2 Samweli 3:22-39, 2 Samweli 4:1-12, 2 Samweli 5:1-5 NEN

2 Samweli 3:22-39

Yoabu Amuua Abneri

Wakati huo huo, watu wa Daudi na Yoabu walirudi kutoka kwenye kushambulia, nao wakarudi na nyara nyingi mno. Lakini Abneri hakuwa tena pamoja na Daudi huko Hebroni, kwa sababu Daudi alikuwa amemruhusu aende zake, naye akaenda kwa amani. Yoabu na askari wote aliokuwa nao walipowasili, aliambiwa kwamba Abneri mwana wa Neri alikuwa amekuja kwa mfalme na kwamba mfalme alikuwa amemruhusu aende zake, na kwamba alikwisha ondoka kwa amani.

Basi Yoabu alikwenda kwa mfalme na kumwambia, “Ni nini hiki ulichofanya? Tazama, Abneri alikuja kwako. Kwa nini ukamwacha aende? Sasa amekwenda! 3:25 Hes 27:17; Kum 28:6; 1Sam 29:6; Za 121:8; Isa 37:28Wajua Abneri mwana wa Neri alikuja kukudanganya na kuchunguza nyendo zako na kupata kila kitu unachokifanya.”

Ndipo Yoabu akamwacha Daudi na kutuma wajumbe wamfuate Abneri, nao wakamrudisha kutoka kisima cha Sira. Lakini Daudi hakufahamu jambo hili. 3:27 2Sam 2:8; 4:1; 1Fal 2:5, 32; Kut 21:14; Amu 3:21; 2Sam 2:22-23; 20:9-10Basi Abneri aliporudi Hebroni, Yoabu akamchukua kando ndani ya lango, kama vile kuzungumza naye faraghani. Ili kulipiza kisasi damu ya nduguye Asaheli, Yoabu akamchoma mkuki tumboni palepale, naye akafa.

3:28 Kum 21:9Baadaye, Daudi aliposikia kuhusu jambo hili, akasema, “Mimi na ufalme wangu kamwe hatuna hatia mbele za Bwana kuhusu damu ya Abneri mwana wa Neri. 3:29 Law 20:9; 1Fal 2:31-33; Law 15:2; Amu 9:54-57; Za 7:11-16; Mit 2:22; 5:22Damu yake na iwe juu ya kichwa cha Yoabu na juu ya nyumba yote ya baba yake! Kamwe asikosekane yeyote katika nyumba ya Yoabu mwenye kidonda chenye usaha, au ukoma au mwenye kuegemea fimbo au aangukaye kwa upanga au kupungukiwa na chakula.”

3:30 2Sam 2:23(Yoabu na Abishai ndugu yake walimuua Abneri kwa sababu alikuwa amemuua Asaheli ndugu yao katika vita huko Gibeoni.)

3:31 Za 30:11; 35:13; 69:11; Isa 20:2; Mwa 37:34; Yos 6:7; Amu 11:35; 2Fal 19:1; Ay 16:15; Yoe 1:8Kisha Daudi akamwambia Yoabu na watu wote aliokuwa pamoja nao, “Rarueni nguo zenu na mvae nguo za gunia na mtembee mkiomboleza mbele ya Abneri.” Mfalme Daudi mwenyewe akatembea nyuma ya jeneza. 3:32 Hes 14:1; Mit 24:17; 1Sam 31:4; 2Sam 18:33Wakamzika Abneri huko Hebroni, naye mfalme akalia kwa sauti kwenye kaburi la Abneri. Pia watu wote wakalia.

3:33 Mwa 50:10; 2Sam 1:19; 13:13; Mhu 2:15-16Mfalme akaimba ombolezo hili kwa ajili ya Abneri:

“Je, ilipasa Abneri afe kama afavyo mpumbavu?

3:34 Ay 36:8; Za 2:3; 149:8; Isa 45:14; Nah 3:10Mikono yako haikufungwa,

miguu yako haikufungwa pingu.

Ulianguka kama yeye aangukaye

mbele ya watu waovu.”

Nao watu wote wakamlilia tena.

3:35 Rut 1:17; 1Sam 31:13; 2Sam 12:17; Yer 16:7; 1Sam 3:17Kisha watu wote wakaja kumsihi Daudi ale chochote kulipokuwa kungali bado mchana; lakini Daudi akaapa, akisema, “Mungu na anishughulikie, tena kwa ukali, kama nikionja mkate au kitu kingine chochote kabla ya jua kutua!”

Watu wote wakaona hilo nao ikawapendeza; naam, kila kitu mfalme alichofanya kiliwapendeza. Kwa hiyo siku ile watu wote na Israeli yote wakajua kwamba mfalme hakushiriki katika mauaji ya Abneri mwana wa Neri.

3:38 2Sam 1:19Kisha mfalme akawaambia watu wake, “Je, hamfahamu kwamba mkuu na mtu mashuhuri ameanguka katika Israeli leo? 3:39 2Sam 2:18; 16:9; 18:11; Amu 18:26; 1Fal 2:32; Za 41:10; 101:8; 2Sam 19:7, 13; Za 28:4; 62:12; 2Tim 4:14Nami leo ingawa ni mfalme mpakwa mafuta, mimi ni dhaifu, nao hawa wana wa Seruya wananizidi nguvu. Bwana na amlipize mtenda maovu sawasawa na matendo yake maovu!”

Read More of 2 Samweli 3

2 Samweli 4:1-12

Ish-Boshethi Auawa

4:1 2Sam 3:27; Ezr 4:4Ish-Boshethi mwana wa Sauli aliposikia kwamba Abneri amekufa huko Hebroni, akakosa ujasiri, nayo Israeli yote wakatiwa hofu kuu. 4:2 Yos 9:17; 18:25Basi mwana wa Sauli alikuwa na watu wawili waliokuwa viongozi wa vikundi vya uvamizi. Mmoja aliitwa Baana na mwingine Rekabu, waliokuwa wana wa Rimoni, Mbeerothi, kutoka kabila la Benyamini. Beerothi alihesabiwa kuwa sehemu ya Benyamini, 4:3 Neh 11:33kwa sababu watu wa Beerothi walikimbilia huko Gitaimu na wameishi huko kama wageni mpaka siku hii ya leo.

4:4 1Sam 18:1; 31:9; Law 21:18; 2Sam 9:8-12; 16:1-4; 19:24; 21:7-8; 1Nya 8:34; 9:40(Yonathani mwana wa Sauli alikuwa na mwana aliyekuwa mlemavu miguu yote miwili. Alikuwa na miaka mitano wakati habari kuhusu Sauli na Yonathani zilipofika kutoka Yezreeli. Yaya wake akambeba ili kukimbia, lakini yaya alipokuwa anaharakisha kuondoka, mtoto alianguka akawa kiwete. Jina lake aliitwa Mefiboshethi.)

4:5 2Sam 2:8; Rut 2:7Basi Rekabu na Baana, wana wa Rimoni Mbeerothi wakaenda nyumbani kwa Ish-Boshethi, nao walifika huko wakati alipokuwa kwenye mapumziko yake ya mchana. 4:6 2Sam 2:23; Amu 5:25; Za 147:14Wakaingia kwenye chumba cha ndani kana kwamba wanachukua ngano, wakamchoma Ish-Boshethi mkuki wa tumboni. Ndipo Rekabu na Baana nduguye wakatoroka.

4:7 Kum 3:17; 1Sam 17:54; 31:9; Mt 14:11Walikuwa wameingia ndani ya nyumba wakati alipokuwa amelala kitandani chumbani kwake. Baada ya kumchoma mkuki na kumuua, walikata kichwa chake. Wakiwa wamekichukua, walitembea usiku kucha kwa njia ya Araba. 4:8 2Sam 20:21; 2Fal 10:7; 1Sam 24:4; 25:29; Hes 31:3; 1Sam 23:15Wakamletea Daudi kichwa cha Ish-Boshethi huko Hebroni, wakamwambia mfalme, “Hiki hapa kichwa cha Ish-Boshethi mwana wa Sauli, adui yako, aliyejaribu kuondoa uhai wako. Siku hii ya leo Bwana amemlipia kisasi mfalme bwana wangu dhidi ya Sauli na mzao wake.”

4:9 Mwa 48:16; 1Fal 1:29; Za 31:7; 103:4; 106:10Daudi akawajibu Rekabu na Baana nduguye, wana wa Rimoni, Mbeerothi, akasema, “Hakika kama Bwana aishivyo, ambaye ameniokoa kutoka taabu zote, 4:10 2Sam 1:2-16yule mtu aliponiambia, ‘Sauli amekufa,’ akadhani ananiletea habari njema, nilimkamata, nikamuua huko Siklagi. Hiyo ndiyo zawadi niliyompa kwa ajili ya taarifa yake! 4:11 Mwa 4:10; 9:5; Za 9:12; 72:14Je, ni mara ngapi zaidi wakati watu waovu wamemuua mtu asiye na hatia akiwa ndani ya nyumba yake mwenyewe na kwenye kitanda chake mwenyewe? Je, sasa nisidai damu yake mikononi mwenu na kuwaondoa duniani?”

4:12 2Sam 1:15; 3:32Kwa hiyo Daudi akawaamuru watu wake, wakawaua. Wakakata mikono yao na miguu, na kutundika viwiliwili vyao kando ya dimbwi huko Hebroni. Lakini wakakichukua kichwa cha Ish-Boshethi na kukizika katika kaburi la Abneri huko Hebroni.

Read More of 2 Samweli 4

2 Samweli 5:1-5

Daudi Atawazwa Mfalme Juu Ya Israeli

(1 Nyakati 11:1-9; 14:1-7)

5:1 2Sam 19:43; Mwa 29:14; 35:26; 1Nya 11:1; 12:23Makabila yote ya Israeli yakamjia Daudi huko Hebroni na kumwambia, “Sisi tu nyama yako na damu yako hasa. 5:2 1Sam 8:5, 13, 16; 11:6; Mwa 48:15; 1Sam 16:1; 2Sam 7:7; Mt 2:6; Yn 12:16; 1Sam 12:12; 13:14; 6:21; 25:30; Za 78:71Zamani, wakati Sauli alikuwa mfalme juu yetu, wewe ndiwe uliyeiongoza Israeli vitani. Naye Bwana alikuambia, ‘Wewe utawachunga watu wangu Israeli, na utakuwa mtawala wao.’ ”

5:3 2Sam 3:21; Kum 17:15; 2Sam 2:4; 1Nya 11:3; 2Fal 11:17; Amu 11:11; 1Sam 23:18Wazee wote wa Israeli wakamwendea Mfalme Daudi huko Hebroni, mfalme akafanya mapatano nao huko Hebroni mbele za Bwana, nao wakamtia Daudi mafuta kuwa mfalme wa Israeli.

5:4 Mwa 37:2; Lk 3:23; 1Fal 2:11; 1Nya 3:4; 26:31; 29:27Daudi alikuwa na miaka thelathini alipoanza kutawala, naye akatawala Israeli miaka arobaini. 5:5 2Sam 2:11; 1Fal 2:11; 1Nya 3:4Huko Hebroni alitawala Yuda kwa miaka saba na miezi sita, na katika Yerusalemu alitawala Israeli yote na Yuda kwa miaka thelathini na mitatu.

Read More of 2 Samweli 5