1 Samweli 17:38-58, 1 Samweli 18:1-30 NEN

1 Samweli 17:38-58

17:38 Mwa 41:42Ndipo Sauli akamvika Daudi silaha zake mwenyewe za vita. Akamvika dirii na chapeo ya shaba kichwani mwake. Daudi akajifunga upanga juu ya hayo mavazi na kujaribu kutembea kwa sababu alikuwa hana uzoefu navyo.

Daudi akamwambia Sauli, “Siwezi kwenda nikiwa nimevaa hivi, kwa sababu sina uzoefu navyo.” Hivyo akavivua. Kisha akachukua fimbo yake mkononi, akachagua mawe laini matano kutoka kwenye kijito, akayaweka kwenye kifuko ndani ya mfuko wake wa kichungaji, akiwa na kombeo yake mkononi mwake, akamkaribia yule Mfilisti.

Wakati ule ule, yule Mfilisti, akiwa na mbeba ngao wake mbele yake, akaendelea kujongea karibu na Daudi. 17:42 1Sam 16:12; Za 123:3-4; Mit 16:18; 1Kor 1:27, 28Mfilisti akamwangalia Daudi kote na kumwona kuwa ni kijana tu, mwekundu na mzuri wa kupendeza, naye akamdharau. 17:43 1Sam 24:14; 2Sam 3:8; 9:8; 2Fal 8:13Akamwambia Daudi, “Je, mimi ni mbwa, hata unanijia na fimbo?” Yule Mfilisti akamlaani Daudi kwa miungu yake. 17:44 Mwa 40:19; Ufu 19:7; 2Sam 21:10; Yer 34:20; 1Fal 20:10-11Tena Mfilisti akamwambia, “Njoo hapa, nami nitawapa ndege wa angani na wanyama wa mwituni nyama yako.”

17:45 Kum 20:1; 2Nya 13:12; 14:11; 32:8; Za 20:7-8; 124:8; Ebr 11:32-34; 2Sam 22:33, 35; 2Nya 32:8; Za 124:8; 125:1; Mit 18:10; Flp 4:13Daudi akamwambia yule Mfilisti. “Wewe unanijia na upanga, mkuki na fumo, lakini mimi ninakujia kwa jina la Bwana Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa majeshi ya Israeli, ambaye wewe umemtukana. 17:46 1Sam 14:12; Kum 28:26; Yos 4; 24; Isa 11:9; 1Fal 18:36; 2Fal 5:8; 19:19; Isa 37:20; Za 44:6-7; Zek 4:6Siku hii leo Bwana atakutia mkononi mwangu, nami nitakupiga na kukukata kichwa chako. Leo nitawapa ndege wa angani na wanyama wa nchi mizoga ya jeshi la Wafilisti, nayo dunia yote itajua kuwa yuko Mungu katika Israeli. 17:47 1Sam 25:29; 2Sam 23:21; Za 44:6, 7; Hos 1:7; Zek 4:6; 2Nya 20:15Wale wote waliokusanyika hapa watajua kuwa Bwana haokoi kwa upanga wala kwa mkuki; kwa kuwa vita ni vya Bwana, naye atawatia wote mikononi mwetu.”

Yule Mfilisti aliposogea karibu ili kumshambulia, Daudi akaenda mbio kuelekea safu ya vita kukutana naye. Daudi akatia mkono wake mfukoni na kuchukua jiwe, akalirusha kwa kombeo, nalo likampiga yule Mfilisti kwenye paji la uso. Lile jiwe likaingia kipajini mwa uso, akaanguka chini kifudifudi.

17:50 Ebr 11:34; 1Sam 21:9; 22:10; Amu 3:31; 15:15; 2Sam 23:21Basi Daudi akamshinda huyo Mfilisti kwa kombeo na jiwe; bila kuwa na upanga mikononi mwake akampiga huyo Mfilisti na kumuua.

17:51 Ebr 11:34Daudi akakimbia na kusimama juu yake. Akaushika upanga wa huyo Mfilisti na kuuvuta toka kwenye ala yake. Baada ya kumuua, akakata kichwa chake kwa ule upanga.

Wafilisti walipoona kuwa shujaa wao amekufa, wakageuka na kukimbia. 17:52 Yos 15:11; 15:36Ndipo watu wa Israeli na Yuda wakainuka kwenda mbele wakipiga kelele na kufuatia Wafilisti mpaka kwenye ingilio la Gathi kwenye malango ya Ekroni. Maiti zao zilitawanyika kando ya barabara ya Shaaraimu hadi Gathi na Ekroni. Waisraeli waliporudi kutoka kuwafukuza Wafilisti, waliteka nyara kutoka kambi yao. Daudi akachukua kichwa cha yule Mfilisti na kukileta Yerusalemu, naye akaweka silaha za huyo Mfilisti katika hema lake mwenyewe.

17:55 1Sam 16:21; 26:5Sauli alipomwona Daudi anakwenda kukabiliana na huyo Mfilisti, alimwambia Abneri, jemadari wa jeshi, “Abneri, yule kijana ni mwana wa nani?”

Abneri akajibu, “Hakika kama uishivyo, ee mfalme, mimi sifahamu.”

Mfalme akasema, “Uliza huyu kijana ni mwana wa nani.”

Mara Daudi aliporudi kutoka kumuua huyo Mfilisti, Abneri akamchukua na kumleta mbele ya Sauli. Daudi alikuwa bado anakishikilia kichwa cha yule Mfilisti.

17:58 Rut 4:17Sauli akamuuliza, “Kijana, wewe ni mwana wa nani?”

Daudi akasema, “Mimi ni mwana wa mtumishi wako Yese wa Bethlehemu.”

Read More of 1 Samweli 17

1 Samweli 18:1-30

Sauli Amwonea Daudi Wivu

18:1 1Sam 19:1; 20:16; 31:2; 2Sam 4:4; 1:26; Mwa 44:30; Kol 2:2; Kum 13:6; 1Sam 20:17; Mit 18:24; Yn 15:17-19; 1Yn 3:12-14Baada ya Daudi kumaliza kuongea na Sauli, roho ya Yonathani ikaambatana na roho ya Daudi, naye akampenda kama nafsi yake mwenyewe. 18:2 1Sam 8:11; 14:52; 17:15Kuanzia siku ile Sauli akamchukua Daudi naye hakumruhusu kurudi nyumbani kwa baba yake. 18:3 1Sam 20:8, 16, 17, 42; 22:8; 23:18; 24:21; 2Sam 21:7Yonathani akafanya agano na Daudi kwa sababu alimpenda kama nafsi yake mwenyewe. 18:4 Mwa 41:42; 2Sam 18:11Yonathani akavua joho alilokuwa amevaa na kumpa Daudi, pamoja na koti lake, silaha zake, hata pamoja na upanga wake, upinde wake na mshipi wake.

18:5 2Sam 5:2Lolote Sauli alilomtuma Daudi kufanya, alitenda kwa hekima, hata Sauli akampa cheo cha juu katika jeshi. Jambo hili likawapendeza watu wote, hata maafisa wa Sauli pia.

18:6 Kut 15:20; 2Sam 1:20; Za 68:25; Amu 11:34; Yer 31:4Watu walipokuwa wanarudi nyumbani baada ya Daudi kumuua yule Mfilisti, wanawake wakaja kutoka pande zote za miji ya Israeli kumlaki Mfalme Sauli kwa kuimba na kucheza, kwa nyimbo za furaha na kwa matari na zeze.

18:7 Kut 15:21; 1Sam 21:11; 29:5; 2Sam 18:3; Amu 5:3; 2Nya 5:13; Za 24:1-10; Isa 5:1Walipokuwa wanacheza, wakaimba:

“Sauli amewaua elfu zake,

naye Daudi makumi elfu yake.”

18:8 1Sam 13:14; 15:8; Mhu 4:4Sauli akakasirika sana; sehemu hii ya kurudia rudia ya wimbo huu ilimkasirisha sana. Akafikiri kuwa, “Wamempa Daudi makumi elfu, lakini mimi wamenipa elfu tu. Apate nini zaidi isipokuwa ufalme?” 18:9 Mwa 4:5; 31:2, 5; Mt 20:15; Lk 15:28Kuanzia wakati ule na kuendelea Sauli akawa na jicho la wivu juu ya Daudi.

18:10 Amu 9:23; 1Sam 16:14; 10:5; 16:21; 19:7; 17; 6; 1Fal 18:29; Mdo 16:16Kesho yake roho mbaya iliyoachiwa nafasi na Mungu ikaja kwa nguvu juu ya Sauli. Alikuwa akitabiri nyumbani mwake, wakati Daudi alikuwa akipiga kinubi, kama alivyozoea. Sauli alikuwa na mkuki mkononi mwake; 18:11 1Sam 20:7, 33; 19:10; Za 132:1akautupa kwa nguvu, akijiambia mwenyewe, “Nitamchoma kwa mkuki abaki hapo ukutani.” Lakini Daudi akamkwepa mara mbili.

18:12 1Sam 16:13; Yos 1:5; 1Sam 17:37; 20:13; 1Nya 22:11; Amu 16:20Sauli akamwogopa Daudi, kwa sababu Bwana alikuwa pamoja na Daudi, lakini alikuwa amemwacha yeye. 18:13 Hes 27:17; 2Sam 5:2Kwa hiyo Sauli akamwondoa Daudi mbele yake na kumpa kuwa kiongozi wa watu elfu moja, naye Daudi akatoka na kuingia akiongoza vikosi katika vita. 18:14 Mwa 39:2, 3; Hes 14:43; 2Sam 7:9; Yos 6:27Katika kila kitu alichofanya, Daudi alipata mafanikio makubwa, kwa sababu Bwana alikuwa pamoja naye. Sauli alipoona jinsi alivyokuwa akifanikiwa, akamwogopa. 18:16 2Sam 5:2Lakini Israeli wote na Yuda walimpenda Daudi, kwa sababu ndiye alikuwa akiwaongoza katika vita vyao.

18:17 1Sam 17:25; Mwa 29:26; Hes 21:14; 1Sam 20:33; 25:28Sauli akamwambia Daudi, “Huyu hapa binti yangu mkubwa Merabu. Nitakupa umwoe, endapo tu utanitumikia kwa ushujaa na kupigana vita vya Bwana.” Kwa maana Sauli alisema moyoni mwake, “Sitainua mkono wangu dhidi yake. Acha mkono wa Wafilisti uwe juu yake.”

18:18 Kut 3:11; 1Sam 9:21; 2Sam 7:18; Rut 2:10; Mit 15:33Lakini Daudi akamwambia Sauli, “Mimi ni nani, nayo jamaa yangu ni nini au ukoo wa baba yangu katika Israeli, kwamba mimi niwe mkwewe mfalme?” 18:19 2Sam 21:8; Amu 7:22Basi ulipofika wakati wa Daudi kupewa Merabu, binti Sauli, huyo binti aliozwa kwa Adrieli, Mmeholathi.

18:20 Mwa 29:26Basi Mikali binti Sauli alimpenda Daudi, nao walipomwambia Sauli juu ya jambo hili, likampendeza. 18:21 Kut 10:7; 7:16; Za 7:14-16; Mit 26:24-26; Yer 5:26; 9:8Sauli akawaza, “Nitampa Daudi binti yangu, ili apate kuwa mtego kwake, ili kwamba mkono wa Wafilisti upate kuwa juu yake.” Hivyo Sauli akamwambia Daudi, “Sasa unayo nafasi ya pili ya kuwa mkwe wangu.”

Ndipo Sauli akawaagiza watumishi wake, akisema, “Zungumzeni na Daudi kwa siri na kumwambia, ‘Tazama, mfalme amependezwa nawe, nao watumishi wake wote wanakupenda. Basi na uwe mkwewe mfalme.’ ”

Watumishi wa Sauli wakarudia hayo maneno kwa Daudi. Lakini Daudi akasema, “Je, mnafikiri ni jambo dogo kuwa mkwewe mfalme? Mimi ni mtu maskini tu, na nisiyejulikana sana.”

Watumishi wa Sauli walipomweleza yale Daudi aliyoyasema, 18:25 Mwa 34:12; Za 8:2; 44:16; Yer 20:10; Kut 22:17Sauli akajibu, “Mwambieni Daudi, ‘Mfalme hataki zawadi nyingine kuwa mahari isipokuwa magovi 100 ya Wafilisti, ili kulipiza kisasi juu ya adui zake.’ ” Mawazo ya Sauli yalikuwa Daudi akaanguke mikononi mwa Wafilisti.

Watumishi walipomwambia Daudi mambo haya, ikampendeza kuwa mkwewe mfalme. Basi kabla siku iliyopangwa haijafika, 18:27 2Sam 3:14; 6:16Daudi na watu wake walitoka na kuwaua Wafilisti mia mbili. Akayaleta magovi yao na kupeleka hesabu kamilifu kwa mfalme, ili kwamba apate kuwa mkwewe mfalme. Ndipo Sauli akamwoza Daudi Mikali binti yake.

Sauli alipotambua kuwa Bwana alikuwa pamoja na Daudi na kwamba Mikali binti yake anampenda Daudi, 18:29 1Sam 18:20; Mhu 4:4; Yak 2:13Sauli akazidi kumwogopa Daudi, naye Sauli akabaki kuwa adui yake siku zote za maisha yake.

18:30 1Sam 11:1; Lk 21:15Majemadari wa jeshi la Wafilisti waliendelea kupigana vita na kadiri walivyoendelea kupigana, Daudi akazidi kutenda kwa hekima kuliko maafisa wengine wa Sauli, nalo jina lake likajulikana sana.

Read More of 1 Samweli 18