2 Samweli 5:6-25, 2 Samweli 6:1-23 NEN

2 Samweli 5:6-25

Daudi Ateka Yerusalemu

5:6 Amu 1:8; Yos 15:8; Amu 1:21; 19:11Mfalme na watu wake wakaenda Yerusalemu kuwashambulia Wayebusi walioishi humo. Wayebusi wakamwambia Daudi, “Wewe hutaingia humu, kwani hata vipofu na viwete wanaweza kukufukuza.” Walidhani, “Daudi hawezi kuingia humu.” 5:7 Za 76:2; Yer 21:13; 2Sam 6:12; 1Fal 2:10; 8:1; Isa 29:1; Yer 25:29Hata hivyo, Daudi akaiteka ngome ya Sayuni, Mji wa Daudi.

5:8 Yos 15:8; 17:15; 18:16; 1Nya 11:6Siku ile, Daudi akasema, “Yeyote ambaye atawashinda Wayebusi, atatumia huo mfereji kuwafikia hao ‘viwete na vipofu’ ambao ni adui za Daudi.” Ndiyo sababu wanasema, “ ‘Vipofu na viwete’ hawataingia kwenye jumba la ufalme.”

5:9 2Fal 7:6; 1Fal 9:15, 24; 2Nya 32:5Ndipo Daudi akafanya makao ndani ya ngome na kuiita Mji wa Daudi. Akajenga eneo linalozunguka kuanzia Milo5:9 Milo maana yake Boma la Ngome. kuelekea ndani. 5:10 2Sam 3:1; Za 24:10; 2Fal 7:9Daudi akazidi kuwa na nguvu zaidi na zaidi, kwa sababu Bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote alikuwa pamoja naye.

5:11 1Fal 15:1, 18; 2Nya 2:3; 1Fal 5:2; 1Nya 14:1Basi Hiramu mfalme wa Tiro akawatuma wajumbe kwa Daudi, wakiwa na magogo ya mierezi, maseremala na waashi, nao wakajenga jumba la kifalme kwa ajili ya Daudi. 5:12 Hes 24:7; 1Fal 10:9; 2Nya 2:11; Es 4:14; Isa 45:4Naye Daudi akafahamu kuwa Bwana amemwimarisha kuwa mfalme juu ya Israeli na ameinua ufalme wake kwa ajili ya Israeli, watu wake.

5:13 Kum 17:17; 1Nya 3:9; Mwa 25:5-6Baada ya Daudi kuondoka Hebroni, akajitwalia masuria zaidi na wake huko Yerusalemu, nao wana na binti wengi walizaliwa kwake. 5:14 1Nya 3:5; Lk 3:31Haya ndiyo majina ya watoto waliozaliwa kwake huko: Shamua, Shobabu, Nathani, Solomoni, Ibihari, Elishua, Nefegi, Yafia, Elishama, Eliada na Elifeleti.

Daudi Awashinda Wafilisti

(1 Nyakati 14:8-17)

5:17 2Sam 23:14; 1Nya 11:16Wafilisti waliposikia kuwa Daudi ametiwa mafuta kuwa mfalme wa Israeli, wakapanda na jeshi lao lote kwenda kumsaka, lakini Daudi akapata habari hizo, naye akateremka kwenye ngome. 5:18 Yos 15:8; 17:15; 18:16; Isa 17:5Basi Wafilisti walikuwa wamekuja na kusambaa kwenye Bonde la Warefai, 5:19 Amu 18:5; 1Sam 23:2; Hes 27:21; Yos 9:14kwa hiyo Daudi akamuuliza Bwana, “Je, niende kuwashambulia Wafilisti? Je, utawatia mikononi mwangu?”

Bwana akamjibu, “Nenda, kwa maana hakika nitawatia Wafilisti mikononi mwako.”

5:20 Mwa 38:29; Isa 28:21Ndipo Daudi akaenda mpaka Baal-Perasimu, na huko akawashinda Wafilisti. Akasema, “Kama mafuriko yafurikavyo, Bwana amewafurikia adui zangu mbele yangu.” Kwa hiyo mahali hapo pakaitwa Baal-Perasimu.5:20 Maana yake Bwana Afurikae. 5:21 Kum 7:5; Isa 46:2Wafilisti wakaiacha miungu yao huko, naye Daudi na watu wake wakaichukua.

Wafilisti walikwea kwa mara nyingine na kusambaa katika Bonde la Warefai. Kwa hiyo Daudi akamuuliza Bwana, naye akamjibu, “Usipande moja kwa moja, bali wazungukie kwa nyuma na uwashambulie mbele ya miti ya miforosadi. 5:24 Kut 14:24; Amu 4:14; 2Fal 7:6Mara utakaposikia sauti ya kutembea kutoka kwenye vilele vya miti ya miforosadi, nenda haraka, kwa sababu hiyo itamaanisha kuwa Bwana ametangulia mbele yako kupiga jeshi la Wafilisti.” 5:25 2Sam 8:12; 21:15; Isa 28:21; Yos 10:33; 1Nya 14:16Basi Daudi akafanya kama Bwana alivyomwagiza, naye akawaangusha Wafilisti njia yote kuanzia Geba5:25 Kwa Kiebrania mji huu uliitwa Gibeoni (ona 1Nya 14:16). hadi Gezeri.

Read More of 2 Samweli 5

2 Samweli 6:1-23

Sanduku La Mungu Laletwa Yerusalemu

(1 Nyakati 13:1-14; 15:25–16:6, 43)

6:1 Za 80:1; 1Nya 13:5Tena Daudi akakusanya watu 30,000 wa Israeli waliochaguliwa. 6:2 Yos 15:9; 1Sam 4:4; 7:1; Law 24:16; Kum 28:10; Isa 63:10; Za 99:1; 132:14; Mwa 3:24; Kut 25:22Yeye na watu wake wote wakatoka Baala ya Yuda6:2 Baala ya Yuda ni jina la Kiebrania; yaani Kiriath-Yearimu. kulipandisha Sanduku la Mungu kutoka huko, linaloitwa kwa Jina, naam, jina la Bwana Mwenye Nguvu Zote, ambaye anaketi katika kiti cha enzi kati ya makerubi walioko juu ya hilo Sanduku. 6:3 Hes 7:4-6; 1Sam 6:7; 2Sam 7:1Wakaweka hilo Sanduku la Mungu juu ya gari jipya la kukokotwa na kulileta kutoka nyumba ya Abinadabu, iliyokuwa juu ya kilima. Uza na Ahio, wana wa Abinadabu, walikuwa wakiongoza hilo gari jipya la kukokotwa likiwa na Sanduku la Mungu juu yake, naye Ahio alikuwa anatembea akiwa mbele yake. 6:5 Kut 15:20; Ezr 3:10; Neh 12:27; Za 105:5Daudi na nyumba yote ya Israeli walikuwa wanacheza mbele za Bwana kwa nguvu zao zote, kwa nyimbo, vinubi, zeze, matari, kayamba na matoazi.

6:6 Hes 4:15, 19-20; 1Nya 13:9Walipofika kwenye uwanja wa kupuria nafaka wa Nakoni, Uza akanyoosha mkono na kulishika Sanduku la Mungu kwa sababu maksai walijikwaa. 6:7 1Nya 15:13-15; Kut 19:23; 1Sam 5:6; 6:19; 25:32Hasira ya Bwana ikawaka dhidi ya Uza kwa sababu ya kitendo chake cha kukosa heshima, kwa hiyo Mungu akampiga akafia papo hapo kando ya Sanduku la Mungu.

6:8 Za 7:11; Mwa 38:29Ndipo Daudi akakasirika kwa sababu ghadhabu ya Bwana ilifurika dhidi ya Uza, hivyo hadi leo mahali hapo panaitwa Peres-Uza.

6:9 1Sam 6:20; Za 119:120; Hes 17:12-13; 1Sam 5:10-11; Lk 5:8Daudi akamwogopa Bwana siku ile, akasema, “Ni jinsi gani Sanduku la Bwana litakavyoweza kunijia?” 6:10 1Nya 15:18; 26:4-5; 13:13Hakuwa radhi kulichukua Sanduku la Bwana kwake katika Mji wa Daudi. Badala yake akalipeleka kwenye nyumba ya Obed-Edomu, Mgiti. 6:11 Mwa 30:27; 39:5; Mit 3:9-10; Isa 61:9Sanduku la Bwana likabaki katika nyumba ya Obed-Edomu, Mgiti, kwa miezi mitatu, naye Bwana akambariki pamoja na nyumba yake yote.

6:12 1Fal 8:1; 1Nya 15:25Kisha Mfalme Daudi akaambiwa, “Bwana ameibariki nyumba ya Obed-Edomu pamoja na kila alicho nacho, kwa sababu ya Sanduku la Mungu.” Basi Daudi akateremka na kulipandisha Sanduku la Mungu kutoka nyumba ya Obed-Edomu hadi Mji wa Daudi kwa shangwe. 6:13 1Fal 8:5, 62; Ezr 6:17; Hes 4:15; Yos 3:3; 1Nya 15:2, 15; 2Nya 5:6Wale waliokuwa wamebeba Sanduku la Bwana walipokuwa wametembea hatua sita, Daudi alitoa dhabihu fahali na ndama aliyenoneshwa. 6:14 Kut 19:6; 1Sam 2:18; Kut 15:20; Amu 11:34; 21:21; Za 30:11; 1Nya 15:27Daudi, akiwa amevaa kisibau cha kitani, alicheza mbele za Bwana kwa nguvu zake zote, 6:15 Yos 6:5; Za 47:5; 98:6wakati yeye na nyumba yote ya Israeli walipopandisha Sanduku la Bwana kwa shangwe na sauti za tarumbeta.

6:16 2Sam 5:7; 1Sam 18:27Ikawa Sanduku la Bwana lilipokuwa linaingia katika Mji wa Daudi, Mikali binti Sauli akachungulia dirishani. Naye alipomwona Mfalme Daudi akirukaruka na kucheza mbele za Bwana, akamdharau moyoni mwake.

6:17 1Fal 8:6; 1Nya 15:1; 2Nya 1:4; Law 1:1-17; 1Fal 8:62-64; Za 132:8Wakaleta Sanduku la Bwana na kuliweka mahali pake ndani ya hema ambalo Daudi alikuwa amelisimamisha kwa ajili yake, naye Daudi akatoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani mbele za Bwana. 6:18 1Fal 8:22; Kut 39:43Baada ya kumaliza kutoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani, Daudi akawabariki watu katika jina la Bwana Mwenye Nguvu Zote. 6:19 Hos 3:1; Kum 26:13; Neh 8:10Kisha akatoa mkate, andazi la tende na andazi la zabibu kavu kwa kila mtu katika mkutano wote wa Waisraeli, wanaume kwa wanawake. Nao watu wote wakaenda nyumbani kwao.

6:20 1Sam 19:24; Mhu 7:16; Isa 59:15; Amu 9:4Daudi aliporudi ili kuwabariki watu wa nyumbani mwake, Mikali binti Sauli akatoka nje kumlaki, akamwambia, “Tazama jinsi mfalme wa Israeli alivyojibainisha mwenyewe leo kwa kuvua mavazi yake machoni pa vijakazi wa watumishi wake, kama vile ambavyo mtu asiye na adabu angelifanya!”

6:21 1Sam 13:14; 15:28; 2Sam 5:2; 7:8; 1Nya 5:2; 17:7; Mik 5:2Daudi akamwambia Mikali, “Nilifanya hivyo mbele za Bwana ambaye alinichagua mimi badala ya baba yako au mwingine yeyote kutoka nyumba yake wakati aliponiweka niwe mtawala juu ya Israeli, watu wa Bwana. Kwa hiyo nitacheza mbele za Bwana. Nitakuwa asiye na heshima zaidi kuliko sasa, nami nitajishusha machoni pangu mwenyewe. Lakini kwa hawa vijakazi uliosema habari zao nitaheshimiwa.”

6:23 1Sam 15:35; Isa 22:14Naye Mikali binti Sauli hakuwa na watoto mpaka siku ya kufa kwake.

Read More of 2 Samweli 6