Waefeso 5:8-33 NEN

Waefeso 5:8-33

5:8 Efe 2:2; Yn 8:12Kwa maana zamani ninyi mlikuwa giza, lakini sasa ninyi ni nuru katika Bwana. Enendeni kama watoto wa nuru 5:9 Gal 5:22; Mt 7:16-20; Rum 15:14(kwa kuwa tunda la nuru hupatikana katika wema wote, haki na kweli), 5:10 1Tim 5:4; Rum 12:2; Flp 1:10; 1The 5:21; 1Tim 2:3nanyi tafuteni yale yanayompendeza Bwana. 5:11 Rum 13:12; 2Kor 6:14; Yn 16:8Msishiriki matendo ya giza yasiyofaa, bali yafichueni. 5:12 Rum 1:24, 26; Efe 5:3Kwa maana ni aibu hata kutaja mambo yale ambayo wasiotii wanayafanya sirini. 5:13 Yn 3:20, 21Lakini kila kitu kilichowekwa nuruni, huonekana, 5:14 Rum 13:11; Yn 5:25; Isa 60:1kwa kuwa nuru ndiyo hufanya kila kitu kionekane. Hii ndiyo sababu imesemekana:

“Amka, wewe uliyelala,

ufufuke kutoka kwa wafu,

naye Kristo atakuangazia.”

Kwa hiyo angalieni sana jinsi mnavyoenenda, si kama watu wasio na hekima, bali kama wenye hekima, 5:16 Kol 4:5; Efe 6:13mkiukomboa wakati, kwa sababu nyakati hizi ni za uovu. 5:17 Rum 12:2; Kol 1:9Kwa hiyo msiwe wajinga, bali mpate kujua nini mapenzi ya Bwana. 5:18 Isa 28:7; Lk 1:15Pia msilewe kwa mvinyo, ambamo ndani yake mna upotovu, bali mjazwe Roho. 5:19 Za 27:6Msemezane ninyi kwa ninyi kwa zaburi, nyimbo na tenzi za rohoni, mkimwimbia na kumsifu Bwana mioyoni mwenu, 5:20 Ay 1:21siku zote mkimshukuru Mungu Baba kwa kila jambo katika Jina la Bwana wetu Yesu Kristo.

5:21 Gal 5:13; 1Pet 5:5; Flp 2:3Nyenyekeaneni ninyi kwa ninyi kwa heshima kwa ajili ya Kristo.

Mafundisho Kuhusu Wake Na Waume

5:22 Mwa 3:16; Tit 2:5; Efe 6:5Ninyi wake, watiini waume zenu kama kumtii Bwana. 5:23 1Kor 11:3; Efe 1:22Kwa maana mume ni kichwa cha mkewe kama vile Kristo alivyo kichwa cha Kanisa, ambalo ni mwili wake, naye Kristo ni Mwokozi wake. 5:24 Kol 3:20; Tit 2:9Basi, kama vile Kanisa linavyomtii Kristo, vivyo hivyo na wake nao imewapasa kuwatii waume zao kwa kila jambo.

5:25 Kol 3:19Ninyi waume, wapendeni wake zenu, kama vile Kristo alivyolipenda Kanisa akajitoa kwa ajili yake 5:26 Mdo 22:16kusudi alifanye takatifu, akilitakasa kwa kuliosha kwa maji katika Neno lake, 5:27 Efe 1:4; Kol 1:22apate kujiletea Kanisa tukufu lisilo na doa wala kunyanzi au waa lolote, bali takatifu na lisilo na hatia. Vivyo hivyo imewapasa waume kuwapenda wake zao kama miili yao wenyewe. Ampendaye mkewe hujipenda mwenyewe. Hakuna mtu anayeuchukia mwili wake mwenyewe, bali huulisha na kuutunza vizuri, kama Kristo anavyolitunza Kanisa lake. 5:30 1Kor 12:27Sisi tu viungo vya mwili wake. 5:31 Mwa 2:24; Mt 19:5“Kwa sababu hii, mwanaume atamwacha baba yake na mama yake, naye ataambatana na mkewe, na hao wawili watakuwa mwili mmoja.” Siri hii ni kubwa, bali mimi nanena kuhusu Kristo na Kanisa. Hata hivyo, kila mmoja wenu ampende mkewe kama anavyoipenda nafsi yake mwenyewe, naye mke lazima amheshimu mumewe.

Read More of Waefeso 5