1 Yohana 1:1-10, 1 Yohana 2:1-29 NEN

1 Yohana 1:1-10

Neno La Uzima

1:1 Yn 1:2; 2Pet 1:16; Yn 20:27Tunawajulisha lile lililokuwepo tangu mwanzo, lile tulilosikia, ambalo tumeliona kwa macho yetu, ambalo tumelitazama na kuligusa kwa mikono yetu, kuhusu Neno la uzima. 1:2 Yn 14:6; 1Pet 1:20Uzima huo ulidhihirishwa; nasi tumeuona na kuushuhudia, nasi twawatangazia uzima wa milele, ambao ulikuwa pamoja na Baba, nao ukadhihirishwa kwetu. 1:3 1Kor 1:9; 1Yn 1:1; Mdo 4:20; Yn 17:21; 1Yn 2:24Twawatangazia lile tuliloliona na kulisikia, ili nanyi mwe na ushirika nasi. Na ushirika wetu hasa ni pamoja na Baba na Mwanawe, Yesu Kristo. Tunaandika mambo haya ili furaha yetu ipate kuwa timilifu.

Kutembea Nuruni

1:5 1Yn 3:11; 2Yn 12Huu ndio ujumbe tuliosikia kutoka kwake na kuwatangazia ninyi: kwamba Mungu ni nuru na ndani yake hamna giza lolote. 1:6 Efe 5:8; 1Yn 4:20Kama tukisema kwamba twashirikiana naye huku tukienenda gizani, twasema uongo, wala hatutendi lililo kweli. 1:7 Ufu 7:14; Ebr 9:14; Ufu 1:5Lakini tukienenda nuruni, kama yeye alivyo nuruni, twashirikiana sisi kwa sisi na damu yake Yesu, Mwana wake, yatusafisha dhambi yote.

1:8 Yer 2:35; Yn 8:44Kama tukisema kwamba hatuna dhambi, twajidanganya wenyewe wala kweli haimo ndani yetu. 1:9 Mit 28; 13; Za 32:5; 51:2; Mit 28:13; 1Yn 1:7; Mik 7:18-20; Ebr 10:22Kama tukiziungama dhambi zetu, yeye ni mwaminifu na wa haki, atatusamehe dhambi zetu na kutusafisha kutoka kwenye udhalimu wote. 1:10 1Yn 5:10; Yn 5:38; 1Yn 1:8; 5:10; Yn 5:38; 2:15Kama tukisema hatukutenda dhambi, twamfanya yeye kuwa mwongo na neno lake halimo ndani yetu.

Read More of 1 Yohana 1

1 Yohana 2:1-29

Kristo Mwombezi Wetu

2:1 1The 2:11; Ebr 7:25; 1Tim 2:5Watoto wangu wapendwa, nawaandikia haya ili msitende dhambi. Lakini kama mtu yeyote akitenda dhambi, tunaye Mwombezi kwa Baba: ndiye Yesu Kristo, Mwenye Haki. 2:2 1Yn 4:10; Rum 3:25; Mt 1:21; Yn 3:17Yeye ndiye dhabihu ya upatanisho kwa ajili ya dhambi zetu, wala si kwa ajili ya dhambi zetu tu, bali pia kwa ajili ya dhambi za ulimwengu wote.

2:3 Yn 14:15; 1Yn 2:5; 3:24; 4:13; 5:2; 2:4Basi katika hili twajua ya kuwa tumemjua, tukizishika amri zake. 2:4 1Yn 1:6, 8; 2:3; Tit 1:16; 1Yn 3:6; 4:7, 8Mtu yeyote asemaye kuwa, “Ninamjua,” lakini hazishiki amri zake, ni mwongo, wala ndani ya mtu huyo hamna kweli. 2:5 Yn 14:15, 21, 23; 1Yn 4:12Lakini mtu yeyote anayelitii neno lake, upendo wa Mungu umekamilika ndani yake kweli kweli. Katika hili twajua kuwa tumo ndani yake. 2:6 Mt 11:29; 2Pet 2:21Yeyote anayesema anakaa ndani yake hana budi kuenenda kama Yesu alivyoenenda.

Amri Mpya

2:7 1Kor 10:14; 1Yn 2:24; 3:11, 23; 4:2Wapendwa, siwaandikii ninyi amri mpya bali ile ya zamani, ambayo mmekuwa nayo tangu mwanzo. Amri hii ya zamani ni lile neno mlilosikia. 2:8 Yn 13:34; Ebr 10:25; Yn 1:9; Efe 5:8; 1The 5:5Lakini nawaandikia amri mpya, yaani, lile neno lililo kweli ndani yake na ndani yenu, kwa sababu giza linapita na ile nuru ya kweli tayari inangʼaa.

2:9 1Yn 2:11; Law 19:17; 1Yn 3:10; 4:20, 21; 1:5Yeyote anayesema yumo nuruni lakini anamchukia ndugu yake bado yuko gizani. 2:10 1Yn 3:14; 2:11; Za 119:165; Rum 14:13, 15; Yn 11:9Yeye ampendaye ndugu yake anakaa nuruni, wala hakuna kitu chochote ndani yake cha kumkwaza. 2:11 Yn 11:9; 11:10; 12:35; 1Yn 1:6; Yn 12:35Lakini yeyote amchukiaye ndugu yake, yuko gizani na anaenenda gizani, wala hajui anakokwenda, kwa sababu giza limempofusha macho.

2:12 1Yn 2:9; 3:23Nawaandikia ninyi, watoto wadogo,

kwa sababu dhambi zenu

zimesamehewa kwa ajili ya Jina lake.

2:13 Mt 5:37; Yn 1:1; 16:33; 1Yn 2:14; 2:13Nawaandikia ninyi, akina baba,

kwa sababu mmemjua

yeye aliye tangu mwanzo.

Nawaandikia ninyi vijana

kwa sababu mmemshinda yule mwovu.

Nawaandikia ninyi watoto wadogo,

kwa sababu mmemjua Baba.

2:14 Efe 6:10; Yn 5:38; 1Yn 1:10Nawaandikia ninyi akina baba,

kwa sababu mmemjua

yeye aliye tangu mwanzo.

Nawaandikia ninyi vijana,

kwa sababu mna nguvu,

na neno la Mungu linakaa ndani yenu,

nanyi mmemshinda yule mwovu.

Msiupende Ulimwengu

2:15 Rum 12:2; Yak 4:4Msiupende ulimwengu wala mambo yaliyo ulimwenguni. Kama mtu yeyote akiupenda ulimwengu, upendo wa Baba haumo ndani yake. 2:16 Efe 2:8; Mit 27:20Kwa maana kila kitu kilichomo ulimwenguni, yaani tamaa ya mwili, tamaa ya macho na kiburi cha uzima, havitokani na Baba bali hutokana na ulimwengu. 2:17 Ebr 12:27; Mt 12:50; 1Kor 7:31; Yak 1:10; 4:14; 1Pet 1:24Nao ulimwengu unapita, pamoja na tamaa zake, bali yeye afanyaye mapenzi ya Mungu adumu milele.

Onyo Dhidi Ya Wapinga Kristo

2:18 1Yn 4:1; 2Yn 7Watoto wadogo, huu ni wakati wa mwisho! Kama mlivyosikia kwamba mpinga Kristo anakuja, hivyo basi wapinga Kristo wengi wamekwisha kuja. Kutokana na hili twajua kwamba huu ni wakati wa mwisho. 2:19 Mk 1:24; Yer 31:34Walitoka kwetu, lakini hawakuwa wa kwetu hasa. Kwa maana kama wangelikuwa wa kwetu, wangelikaa pamoja nasi, lakini kutoka kwao kulionyesha kwamba hakuna hata mmoja wao aliyekuwa wa kwetu.

2:20 1Yn 2:27; 2Kor 1:21; Mk 1:24; Yer 31:34; Mt 13:11; Yn 14:26Lakini ninyi mmetiwa mafuta na yeye Aliye Mtakatifu, nanyi nyote mnaijua kweli. 2:21 2Pet 1:12; Yud 5Siwaandikii kwa sababu hamuijui kweli, bali kwa sababu mnaijua, nanyi mnajua hakuna uongo utokao katika kweli. 2:22 1Yn 4:13; 2Yn 7Je, mwongo ni nani? Mwongo ni mtu yule asemaye kwamba Yesu si Kristo. Mtu wa namna hiyo ndiye mpinga Kristo, yaani, yeye humkana Baba na Mwana. 2:23 Yn 14:7; 2Yn 9Hakuna yeyote amkanaye Mwana aliye na Baba. Yeyote anayemkubali Mwana anaye na Baba pia.

2:24 2Yn 9Hakikisheni kwamba lile mlilosikia tangu mwanzo linakaa ndani yenu. Kama lile mlilosikia tangu mwanzo linakaa ndani yenu, ninyi nanyi mtakaa ndani ya Mwana na ndani ya Baba. 2:25 Mt 25:46; Yn 17:3; 1Yn 1:2; 5:11Hii ndiyo ahadi yake kwetu, yaani, uzima wa milele.

2:26 1Yn 3:7; 2Yn 7Nawaandikia mambo haya kuhusu wale watu ambao wanajaribu kuwapotosha. 2:27 1Yn 2:20; Yer 31:33, 34; Ebr 8:10, 11; Yn 14:26; 16:13Nanyi, upako mlioupata kutoka kwake unakaa ndani yenu, wala ninyi hamna haja ya mtu yeyote kuwafundisha. Lakini kama vile upako wake unavyowafundisha kuhusu mambo yote nayo ni kweli wala si uongo, basi kama ulivyowafundisha kaeni ndani yake.

Watoto Wa Mungu

2:28 Kol 3:4; 1Yn 3:2; Efe 3:12; 1The 2:19Sasa basi, watoto wapendwa, kaeni ndani yake, ili atakapofunuliwa, tuwe na ujasiri, wala tusiaibike mbele zake wakati wa kuja kwake.

2:29 1Yn 3:7; Mdo 22:14; Yn 1:13Kama mkijua kuwa yeye ni mwenye haki, mwajua kwamba kila atendaye haki amezaliwa naye.

Read More of 1 Yohana 2