Kumbukumbu 1:1-46, Kumbukumbu 2:1-23 NEN

Kumbukumbu 1:1-46

Amri Ya Kuondoka Mlima Horebu

1:1 Hes 13:29; Kum 4:46; 2:8; 3:17; Yos 3:16; 8:14; 11:2; Eze 47:8; Hes 10:12Haya ni maneno Mose aliyoyasema kwa Israeli yote jangwani mashariki ya Yordani, ambayo iko Araba, inayokabiliana na Sufu, kati ya Parani na Tofeli, Labani, Haserothi na Dizahabu. 1:2 Kut 3:1; Mwa 14:7; Kum 2:14; 9:23; Yos 15:3; Hes 24:18; 1Fal 3:8; 2Kor 11:28(Ni mwendo wa siku kumi na moja kutoka Horebu kwa njia ya Mlima Seiri mpaka Kadesh-Barnea.)

1:3 Hes 14:33; 32:13; Kum 8:2; Ebr 3:7-9; Mwa 50:3; Kum 34:8; Yos 4:19; Kum 4:1-2Katika mwaka wa arobaini, siku ya kwanza ya mwezi wa kumi na moja, Mose aliwatangazia Waisraeli yale yote Bwana aliyomwamuru kuwahusu. 1:4 Hes 21:21-26; Mwa 10:16; 14:17; Hes 21:25; 21:33-35; Kum 3:10; Yos 9:10; 12:4; 1Nya 11:44Hii ilikuwa baada ya kumshinda Sihoni mfalme wa Waamori, ambaye alitawala Heshboni, na pia huko Edrei alikuwa amemshinda Ogu mfalme wa Bashani, ambaye alitawala huko Ashtarothi. 1:5 Hes 21:11Huko mashariki ya Yordani katika nchi ya Moabu, Mose alianza kuielezea sheria hii, akisema:

1:6 Hes 10:13; Kut 3:1; Kum 2:3Bwana Mungu wetu alisema nasi huko Horebu, “Mmekaa vya kutosha katika mlima huu. 1:7 Kum 2:24; 7:1; Yos 10:5; Hes 21:1; Yos 11:16; 12:8; 2Sam 24:7; Mwa 10:18; Kum 11:24; Mwa 2:14Vunjeni kambi, msonge mbele kuelekea nchi ya vilima ya Waamori; nendeni kwa watu wote ambao ni majirani wa Araba, katika milima, upande wa magharibi chini ya vilima, katika Negebu na kandokando ya pwani, mpaka nchi ya Wakanaani hadi Lebanoni, na kufika mto mkubwa Frati. 1:8 Yos 23:13; Hes 34:2; Kut 13:11; Hes 14:23; Ebr 6:13-14Tazama, nimewapa ninyi nchi hii. Ingieni mkaimiliki nchi ambayo Bwana aliapa kuwa angaliwapa baba zenu, Abrahamu, Isaki na Yakobo, pamoja na vizazi vyao baada yao.”

Uteuzi Wa Viongozi

(Kutoka 18:13-27)

1:9 Hes 11:14; Za 30:4; Kut 18:18Wakati ule niliwaambia, “Ninyi mmekuwa mzigo mzito sana kwangu kuwachukua peke yangu. 1:10 Eze 16:7; Kum 7:13; Mwa 15:5; Isa 51:2; 60:22; Eze 33:24; Mwa 22:17; Hes 10:36Bwana Mungu wenu ameongeza hesabu yenu, hivi kwamba leo ninyi ni wengi kama nyota za angani. 1:11 Kut 32:13; 2Sam 24:3; 1Nya 21:3Naye Bwana, Mungu wa baba zenu na awaongeze mara elfu na kuwabariki kama alivyoahidi! 1:12 Kut 5:22; 18:18Lakini mimi nitawezaje kubeba matatizo yenu, na mizigo yenu, na magomvi yenu peke yangu? 1:13 Mwa 47:6; 1Chagueni baadhi ya watu wenye hekima, wenye ufahamu na wanaoheshimika kutoka kila kabila lenu, nami nitawaweka juu yenu.”

Mlinijibu, “Shauri ulilolitoa ni zuri.”

1:15 Kut 18:25; 5:14; Hes 11:16; Yos 1:10; 3:2; Mwa 47:6; Hes 31:14; 1Sam 8:12; 22:7; 1Fal 14:27; Hes 1:4Kwa hiyo niliwachukua wanaume viongozi wa makabila yenu, wenye hekima na wanaoheshimika, nami nikawateua wawe na mamlaka juu yenu kama majemadari wa maelfu, wa mamia, wa hamsini, na wa makumi, na kama maafisa wa makabila. 1:16 1Fal 3:9; Za 72:1; Mit 2:9; Mwa 31:37; Yn 7:24; Kut 12:19; 22:21Nami wakati ule nikawaagiza waamuzi wenu: Sikilizeni magomvi kati ya ndugu zenu na mwamue kwa haki, hata kama shauri ni kati ya ndugu wa Kiisraeli, au kati ya mmoja wa ndugu wa Kiisraeli na mgeni. 1:17 Kut 18:16; Law 19:15; Mdo 10:34; Yak 2:1; Mit 29:25; Kut 18:26Msionyeshe upendeleo katika maamuzi; wasikilizeni wote sawasawa, wadogo kwa wakubwa. Msimwogope mtu yeyote, kwa kuwa hukumu ni ya Mungu. Mniletee mimi shauri lolote lililo gumu sana kwenu, nami nitalisikiliza. 1:18 Mwa 39:11Nami wakati ule niliwaambia kila kitu ambacho mngefanya.

Wapelelezi Wanatumwa

(Hesabu 13:1-33)

1:19 Kum 2:7; 8:15; 32:10; Za 136:16; Yer 2:2-6; Hos 13:5; Hes 13:26Kisha, kama Bwana Mungu wetu alivyotuamuru, tuliondoka kutoka Horebu na kwenda kuelekea nchi ya vilima ya Waamori, kupitia jangwa lile kubwa lote la kutisha, lile mliloliona, nasi tukafika Kadesh-Barnea. Kisha niliwaambia, “Mmefika katika nchi ya vilima ya Waamori, ambayo Bwana Mungu wetu anatupa. 1:21 Kum 29:23; Hes 14:9; Yos 1:6-9, 18; 2Sam 10:12; Za 27:14; Kum 7:18; Yos 8:1; 10:8Tazama, Bwana Mungu wenu amewapa nchi. Pandeni mkaimiliki kama Bwana, Mungu wa baba zenu, alivyowaambia. Msiogope, wala msikate tamaa.”

1:22 Hes 13:1-3; Mwa 42:9Ndipo ninyi nyote mkanijia na kusema, “Tupeleke watu watutangulie kuipeleleza nchi kwa ajili yetu, na kutuletea taarifa kuhusu njia tutakayopita, na miji tutakayoiendea.”

1:23 Hes 13:1-3Wazo hilo lilionekana zuri kwangu; kwa hiyo niliwachagua watu wenu kumi na wawili, mwanaume mmoja kutoka kila kabila. 1:24 Hes 13:21-25; 32:9Waliondoka na kukwea katika nchi ya vilima, wakafika katika Bonde la Eshkoli na kuipeleleza. 1:25 Hes 13:27; 14:7; Yos 1:2Wakachukua baadhi ya matunda ya nchi, wakatuletea na kutuarifu, “Ni nchi nzuri ambayo Bwana Mungu wetu anatupa.”

Uasi Dhidi Ya Bwana

(Hesabu 14:20-45)

1:26 Hes 14:1-4; 14:9; Za 106:24Lakini hamkuwa tayari kukwea, mkaasi dhidi ya amri ya Bwana Mungu wenu. 1:27 Kum 9:28; Za 106:25Mkanungʼunika ndani ya mahema yenu na kusema, “Bwana anatuchukia, kwa hiyo alitutoa Misri ili kututia mikononi mwa Waamori kutuangamiza. 1:28 Hes 13:32-33; Kum 9:1-3Twende wapi? Ndugu zetu wametufanya kufa moyo. Wanasema, ‘Watu wa huko wana nguvu zaidi na ni warefu kuliko sisi tulivyo; miji ni mikubwa, yenye kuta zilizofika juu angani. Zaidi ya hayo, tumewaona Waanaki huko.’ ”

1:29 Kum 3:22; 20:3; Neh 4:14; Kum 7:18; 20:1; 31:6Ndipo nikawaambia, “Msihofu, wala msiwaogope. 1:30 Kut 14:14; Neh 4:20Bwana Mungu wenu anayewatangulia, atawapigania, kama alivyofanya kwa ajili yenu huko Misri, mbele ya macho yenu hasa, 1:31 Kut 19:4; Kum 32:10-12; Za 28:9; Isa 46:3-4; 63:9; Hos 11:3; Mdo 13:18; Yer 31:32na pia huko jangwani. Huko mliona jinsi Bwana Mungu wenu alivyowachukua, kama baba amchukuavyo mwanawe, katika njia yote mliyoiendea mpaka mkafika mahali hapa.”

1:32 Hes 14:11; Kum 9:23; Za 78:22; 106:24; Sef 3:2; Ebr 3:19; Yud 5Pamoja na hili, hamkumtegemea Bwana Mungu wenu, 1:33 Kut 13:21; Hes 9:15-23; Neh 9:12; 9:12; Za 78:14; Hes 10:33ambaye aliwatangulia katika safari yenu, kwa moto usiku na kwa wingu mchana, kuwatafutia mahali penu pa kupiga kambi na kuwaonyesha njia mtakayoiendea.

1:34 Hes 11:1; 32:14; 14:23; 28:30; Eze 20:15; Ebr 3:11Wakati Bwana aliposikia lile mlilosema, alikasirika, akaapa, akasema: 1:35 Hes 14:29; 14:22; Za 95:11“Hakuna mtu wa kizazi hiki kiovu atakayeona nchi nzuri niliyoapa kuwapa baba zenu, 1:36 Hes 13:6; 14:24isipokuwa Kalebu mwana wa Yefune. Yeye ataiona, nami nitampa yeye na wazao wake nchi aliyoikanyaga kwa miguu, kwa sababu alimfuata Bwana kwa moyo wote.”

1:37 Za 106:32; Hes 27:13, 14; Kum 3:26; 4:21; 34:4Kwa sababu yenu Bwana pia alinikasirikia mimi, akasema, “Hutaingia hiyo nchi pia. 1:38 Hes 11:28; Kum 31:7; 3:28; Yos 11:23; Za 78:55; 136:21Lakini msaidizi wako, Yoshua mwana wa Nuni, ataingia. Mtie moyo, kwa sababu atawaongoza Waisraeli kuirithi hiyo nchi. 1:39 Hes 14:3; Isa 7:15-16Wale watoto ambao mliwasema wangelichukuliwa mateka, yaani watoto wenu ambao bado hawajui jema na baya, wataingia katika nchi. Nitawapa hiyo nchi, nao wataimiliki. 1:40 Kut 14:27; Amu 11:16Bali ninyi geukeni, mwondoke kuelekea jangwani kwa kufuata njia ya Bahari ya Shamu.”

Ndipo mkanijibu, “Tumemtenda Bwana dhambi. Tutakwenda kupigana, kama Bwana Mungu wetu alivyotuamuru.” Hivyo kila mmoja wenu akachukua silaha zake, huku mkifikiri kuwa ni rahisi kukwea katika nchi ya vilima.

1:42 Hes 14:41-43Lakini Bwana aliniambia, “Waambie, ‘Msipande kupigana, kwa sababu sitakuwa pamoja nanyi. Mtashindwa na adui zenu.’ ”

1:43 Hes 14:44Hivyo niliwaambia, lakini hamkutaka kusikia. Mliasi dhidi ya amri ya Bwana, na katika kiburi chenu mlienda katika nchi ya vilima. 1:44 Za 118:12; Hes 28:18; 14:45; Kum 28:25; 32:30; Isa 7:18Waamori ambao waliishi katika vilima hivyo waliinuka dhidi yenu, wakawafukuza kama kundi la nyuki wakiwapiga njia yote ya Seiri mpaka Horma. 1:45 Hes 14:1; Ay 27:9; 35:13; Za 18:41; 66:18; Mit 1:28; Isa 1:15; Yer 14:12; Mao 3:8; Mik 3:4; Yn 9:31; Za 28:1; 39:12; Mit 28:9Mlirudi na kulia mbele za Bwana, lakini Mungu hakusikiliza kilio chenu, wala hakuwajali. 1:46 Hes 20:1; 13:25; Amu 11:27Hivyo mlikaa Kadeshi kwa siku nyingi, kwa muda ule wote mliokaa huko.

Read More of Kumbukumbu 1

Kumbukumbu 2:1-23

Kutangatanga Jangwani

2:1 Kut 14:27; Hes 21:4; 24:18Kisha tukageuka nyuma na kusafiri kuelekea jangwani kwa njia inayoelekea Bahari ya Shamu, kama Bwana alivyonielekeza. Kwa muda mrefu tulitembea kuzunguka vilima katika nchi ya Seiri.

Kisha Bwana akaniambia, 2:3 Kum 1:6“Umetembea kuzunguka hii nchi ya vilima kwa muda wa kutosha; sasa geukia kaskazini. 2:4 Hes 20:14-21; Mwa 36:8; Kut 15:16Wape watu maagizo haya: ‘Mko karibu kupita katikati ya nchi ya ndugu zako ambao ni wazao wa Esau, ambao wanaishi Seiri. Watawaogopa, lakini mwe waangalifu. 2:5 Yos 24:4; Mwa 36:8; Kum 32:8; 2Nya 20:10-12; Mdo 17:26Msiwachokoze kwa vita kwa maana sitawapa ninyi sehemu yoyote ya nchi yao, hata sehemu ya kutosha kuweka wayo wenu juu yake. Nimempa Esau nchi ya vilima ya Seiri kama yake mwenyewe. Mtawalipa fedha kwa chakula mtakachokula na maji mtakayokunywa.’ ”

2:7 Kum 8:2-4; Kut 13:21; Kum 1:19; Hes 14:33; 32:13; Yos 5:6; Neh 9:21; Amo 2:10Bwana Mungu wenu amewabariki kwa kazi yote ya mikono yenu. Amewalinda katika safari yenu katikati ya jangwa hili kubwa. Kwa miaka hii arobaini Bwana Mungu wenu amekuwa pamoja nanyi, na hamkupungukiwa na kitu chochote.

2:8 Hes 20:8; 33:35; 1Fal 9:26; Hes 21:4Basi tulipita kwa ndugu zetu wazao wa Esau ambao wanaishi Seiri. Tuligeuka kutoka njia ya Araba ambayo inatokea Elathi na Esion-Geberi, tukasafiri kufuata njia ya jangwa la Moabu.

2:9 Hes 21:15; Mwa 19:38; Za 83:8Kisha Bwana akaniambia, “Usiwasumbue Wamoabu kwa vita, kwa kuwa sitawapa sehemu yoyote ya nchi yao. Nimetoa nchi ya Ari kwa wazao wa Loti kama milki yao.”

2:10 Mwa 14:5; Hes 13:22; 33; Kum 9:2(Waemi walikuwa wakiishi huko hapo zamani, watu wenye nguvu na wengi, warefu kama Waanaki. 2:11 Mwa 14:5Kama walivyokuwa Waanaki, hao pia walikuwa kama Warefai, lakini Wamoabu waliwaita Waemi. 2:12 Mwa 14:6; Hes 21:25-35Wahori waliishi Seiri, lakini wazao wa Esau waliwafukuza. Waliwaangamiza Wahori na kukaa mahali pao, kama Waisraeli walivyofanya katika nchi ambayo Bwana aliwapa kama milki yao.)

2:13 Hes 21:12Bwana akasema, “Sasa ondokeni mvuke Bonde la Zeredi.” Hivyo tukavuka bonde.

2:14 Kum 1:2; Hes 13:26; 14:29-35; Kum 1:34-35; Yos 5:6Miaka thelathini na minane ilipita tangu wakati tulipoondoka Kadesh-Barnea mpaka tulipovuka Bonde la Zeredi. Kwa wakati huo kile kizazi chote cha wanaume kuanzia wale wawezao kwenda vitani kilikuwa kimekufa, kama Bwana alivyokuwa amewaapia. 2:15 Za 106:26; Yud 5; 1Sam 5:6-11; 7:13; Za 95:10, 11; Ebr 4:1-5Mkono wa Bwana uliwakabili hadi alipowaangamiza wote huko kambini.

Ikawa baada ya mtu wa mwisho kuanzia wale wawezao kwenda vitani kufa, Bwana akaniambia, 2:18 Hes 21:15“Leo utapita katika nchi ya Moabu huko Ari. 2:19 Mwa 19:38; 2Nya 20:10Utakapokuja kwa Waamoni, msiwasumbue wala kuwachokoza kwa vita, kwa kuwa sitawapa ardhi yoyote iliyo ya Waamoni kuwa milki yenu. Nimeitoa kama milki ya wazao wa Loti.”

2:20 Mwa 14:5(Hiyo pia ilidhaniwa kuwa nchi ya Warefai waliokuwa wakiishi huko, lakini Waamoni waliwaita Wazamzumi. Walikuwa watu wenye nguvu na wengi, warefu kama Waanaki. Bwana akawaangamiza kutoka mbele ya Waamoni, ambao waliwafukuza na kukaa mahali pao. 2:22 Mwa 14:6; 36:8; Ay 12:23Bwana alikuwa amefanya vivyo hivyo kwa wazao wa Esau, ambao waliishi Seiri, wakati alipowaangamiza Wahori watoke mbele yao. Waliwafukuza na wao wakaishi mahali pao mpaka leo. 2:23 Yos 13:3; 18:23; 2Fal 17:31; Mwa 10:14; 19; Yer 47:4; Amo 9:7; Sef 2:4Nao Waavi ambao waliishi katika vijiji mpaka Gaza, Wakaftori waliokuja kutoka Kaftori waliwaangamiza na kukaa mahali pao.)

Read More of Kumbukumbu 2