2 Nyakati 7:11-22, 2 Nyakati 8:1-18, 2 Nyakati 9:1-31 NEN

2 Nyakati 7:11-22

Bwana Mungu Amtokea Solomoni

(1 Wafalme 9:1-9)

Solomoni alipomaliza kujenga Hekalu la Bwana na jumba la kifalme, naye akiwa amefanikiwa kutenda yale yote aliyokuwa nayo moyoni mwake kufanya katika Hekalu la Bwana na katika jumba lake mwenyewe la kifalme, 7:12 Kum 12:5; Mwa 12:7; Za 78:68-69Bwana akamtokea Solomoni usiku na kumwambia:

“Nimesikia maombi yako nami nimechagua mahali hapa kwa ajili yangu mwenyewe kuwa Hekalu kwa ajili ya dhabihu.

7:13 2Nya 6:26; Kum 11:17; Amo 4:7“Wakati nitakapofunga mbingu ili isiwepo mvua, au nikiamuru nzige kula mazao ya nchi au nikituma tauni miongoni mwa watu wangu, 7:14 Yak 4:10; Eze 18:32; Kut 10:3; 1Nya 16:11; Kut 15:26; 2Nya 6:27kama watu wangu, wanaoitwa kwa Jina langu, watajinyenyekesha na kuomba na kuutafuta uso wangu na kuacha njia zao mbaya, basi nitasikia toka mbinguni na kuwasamehe dhambi yao na nitaiponya nchi yao. 7:15 1Fal 8:29; 2Nya 6:40; Neh 1:6Sasa macho yangu yatafumbuka na masikio yangu yatasikiliza kwa makini maombi yaombwayo mahali hapa. 7:16 Kum 12:5; 2Nya 6:6Kwa maana sasa nimechagua na kutakasa Hekalu hili ili kwamba Jina langu lipate kuwa huko milele. Macho yangu na moyo wangu utakuwepo huko daima.

7:17 1Fal 9:4“Kwa habari yako wewe, kama ukienenda mbele zangu kama Daudi baba yako alivyoenenda na kufanya yote nikuamuruyo, nawe ukizishika amri zangu na sheria zangu, 7:18 Mik 5:2; 2Sam 17:13; 1Nya 17:12; 2Nya 6:16Nitakiimarisha kiti chako cha enzi kama nilivyoagana na Daudi baba yako niliposema, ‘Hutakosa kamwe mtu wa kutawala juu ya Israeli.’

7:19 Kum 28:15; Law 26:14, 33“Lakini kama ukigeuka na kuyaacha maagizo na amri nilizowapa na kwenda kuitumikia miungu mingine na kuiabudu, 7:20 Kum 28:37; 29:28; 1Fal 14:15; Yer 12:14; 16:13; 50:11; Za 5:5ndipo nitakapoingʼoa Israeli kutoka nchi yangu niliyowapa, nami nitalikataa Hekalu hili nililolitakasa kwa ajili ya Jina langu. Nitalifanya kitu cha kudharauliwa na kitu cha kudhihakiwa miongoni mwa watu wote. 7:21 Kum 29:24; Yer 22:8; Mao 2:15; Yer 7:14Ingawa Hekalu hili linavutia sana sasa, wote watakaolipita watashangaa na kusema, ‘Kwa nini Bwana amefanya kitu kama hiki katika nchi hii na kwa Hekalu hili?’ 7:22 Amu 2:13; Dan 9:12; 2Fal 17:18; 2Nya 36:16Watu watajibu, ‘Ni kwa sababu wamemwacha Bwana, Mungu wa baba zao, aliyewatoa Misri, nao wamekumbatia miungu mingine, wakaiabudu na kuitumikia, ndiyo sababu ameyaleta maafa haya yote juu yao.’ ”

Read More of 2 Nyakati 7

2 Nyakati 8:1-18

Shughuli Nyingine Za Solomoni

(1 Wafalme 9:10-28)

8:1 1Fal 9:10Miaka ishirini ilipopita, ambayo katika hiyo Solomoni alilijenga Hekalu la Bwana na jumba lake mwenyewe la kifalme, Solomoni akajenga tena vijiji vile ambavyo Hiramu alikuwa amempa, naye akawapa Waisraeli waishi humo. 8:3 Hes 13:21; 2Sam 8:2-3Kisha Solomoni akaenda Hamath-Soba na kuuteka. 8:4 1Fal 9:14Pia akajenga mji wa Tadmori katika jangwa na miji yote ya kuhifadhia vitu katika Hamathi. 8:5 Yos 10:10; 1Nya 7:24; Hes 13:21Akajenga tena Beth-Horoni ya Juu na Beth-Horoni ya Chini, miji yenye ngome, kuta, malango na makomeo. 8:6 Yos 15:11Solomoni pia akajenga Baalathi na miji yake yote ya kuhifadhia vitu, na miji kwa ajili ya magari yake na kwa ajili ya farasi wake, chochote alichotaka kujenga katika Yerusalemu, katika Lebanoni na katika nchi yote aliyotawala.

8:7 Mwa 15:18-21; 1Fal 9:20; Ezr 9:1; Mwa 10:15Watu wote waliosalia kutoka kwa Wahiti, Waamori, Waperizi, Wahivi na Wayebusi (haya mataifa hayakuwa Waisraeli), 8:8 1Fal 9:21; 2Nya 2:18yaani, wazao wao waliobakia katika nchi, ambao Waisraeli hawakuwa wamewaangamiza: hawa Solomoni akawalazimisha kuwa watumwa katika shokoa, kama ilivyo hadi leo. 8:9 Kut 19:5; Kum 23:19; Law 25:39; Gal 4:28-31Lakini Solomoni hakuwafanya Waisraeli watumwa kwa ajili ya kazi yake, bali walikuwa wapiganaji, majemadari, maafisa wake, majemadari wa magari yake ya vita na waendesha magari ya vita. 8:10 1Fal 5:16; 9:23; 2Nya 2:18Pia walikuwa maafisa wakuu wa Mfalme Solomoni, yaani, maafisa wakaguzi 250 waliosimamia watu.

8:11 1Fal 7:8; 9:24Solomoni akampandisha mke wake binti Farao kutoka Mji wa Daudi na kumleta jumba la kifalme alilokuwa amemjengea, kwa kuwa alisema, “Mke wangu hataishi katika jumba la kifalme la Daudi mfalme wa Israeli, kwa sababu mahali ambapo Sanduku la Bwana limefika ni patakatifu.”

8:12 1Fal 8:64; 1Nya 4:1Mfalme Solomoni akamtolea Bwana dhabihu za kuteketezwa juu ya madhabahu ya Bwana ambayo alikuwa ameijenga mbele ya ukumbi, 8:13 Kut 29:38; Hes 28:3-9; Kut 23:14-16; Kum 16:16; 1Fal 9:25kulingana na mahitaji ya kila siku kwa ajili ya sadaka zilizoamriwa na Mose kwa ajili ya Sabato, Mwezi Mwandamo na sikukuu nyingine tatu za mwaka, yaani, Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu, Sikukuu ya Majuma na Sikukuu ya Vibanda. 8:14 1Nya 24:1; 9:17; Neh 12:24, 36, 45; 1Nya 23:6; 2Sam 23:2; 2Nya 5:11; 31:2; 1Nya 25:1; 26:1Kwa kushika maagizo ya Daudi baba yake, aliweka migawanyo ya makuhani kwa ajili ya kazi zao, nao Walawi kuongoza kusifu na kusaidia makuhani kufuatana na mahitaji ya kila siku. Pia akaweka mabawabu katika migawanyo kwa ajili ya malango mbalimbali, kwa sababu hili ndilo Daudi mtu wa Mungu alilokuwa ameagiza. Nao hawakuziacha amri za mfalme alizoamuru makuhani au Walawi katika jambo lolote, ikiwa ni pamoja na zile za hazina.

Kazi yote ya Mfalme Solomoni ilifanyika kuanzia siku msingi wa Hekalu la Bwana ulipowekwa mpaka kukamilika kwake. Kwa hiyo Hekalu la Bwana likamalizika kujengwa.

8:17 Kum 2:8; 2Fal 14:22; 1Fal 9:26Ndipo Solomoni akaenda Esion-Geberi na Elathi katika pwani ya Edomu. 8:18 1Fal 9:27; Isa 13:12; 2Nya 9:9; Mwa 10:29; Ay 22:24Naye Hiramu alimpelekea meli zilizoongozwa na maafisa wake mwenyewe, watu waliokuwa na ujuzi wa baharini. Hawa watu pamoja na wale wa Solomoni wakasafiri kwa bahari mpaka Ofiri, wakaleta kutoka huko talanta 450 za dhahabu, ambazo walimkabidhi Mfalme Solomoni.

Read More of 2 Nyakati 8

2 Nyakati 9:1-31

Malkia Wa Sheba Amtembelea Solomoni

(1 Wafalme 10:1-13)

9:1 Mwa 10:7; Eze 20:49; Lk 11:31; Mt 12:42; 13:11, 35; Za 49:4; 78:2; Mit 1:5Malkia wa Sheba aliposikia habari za umaarufu wa Solomoni, huyo malkia akaja Yerusalemu kumjaribu kwa maswali magumu. Alifika akiwa na msafara mkubwa sana, pamoja na ngamia waliobeba vikolezi, kiasi kikubwa cha dhahabu na vito vya thamani, alikuja kwa Solomoni na kuzungumza naye kuhusu yote ambayo alikuwa nayo moyoni mwake. Solomoni akamjibu maswali yake yote, wala hakukuwa na jambo lolote lililokuwa gumu kwake asiweze kumwelezea. 9:3 1Fal 5:12Malkia wa Sheba alipoona hekima yote ya Solomoni na jumba la kifalme alilokuwa amejenga, chakula kilichokuwa mezani pake, jinsi maafisa wake walivyokaa, wahudumu katika majoho yao, wanyweshaji wake na sadaka za kuteketezwa alizotoa katika Hekalu la Bwana alipatwa na mshangao.

Akamwambia mfalme, “Taarifa niliyosikia kwenye nchi yangu mwenyewe kuhusu mafanikio na hekima yako ni kweli. 9:6 2Nya 6:32Lakini sikuamini yaliyosemwa hadi nilipokuja na kuona kwa macho yangu mwenyewe. Naam, sikuambiwa hata nusu yake; katika hekima na mali umezidi sana kuliko ile taarifa niliyoisikia. Heri watu wako! Heri hawa maafisa wako wasimamao mbele yako daima na kusikia hekima yako! 9:8 1Fal 2:12; 1Nya 28:5; Za 72:8-9Ahimidiwe Bwana Mungu wako, ambaye amependezwa sana nawe, na akakuweka juu ya kiti chake cha ufalme utawale kwa niaba ya Bwana Mungu wako. Kwa sababu ya upendo wa Mungu wako kwa Israeli na shauku yake ya kuwadhibitisha milele, amekufanya wewe mfalme juu yao, ili kudumisha haki na uadilifu.”

9:9 2Nya 8:18Naye akampa mfalme talanta 1209:9 Talanta 120 za dhahabu ni sawa na tani 4.5. za dhahabu, kiasi kikubwa cha vikolezi na vito vya thamani. Haikuwahi kamwe kuletwa vikolezi vizuri kama vile Malkia wa Sheba alivyompa Mfalme Solomoni.

9:10 1Fal 5:2-6; 2Nya 8:18; 1Fal 9:27-28; 10:11; Za 72:10(Watumishi wa Hiramu na wa Solomoni wakaleta dhahabu kutoka Ofiri, tena wakaleta shehena kubwa ya miti ya msandali na vito vya thamani. Mfalme akatumia hiyo miti ya msandali kuwa ngazi kwa ajili ya Hekalu la Bwana na kwa jumba la kifalme, pia kwa kutengeneza vinubi na zeze kwa ajili ya waimbaji. Kiasi hicho kingi cha msandali hakijawahi kuingizwa Yuda tangu siku ile.)

Mfalme Solomoni akampa Malkia wa Sheba kila kitu alichotamani na kukiomba, zaidi ya vile alivyokuwa amemletea mfalme. Kisha malkia akaondoka na kurudi katika nchi yake, yeye na watumishi wake.

Fahari Ya Solomoni

(1 Wafalme 10:14-25)

Uzito wa dhahabu ambayo Solomoni alipokea kwa mwaka ulikuwa talanta 666,9:13 Talanta 666 za dhahabu ni sawa na tani 25. 9:14 Isa 21:13; Eze 27:21; Yer 25:24; Isa 45:14; Za 68:29; 72:10; Isa 60:6mbali na mapato yaliyoletwa na wafanyabiashara na wachuuzi. Wafalme wote wa Arabuni na watawala wa nchi wakamletea Solomoni dhahabu na fedha.

Mfalme Solomoni akatengeneza ngao kubwa 200 kwa dhahabu iliyofuliwa. Kila ngao ilikuwa na dhahabu yenye uzito wa shekeli 6009:15 Shekeli 600 za dhahabu ni sawa na kilo 3.5. 9:16 2Nya 12:9; 1Fal 7:2Akatengeneza pia ngao ndogo 300 za dhahabu iliyofuliwa, kila ngao ikiwa na uzito wa mane tatu9:16 Mane tatu za dhahabu ni sawa na kilo 1.7. za dhahabu. Mfalme akaziweka katika Jumba la Kifalme la Msitu wa Lebanoni.

9:17 1Fal 22:39Kisha mfalme akatengeneza kiti kikubwa cha kifalme kwa kutumia pembe za ndovu na kukifunika kwa dhahabu safi. Kiti hicho kilikuwa na ngazi sita na mahali pa kuwekea miguu vyote vya dhahabu. Pande zote za kiti kulikuwa na mahali pa kuegemeza mikono, na simba wawili wakisimama kando ya hiyo mikono. Simba kumi na wawili walisimama kwenye ngazi sita, mmoja katika kila upande wa kila ngazi. Hakuna kitu kama hicho kilichokuwa kimefanyika kwenye ufalme mwingine wowote. Vikombe vyote vya Mfalme Solomoni vya kunywea vilikuwa vya dhahabu na vyombo vyote vya nyumbani katika Jumba la Kifalme la Msitu wa Lebanoni vilikuwa vya dhahabu safi. Hakukuwa na kitu kilichotengenezwa kwa fedha, kwa sababu fedha ilionekana ya thamani ndogo wakati wa Solomoni. 9:21 1Fal 10:22; Isa 2:16; Yer 10:9; Yn 1:3; 1Fal 22:48; Za 48:7; Isa 60:9; Za 72:10Mfalme alikuwa na meli nyingi za biashara9:21 Au: za Tarshishi (ona pia 1Fal 10:22; 22:48; 2Nya 20:36; Isa 2:16; 60:9). baharini zilizoendeshwa na watu wa Hiramu. Kwa mara moja kila miaka mitatu zilirudi, zikiwa zimebeba dhahabu, fedha, pembe za ndovu na nyani wakubwa na wadogo.

9:22 1Fal 3:13; 2Nya 1:12; Kol 2:2-3; Mt 12:42; 1Fal 10:23-24; Za 89:27Mfalme Solomoni alikuwa mkuu zaidi kwa utajiri na hekima kuliko wafalme wote wa dunia. 9:23 1Fal 4:34Wafalme wote wa dunia wakatafuta kukutana na Solomoni ili kusikia hekima ambayo Mungu alikuwa ameiweka katika moyo wake. 9:24 Za 45:12; Isa 18:7; Za 72:10-15Mwaka baada ya mwaka, kila mmoja ambaye alikuja, alileta zawadi, vyombo vya fedha na dhahabu, majoho, silaha na vikolezi, farasi na nyumbu.

9:25 1Sam 8:11; 1Fal 4:26; 10:26; 2Nya 1:14Solomoni alikuwa na mabanda 4,000 kwa ajili ya farasi na magari ya vita, farasi 12,000 ambao aliwaweka katika miji ya magari ya vita na katika Yerusalemu pamoja naye. 9:26 1Fal 2:21; Za 72:8-9; Mwa 15:18-21; 1Fal 4:21Solomoni akatawala juu ya wafalme wote kuanzia Mto Frati mpaka kwenye nchi ya Wafilisti na kuendelea hadi mpaka wa Misri. 9:27 1Fal 10:27Mfalme akafanya fedha kuwa kitu cha kawaida kama mawe huko Yerusalemu, mierezi akaifanya kuwa mingi kama mikuyu vilimani. 9:28 Kum 17:16; 1Fal 10:26; Isa 31:1; 2:7; 2Nya 1:16Farasi wa Solomoni waliletwa kutoka Misri na kutoka nchi nyingine zote.

Kifo Cha Solomoni

(1 Wafalme 11:41-43)

9:29 2Sam 7:2; 1Nya 29:29; 1Fal 11:29; 2Nya 10:2; 12:15; 13:22Kwa habari za matukio mengine ya utawala wa Solomoni, kuanzia mwanzo hadi mwisho, je, hayakuandikwa katika kumbukumbu za nabii Nathani, katika unabii wa Ahiya Mshiloni na katika maono ya Ido mwonaji kuhusu Yeroboamu mwana wa Nebati? 9:30 1Fal 11:42-43Solomoni alitawala Israeli yote miaka arobaini, akiwa Yerusalemu. 9:31 1Fal 2:10Kisha Solomoni akalala pamoja na baba zake, naye akazikwa katika mji wa Daudi baba yake. Naye Rehoboamu mwanawe akawa mfalme baada yake.

Read More of 2 Nyakati 9