2 Wakorintho 1:23, 2 Wakorintho 2:1-11 NEN

2 Wakorintho 1:23

1:23 Rum 1:9; 1Kor 4:21; 2Kor 2:1-3; 13:2-10Mungu ni shahidi wangu kwamba ilikuwa ni kwa ajili ya kuwahurumia ninyi sikurudi Korintho.

Read More of 2 Wakorintho 1

2 Wakorintho 2:1-11

2:1 2Kor 1:23; 12:20, 21; 13:10Hivyo nilikusudia moyoni mwangu nisifanye ziara nyingine yenye kuwaumiza ninyi. 2:2 2Kor 7:8Kwa kuwa kama nikiwahuzunisha ninyi, ni nani aliyebaki wa kunifurahisha isipokuwa ninyi ambao nimewahuzunisha? 2:3 2Kor 7:8-12; 12:21; 7:16; 8:22; Gal 5:10; 2The 3:4Niliandika hivyo kama nilivyofanya, ili nikija nisihuzunishwe na wale watu ambao wangenifanya nifurahi. Nina uhakika na ninyi nyote, kwamba wote mngeshiriki furaha yangu. 2:4 2Kor 7:8-12; 12:20, 21; 13:10Kwa maana niliwaandikia kutokana na dhiki kubwa na kutaabika sana kwa moyo wangu tena kwa machozi mengi, shabaha yangu si ili niwasababishe mhuzunike bali kuwaonyesha kina cha upendo wangu kwenu.

Msamaha Kwa Mwenye Dhambi

2:5 1Kor 5:1-2; Gal 4:12; 1Kor 5:1Lakini ikiwa mtu yeyote amesababisha huzuni, kwa kiasi fulani hakunihuzunisha mimi kama vile alivyowahuzunisha ninyi nyote, ili nisiwe mkali kupita kiasi. 2:6 1Kor 5:4-5; 2Kor 7:11Adhabu hii aliyopewa na wengi inamtosha. 2:7 Gal 6:1; Efe 4:32; Kol 3:13Basi sasa badala yake, inawapasa kumsamehe na kumfariji, ili asigubikwe na huzuni kupita kiasi. Kwa hiyo, nawasihi, mpate kuuthibitisha tena upendo wenu kwa ajili yake. 2:9 2Kor 7:8-12; 7:15; 10:6Sababu ya kuwaandikia ni kuona kama mngeweza kushinda hilo jaribio na kutii katika kila jambo. 2:10 Lk 10:16Kama ninyi mkimsamehe mtu yeyote, mimi pia nimemsamehe. Kile nilichosamehe, kama kulikuwa na kitu chochote cha kusamehe, nimekwisha kusamehe mbele ya Kristo kwa ajili yenu, 2:11 Mt 4:10; Lk 22:31; 2Kor 4:4; 1Pet 5:8ili Shetani asitushinde. Kwa maana hatuachi kuzijua hila zake.

Read More of 2 Wakorintho 2