Matendo 4:23-37, Matendo 5:1-11 NEN

Matendo 4:23-37

Maombi Ya Waumini

4:23 Mdo 12; 12Punde Petro na Yohana walipoachiliwa, walirudi kwa waumini wenzao wakawaeleza waliyoambiwa na viongozi wa makuhani na wazee. 4:24 2Fal 19:15; Kut 20:11; Za 146:6; Isa 37:16; Lk 2:29; Ufu 6:10Watu waliposikia hayo, wakainua sauti zao, wakamwomba Mungu kwa pamoja, wakisema, “Bwana Mwenyezi, uliyeziumba mbingu na nchi na bahari, na vitu vyote vilivyomo. 4:25 Za 2:1, 2Wewe ulisema kwa Roho Mtakatifu kupitia kwa kinywa cha baba yetu Daudi, mtumishi wako, ukasema:

“ ‘Mbona mataifa wanaghadhibika,

na kabila za watu zinawaza ubatili?

4:26 Dan 9:25; Lk 4:18Wafalme wa dunia wamejipanga,

na watawala wanakusanyika pamoja

dhidi ya Bwana

na dhidi ya Mpakwa Mafuta wake.’

4:27 Mt 14:1; 27:2; Lk 23:12; Mdo 3:13-14Ni kweli Herode na Pontio Pilato pamoja na watu wa Mataifa na Waisraeli, walikusanyika katika mji huu dhidi ya mwanao mtakatifu Yesu uliyemtia mafuta. 4:28 Mdo 2:23Wao wakafanya yale ambayo uweza wako na mapenzi yako yalikuwa yamekusudia yatokee tangu zamani. 4:29 Za 138:3; Efe 6:19Sasa, Bwana angalia vitisho vyao na utuwezeshe sisi watumishi wako kulinena neno lako kwa ujasiri mkuu. 4:30 Yn 4:48Nyoosha mkono wako ili kuponya wagonjwa na kutenda ishara na miujiza kwa jina la Mwanao mtakatifu Yesu.”

4:31 Mdo 2:2, 4; 16:26; Lk 1:15; Ebr 4:12Walipokwisha kuomba, mahali walipokuwa wamekutanika pakatikiswa, wote wakajazwa na Roho Mtakatifu, wakanena neno la Mungu kwa ujasiri.

Walioamini Washirikiana Mali Zao

4:32 Mdo 2:44Wale walioamini wote walikuwa na moyo mmoja na nia moja. Wala hakuna hata mmoja aliyesema chochote alichokuwa nacho ni mali yake mwenyewe, lakini walishirikiana kila kitu walichokuwa nacho. 4:33 Lk 24:48; Mdo 1:22Mitume wakatoa ushuhuda wa kufufuka kwa Bwana Yesu kwa nguvu nyingi na neema ya Mungu ilikuwa juu yao wote. 4:34 Mt 19; 21; Mdo 2:45Wala hapakuwepo mtu yeyote miongoni mwao aliyekuwa mhitaji, kwa sababu mara kwa mara wale waliokuwa na mashamba na nyumba waliviuza, wakaleta thamani ya vitu vilivyouzwa, 4:35 Mdo 5:2; 2:45; 6:1wakaiweka miguuni pa mitume, kila mtu akagawiwa kadiri ya mahitaji yake.

4:36 1Kor 9:6; Gal 2:1, 9-13Yosefu, Mlawi kutoka Kipro, ambaye mitume walimwita Barnaba (maana yake Mwana wa Faraja), 4:37 Mdo 5:2aliuza shamba alilokuwa nalo, akaleta hizo fedha alizopata na kuziweka miguuni pa mitume.

Read More of Matendo 4

Matendo 5:1-11

Anania Na Safira

Lakini mtu mmoja jina lake Anania pamoja na mkewe Safira waliuza kiwanja. 5:2 Mdo 4:35-37Huku mkewe akijua kikamilifu, Anania alificha sehemu ya fedha alizopata, akaleta kiasi kilichobaki na kukiweka miguuni pa mitume.

5:3 Mt 4:10; Yn 13:2, 27Petro akamuuliza, “Anania, mbona Shetani ameujaza moyo wako ili kumwambia uongo Roho Mtakatifu, ukaficha sehemu ya fedha ulizopata kutokana na kiwanja? 5:4 Kum 23:22; Law 6:2Je, kabla hujauza hicho kiwanja si kilikuwa mali yako? Hata baada ya kukiuza, fedha ulizopata si zilikuwa kwenye uwezo wako? Kwa nini basi umewaza hila hii moyoni mwako kufanya jambo kama hili? Wewe hukumwambia uongo mwanadamu bali Mungu.”

5:5 Za 5:6; Mdo 5:10Anania aliposikia maneno haya akaanguka chini na kufa. Hofu kuu ikawapata wote waliosikia jambo lililokuwa limetukia. 5:6 Yn 19:40Vijana wakaja, wakaufunga mwili wake sanda, wakamchukua nje kumzika.

Saa tatu baadaye mkewe Anania akaingia, naye hana habari ya mambo yaliyotukia. 5:8 Mdo 5:2Petro akamuuliza, “Niambie, je, mliuza kiwanja kwa thamani hii?” Akajibu, “Ndiyo, tuliuza kwa thamani hiyo.”

5:9 Mdo 5:3; Mt 4:7Ndipo Petro akamwambia, “Imekuwaje mkakubaliana kumjaribu Roho wa Bwana? Tazama! Nyayo za vijana waliomzika mumeo ziko mlangoni, wewe nawe watakuchukua nje.”

5:10 Mdo 5:5, 6Saa ile ile akaanguka chini miguuni mwake na kufa. Nao wale vijana wakaingia, wakamkuta amekufa, wakamchukua wakamzika kando ya mumewe. 5:11 Mdo 19:7Hofu kuu ikalipata kanisa lote pamoja na watu wote waliosikia juu ya matukio haya.

Read More of Matendo 5