2 Wakorintho 12:1-10 NEN

2 Wakorintho 12:1-10

Maono Ya Paulo Na Mwiba Aliokuwa Nao

12:1 2Kor 11:16; 1Kor 2:10Yanipasa nijisifu, ingawa haifaidi kitu. Nitaenda kwenye maono na ufunuo kutoka kwa Bwana. 12:2 Rum 16:3; Mdo 8:39; Efe 4:10; 2Kor 11:11Namjua mtu mmoja katika Kristo ambaye miaka kumi na minne iliyopita alichukuliwa juu hadi mbingu ya tatu. Kama ni katika mwili au nje ya mwili, sijui, Mungu ajua. Nami najua ya kwamba mtu huyu, kwamba ni katika mwili au nje ya mwili mimi sijui, lakini Mungu ajua, 12:4 Lk 23:43; Ufu 2:7; 12; 5; 1Kor 2:3alinyakuliwa hadi Paradiso.12:4 Paradiso hapa ina maana mbinguni. Huko alisikia mambo yasiyoelezeka, mambo ambayo binadamu hana ruhusa ya kuyasimulia. 12:5 1Kor 2:3; 2Kor 11:9, 10, 30Nitajisifu kwa ajili ya mtu kama huyo, lakini sitajisifu kuhusu mimi mwenyewe ila mimi nitajisifia udhaifu wangu. 12:6 2Kor 10:8; 11:16Hata kama ningependa kujisifu, sitakuwa mjinga, kwa maana nitakuwa nasema kweli. Lakini najizuia, ili mtu yeyote asije akaniona mimi kuwa bora zaidi kuliko ninavyoonekana katika yale ninayotenda na kusema.

12:7 1Kor 2:10; Hes 33:55; Mt 4:10Ili kunizuia nisijivune kwa sababu ya ufunuo huu mkuu, nilipewa mwiba katika mwili wangu, mjumbe wa Shetani, ili anitese. 12:8 Mt 26:39, 44Kwa habari ya jambo hili nilimsihi Bwana mara tatu aniondolee mwiba huu. 12:9 Rum 3:24; Flp 4:13; 1Fal 19:12Lakini aliniambia, “Neema yangu inakutosha, kwa kuwa uweza wangu hukamilika katika udhaifu.” Kwa hiyo nitajisifu kwa furaha zaidi kuhusu udhaifu wangu, ili uweza wa Kristo ukae juu yangu. 12:10 Mt 5:12; 2Kor 6:4; 2The 1:4; 2Kor 13:4Hii ndiyo sababu, kwa ajili ya Kristo, nafurahia udhaifu, katika kutukanwa, katika taabu, katika mateso na katika shida, kwa maana ninapokuwa dhaifu, ndipo nina nguvu.

Read More of 2 Wakorintho 12