1 Samweli 19:1-24, 1 Samweli 20:1-42 NEN

1 Samweli 19:1-24

Sauli Ajaribu Kumuua Daudi

19:1 1Sam 18:1-9; Mit 27:4Sauli akamwambia mwanawe Yonathani na watumishi wake wote wamuue Daudi. Lakini Yonathani mwana wa Sauli alimpenda sana Daudi. 19:2 Mdo 23:16Yonathani akamwonya Daudi, akisema, “Baba yangu Sauli anatafuta nafasi ya kukuua. Ujilinde kesho asubuhi, nenda mahali pa siri na ukae huko. 19:3 1Sam 20:12Nitatoka na kukaa na baba yangu shambani mahali uliko. Nitazungumza naye juu yako, nami nitakueleza nitakachogundua.”

19:4 1Sam 20:32; 22:14; Mit 31:8-9; Yer 18:20; 1Sam 25:21; Mit 17:13; Mwa 42:22; 1Nya 6:22; Za 35:12; 109:5; Yer 18:20; 1Kor 8:12; 1Yn 3:15Yonathani akanena mema juu ya Daudi kwa Sauli baba yake na kumwambia, “Mfalme asitende mabaya kwa mtumishi wake Daudi; hajakukosea, aliyoyafanya yamekuwa ya faida sana kwako. 19:5 Amu 9:17; 1Sam 11:13; Mwa 31:36; Kum 19:10-13; 1Sam 17:49-50; 1Nya 11:14; Mt 27:4; Za 119:109; Mt 27:14Alihatarisha maisha yake alipomuua yule Mfilisti. Bwana akajipatia ushindi mkubwa kwa ajili ya Israeli wote, nawe uliuona na ukafurahi. Kwa nini basi utende mabaya kwa mtu asiye na hatia kama Daudi kwa kumuua bila sababu?”

Sauli akamsikiliza Yonathani na kuapa hivi: “Hakika kama Bwana aishivyo, Daudi hatauawa.”

19:7 1Sam 16:21; 18:10Basi Yonathani akamwita Daudi na kumweleza mazungumzo yote. Akamleta kwa Sauli, naye Daudi akawa pamoja na Sauli kama kwanza.

Vita vilitokea tena, naye Daudi akatoka na kupigana na Wafilisti. Akawapiga kwa nguvu nyingi hata wakakimbia mbele yake.

19:9 Amu 9:23; 1Sam 10:5; 16:14Lakini roho mbaya iliyoachiwa nafasi na Bwana ikaja juu ya Sauli alipokuwa ameketi katika nyumba yake akiwa na mkuki mkononi mwake. Daudi alipokuwa anampigia kinubi, 19:10 1Sam 18:11; Ay 5:2; Za 5:6; Mit 1:16; 29:10Sauli akajaribu kumchomea Daudi ukutani kwa huo mkuki wake, lakini Daudi akauhepa huo mkuki wa Sauli ukakita ukutani. Usiku ule ule Daudi akakimbia na kuokoka.

19:11 Za 59; Amu 16:2Sauli akatuma watu nyumbani mwa Daudi wailinde hiyo nyumba na kumuua asubuhi. Lakini Mikali, mkewe Daudi, akamwonya akisema, “Kama hukukimbia kuokoa maisha yako usiku huu, kesho yake utauawa.” 19:12 Yos 2:15; Mdo 9:25; 2Kor 11:33Basi Mikali akamteremsha Daudi kupitia dirishani, naye akakimbia na kuokoka. 19:13 Mwa 31:19; Amu 17:5Kisha Mikali akachukua kinyago, akakilaza kitandani, akakifunika kwa vazi na kukiwekea singa za mbuzi kichwani.

19:14 Kum 1:19; Yos 2:4Sauli alipotuma watu kumkamata Daudi, Mikali akasema, “Yeye ni mgonjwa.”

Kisha Sauli akatuma watu tena kumwona Daudi naye akawaambia, “Mleteni kwangu juu ya kitanda chake ili nipate kumuua.” Lakini wale watu walipoingia, kumbe ni kinyago tu kilichokuwa kitandani na kwenye kichwa kulikuwepo na singa za mbuzi.

19:17 2Sam 2:22Sauli akamwambia Mikali, “Kwa nini umenidanganya mimi hivi na kumwacha adui yangu aende zake ili apate kuokoka?”

Mikali akamwambia, “Yeye aliniambia, ‘Niache niende zangu. Kwa nini nikuue?’ ”

19:18 1Sam 7:17; Mit 17:17; Mal 2:7Daudi alipokuwa amekimbia na kuokoka, alimwendea Samweli huko Rama na kumwambia yale yote Sauli alimfanyia. Ndipo Daudi na Samweli wakaenda Nayothi kukaa huko. Habari zikamfikia Sauli kusema: “Daudi yuko Nayothi huko Rama.” 19:20 Hes 11:25-29; 1Sam 10:5; Yoe 2:28; Yn 7:32, 45; 1Kor 14:3, 24, 25Basi Sauli akatuma watu kumkamata Daudi, lakini walipoona kundi la manabii wakitoa unabii, wakiwa pamoja na Samweli akiwa amesimama hapo kama kiongozi wao, Roho wa Mungu akaja juu ya watu wa Sauli, nao pia wakatoa unabii. Sauli akaelezwa juu ya hilo, naye akapeleka watu wengine zaidi, nao wakatoa unabii pia. Sauli akatuma watu mara ya tatu, nao pia wakatoa unabii. Mwishowe, yeye mwenyewe akaondoka kwenda Rama na kwenda hadi kwenye kile kisima kikubwa kilichoko huko Seku. Naye akauliza, “Wako wapi Samweli na Daudi?”

Wakasema, “Wako Nayothi huko Rama.”

19:23 1Sam 10:13; Mwa 31:24; Hes 23:5; 24:2; Mit 21:1; Dan 4:35; Mt 7:22; Yn 11:51; 1Kor 13:2Hivyo Sauli akaenda Nayothi huko Rama. Lakini Roho wa Mungu akaja juu yake hata yeye, akawa anatembea huku anatoa unabii hadi akafika Nayothi. 19:24 2Sam 6:20; Isa 20:2; 1Sam 15:35; 10:11; Mik 1:8; Mdo 9:21Akavua majoho yake na pia akatoa unabii mbele ya Samweli. Akalala hali hiyo ule mchana kutwa na usiku kucha. Hii ndiyo sababu watu husema, “Je, Sauli pia yumo miongoni mwa manabii?”

Read More of 1 Samweli 19

1 Samweli 20:1-42

Daudi Na Yonathani

20:1 1Sam 24:9; 22:23; 23:15; 24:11; 25:29; Za 40:14; 54:3; 63:9; 70:2Kisha Daudi akakimbia kutoka Nayothi huko Rama akamwendea Yonathani na kumuuliza, “Kwani nimefanya nini? Kosa langu ni nini? Nimemkosea baba yako kwa jinsi gani, hata kwamba anajaribu kuuondoa uhai wangu?”

20:2 Mwa 44:7; Yos 22:29Yonathani akajibu, “La hasha! Hutakufa! Tazama, baba yangu hafanyi kitu chochote, kikubwa au kidogo, bila kuniambia mimi. Kwa nini anifiche hili? Sivyo ilivyo!”

20:3 Kum 6:13Lakini Daudi akaapa na kusema, “Baba yako anajua kabisa kwamba nimepata kibali mbele yako, naye amesema moyoni mwake, ‘Yonathani sharti asilijue hili, la sivyo atahuzunika.’ Lakini kweli kama Bwana aishivyo na kama uishivyo, kuna hatua moja tu kati yangu na mauti.”

Yonathani akamwambia Daudi, “Chochote unachotaka nifanye, nitakufanyia.”

20:5 Hes 10:10; 25:11; 1Sam 9:12; 2Fal 4:23; 1Nya 23:31; 2Nya 2:4; Ezr 3:5; Neh 10:33; Za 81:3; Isa 1:13; Eze 45:17; 46:6; Za 55:13; Yn 8:59Basi Daudi akamwambia, “Angalia, kesho ni sikukuu ya Mwezi Mwandamo, nami inanipasa kula chakula pamoja na mfalme; lakini niache niende kujificha shambani mpaka kesho kutwa. 20:6 1Sam 17:58; 1:3; 16:4; 9:12Kama baba yako akiona ya kuwa sipo, mwambie, ‘Daudi aliniomba sana ruhusa kuwahi Bethlehemu, mji wake wa nyumbani, kwa sababu dhabihu ya mwaka inafanywa huko kwa ajili ya ukoo wake wote.’ 20:7 1Sam 10:27; 25:17; 18:11; Kum 1:23Kama akisema, ‘Ni vyema sana,’ basi mtumishi wako yu salama. Lakini kama akikasirika, unaweza kuwa na hakika kwamba anakusudia kunidhuru. 20:8 1Sam 18:3; 23:18; 2Sam 14:32; Yos 2:14; Rut 1:8Lakini kwa habari yako wewe, mtende wema mtumishi wako, kwa sababu mmeingia kwenye agano pamoja naye mbele za Bwana. Kama nina hatia, basi niue wewe mwenyewe! Kwa nini unikabidhi kwa baba yako?”

Yonathani akasema, “La hasha! Kama ningekuwa na kidokezo kidogo kwamba baba yangu amekusudia kukudhuru wewe, je, nisingekuambia?”

Daudi akamuuliza, “Je, nani atakayeniambia kama baba yako atakujibu kwa ukali?”

Yonathani akamwambia, “Njoo, twende shambani.” Basi wakaenda huko pamoja.

20:12 1Sam 19:3; Yos 22:22Kisha Yonathani akamwambia Daudi, “Ninakuahidi kwa jina la Bwana, Mungu wa Israeli, hakika nitamchunguza baba yangu wakati kama huu kesho kutwa! Kama ameweka utaratibu wa kufaa kukuhusu wewe, je, sitakutumia ujumbe na kukufahamisha? 20:13 Rut 1:17; 1Sam 16:18; 18:12Lakini ikiwa baba yangu amenuia kukudhuru, Bwana na anishughulikie kwa ukali, iwapo sitakufahamisha na kukuaga uende salama. Bwana na awe pamoja nawe kama alivyokuwa pamoja na baba yangu. Lakini nitendee wema usiokoma kama ule wa Bwana siku zote za maisha yangu, ili nisije nikauawa, 20:15 1Sam 24:21; 2Sam 9:7; Mwa 21:23wala usiuondoe wema wako kwa jamaa yangu, hata kama ni wakati ule Bwana atakapokuwa amekatilia mbali kila adui wa Daudi kutoka kwenye uso wa dunia.”

20:16 1Sam 18:1-3; 25:22-23; Yos 22:23; 2Sam 4:7; 21:8Basi Yonathani akafanya agano na nyumba ya Daudi, akisema: “Bwana na awaangamize adui za Daudi.” 20:17 Yos 9:18; 1Sam 18:3; 2Sam 1:26Naye Yonathani akamtaka Daudi athibitishe tena kiapo chake cha kumpenda, kwa sababu Yonathani alimpenda Daudi kama nafsi yake mwenyewe.

Kisha Yonathani akamwambia Daudi, “Kesho ni sikukuu ya Mwezi Mwandamo. Itajulikana kwamba haupo kwa kuwa kiti chako kitakuwa hakina mtu. 20:19 1Sam 19:2Kesho kutwa, inapokaribia jioni, nenda mahali pale ulipojificha wakati tatizo hili lilipoanza na usubiri karibu na jiwe la Ezeli. 20:20 2Fal 13:15Nitapiga mishale mitatu kando yake, kama kwamba nilikwenda kulenga shabaha. 20:21 Kum 6:13; 10:20; Isa 65:16; Yer 4:2Kisha nitamtuma mvulana na kumwambia, ‘Nenda ukaitafute mishale.’ Kama nikimwambia, ‘Tazama mishale iko upande huu wako! Uilete hapa,’ basi uje, kwa sababu hakika kama Bwana aishivyo, wewe ni salama, hakuna hatari. Lakini kama nikimwambia huyo mvulana, ‘Angalia, mishale iko mbele yako,’ basi inakupasa uondoke, kwa sababu Bwana amekuruhusu uende zako. 20:23 Mwa 31:50Kuhusu yale tuliyozungumza wewe na mimi: kumbuka, Bwana ndiye shahidi kati yako wewe na mimi milele.”

20:24 Hes 10:10; Mit 27:12Basi Daudi akajificha shambani, na sikukuu ya Mwezi Mwandamo ilipowadia, mfalme akaketi ili ale. 20:25 1Sam 14:50Akaketi mahali pake pa kawaida karibu na ukuta, kuelekeana na Yonathani, naye Abneri akaketi karibu na Mfalme Sauli, lakini kiti cha Daudi kilikuwa wazi. 20:26 Law 15:5; 1Sam 16:5; Law 6:2; 7:21; Hes 19:16; 1Kor 15:33; 2Kor 6:17; Efe 2:1-3; 5:11Sauli hakusema chochote siku ile kwa kuwa alifikiri, “Kuna kitu cha lazima kimetokea kwa Daudi ambacho kimemfanya najisi asihudhurie karamuni, hakika yeye yu najisi.” Lakini siku iliyofuata, siku ya pili ya mwezi, kiti cha Daudi kilikuwa wazi tena. Kisha Sauli akamwambia mwanawe Yonathani, “Kwa nini mwana wa Yese hajaja chakulani jana wala leo?”

Yonathani akamjibu, “Daudi alinisihi sana nimpe ruhusa aende Bethlehemu. 20:29 Mwa 8:20Alisema, ‘Niruhusu niende, kwa sababu jamaa yetu wana dhabihu mjini, na ndugu yangu ameniagiza niwepo huko. Kama nimepata kibali mbele yako, niruhusu niende kuona ndugu zangu.’ Hii ndiyo sababu hakuja mezani pa mfalme.”

Hasira ya Sauli ikawaka dhidi ya Yonathani na kumwambia, “Wewe mwana wa mwanamke mkaidi na mwasi! Je, sijui kuwa umekuwa upande wa mwana wa Yese kwa aibu yako mwenyewe na kwa aibu ya mama yako aliyekuzaa? 20:31 1Sam 23:17; 24:20Maadamu mwana wa Yese angali anaishi katika dunia hii wewe wala ufalme wako hautasimama. Sasa tuma aitwe umlete kwangu, kwa kuwa ni lazima afe!”

20:32 1Sam 19:4-5; Mt 23:27; Mwa 31:36; Lk 23:22; Za 25:3; 69:4; Mit 14:25; 24:11; Mt 27:23; Yn 7:31; 15:25Yonathani akamuuliza baba yake, “Kwa nini auawe? Kwani amefanya nini?” 20:33 1Sam 18:11, 17Lakini Sauli akamtupia Yonathani mkuki wake kwa nguvu ili amuue. Hapo ndipo Yonathani alipotambua kwamba baba yake alikusudia kumuua Daudi.

Yonathani akainuka kutoka mezani kwa hasira kali. Siku ile ya pili ya mwezi hakula chakula, kwa kuwa alikuwa amehuzunishwa na vitendo vya aibu ambavyo baba yake alikuwa anamtendea Daudi.

Kesho yake asubuhi Yonathani alikwenda shambani kukutana na Daudi. Alikuwa amefuatana na mvulana mdogo, naye Yonathani akamwambia yule mvulana, “Kimbia ukatafute mishale nitakayorusha.” Mvulana alipokuwa akikimbia, akarusha mishale mbele yake. Yule mvulana alipofika mahali pale ambapo mshale wa Yonathani ulipokuwa umeanguka, Yonathani akamwita, “Je, mshale hauko mbele yako?” Yonathani akampigia kelele, “Harakisha, nenda haraka! Usisimame!” Mvulana akaokota mshale na kurudi kwa bwana wake. (Mvulana hakujua chochote juu ya hayo yote; Yonathani na Daudi tu ndio waliojua.) Basi Yonathani akampa yule mvulana silaha zake na kumwambia, “Nenda, zirudishe mjini.”

20:41 Mwa 33:3; Rut 2:10; 1Sam 24:8; 25:23; 2Sam 1:2Baada ya mvulana kwenda, Daudi akainuka kutoka upande wa kusini wa lile jiwe, naye akasujudu uso wake mpaka nchi mara tatu mbele ya Yonathani. Kisha kila mmoja akambusu mwenzake, wakalia pamoja. Lakini Daudi akalia zaidi.

20:42 1Sam 1:17; Mdo 15:33; Mwa 40:14; 2Sam 1:26; Mit 18:24; Isa 48:1; Mwa 31:50; 1Sam 18:3; 2Sam 9; 1Yonathani akamwambia Daudi, “Nenda kwa amani, kwa kuwa tumeapiana kiapo cha urafiki kati yetu kwa jina la Bwana, tukisema, ‘Bwana ndiye shahidi kati yako na mimi, na kati ya wazao wako na wazao wangu milele.’ ” Kisha Daudi akaondoka, naye Yonathani akarudi mjini.

Read More of 1 Samweli 20