Ezekieli 36:1-38, Ezekieli 37:1-28 NEN

Ezekieli 36:1-38

Unabii Kwa Milima Ya Israeli

36:1 Eze 6:2, 3; 17:22“Mwanadamu, itabirie milima ya Israeli na useme, ‘Ee milima ya Israeli, sikieni neno la Bwana. 36:2 Eze 25:3; Kum 32:13; Eze 35:10; Hab 3:19; Eze 6:2-3Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Kwa sababu adui wanasema juu yako, “Aha! Mahali palipoinuka pa zamani pamekuwa milki yetu.” ’ 36:3 Za 44:12-14; Mao 3:62; Oba 1:13; Mao 2:16Kwa hiyo tabiri na useme, ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Kwa sababu wamewafanya ukiwa na kuwagandamiza kila upande ili mpate kuwa milki ya mataifa mengine na kuwa kitu cha kusimangwa na kudhihakiwa miongoni mwa watu, 36:4 Eze 6:3; Kum 11:11; Za 79:4; Eze 33:24; Law 26:43; Yer 2:26; Eze 33:28-29kwa hiyo, ee milima ya Israeli, sikieni neno la Bwana Mwenyezi: Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo kwa milima na vilima, kwa makorongo na mabonde, kwa mahame yaliyo ukiwa, miji iliyoachwa ambayo imetekwa nyara na kudharauliwa na mataifa mengine yanayowazunguka, 36:5 Kum 4:24; Isa 66:16; Yoe 3:2-14; Zek 1:15; Yer 25:31; Kum 29:20hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Katika wivu wangu uwakao nimenena dhidi ya mataifa mengine na dhidi ya Edomu yote, kwa maana kwa furaha na hila katika mioyo yao waliifanya nchi yangu kuwa milki yao ili wapate kuteka nyara sehemu yake ya malisho.’ 36:6 Za 123:3-4; Eze 34:29Kwa hiyo tabiri kuhusu nchi ya Israeli na uiambie milima na vilima, makorongo na vijito na mabonde: ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Ninanena katika wivu wa ghadhabu yangu kwa sababu mmedharauliwa na mataifa. 36:7 Yer 25:9; Hes 14:30Kwa hiyo hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Ninaapa kwa mkono wangu ulioinuliwa kwamba mataifa wanaowazunguka nao pia watadharauliwa.

36:8 Isa 4:2; 27:6; Eze 20:5; 47:12“ ‘Lakini ninyi, ee milima ya Israeli, mtatoa matawi na matunda kwa ajili ya watu wangu Israeli, kwa sababu hivi karibuni watakuja nyumbani. Mimi ninawajibika nanyi na nitawaangalia kwa upendeleo, mtalimwa na kupandwa mbegu, 36:10 Isa 49:17-23; Yer 30:18; Isa 61:4; Amo 9:14nami nitaizidisha idadi ya watu kwenu, naam, nyumba yote ya Israeli. Miji itakaliwa na watu na magofu yatajengwa upya. 36:11 Mik 7:14; Law 26:9; Ay 42:13; Hos 2:20; 1Nya 5:20; Yer 31:28; Zek 10:8Nitaongeza idadi ya watu na wanyama juu yenu, nao watazaana sana na kuwa wengi mno. Nitawakalisha watu ndani yenu kama ilivyokuwa wakati uliopita, nami nitawafanya mfanikiwe kuliko hapo kwanza. Ndipo mtakapojua kuwa Mimi ndimi Bwana. 36:12 Eze 47:14; Oba 1:17Nitawafanya watu, watu wangu Israeli, kutembea juu yenu. Watawamiliki ninyi, nanyi mtakuwa urithi wao, kamwe hamtawaondolea tena watoto wao.

36:13 Hes 13:32“ ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Kwa sababu watu wanakuambia, “Unawala watu na kuliondolea taifa lako watoto wake,” kwa hiyo hutakula tena watu wala kulifanya tena taifa lako lisiwe na watoto, asema Bwana Mwenyezi. 36:15 Isa 54:4; Za 89:50-51; Sef 3:19-20; Eze 34:29Sitakufanya tena usikie dhihaka za mataifa, wala kudharauliwa na kabila za watu, wala kulifanya taifa lako lianguke, asema Bwana Mwenyezi.’ ”

Neno la Bwana likanijia tena, kusema: 36:17 Za 106; 37:38; Law 15:19; Yer 2:7; Law 12:2; Yer 2:7“Mwanadamu, nyumba ya Israeli walipokuwa wakiishi katika nchi yao wenyewe, waliinajisi kwa mwenendo wao na matendo yao. Mwenendo wao mbele zangu ulikuwa kama mwanamke aliye katika hedhi. 36:18 2Nya 34:21; Eze 16:36, 38; 23:37Hivyo nilimwaga ghadhabu yangu juu yao kwa sababu walikuwa wamemwaga damu katika nchi na kwa sababu walikuwa wameitia nchi unajisi kwa sanamu zao. 36:19 Kum 28:64; Law 18:24-28; Eze 7:8; 24:14; 39:24Nikawatawanya miongoni mwa mataifa, nao wakaenda huku na huko katika nchi mbalimbali, nikawahukumu sawasawa na mwenendo wao na matendo yao. 36:20 Law 18:21; Rum 2:24; Isa 52:5; Yer 33:24; 42:10; Eze 17:22; 12:16Tena popote walipokwenda miongoni mwa mataifa walilitia unajisi Jina langu takatifu, kwa kuwa watu walisema kuwahusu, ‘Hawa ndio watu wa Bwana, lakini imewapasa kuondoka katika nchi yake.’ 36:21 Za 74:18; Isa 48:9Lakini niliwahurumia kwa ajili ya Jina langu takatifu, ambalo nyumba ya Israeli imelitia unajisi miongoni mwa mataifa huko walikokwenda.

36:22 Rum 2:24; Kum 9:5-6; Za 106:8; Eze 20:9; Kum 9:5-6; Isa 37:35“Kwa hiyo iambie nyumba ya Israeli, ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Si kwa ajili yako, ee nyumba ya Israeli, kwamba ninafanya mambo haya, bali ni kwa ajili ya Jina langu takatifu, ambalo mmelitia unajisi miongoni mwa mataifa mliyoyaendea. 36:23 Isa 5:16; 37:23; Za 46:10; 126:2; Eze 20:14; 20:41; Hes 6:27Nitauonyesha utakatifu wa Jina langu kuu, ambalo limetiwa unajisi miongoni mwa mataifa, jina ambalo limetiwa unajisi miongoni mwao. Ndipo mataifa watakapojua kuwa Mimi ndimi Bwana, asema Bwana Mwenyezi, nitakapojionyesha mwenyewe kuwa mtakatifu kwa kuwapitia ninyi mbele ya macho yao.

36:24 Isa 43:5-6; Eze 34:13; 37:21“ ‘Kwa kuwa nitawaondoa ninyi toka mataifa, nitawakusanya kutoka nchi zote na kuwarudisha kwenye nchi yenu wenyewe. 36:25 Ebr 9:13; 10:22; Law 14:7; Zek 3:4; Za 51:2-7; Mdo 22:16; Yoe 3:21Nitawanyunyizia maji safi, nanyi mtakuwa safi, nitawatakasa kutoka uchafu wenu wote na kutoka sanamu zenu zote. 36:26 Yer 24:7; Za 51:10; 2Kor 3:3, 18; Yn 3:3-5; Eze 18:31Nitawapa moyo mpya na kuweka roho mpya ndani yenu, nitaondoa ndani yenu moyo wenu wa jiwe na kuwapa moyo wa nyama. 36:27 Efe 1:13; Yoe 2:29; Yn 3:5; Rum 8:4-9; Eze 37:14; Isa 44:3; Yer 50:20Nami nitaweka Roho yangu ndani yenu na kuwafanya ninyi mfuate amri zangu na kuwafanya kuwa waangalifu kuzishika sheria zangu. 36:28 Yer 30:22; 31:33; Eze 11:17; 14:11; 34:24; 37:14; Zek 8:8Mtaishi katika nchi niliyowapa baba zenu, ninyi mtakuwa watu wangu nami nitakuwa Mungu wenu. 36:29 Eze 34:29; Mt 1:21; Rum 11:26; Za 105:16Nitawaokoa ninyi kutoka unajisi wenu wote. Nitaiita nafaka na kuiongeza iwe nyingi sana nami sitaleta njaa juu yenu. 36:30 Law 26:4-5; Hos 2:21-22; Eze 34:13-14Nitaongeza matunda ya miti na mazao ya mashamba, ili kwamba msipate tena aibu miongoni mwa mataifa kwa ajili ya njaa. 36:31 Isa 6:5; Yer 31:19; Eze 6:9; 34:13-14Ndipo mtakapozikumbuka njia zenu za uovu na matendo yenu maovu, nanyi mtajichukia wenyewe kwa ajili ya dhambi zote na matendo yenu ya kuchukiza. 36:32 Dan 9:19; Kum 9:5Ninataka ninyi mjue kwamba sifanyi hili kwa ajili yenu, asema Bwana Mwenyezi. Oneni aibu na mkatahayari kwa ajili ya mwenendo wenu, ee nyumba ya Israeli!

36:33 Rum 8:30-32; Isa 49:8; Law 16:30; 26:31“ ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Siku ile nitakapowasafisha kutoka dhambi zenu zote, nitarudisha watu waishi katika miji yenu na magofu yatajengwa upya. 36:34 Yer 51:3Nchi iliyokuwa ukiwa italimwa badala ya kukaa ukiwa machoni mwa wale wote wanaopita ndani yake. 36:35 Mwa 2:8; Isa 51:3; Yoe 2:3; Amo 9:14Watasema, “Hii nchi iliyokuwa imeachwa ukiwa sasa imekuwa kama bustani ya Edeni, miji ile iliyokuwa magofu, ukiwa na kuangamizwa, sasa imejengewa ngome na kukaliwa na watu.” 36:36 Eze 3:26-27; 24:27; 29:21; 17:22; Lk 1:64; Yer 42:10Ndipo mataifa yanayowazunguka yaliyobakia watakapojua kuwa Mimi Bwana nimejenga tena kile kilichoharibiwa na nimepanda tena kile kilichokuwa ukiwa. Mimi Bwana nimenena, nami nitalifanya.’

36:37 Zek 10:6; 13:9; 13:9; Yer 29:12-14“Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Mara nyingine tena nitasikia maombi ya nyumba ya Israeli na kuwatendea jambo hili: Nitawafanya watu wake kuwa wengi kama kondoo, 36:38 1Fal 8:63; 2Nya 35:7-9; Kut 6:2kuwa wengi kama kundi la kondoo kwa ajili ya dhabihu huko Yerusalemu wakati wa sikukuu zao za wakati ulioamriwa. Hivyo ndivyo miji iliyokuwa magofu itajazwa na makundi ya watu. Ndipo watakapojua kuwa Mimi ndimi Bwana.”

Read More of Ezekieli 36

Ezekieli 37:1-28

Bonde La Mifupa Mikavu

37:1 Eze 8:3; 11:24; Yer 7:32; 40:1; Lk 4:1; Yer 8:2; Mdo 8:39Mkono wa Bwana ulikuwa juu yangu, naye akanitoa nje kwa Roho wa Bwana na kuniweka katikati ya bonde lililokuwa limejaa mifupa tele. Akanipitisha pande zote kwenye hiyo mifupa, nami nikaona mifupa mingi sana ndani ya lile bonde, mifupa iliyokuwa imekauka sana. 37:3 1Sam 2:6; 1Kor 15:35; Rum 4:17; Isa 26:19Akaniuliza, “Mwanadamu, mifupa hii yaweza kuishi?”

Nikajibu, “Ee Bwana Mwenyezi, wewe peke yako wajua.”

37:4 Yer 22:29; Rum 10:17Ndipo akaniambia, “Itabirie mifupa hii na uiambie, ‘Enyi mifupa mikavu, sikieni neno la Bwana! 37:5 Mwa 2:7; Ufu 11:11Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo kwa hii mifupa: Nitatia pumzi37:5 Pumzi pia ina maana ya roho kwa Kiebrania. ndani yenu, nanyi mtaishi. 37:6 Kut 6:2; Yoe 2:27; Eze 38:23Nitawawekea mishipa, nami nitaifanya nyama ije juu yenu na kuwafunika kwa ngozi. Nitatia pumzi ndani yenu, nanyi mtakuwa hai. Ndipo mtakapojua kuwa Mimi ndimi Bwana.’ ”

Basi nikatabiri kama nilivyoamriwa. Wakati nilipokuwa ninatabiri, kukawa na sauti, sauti ya kugongana, nayo mifupa ikasogeleana, mfupa kwa mfupa mwenziwe. Nikatazama, mishipa na nyama vikatokea juu ya mifupa na ngozi ikaifunika, lakini hapakuwepo pumzi ndani yake.

37:9 Isa 32:15; Zek 12:10; Eze 39:29; Za 104:30; Yer 49:36; Zek 6:5; Dan 7:2Ndipo aliponiambia, “Utabirie upepo, tabiri, mwanadamu na uuambie, ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Njoo kutoka pande nne, ee pumzi, nawe upulizie pumzi ndani ya hawa waliouawa, ili wapate kuishi.’ ” 37:10 Ufu 11:11; Eze 12:7Hivyo nikatabiri kama alivyoniamuru, nayo pumzi ikawaingia, wakawa hai na wakasimama kwa miguu yao, jeshi kubwa mno.

37:11 Ay 17:15; Mao 3:54; Isa 49:14Ndipo akaniambia: “Mwanadamu, mifupa hii ni nyumba yote ya Israeli. Nao wanasema, ‘Mifupa yetu imekauka na tumaini letu limetoweka, tumekatiliwa mbali.’ 37:12 Sef 3:20; Yer 29:14; Amo 9:14; 1Sam 2:9; Kum 32:39; Isa 26:19; Hos 13:14Hivyo watabirie na uwaambie: ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Enyi watu wangu, nitayafunua makaburi yenu na kuwatoa ndani yake, nami nitawarudisha tena katika nchi ya Israeli. 37:13 Kut 6:2; Eze 17:24; Hos 13:14Ndipo ninyi watu wangu, mtakapojua kuwa Mimi ndimi Bwana, nitakapoyafunua makaburi yenu na kuwatoa humo. 37:14 Isa 11:2; Yoe 2:28-29; Eze 36:27-28; Yer 43:2; Ufu 11:11Nitatia Roho yangu ndani yenu nanyi mtaishi, nami nitawakalisha katika nchi yenu wenyewe. Ndipo mtakapojua kwamba Mimi Bwana nimenena, nami nitalitenda, asema Bwana!’ ”

Taifa Moja Chini Ya Mfalme Mmoja

Neno la Bwana likanijia kusema: 37:16 Hes 17:2; 1Fal 12:20; 2Nya 10:17-19; 15:9“Mwanadamu, chukua fimbo na uandike juu yake, ‘Hii ni kwa ajili ya Yuda na Waisraeli waliofungamana naye.’ Kisha chukua fimbo nyingine, uandike juu yake, ‘Fimbo ya Efraimu, ni kwa ajili ya Yosefu na nyumba yote ya Israeli wanaofungamana naye.’ 37:17 Isa 11:13; Hos 1:11; Yer 50:4Ziunganishe pamoja kuwa fimbo moja ili kwamba ziwe fimbo moja katika mkono wako.

37:18 Eze 24:19; 12:9“Watu wako watakapokuuliza, ‘Je, hutatuambia ni nini maana ya jambo hili?’ 37:19 Zek 10:6Waambie, ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Nitaichukua fimbo ya Yosefu, iliyoko mikononi mwa Efraimu na ya makabila ya Israeli yanayofungamana naye na kuiunganisha na fimbo ya Yuda, nikizifanya kuwa fimbo moja, nao watakuwa wamoja katika mkono wangu.’ 37:20 Eze 12:3Inua mbele ya macho yao zile fimbo ulizoziandika 37:21 Isa 43:5-6; Mik 4:6; Eze 20:42; 39:27kisha waambie, ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Nitawatoa Waisraeli katika mataifa walikokuwa wamekwenda. Nitawakusanya popote walipo na kuwarudisha katika nchi yao wenyewe. 37:22 Isa 11:13; Yer 3:18; Yn 10:16; Eze 17:22; 34:13-14; Yer 33:24Nitawafanya kuwa taifa moja katika nchi, katika milima ya Israeli. Patakuwa na mfalme mmoja juu yao wote na kamwe hawatagawanyika tena kuwa mataifa mawili au kugawanyika katika falme mbili. 37:23 Isa 2:18; Nah 2:2; Eze 11:18; Hos 14:8; Zek 13:2-3; Yer 7:24; Eze 43:7Hawatajitia tena unajisi kwa sanamu zao na vinyago vyao visivyo na maana wala kwa makosa yao yoyote, kwa maana nitawaokoa kutoka dhambi zao zote zilizowarudisha nyuma, nami nitawatakasa. Wao watakuwa watu wangu, nami nitakuwa Mungu wao.

37:24 Isa 55:4; Hos 3:5; Amo 9:15; Za 78:70-71; Yer 30:21; 1Sam 13:14“ ‘Mtumishi wangu Daudi atakuwa mfalme juu yao, nao wote watakuwa na mchungaji mmoja. Watafuata sheria zangu na kuzishika amri zangu kwa uangalifu. 37:25 Ezr 9:12; Amo 9:15; Za 89:3-4; Eze 28:25; Isa 11:1; Eze 34:23-24Wataishi katika nchi niliyompa mtumishi wangu Yakobo, nchi ambamo baba zenu waliishi. Wao na watoto wao na watoto wa watoto wao wataishi humo milele, naye Daudi mtumishi wangu atakuwa mkuu wao milele. 37:26 Hes 25:12; Isa 55:3; Yer 30:19; Eze 16:62; Mwa 9:16; Kum 29:14Nitafanya nao Agano la amani, litakuwa Agano la milele. Nitawafanya imara na kuongeza idadi yao, nami nitaweka mahali patakatifu pangu miongoni mwao milele. 37:27 Law 26:11; Yn 1:14; Eze 34:30; 2Kor 6:16; Eze 36:28Maskani yangu yatakuwa pamoja nao, nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu. 37:28 Kut 31:13; Eze 20:12; Hos 1:10-11; Eze 43:9; Sef 3:15Ndipo mataifa watakapojua kwamba Mimi Bwana ndiye ninayeifanya Israeli kuwa takatifu, wakati mahali patakatifu pangu patakapokuwa miongoni mwao milele.’ ”

Read More of Ezekieli 37