Mwanzo 19:1-38, Mwanzo 20:1-18 NEN

Mwanzo 19:1-38

Kuangamizwa Kwa Sodoma Na Gomora

19:1 Mwa 11:27; 17:3; 18:1, 2, 22; 48:12; Rut 2:10; 1Sam 25:23; 2Sam 14:33; 2Fal 2:15; Ebr 13:2Malaika wale wawili wakafika Sodoma wakati wa jioni, naye Loti alikuwa ameketi kwenye lango la mji. Wakati alipowaona, aliondoka kwenda kuwalaki na kuwasujudia hadi chini. 19:2 Mwa 18:4; Lk 7:44; Amu 19:15, 20Akasema, “Bwana zangu, tafadhali karibuni kwenye nyumba ya mtumishi wenu. Mnaweza kunawa miguu na kulala hapa kisha asubuhi na mapema mwendelee na safari yenu.”

Wakamjibu, “La hasha, tutalala hapa nje uwanjani.”

19:3 Mwa 18:6; 33:11; Ay 31:32; Kut 12:39Lakini akasisitiza kwa nguvu kwamba waingie pamoja naye nyumbani kwake. Akawaandalia chakula, mikate isiyotiwa chachu, nao wakala. 19:4 Mwa 13:13Kabla hawajaenda kulala, watu wote kutoka kila sehemu ya mji wa Sodoma, vijana kwa wazee, waliizunguka nyumba. 19:5 Mwa 13:13; Law 18:22; Kum 23:18; Amu 19:22; Rum 1:24-27Wakamwita Loti wakisema, “Wako wapi wale watu ambao walikuja kwako jioni hii? Watoe nje kwetu ili tuweze kuwalawiti.”

19:6 Amu 19:23Loti akatoka nje kuonana nao, akaufunga mlango nyuma yake, akasema, “La hasha, rafiki zangu. Msifanye jambo hili ovu. 19:8 Amu 19:24; 2Pet 2:7-8Tazama, ninao binti wawili ambao kamwe hawajakutana kimwili na mwanaume. Acha niwatoe nje kwenu, nanyi mnaweza kuwafanyia lolote mnalotaka. Lakini msiwafanyie chochote watu hawa, kwa sababu wako kwenye ulinzi chini ya dari langu.”

19:9 Mwa 13:8; 23:4; Mdo 7:27Wakamjibu, “Tuondokee mbali.” Wakaendelea kusema, “Huyu mtu alikuja hapa kama mgeni na sasa anataka kuwa mwamuzi wetu! Tutakutenda vibaya kuliko wao.” Waliendelea kumlazimisha Loti na kusonga mbele ili kuvunja mlango.

19:10 Mwa 18:2Lakini watu wale waliokuwa ndani wakanyoosha mkono wakamvuta Loti ndani ya nyumba na kufunga mlango. 19:11 Kum 28:28-29; 2Fal 6:18; Mdo 13:11Kisha wakawapiga kwa upofu wale watu waliokuwa mlangoni mwa ile nyumba, vijana kwa wazee, hivyo hawakuweza kuupata mlango.

19:12 Mwa 6:18; 7:1Wale watu wawili wakamwambia Loti, “Una mtu mwingine yeyote hapa, wakwe zako, wana au binti, ama yeyote mwingine aliye wako katika mji huu? Waondoe hapa, 19:13 Kut 12:29; 2Sam 24:16; 2Fal 19:35; 1Nya 21:12, 15; 2Nya 32:21; Mwa 18:20; Za 78:49; Yer 21:12; 25:18; 44:22; 51:45kwa sababu tunapaangamiza mahali hapa. Kilio kwa Bwana dhidi ya watu wa hapa ni kikubwa kiasi kwamba ametutuma kupaangamiza.”

19:14 Hes 16:21; Ufu 18:4; Kut 9:21; 1Fal 13:18; Yer 5:12; 43:2; Lk 17:28Kwa hiyo Loti alitoka ili kuzungumza na wakwe zake, waliokuwa wamewaposa binti zake. Akawaambia, “Fanyeni haraka kuondoka mahali hapa, kwa kuwa Bwana yu karibu kuangamiza mji huu!” Lakini wakwe zake walifikiri kwamba alikuwa akitania.

19:15 Hes 16:26; Ay 21:18; Za 58:9; 73:19; 90:5; Ufu 18:4Kunako mapambazuko, malaika wakamhimiza Loti, wakamwambia, “Fanya haraka! Mchukue mke wako na binti zako wawili walioko hapa, la sivyo utaangamizwa wakati mji utakapoadhibiwa.”

19:16 2Pet 2:7; Kut 34:6; Za 33:8-9Alipositasita, wale watu wakamshika mkono wake na mikono ya mke wake na binti zake wawili na kuwaongoza salama nje ya mji, kwa kuwa Bwana alikuwa na huruma kwao. 19:17 1Fal 19:3; Yer 48:6; Mwa 13:12; 14:10; Mt 24:16Mara walipokwisha kuwatoa nje, mmoja wao akawaambia, “Mkimbie kwa usalama wenu! Msitazame nyuma, wala msisimame popote katika nchi tambarare! Kimbilieni milimani, ama sivyo mtaangamizwa!”

Lakini Loti akawajibu, “La hasha, bwana zangu, tafadhalini! 19:19 Mwa 6:8; 18:3; 24:12; 39:21; 40:14; 47:29; Rut 1:8; 2:20; 3:10Mtumishi wenu amepata kibali mbele ya macho yenu, nanyi mmeonyesha wema mkubwa kwangu kwa kuokoa maisha yangu. Lakini siwezi kukimbilia milimani, janga hili litanikumba, nami nitakufa. Tazama, hapa kuna mji karibu wa kukimbilia, nao ni mdogo. Niruhusuni nikimbilie humo, ni mdogo sana, ama sivyo? Ndipo maisha yangu yatasalimika.”

19:21 1Sam 25:35; 2Sam 14:8; Ay 42:9Akamwambia, “Vema sana, nitalikubali hili ombi pia, sitauangamiza mji ulioutaja. 19:22 Mwa 13:10Lakini ukimbilie huko haraka, kwa sababu sitaweza kufanya lolote mpaka ufike huko.” (Ndiyo maana mji huo ukaitwa Soari.19:22 Soari maana yake Mdogo.)

19:23 Mwa 13:10Wakati Loti alipofika Soari, jua lilikuwa limechomoza katika nchi. 19:24 Ay 18:15; Za 11:6; Isa 30:33; 34:9; Eze 38:22; Kum 29:23; Isa 1:9; 13:19; Yer 49:18; 50:40; Amo 4:11; Mwa 18:17; Law 10:2; Mt 10:15; Lk 17:29; Yud 7Ndipo Bwana akanyesha moto wa kiberiti uliotoka mbinguni kwa Bwana juu ya Sodoma na Gomora. 19:25 Eze 16:48; 26:16; Sef 3:8; Hag 2:22; Mwa 13:12; Za 107:34; Isa 1:10; Yer 20:16; 23:14; Mao 4:6Hivyo akaiteketeza miji ile na eneo lote la tambarare, pamoja na wote waliokuwa wanaishi katika miji, hata pia mimea yote katika nchi. 19:26 Lk 17:32Lakini mke wa Loti akatazama nyuma, hivyo akawa nguzo ya chumvi.

19:27 Mwa 18:22Asubuhi na mapema siku iliyofuata, Abrahamu akaamka na kurudi mahali pale aliposimama mbele za Bwana. 19:28 Mwa 15:17; Kut 19:18; Ufu 9:2, 18Akatazama upande wa Sodoma na Gomora, kuelekea nchi yote ya tambarare, akaona moshi mzito ukipanda kutoka kwenye nchi, kama moshi utokao kwenye tanuru.

19:29 Mwa 8:1; 13:12; 14:12; Eze 14:16; 2Pet 2:7Kwa hiyo Mungu alipoiangamiza miji ya tambarare alimkumbuka Abrahamu, akamtoa Loti kutoka kwenye lile janga lililoharibu miji ile ambamo Loti alikuwa ameishi.

Loti Na Binti Zake

19:30 Mwa 13:10; 14:10Loti na binti zake wawili waliondoka Soari na kufanya makao yao kule milimani, kwa maana aliogopa kukaa Soari. Yeye na binti zake wawili waliishi katika pango. Siku moja binti mkubwa akamwambia yule mdogo, “Baba yetu ni mzee na hakuna mwanaume mahali hapa atakayekutana na sisi kimwili, kama ilivyo desturi ya mahali pote duniani. 19:32 Mwa 16:2; 38:18Tumnyweshe baba yetu mvinyo kisha tukutane naye kimwili ili tuhifadhi uzao wetu kupitia baba yetu.”

Usiku ule walimnywesha baba yao mvinyo, alipolewa binti yake mkubwa akaingia na kukutana naye kimwili. Baba yao hakujua wakati binti yake alipoingia kulala naye wala alipotoka.

Siku iliyofuata binti mkubwa akamwambia yule mdogo, “Usiku uliopita mimi nilikutana kimwili na baba yangu. Tumnyweshe divai tena, usiku huu nawe ukutane naye kimwili ili tuweze kuhifadhi uzao wetu kupitia baba yetu.” 19:35 Mwa 9:21Kwa hiyo wakamnywesha baba yao mvinyo tena usiku ule, naye binti yake mdogo akaingia, akakutana naye kimwili. Kwa mara nyingine baba yao hakujua binti yake alipolala naye wala alipoondoka.

Hivyo binti wawili wa Loti wakapata mimba kwa baba yao. 19:37 Mwa 36:35; Kut 15:15; Hes 25:1; Isa 15:1; 25:10; Yer 25:21; 48:1; Eze 25:8; Sef 2:9; Hes 22:4; 24:17; Rut 1:4, 22; 1Sam 14:47; 22:3-4; 2Sam 8:2; 2Fal 3:4; Ezr 9:1; Za 108:9Binti mkubwa akamzaa mwana, akamwita jina lake Moabu; ndio baba wa Wamoabu hata leo. 19:38 Hes 21:24; Kum 2:19; 23:3; Yos 12:2; Amu 3:13; 10:6-7; 1Sam 11:1-11; 14:47; 1Nya 19:1; 2Nya 20:23; 26:8; 27:5; Neh 2:19; 4:3; Yer 25:21; 40:14; 49:1; Eze 21:28; 25:2; Amo 1:13Binti mdogo naye pia akamzaa mwana, naye akamwita Benami; ndiye baba wa Waamoni hata leo.

Read More of Mwanzo 19

Mwanzo 20:1-18

Abrahamu Na Abimeleki

20:1 Mwa 18:1; 12:9; 14:7; 16:7; 26:3Basi Abrahamu akaendelea mbele kutoka huko hadi nchi ya Negebu na akaishi kati ya Kadeshi na Shuri. Kwa muda mfupi alikaa Gerari kama mgeni, 20:2 Mwa 12:13, 15; 26:1huko Abrahamu akasema kuhusu Sara mkewe, “Huyu ni dada yangu.” Kisha Abimeleki mfalme wa Gerari akatuma Sara aletwe, naye akamchukua.

20:3 Hes 12:6; 22:9, 20; Mwa 26:11; 28:12; 31:10, 24; 37:5-9; 40:5; 41:1; Kum 13:1; Kut 10:7; 12:33; Ay 33:15; Dan 2:1; 4:5; 1Nya 16:21; Za 105:14, 28Lakini Mungu akamjia Abimeleki katika ndoto wakati wa usiku na kumwambia, “Wewe ni kama mfu kwa sababu ya huyu mwanamke uliyemchukua; yeye ni mke wa mtu.”

20:4 Mwa 18:25Wakati huo Abimeleki alikuwa bado hajamsogelea, kwa hiyo akasema, “Je, Bwana utaliharibu taifa lisilo na hatia? 20:5 Mwa 12:19; 17:1; Za 7:8; 25:21; 26:6; 41:12Hakusema kwangu, ‘Huyu ni dada yangu,’ naye Sara pia hakusema, ‘Huyu ni kaka yangu’? Nimefanya haya kwa dhamiri njema na mikono safi.”

20:6 1Sam 25:26, 34; Mwa 13:13; Za 41:4; 51:4Kisha Mungu akamwambia katika ndoto, “Ndiyo, najua ya kwamba umefanya haya kwa dhamiri safi, kwa hiyo nimekuzuia usinitende dhambi. Ndiyo sababu sikukuacha umguse. 20:7 Kum 18:18; 34:10; 2Fal 3:11; 5:3; 1Nya 16:22; Za 105:15; Kut 8:8; Hes 11:2; 12:13; 1Sam 7:5; 1Fal 13:6; Ay 42:8; Yer 18:20; 37:3; 42:2; Za 9:5Sasa umrudishe huyo mke wa mtu, kwa maana ni nabii, naye atakuombea nawe utaishi. Lakini kama hutamrudisha, ujue kwa hakika kuwa wewe na watu wako wote mtakufa.”

Kesho yake asubuhi na mapema Abimeleki akawaita maafisa wake wote, na baada ya kuwaambia yote yaliyotokea, waliogopa sana. 20:9 Mwa 12:18; 34:7Kisha Abimeleki akamwita Abrahamu na kumwambia, “Wewe umetufanyia nini? Nimekukosea nini hata ukaleta hatia kubwa namna hii juu yangu na ufalme wangu? Umenifanyia mambo ambayo hayakupasa kufanyika.” Abimeleki akamuuliza Abrahamu, “Ulikuwa na kusudi gani kufanya hivi?”

20:11 Mwa 12:12; 31:31; 42:18; Neh 5:15; Ay 31:23; Za 36:1; Mit 16:6Abrahamu akajibu, “Niliwaza kwamba, ‘Hakika hakuna hofu ya Mungu mahali hapa, nao wataniua kwa sababu ya mke wangu.’ 20:12 Mwa 12:13Pamoja na hayo, ni kweli kwamba yeye ni dada yangu, binti wa baba yangu ingawa si mtoto wa mama yangu; basi akawa mke wangu. 20:13 Kum 26:5; 1Nya 16:20; Isa 30:28; 63:17; Mwa 12:1Wakati Bwana aliponifanya nisafiri mbali na nyumbani mwa baba yangu, nilimwambia, ‘Hivi ndivyo utakavyoonyesha pendo lako kwangu: Kila mahali tutakapokwenda, kuhusu mimi sema, “Huyu ni kaka yangu.” ’ ”

20:14 Mwa 12:16Kisha Abimeleki akatwaa kondoo na ngʼombe, na watumwa wa kiume na wa kike akampa Abrahamu, akamrudisha Sara kwa mumewe. 20:15 Mwa 13:9; 45:18Abimeleki akasema, “Nchi yangu iko mbele yako, ishi popote unapotaka.”

Akamwambia Sara, “Ninampa kaka yako shekeli elfu moja za fedha. Hii ni kufidia kosa lililofanyika dhidi yako mbele ya wote walio pamoja nawe; haki yako imethibitishwa kabisa.”

20:17 Ay 42:9Kisha Abrahamu akamwomba Mungu, naye Mungu akamponya Abimeleki, mke wake, na watumwa wake wa kike kwamba waweze kupata watoto tena, 20:18 Mwa 12:17kwa kuwa Bwana alikuwa ameyafunga matumbo ya wote katika nyumba ya Abimeleki kwa sababu ya Sara, mke wa Abrahamu.

Read More of Mwanzo 20