mwa 12:6Basi, ndugu zake walikuwa wamekwenda kuchunga makundi ya baba yao karibu na Shekemu, 37:13 Mwa 17:5naye Israeli akamwambia Yosefu, “Kama ujuavyo, ndugu zako wanachunga makundi huko karibu na Shekemu. Njoo, nitakutuma kwao.”

Yosefu akajibu, “Vema sana, niko tayari.”

37:14 1Sam 17:18Kwa hiyo akamwambia, “Nenda uone kama mambo yote ni salama kwa ndugu zako na makundi, kisha uniletee habari.” Ndipo akamtuma Yosefu kutoka Bonde la Hebroni.

Yosefu alipofika Shekemu, mtu mmoja akamkuta akizungukazunguka mashambani na akamuuliza, “Unatafuta nini?”

Akajibu, “Ninawatafuta ndugu zangu. Unaweza kuniambia wanachunga wapi makundi yao?”

37:17 2Fal 6:13Yule mtu akajibu, “Wamehama hapa. Nilisikia wakisema, ‘Twende Dothani.’ ”

Kwa hiyo Yosefu akawafuatilia ndugu zake na kuwakuta karibu na Dothani. 37:18 Mk 14:1Ndugu zake walipomwona akiwa mbali, kabla hajawafikia, wakapanga shauri baya la kumuua.

37:19 Mwa 28:12Wakaambiana, “Yule mwota ndoto anakuja! 37:20 Mwa 50:20Njooni sasa, tumuue na kumtupa katika shimo mojawapo na tuseme kwamba mnyama mkali amemrarua. Kisha tutaona matokeo ya ndoto zake.”

37:21 Mwa 42:22Reubeni aliposikia jambo hili, akajaribu kumwokoa kutoka mikononi mwao akasema, “Tusiutoe uhai wake. 37:22 Mwa 37:20Tusimwage damu yoyote. Mtupeni katika shimo lililoko hapa jangwani, lakini msimguse.” Reubeni alisema hivyo ili amwokoe kutoka mikononi mwao, kisha amrudishe nyumbani kwa baba yake.

37:23 Mwa 37:3Kwa hiyo Yosefu alipowafikia ndugu zake, walimvua lile joho lake, lile joho lililorembwa vizuri alilokuwa amevaa. 37:24 Mwa 37:4Kisha wakamchukua wakamtupa katika shimo. Wakati huo shimo lilikuwa tupu, halikuwa na maji ndani yake.

37:25 Mwa 37:28Walipokaa ili wale chakula chao, wakainua macho wakaona msafara wa Waishmaeli ukija kutoka Gileadi. Ngamia wao walikuwa wamepakizwa mizigo ya vikolezo, uvumba na manemane, nao walikuwa njiani kuvipeleka Misri.

37:26 Mwa 4:10Yuda akawaambia ndugu zake, “Tutafaidi nini ikiwa tutamuua ndugu yetu na kuificha damu yake? 37:27 Mwa 42:21Njooni, tumuuze kwa hawa Waishmaeli. Tusimguse, kwa kuwa hata hivyo yeye ni ndugu yetu, nyama yetu na damu yetu wenyewe.” Ndugu zake wakakubali.

37:28 Kut 21:16; Za 105:17Kwa hiyo wale wafanyabiashara Wamidiani walipofika pale, ndugu zake wakamtoa Yosefu kutoka kwenye lile shimo, na kumuuza kwa shekeli ishirini37:28 Shekeli 20 ni sawa na gramu 200. za fedha kwa wale Waishmaeli, ambao walimpeleka Misri.

37:29 Ay 1:20; Yoe 2:13Reubeni aliporudi kutazama kwenye lile shimo na kuona kwamba Yosefu hayupo, alirarua nguo zake. 37:30 Mwa 37:22Akawarudia ndugu zake na kusema, “Kijana hayuko mle! Nielekee wapi sasa?”

Kisha wakalichukua lile joho la Yosefu, wakachinja mbuzi na kulichovya katika damu. Wakalichukua lile joho lililorembwa vizuri na kulipeleka kwa baba yao na kusema, “Tumeliokota hili joho. Uchunguze uone kama ni la mwanao.”

37:33 Mwa 37:20Baba yao akalitambua akasema, “Hili ni joho la mwanangu! Mnyama mkali amemrarua. Hakika Yosefu ameraruliwa vipande vipande.”

37:34 2Sam 3:31; 2Fal 6:30; Ay 16:15Kisha Yakobo akararua nguo zake, akavaa nguo ya gunia na kumwombolezea mwanawe kwa siku nyingi. 37:35 Mwa 42:38; 2Sam 12:23Wanawe wote na binti zake wakaja kumfariji, lakini hakukubali kufarijiwa. Akasema, “Hapana, nitamwombolezea mwanangu mpaka nimfikie kaburini.” Kwa hiyo baba yake akaendelea kumlilia.

37:36 Mwa 39:1; 1Sam 22:14Wakati ule ule, Wamidiani wakamuuza Yosefu huko Misri kwa Potifa, mmojawapo wa maafisa wa Farao, aliyekuwa mkuu wa ulinzi.

Read More of Mwanzo 37