Kutoka 13:1-22, Kutoka 14:1-31 NEN

Kutoka 13:1-22

Kuwekwa Wakfu Kwa Wazaliwa Wa Kwanza

Bwana akamwambia Mose, 13:2 Kut 22:29; 34:20; Law 27:26; Hes 3:13; 8:17; 18:15; Kum 15:19; Neh 10:34; Lk 2:23“Niwekeeni wakfu kila mzaliwa wa kwanza wa kiume. Kila mtoto wa kwanza aliye kifungua tumbo miongoni mwa Waisraeli ni mali yangu, akiwa wa mwanadamu au wa mnyama.”

13:3 Kut 7:4; Law 26:13; Hes 22:5; 26:4; Kum 4:45; 5:6; Za 81:10; 114:1; Kut 3:20; 12:8Ndipo Mose akawaambia watu, “Ikumbukeni siku hii, siku ambayo mlitoka katika nchi ya Misri, katika nchi ya utumwa, kwa sababu Bwana aliwatoa humo kwa mkono wenye nguvu. Msile chochote kilichotiwa chachu. 13:4 Kut 12:2Leo, katika mwezi wa Abibu,13:4 Abibu ni jina la mwezi wa kwanza kwa Wayahudi, ambao ni mwezi wa nne katika kalenda yetu. mnatoka. 13:5 Kut 3:8; 12:25-26Bwana atakapokuleta katika nchi ya Wakanaani, Wahiti, Waamori, Wahivi na Wayebusi, nchi aliyowaapia baba zako kukupa, nchi itiririkayo maziwa na asali, utaiadhimisha sikukuu hii katika mwezi huu: 13:6 Kut 12:15-20Kwa siku saba utakula mikate isiyotiwa chachu na katika siku ya saba utamfanyia Bwana sikukuu. Kwa muda wa siku saba utakula mikate isiyotiwa chachu, pasionekane kitu chochote kilicho na chachu miongoni mwako, wala chachu yoyote isionekane popote ndani ya mipaka yako. 13:8 Kut 10:2; Za 78:5-6Siku ile utamwambia mwanao, ‘Nafanya hivi kwa sababu ya jambo ambalo Bwana alinitendea nilipotoka katika nchi ya Misri.’ 13:9 Isa 44:5; Kum 6:8; 11:18; Mit 3:3; Mt 23:5; Kut 3:20Adhimisho hili, litakuwa kama alama kwenye mkono wako na ukumbusho katika paji lako la uso, kwamba sheria ya Bwana inapaswa iwe kinywani mwako. Kwa kuwa Bwana alikutoa katika nchi ya Misri kwa mkono wake wenye nguvu. 13:10 Kut 12:14; Za 75:2; 102:13Ni lazima uishike amri hii kwa wakati uliopangwa mwaka baada ya mwaka.

13:11 Mwa 22:16; Kum 1:8; Mwa 12:7; 17:19; Za 105:42-45“Baada ya Bwana kukuingiza katika nchi ya Wakanaani na kukupa nchi hiyo, kama alivyokuahidi kwa kiapo na kwa baba zako, 13:12 Mwa 4:4; Law 27:26; Hes 3:13; 18:15-17; Lk 2:23inakupasa kumtolea Bwana mzaliwa wa kwanza wa kila tumbo. Wazaliwa wote wa kwanza wa kiume wa mifugo yako ni mali ya Bwana. 13:13 Law 27:11; Kut 34:20; Isa 66:3; Hes 3:46-47; 18:15Kila mzaliwa wa kwanza wa punda utamkomboa kwa mwana-kondoo, lakini kama hukumkomboa, utamvunja shingo yake. Kila mzaliwa wa kwanza mwanaume miongoni mwa wana wenu utamkomboa.

13:14 Kut 10:2; 20:2; Kum 7:8; 6:20; 28:68“Katika siku zijazo, mwanao akikuuliza, ‘Hii ina maana gani?’ Mwambie, ‘Kwa mkono wenye nguvu Bwana alitutoa katika nchi ya Misri, kutoka nchi ya utumwa. Farao alipokataa kwa ukaidi kuturuhusu kuondoka, Bwana aliua kila mzaliwa wa kwanza wa Wamisri, mwanadamu na wa mnyama. Hii ndiyo sababu ninatoa dhabihu kwa Bwana mzaliwa wa kwanza wa kiume, wa kila tumbo na kumkomboa kila mzaliwa wa kwanza wa wana wangu.’ Jambo hili litakuwa kama ishara kwenye mkono wako na kama alama kwenye paji la uso wako, kwamba Bwana alikutoa katika nchi ya Misri kwa mkono wake wenye nguvu.”

Nguzo Ya Wingu Na Moto

13:17 Kut 14:11; Hes 14:1-4; Kum 17:16; Hos 11:5Farao alipowaachia watu waende, Mungu hakuwaongoza kufuata njia ipitiayo katika nchi ya Wafilisti, ingawa njia hiyo ilikuwa fupi zaidi. Kwa maana Mungu alisema, “Wakikabiliana na vita, wanaweza kubadili mawazo yao na kurudi Misri.” 13:18 Kut 15:22; Za 136:16; Eze 20:10; Yos 4:13Kwa hiyo Mungu akawaongoza watu kupitia njia ya kuzunguka kupitia jangwani, kuelekea Bahari ya Shamu. Waisraeli walipanda kutoka nchi ya Misri wakiwa wamejiandaa kwa vita.

13:19 Yos 24:32; Mdo 7:16; Ebr 11:22; Mwa 47:29-30Mose akachukua mifupa ya Yosefu kwa sababu Yosefu alikuwa amewaapisha wana wa Israeli. Alikuwa amewaambia, “Hakika Mungu atakuja kuwasaidia, nanyi ni lazima mwiichukue mifupa yangu mwende nayo kutoka mahali hapa.”

13:20 Kut 12:37; Hes 33:6Baada ya Waisraeli kuondoka Sukothi wakapiga kambi huko Ethamu pembeni mwa jangwa. 13:21 Kut 32:1; 33:14; Kum 2:7; 31:8; Amu 4:14; 5:4; Za 68:7; 72:20; Yer 2:2; Hab 3:13; Kut 14:19, 24; 24:16; 33:9-10; 34:5; 40:38; Hes 9:16; 12:5; 14:14; Kum 1:33; Neh 9:12, 19; Za 78:14; 99:7; 105:39; Isa 4:5; 1Kor 10:1Wakati wa mchana Bwana aliwatangulia kwa nguzo ya wingu kuwaongoza katika njia yao, na wakati wa usiku aliwatangulia kwa nguzo ya moto kuwaangazia, ili waweze kusafiri mchana au usiku. 13:22 Neh 9:19; Hes 33:7; Yer 44:1; Eze 29:10Ile nguzo ya wingu wakati wa mchana au ile nguzo ya moto wakati wa usiku haikuondoka mahali pake mbele ya watu.

Read More of Kutoka 13

Kutoka 14:1-31

Kuvuka Bahari Ya Shamu

Ndipo Bwana akamwambia Mose, “Waambie Waisraeli wageuke nyuma na wapige kambi karibu na Pi-Hahirothi, kati ya Migdoli na bahari. Watapiga kambi kando ya bahari, mkabala na Baal-Sefoni. Farao atafikiri kwamba, ‘Hao Waisraeli wanatangatanga katika nchi kwa kuchanganyikiwa, nalo jangwa limewafungia.’ 14:4 Kut 4:21; Za 71:11; Kut 9:16; Rum 9:17, 22-23; Kut 6:2; 7:5; Eze 32:15Nami nitaufanya moyo wa Farao mgumu, naye atawafuatilia. Lakini nitajipatia utukufu kwa ajili yangu mwenyewe kupitia Farao na jeshi lake lote, nao Wamisri watajua kuwa mimi ndimi Bwana.” Kwa hiyo Waisraeli wakafanya hivyo.

14:5 Mwa 31:21; Za 105:25Mfalme wa Misri alipoambiwa kuwa Waisraeli wamekimbia, Farao na maafisa wake wakabadili nia zao kuhusu Waisraeli, wakasema, “Tumefanya nini? Tumewaachia Waisraeli waende zao na tumeukosa utumishi wao!” Kwa hiyo akaandaliwa gari lake la vita, naye akaenda pamoja na jeshi lake. 14:7 Kut 15:4Akachukua magari bora mia sita, pamoja na magari mengine yote ya Misri, pamoja na maafisa wa magari hayo yote. 14:8 Kut 11:10; Hes 33:2; Mdo 13:17Bwana akaufanya mgumu moyo wa Farao, mfalme wa Misri, kwa hiyo akawafuatia Waisraeli, waliokuwa wakiondoka Misri kwa ujasiri. 14:9 Mwa 47:17; Yos 24:6; Isa 43:17; Kut 15:9Nao Wamisri, yaani farasi wote wa Farao na magari ya vita, wapanda farasi na vikosi vya askari, wakawafuatia Waisraeli, wakawakuta karibu na Pi-Hahirothi, mkabala na Baal-Sefoni walipokuwa wamepiga kambi kando ya bahari.

14:10 Kut 15:25; Yos 24:7; Neh 9:9; Za 5:2; 34:17; 50:15; 107:6, 28Farao alipokaribia, Waisraeli wakainua macho yao, wakawaona Wamisri wakija nyuma yao. Wakashikwa na hofu, wakamlilia Bwana. 14:11 Kut 5:21; 16:13; 17:3; Hes 11:1; 14:22; 20:4; 21:5; Kum 9:7Wakamwambia Mose, “Je, ni kwamba hayakuwako makaburi huko Misri hata umetuleta tufe huku jangwani? Umetufanyia nini kututoa Misri? 14:12 Kut 5:21; 15:24; 17:2; Za 106:7-8Hatukukuambia tulipokuwa huko Misri, tuache tuwatumikie Wamisri? Ingekuwa vyema zaidi kwetu kuwatumikia Wamisri kuliko kufa jangwani!”

14:13 Mwa 15:1; 1Sam 12:16; 2Nya 20:17; Isa 41:10-14Mose akawajibu Waisraeli, “Msiogope. Simameni imara, nanyi mtauona wokovu Bwana atakaowapatia leo. Hao Wamisri mnaowaona leo kamwe hamtawaona tena. 14:14 Kut 15:3; Kum 1:30; 3:22; 20:4; Yos 10:14; 23:3; 2Sam 5:24; 2Nya 20:29; Neh 4:20; Za 24:8; Isa 42:13; Yer 41:12; 1Sam 12:16; Za 37:7; 46:10; 116:7; Isa 28:12; 30:15; Zek 2:13Bwana atawapigania ninyi, nanyi mnatakiwa kutulia tu.”

14:15 Yos 7:10Ndipo Bwana akamwambia Mose, “Kwa nini wewe unanililia? Waambie Waisraeli waendelee mbele. 14:16 Kut 4:2, 17; Isa 10:26; Hes 20:8-11Inua fimbo yako na unyooshe mkono wako juu ya bahari ili kuyagawa maji, hivyo kwamba Waisraeli wapate kupita mahali pakavu baharini. 14:17 Kut 4:21Nitaifanya mioyo ya Wamisri kuwa migumu kusudi waingie baharini wakiwafuatia. Nami nitajipatia utukufu kupitia Farao pamoja na jeshi lake lote, kupitia magari yake ya vita na wapanda farasi wake. 14:18 Kut 6:2; Eze 32:15Nao Wamisri watajua kwamba Mimi ndimi Bwana nitakapojipatia utukufu kupitia Farao, magari yake ya vita na wapanda farasi wake.”

14:19 Mwa 16:7; Isa 63:9; Kut 13:2; 1Kor 10:1; Isa 26:7; 42:16; 49:10; 52:10; 58:8Ndipo malaika wa Mungu, aliyekuwa akisafiri mbele ya jeshi la Israeli, akaondoka akakaa nyuma yao. Pia ile nguzo ya wingu ikaondoka hapo mbele yao na kusimama nyuma, 14:20 Yos 24:7ikakaa kati ya majeshi ya Misri na Israeli. Usiku kucha wingu likaleta giza upande mmoja na nuru kwa upande mwingine, kwa hiyo hakuna aliyemkaribia mwenzake usiku kucha.

14:21 Kut 7:19; 4:2; Ay 26:12; Isa 14:27; 23:11; 51:15; Yer 31:35; Mdo 7:36; Mwa 41:6; Kut 15:8; 2Sam 22:16; 1Fal 19:11; Ay 38:1; 40:6; Yer 23:19; Nah 1:3; Mwa 8:1; 2Fal 2:8; Za 74:13; 78:13; 114:5; 136:13; Isa 63:12Ndipo Mose akanyoosha mkono wake juu ya bahari, naye Bwana akayasukuma maji ya bahari nyuma kwa upepo mkali wa mashariki usiku ule wote na kupafanya nchi kavu. Maji yakagawanyika, 14:22 Hes 33:8; Yos 24:6; Isa 43:16; 63:11; 1Kor 10:1; Kut 3:12; 15:19; Kum 31:6-8; Yos 3:16; 4:22; Neh 9:11; Za 66:6; 77:19; 106:9; Isa 11:15; 41:10; 43:5; 44:27; 50:2; 51:10; 63:13; Yer 46:28; Nah 1:4; Ebr 11:29; Kut 15:8; Yos 3:13nao Waisraeli wakapita baharini mahali pakavu, maji yakiwa ukuta upande wao wa kuume na upande wao wa kushoto.

Wamisri wakawafuatia ndani ya bahari, pamoja na farasi wote wa Farao, magari ya vita na wapanda farasi. 14:24 Kut 13:21; 1Kor 10:1; Kut 23:27; Yos 10:10; 1Sam 5:9; 5:9; 7:10; 14:15; 2Sam 5:24; 2Fal 7:6; 19:7Karibia mapambazuko, Bwana akaliangalia jeshi la Wamisri kutoka ile nguzo ya moto na ya wingu, akalifadhaisha. 14:25 Kum 32:31; 1Sam 2:2; 4:8; Kut 14:14Mungu akayaondoa magurudumu ya magari yao, kwa hivyo wakayaendesha kwa shida. Nao Wamisri wakasema, “Tuachane na Waisraeli! Bwana anawapigania dhidi ya Misri.”

Wafuatiaji Wazama

Ndipo Bwana akamwambia Mose, “Nyoosha mkono wako juu ya bahari ili maji yarudiane yawafunike Wamisri, magari yao ya vita na wapanda farasi wao.” 14:27 Yos 4:18; Kut 15:1; Kum 1:40; 11:4; Za 78:53; 106:11; 136:15; Ebr 11:29Mose akanyoosha mkono wake juu ya bahari, wakati wa mapambazuko bahari ikarudiana na kuwa kama kawaida. Wamisri wakajaribu kuyakimbia maji, lakini Bwana akawasukumia ndani ya bahari. 14:28 Kut 15:19; Yos 24:7; Kut 15:5; Amu 4:16; Neh 9:11Maji yakarudiana na kuyafunika magari ya vita na wapanda farasi pamoja na jeshi lote la Farao lililokuwa limewafuata Waisraeli ndani ya bahari. Hakuna hata mmoja wao aliyenusurika.

14:29 Yos 24:11; 2Fal 2:8; Za 74:15; 78:13Lakini Waisraeli wakapita baharini mahali pakavu, ukiwepo ukuta wa maji upande wao wa kuume na upande wao wa kushoto. 14:30 1Sam 14:23; 1Nya 11:14; Za 44:7; 106:8-10; Isa 43:3; 50:2; 51:9-10; 60:16Siku ile Bwana akawaokoa Waisraeli kutoka mikononi mwa Wamisri, nao Waisraeli wakawaona Wamisri wamelala ufuoni mwa bahari wakiwa wamekufa. 14:31 Kut 9:16; Za 147:5; Kut 20:18; Kum 31:13; Yos 4:24; 1Sam 12:18; Za 76:6-7; 112:1; Kut 4:5; Za 22:4; 40:3; 106:12; Yn 2:11; 11:45Basi Waisraeli walipoona uwezo mkubwa Bwana aliodhihirisha dhidi ya Wamisri, watu wakamwogopa Bwana na wakaweka tumaini lao kwake na kwa Mose mtumishi wake.

Read More of Kutoka 14