Kutoka 21:1-36, Kutoka 22:1-31 NEN

Kutoka 21:1-36

Watumishi Wa Kiebrania

(Kumbukumbu 15:12-18)

21:1 Kut 24:3; 34:32; Kum 4:14; 6:1“Hizi ndizo sheria utakazoweka mbele ya Waisraeli:

21:2 Kut 22:3; Yer 34:8, 14; Law 25:39; Kum 15:12“Kama ukimnunua mtumwa wa Kiebrania, atakutumikia kwa miaka sita. Lakini katika mwaka wa saba, atakuwa huru naye atakwenda zake pasipo kulipa chochote. Kama akija peke yake, atakwenda huru peke yake, lakini kama akija na mke, ataondoka pamoja naye. 21:4 Law 25:44Kama bwana wake alimpatia mke naye akamzalia wana au binti, mwanamke pamoja na watoto wake watakuwa mali ya bwana wake na huyo mwanaume ataondoka peke yake.

21:5 Kum 15:16“Lakini kama mtumishi akisema, ‘Ninampenda bwana wangu, mke wangu pamoja na watoto na sitaki kuwa huru,’ 21:6 Kut 22:8-9; Kum 17:9; 19:17; 21:5; Za 40:6; Ay 39:9; 41:4ndipo bwana wake atakapolazimika kumpeleka mbele ya waamuzi. Kisha atampeleka kwenye mlango au kizingiti na kutoboa sikio lake kwa shazia. Naye atamtumikia bwana wake maisha yake yote.

21:7 Neh 5:5“Kama mtu akimuuza binti yake kuwa mtumwa, hataachwa huru kama watumwa wa kiume waachiwavyo. Kama hakumpendeza bwana wake aliyemchagua, huyo bwana atamwacha akombolewe. Hatakuwa na haki ya kumuuza kwa wageni, kwa sababu huyo bwana atakuwa amekosa uaminifu. Kama akimchagua aolewe na mwanawe, ni lazima ampe haki za kuwa binti yake. 21:10 1Kor 7:3-5Ikiwa huyo mwana aliyeozwa mtumwa mwanamke ataoa mwanamke mwingine, ni lazima aendelee kumtosheleza huyo mke wa kwanza kwa chakula, mavazi na haki zote za ndoa. Iwapo hatamtosheleza kwa mambo hayo matatu, huyo mke wa kwanza ataondoka na kuwa huru bila malipo yoyote ya fedha.

Majeraha Ya Mwilini

21:12 Mwa 4:14, 23; Kut 31:15; Law 20:9-10; 24:16; 27:29; Hes 1:51; 35:16, 30-31; Kum 13:5; 19:11; 22:22; 27:16; Ay 31:11; Mit 20:20; Mt 26:52; Mwa 9:6“Yeyote ampigaye mtu na kumuua ni lazima auawe hakika. 21:13 Hes 35:10-34; Kum 4:42; 19:2-13; Yos 20:9; 1Sam 24:4; 10:18; Yos 20:2Hata hivyo, kama hakumuua kwa makusudi, lakini Mungu akaruhusu itendeke, basi atakimbilia mahali nitakapomchagulia. 21:14 Mwa 4:8; Hes 35:20; 2Sam 3:27; 20:10; Ebr 10:26; Kum 19:11-12; 1Fal 2:28-34Lakini kama mtu akipanga na kumuua mwingine kwa makusudi, mwondoe katika madhabahu yangu na kumuua.

“Yeyote amshambuliaye baba yake au mama yake ni lazima auawe.

21:16 Mwa 37:28; Kut 22:4; Kum 24:7“Yeyote amtekaye nyara mwingine akamuuza au akamweka kwake, akikamatwa ni lazima auawe.

21:17 Kum 5:16; Mt 15:4; Mk 7:10; Law 20:9; Mit 20:20“Yeyote atakayemlaani baba yake au mama yake ni lazima auawe.

“Kama watu wakigombana na mmoja akimpiga mwingine kwa jiwe au kwa ngumi yake na hakufa bali akaugua na kulala kitandani, 21:19 2Sam 3:29yule aliyempiga ngumi hatahesabiwa kuwa na hatia kama mwenzake ataamka na kujikongoja kwa fimbo yake, lakini hata hivyo, ni lazima amlipe fidia ya muda wake aliopoteza na awajibike mpaka apone kabisa.

21:20 Law 25:43; Efe 6:9“Kama mtu akimpiga mtumwa wake wa kiume au wa kike kwa fimbo na mtumwa huyo akafa papo hapo, ni lazima aadhibiwe 21:21 Law 25:44-46lakini ikiwa mtumwa ataamka baada ya siku moja au mbili, hataadhibiwa, kwa sababu yule mtumwa ni mali yake.

21:22 Kum 22:18, 19“Ikiwa watu wawili wanapigana na wakamuumiza mwanamke mjamzito, naye akazaa kabla ya wakati lakini hakuna majeraha makubwa, mhalifu atatozwa mali kiasi cha madai ya mume wa yule mwanamke, na jinsi mahakama itakavyoamua. 21:23 Law 24:19; Kum 19:21Lakini kukiwa na jeraha kubwa, ni lazima ulipe uhai kwa uhai, 21:24 Kut 21:23; Mt 5:38; Kum 19:21; Mt 5:38; 7:2; Law 24:20jicho kwa jicho, jino kwa jino, mkono kwa mkono, mguu kwa mguu, kuchomwa moto kwa kuchomwa moto, jeraha kwa jeraha, mchubuko kwa mchubuko.

21:26 Kol 4:1“Ikiwa mtu atampiga mtumwa mwanaume au mwanamke kwenye jicho na kuliharibu, ni lazima amwache huru yule mtumwa kama fidia ya hilo jicho. Kama akimvunja jino mtumwa wa kiume au wa kike, ni lazima amwache huru huyo mtumwa kwa kufidia hilo jino.

21:28 Mwa 9:5“Kama fahali akimuua mwanaume au mwanamke kwa kumpiga kwa pembe, fahali huyo ni lazima auawe kwa kupigwa mawe, na nyama yake haitaliwa. Lakini mwenye fahali huyo hatawajibika. Lakini hata hivyo, ikiwa huyo fahali amekuwa na tabia ya kupiga kwa pembe, na mwenyewe ameonywa na hakutaka kumfungia naye akamuua mwanaume au mwanamke, huyo fahali ni lazima auawe kwa mawe na mwenye fahali pia auawe. 21:30 Hes 35:21Lakini ikiwa malipo yatatakiwa kwake, basi anaweza kulipa kinachodaiwa ili kuukomboa uhai wake. Sheria hii pia itatumika ikiwa fahali atampiga kwa pembe mwana au binti. 21:32 Mwa 37:28; Mt 26:15; 27:3, 9; Zek 11:12, 13; Flp 2:7Ikiwa fahali atampiga mtumwa wa kike au wa kiume, mwenye fahali atalipa shekeli thelathini21:32 Shekeli 30 ni sawa na gramu 300. za fedha kwa bwana mwenye mtumwa, na fahali ni lazima auawe kwa mawe.

21:33 Lk 14:5“Kama mtu akiacha shimo wazi, ama akachimba shimo kisha asilifukie, na ngʼombe au punda akatumbukia ndani yake, mwenye shimo ni lazima alipe hasara iliyotokea; ni lazima amlipe mwenye mnyama. Mnyama aliyekufa atakuwa wake.

“Kama fahali wa mtu fulani atamuumiza fahali wa mtu mwingine na akafa, watamuuza yule aliye hai na wagawane sawa fedha pamoja na mnyama aliyekufa. Hata hivyo, kama ikifahamika kwamba fahali huyo alikuwa na tabia ya kupiga kwa pembe na mwenyewe hakumfunga, ni lazima mwenye fahali alipe mnyama kwa mnyama, na mnyama aliyekufa atakuwa wake.

Read More of Kutoka 21

Kutoka 22:1-31

Ulinzi Wa Mali

22:1 Law 6:1-7; 2Sam 12:6; Mit 6:31; Lk 19:8“Kama mtu akiiba maksai au kondoo na kumchinja au kumuuza, ni lazima alipe ngʼombe watano badala ya maksai mmoja na kondoo wanne badala ya kondoo mmoja.

22:2 Ay 24:16; Yer 2:34; Hos 7:1; Mt 6:19-20; 24:43; Hes 35:27; Kut 20:15; Law 19:11; Kum 5:19; Lk 18:20; Rum 13:9; Efe 4:28; 1Pet 4:15“Kama mwizi akishikwa anavunja nyumba akapigwa hata akafa, aliyemuua hana hatia ya kumwaga damu; 22:3 Kut 21:2; Mt 18:25lakini jambo hilo likitokea wakati jua limechomoza, huyo mtu atakuwa na hatia ya kumwaga damu.

“Mwizi huyo sharti alipe, lakini kama hana kitu, lazima auzwe ili alipe kwa ajili ya wizi wake.

22:4 1Sam 12:5; Mwa 43:12; Kut 21:16; Mit 6:31“Kama mnyama aliyeibwa akikutwa hai mikononi mwake, ikiwa ni maksai au punda au kondoo, lazima alipe mara mbili.

“Kama mtu akichunga mifugo yake katika shamba au shamba la mizabibu, na akawaachia wajilishe katika shamba la mtu mwingine, ni lazima alipe vitu bora kutoka kwenye shamba lake mwenyewe au kutoka shamba lake la mizabibu.

22:6 Amu 15:5“Kama moto ukiwaka na kuenea kwenye vichaka vya miiba na kuteketeza miganda ya nafaka au nafaka ambayo haijavunwa, au kuteketeza shamba lote, mtu yule aliyewasha moto lazima alipe.

22:7 Law 6:2; Mwa 43:12“Kama mtu akimpa jirani yake fedha au mali nyingine amtunzie, na kama vikiibwa kutoka nyumba ya huyo jirani, kama mwizi atashikwa, lazima alipe mara mbili. 22:8 Kut 21:6; Kum 17:8-9Lakini mwizi asipopatikana, mwenye nyumba atafika mbele ya waamuzi ili kuthibitisha kuwa hakuchukua mali ya mwenzake. 22:9 Kum 25:1Pakiwepo jambo lolote la mali isiyo halali, ikiwa ni maksai, punda, kondoo, mavazi, ama mali yoyote iliyopotea ambayo fulani atasema, ‘Hii ni mali yangu,’ pande zote mbili wataleta mashauri yao mbele ya waamuzi. Yule ambaye waamuzi watamwona kuwa na hatia atamlipa jirani yake mara mbili.

“Kama mtu akimpa jirani yake punda, ngʼombe, kondoo au mnyama mwingine yeyote amtunzie, akifa au akijeruhiwa au akichukuliwa wakati haonekani na mtu yeyote, 22:11 Law 6:3; 1Fal 8:31; 2Nya 6:22; Ebr 6:16jambo hili kati yao wawili litaamuliwa kwa kuapa kiapo mbele za Bwana, kwamba huyo jirani hakuhusika na wizi wa mali ya jirani yake. Mwenye mali itampasa akubali jambo hili, na hakuna malipo yatakayohitajika. Lakini kama mnyama aliibwa kwa jirani, itampasa amlipe mwenye mnyama. 22:13 Mwa 31:39Kama ameraruliwa na mnyama pori, ataleta mabaki ya mnyama kama ushahidi, naye hatadaiwa kulipa mnyama aliyeraruliwa.

“Kama mtu akimwazima mnyama kutoka kwa jirani yake, na kama akiumia au akafa na mwenye mnyama hayupo, lazima amlipe huyo mnyama. 22:15 Law 19:13; Ay 17:5Lakini mwenye mnyama akiwa angalipo na mnyama wake, mwazimaji hatalazimika kumlipa. Kama mnyama alikuwa amekodishwa, fedha iliyolipwa kwa kukodisha inatosha kwa kufidia hasara.

Uwajibikaji Wa Kijamii

22:16 Kum 22:28; Mwa 34:12“Kama mtu akimshawishi bikira ambaye hajaposwa na akilala naye, lazima alipe mahari, kisha atamwoa msichana huyo. Baba wa msichana akikataa katakata kumpa huyo mtu huyo msichana wake, bado ni lazima huyo mtu atalipa mahari kama inavyostahili malipo ya ubikira.

22:18 Kut 7:11; Law 19:26, 31; 20:27; Kum 18:17; 1Sam 28:3; 2Nya 33:6; Isa 57:3“Usiruhusu mwanamke mchawi aishi.

22:19 Law 18:23; 20:15; Kum 27:21“Mtu yeyote aziniye na mnyama lazima auawe.

22:20 Kut 20:23; 22:21“Mtu awaye yote anayemtolea mungu mwingine dhabihu isipokuwa Bwana, lazima aangamizwe.

“Usimtendee mgeni vibaya au kumwonea, kwa kuwa nanyi mlikuwa wageni huko Misri.

22:22 Kum 10:18; 24:6, 10-17; Ay 22:6-9; 24:3; 21; Za 68:5; 146:9; Mit 23:10; Isa 1:17; Yer 7:5-6; 21:12; 22:3; Eze 18:5-12; Zek 7:9-10; Mal 3:5; Yak 1:27“Usimdhulumu mjane wala yatima. 22:23 Lk 18:7; Kum 10:18; 15:9; 24:15; Ay 34:28; 35:9; Za 10:14-17; 12:5; 18:6; Yak 5:4Kama ukifanya hivyo nao wakinililia, hakika nitasikia kilio chao. 22:24 Za 10:9; 69:24; Mao 5:3Hasira yangu itawaka, nami nitawaua kwa upanga, wake zenu watakuwa wajane na watoto wenu watakuwa yatima.

22:25 Law 25:35-37; Kum 15:7-11; 23:20; Neh 5:7-10; Za 15:5; Eze 18:8“Kama ukimkopesha mmojawapo wa watu wangu fedha ambaye ni mhitaji, usiwe kama mtu mkopesha fedha; usimtoze riba. 22:26 Mit 20:16; Eze 33:15; Amo 2:8Kama ukichukua vazi la jirani kama rehani, ulirudishe kwake kabla jua kuzama, 22:27 Kum 24:13, 17; Ay 22:6; 24:7; 29:11; 31:19-20; Eze 18:12, 16; Kut 34:6; Kum 4:31; 2Nya 30:9; Neh 9:17; Za 99:8; 103:8; 116:5; 145:8; Yoe 2:13; Yon 4:2kwa kuwa vazi lake ndilo pekee alilo nalo la kumfunika mwili wake. Ni nini kingine atajifunika nacho? Atakaponililia, nitasikia, kwa kuwa nina huruma.

22:28 Kut 20:7; 2Sam 16:5, 9; 1Sam 19:21; 1Fal 21:10; 2Fal 2:23; Za 102; 8; Mhu 10:20; Mdo 23:5“Usimkufuru Mungu au kumlaani mtawala wa watu wako.

22:29 Kut 23:15-19; 34:20-26; Law 19:24; 23:10; Hes 18:13; 28:26; Kum 18:4; 26:2, 10; 1Sam 6:3; Neh 10:35; Mit 3:9; Mal 3:10; Kut 13:2; Hes 8:16-17; Lk 2:23“Usiache kutoa sadaka kutoka ghala lako au mapipa yako.

“Lazima unipe mzaliwa wa kwanza wa wana wako. 22:30 Kut 34:19; Kum 15:19; Law 12:3; 22:27; Mwa 17:12Ufanye vivyo hivyo kwa ngʼombe wako na kwa kondoo wako. Waache wakae na mama zao kwa siku saba, lakini siku ya nane unipe.

22:31 Kut 19:6; Law 19:2; 22:31; Ezr 9:2; Law 7:24; 17:15; 22:8; Kum 14:21; Eze 4:14; 44:31“Ninyi mtakuwa watu wangu watakatifu. Kwa hiyo msile nyama ya mnyama aliyeraruliwa na wanyama pori; mtupieni mbwa.

Read More of Kutoka 22