1 Timotheo 2:1-15 NEN

1 Timotheo 2:1-15

Maagizo Kuhusu Kuabudu

2:1 Efe 6:18; Flp 4:6Awali ya yote, nasihi kwamba dua, sala, maombezi na shukrani zifanyike kwa ajili ya watu wote: 2:2 Ezr 6:10; Rum 13:1kwa ajili ya wafalme na wale wote wenye mamlaka, ili tupate kuishi kwa amani na utulivu, katika uchaji wote wa Mungu na utakatifu. 2:3 Mdo 20:1; 1Tim 5:4; Lk 1:42Jambo hili ni jema, tena linapendeza machoni pa Mungu Mwokozi wetu, 2:4 Eze 18:23-32; 1Tim 4:10; 2Tim 2:25anayetaka watu wote waokolewe na wafikie kuijua kweli. 2:5 Rum 10:12; Gal 3:20Kwa maana kuna Mungu mmoja na mpatanishi mmoja kati ya Mungu na wanadamu, yaani mwanadamu Kristo Yesu, 2:6 1Kor 1:6; 1Tim 6:15aliyejitoa mwenyewe kuwa fidia kwa ajili ya wanadamu wote: jambo hili lilishuhudiwa kwa wakati wake ufaao. 2:7 2Tim 1:11; Mdo 9:15; Efe 3:7-8Nami kwa kusudi hili nimewekwa niwe mhubiri na mtume (nasema kweli katika Kristo wala sisemi uongo), mwalimu wa watu wa Mataifa katika imani na kweli.

2:8 Za 24:4; Lk 24:50Nataka kila mahali wanaume wasali wakiinua mikono mitakatifu pasipo hasira wala kugombana.

2:9 1Pet 3:3Vivyo hivyo nataka wanawake wajipambe kwa adabu na kwa heshima katika mavazi yanayostahili, si kwa kusuka nywele, kuvalia dhahabu, lulu au mavazi ya gharama kubwa, 2:10 1Tim 5:10; Mit 31:13bali kwa matendo mazuri kama iwapasavyo wanawake wanaokiri kuwa wanamcha Mungu.

2:11 1Kor 14:34; 1Pet 3:3, 4Mwanamke na ajifunze kwa utulivu na kwa utiifu wote. 2:12 Efe 5:22; 1Kor 14:34; Mwa 3:16Simpi mwanamke ruhusa ya kufundisha au kuwa na mamlaka juu ya mwanaume. Mwanamke inampasa kukaa kimya. 2:13 Mwa 2:7, 22; 1Kor 11:8Kwa maana Adamu aliumbwa kwanza, kisha Eva. 2:14 Mwa 3:1-6, 13; 2Kor 11:3Wala si Adamu aliyedanganywa, bali ni mwanamke aliyedanganywa akawa mkosaji. 2:15 1Tim 1:14Lakini mwanamke ataokolewa kwa kuzaa kwake, kama wakiendelea kudumu katika imani, upendo na utakatifu, pamoja na kuwa na kiasi.

Read More of 1 Timotheo 2