2 Samweli 9:1-13, 2 Samweli 10:1-19 NEN

2 Samweli 9:1-13

Daudi Na Mefiboshethi

9:1 1Sam 20:14-17, 42; 23:18; 18:3; Mit 27:10Daudi akauliza, “Je, hakuna mtu hata mmoja wa nyumba ya Sauli aliyebaki ambaye naweza kumtendea wema kwa ajili ya Yonathani?”

9:2 2Sam 16:1-4; 19:17, 26-29Basi palikuwepo mtumishi wa nyumba ya Sauli aliyeitwa Siba. Wakamwita aje mbele ya Daudi, naye mfalme akamwambia, “Wewe ndiwe Siba?”

Akamjibu, “Naam, mimi ndiye mtumishi wako.”

9:3 1Nya 8:34; Law 21:18; 1Sam 20:14; 2Sam 4:4; Kum 19:15; Mt 5:44; Lk 6:36; Tit 3:3-4Mfalme akauliza, “Je, hakuna yeyote ambaye amebaki wa nyumba ya Sauli ninayeweza kumwonyesha wema wa Mungu?”

Siba akamjibu mfalme, “Bado yupo mwana wa Yonathani, yeye ni kiwete miguu yote.”

9:4 2Sam 17:27-29Mfalme akauliza, “Yuko wapi?”

Siba akajibu, “Yuko nyumbani kwa Makiri mwana wa Amieli huko Lo-Debari.”

Basi Mfalme Daudi akamtaka aletwe kutoka Lo-Debari, kutoka nyumbani kwa Makiri mwana wa Amieli.

9:6 Mwa 37:7; 2Sam 16:4Mefiboshethi mwana wa Yonathani, mwana wa Sauli, alipofika kwa Daudi, akainama kumpa mfalme heshima.

Daudi akamwita, “Mefiboshethi!”

Mefiboshethi akajibu, “Ndimi mtumishi wako.”

9:7 1Sam 20:14-15; 2Sam 19:28; 21:7; 1Fal 2:7; 2Fal 25:29; Yer 52:33; Mwa 43:18; 50:21; 1Sam 12:19-24; Yer 52:33Daudi akamwambia, “Usiogope, kwa maana hakika nitakutendea wema kwa ajili ya baba yako Yonathani. Nitakurudishia ardhi yote iliyokuwa mali ya Sauli baba yako, nawe daima utakula chakula mezani pangu.”

9:8 2Sam 4:4; 3:8; 1Sam 24:14; 2Sam 16:9Mefiboshethi akasujudu akasema, “Mimi mtumishi wako ni nini hata uangalie mbwa mfu kama mimi?”

9:9 Isa 32:8Ndipo mfalme akamwita Siba mtumishi wa Sauli na kumwambia, “Nimempa mwana wa bwana wako kila kitu kilichokuwa mali ya Sauli na jamaa yake. 9:10 2Sam 16:3; 19:28Wewe, wanao na watumishi wako mtamlimia mashamba Mefiboshethi na kumletea mavuno, ili kwamba mwana wa bwana wako apate mahitaji yake. Naye Mefiboshethi mwana wa bwana wako atakula chakula mezani pangu daima.” (Siba alikuwa na wana kumi na watano, na watumishi ishirini.)

9:11 Ay 36:7; Za 113:8; 1Sam 16:1-4; Mit 12:17Ndipo Siba akamwambia mfalme, “Mtumishi wako atafanya chochote bwana wangu mfalme atakachoagiza mtumishi wake kufanya.” Basi Mefiboshethi akala chakula mezani pa Daudi kama mmoja wa wana wa mfalme.

9:12 2Sam 4:4; 1Nya 8:34Mefiboshethi alikuwa na mwanawe mdogo aliyeitwa Mika, nao watu wote wa nyumba ya Siba walikuwa watumishi wa Mefiboshethi. 9:13 2Sam 19:33-36; 2Fal 25:29; Yer 52:33-34Naye Mefiboshethi akaishi huko Yerusalemu, kwa sababu daima alikula mezani pa mfalme, naye alikuwa kiwete miguu yote.

Read More of 2 Samweli 9

2 Samweli 10:1-19

Daudi Awashinda Waamoni

(1 Nyakati 19:1-19)

10:1 1Sam 11:1; 2Sam 17:27; 1Nya 19:1Baada ya muda, mfalme wa Waamoni akafa, naye Hanuni mwanawe akaingia mahali pake. 10:2 1Sam 11:1Daudi akawaza, “Nitamtendea wema Hanuni mwana wa Nahashi, kama vile baba yake alivyonitendea mimi wema.” Hivyo Daudi akatuma wajumbe kuonyesha wema wake kwa Hanuni kuhusu baba yake.

Watu wa Daudi walipofika katika nchi ya Waamoni, 10:3 Hes 21:32wakuu wa Waamoni wakamwambia Hanuni bwana wao, “unadhani Daudi anamheshimu baba yako kwa kukutumia watu ili kuonyesha masikitiko? Je, Daudi hakuwatuma watu hawa kuchunguza na kuupeleleza mji ili kuupindua?” 10:4 Law 19:27; Isa 7:20; 15:2; 50:6; 52:14; Yer 48:37; Eze 5:1; Isa 20:4; 3:17; Yer 13:22; Eze 16:37; Mik 1:11; Nah 3:5Basi Hanuni akawakamata watu wa Daudi, akawanyoa kila mmoja ndevu zake nusu, akakata mavazi yao nyuma katikati kwenye matako, akawaacha waende zao.

Daudi alipoambiwa jambo hili, akatuma wajumbe ili kwenda kuwalaki, kwa maana walikuwa wamevunjiwa heshima sana. Mfalme akasema, “Kaeni huko Yeriko mpaka ndevu zenu ziote ndipo mje.”

10:6 Mwa 34:30; 2Sam 8; 5; Hes 13:21; 1Sam 14:47; Kum 3:14; Amu 11:3-5; 18:28; Kut 5:21; 1Sam 13:4Waamoni walipotambua kuwa wamekuwa machukizo kwa Daudi, wakaajiri askari wa miguu 20,000 Waaramu kutoka Beth-Rehobu na Soba, pia mfalme wa Maaka pamoja na watu 1,000, na vilevile watu 12,000 kutoka Tobu.

10:7 2Sam 2:18; 23:8Daudi aliposikia jambo hili, akamtuma Yoabu na jeshi lote la wapiganaji. Waamoni wakatoka wakajipanga wakiwa tayari kwa vita langoni la mji wao, wakati Waaramu wa Soba, wa Rehobu, watu wa Tobu na Maaka walikuwa peke yao kwenye eneo la wazi.

Yoabu akaona kuwa mbele yake na nyuma yake kumepangwa vita; kwa hiyo akachagua baadhi ya vikosi vilivyo bora sana katika Israeli akavipanga dhidi ya Waaramu. 10:10 1Sam 26:6Akawaweka waliobaki chini ya uongozi wa Abishai nduguye na kuwapanga dhidi ya Waamoni. Yoabu akasema, “Kama Waaramu watanizidi nguvu, basi itawabidi mje kunisaidia. Lakini kama Waamoni watawazidi nguvu, basi nitakuja kuwasaidia. 10:12 Kum 1:21; 31:6; Efe 6:10; Amu 10:15; Neh 4:14; 1Kor 16:3; 1Sam 3:18; 2Nya 19:11; 1Sam 4:9; 2Sam 15:26; 22:31-32; Za 20:7; 37:4-5; Mit 29:25Uwe hodari na tupigane kwa ujasiri kwa ajili ya watu wetu na miji ya Mungu wetu. Bwana atafanya lile lililo jema machoni pake.”

Basi Yoabu na vikosi vyake wakasonga mbele kupigana na Waaramu, nao Waaramu wakakimbia mbele yake. 10:14 2Sam 8:12Waamoni walipoona Waaramu wanakimbia, nao wakakimbia mbele ya Abishai na kuingia ndani ya mji. Basi Yoabu akarudi kutoka kupigana na Waamoni na kufika Yerusalemu.

Baada ya Waaramu kuona wameshindwa na Israeli, wakajikusanya tena. Hadadezeri akaagiza Waaramu walioletwa kutoka ngʼambo ya Mto Frati, wakaenda Helamu pamoja na Shobaki jemadari wa jeshi la Hadadezeri akiwaongoza.

Daudi alipoambiwa haya, akawakusanya Israeli wote, wakavuka Mto Yordani, wakaenda Helamu. Waaramu wakapanga vikosi vyao vya askari kukabiliana na kupigana dhidi ya Daudi. Lakini Waaramu wakakimbia mbele ya Israeli, naye Daudi akawaua waendesha magari mia saba na askari wao wa miguu 40,000. Vilevile alimpiga Shobaki jemadari wa jeshi lao, naye akafa huko. 10:19 2Sam 8:6; 1Fal 11:25; 22:31; 2Fal 5:1; Mwa 14:4Wafalme wote waliokuwa wanamtumikia Hadadezeri walipoona kuwa wameshindwa na Israeli, wakafanya amani na Waisraeli na wakawa chini yao.

Hivyo Waaramu wakaogopa kuwasaidia Waamoni tena.

Read More of 2 Samweli 10