1 Wakorintho 12:1-26 NEN

1 Wakorintho 12:1-26

Karama Za Rohoni

12:1 Rum 1:11; 1Kor 1:7; 14:1, 37; Rum 11:25Basi ndugu zangu, kuhusu karama za rohoni, sitaki mkose kufahamu. 12:2 Efe 2:2; Za 115:5; Yer 10:5; Hab 2:18-19Mnajua kwamba mlipokuwa watu wasiomjua Mungu, kwa njia moja au ingine mlishawishika na kupotoshwa mkielekezwa kwa sanamu zisizonena. 12:3 Rum 9:3; 1Kor 16:22; Yn 13:13; 4:2-3Kwa hiyo nawaambieni ya kuwa hakuna mtu anayeongozwa na Roho wa Mungu anayeweza kusema, “Yesu na alaaniwe.” Pia hakuna mtu awezaye kusema, “Yesu ni Bwana,” isipokuwa ameongozwa na Roho Mtakatifu.

12:4 Rum 12:4-8; Efe 4:11; Ebr 2:4Kuna aina mbalimbali za karama, lakini Roho ni yule yule. 12:5 Rum 12:6; Efe 4:11Kuna huduma za aina mbalimbali, lakini Bwana ni yule yule. 12:6 Efe 4:6; Flp 2:13; Efe 1:23Kisha kuna tofauti za kutenda kazi, lakini ni Mungu yule yule atendaye kazi zote kwa watu wote.

12:7 1Kor 14:12; Efe 4:12Basi kila mmoja hupewa ufunuo wa Roho kwa faida ya wote. 12:8 1Kor 2:6; 2Kor 8:7Maana mtu mmoja kwa Roho hupewa neno la hekima na mwingine neno la maarifa kwa Roho huyo huyo. 12:9 Mt 17:19-20; 1Kor 13:2; Mt 10:1Mtu mwingine imani kwa huyo Roho na mwingine karama za kuponya kwa huyo Roho mmoja. 12:10 Gal 3:5; Efe 4:11; 1Yn 4:1; Mk 16:17Kwa mwingine matendo ya miujiza, kwa mwingine unabii kwa mwingine kupambanua roho, kwa mwingine aina mbalimbali za lugha, na kwa mwingine bado, tafsiri za lugha. 12:11 1Kor 11:4; Rum 12:3; Efe 4:7; 1Kor 7:7Haya yote hufanywa na huyo huyo Roho mmoja, Roho naye humgawia kila mtu, kama apendavyo.

Mwili Mmoja, Wenye Viungo Vingi

12:12 Rum 12:5; 1Kor 11:27Kama vile mwili ulivyo mmoja nao una viungo vingi, navyo viungo vyote vya mwili ingawa ni vingi, ni mwili mmoja, vivyo hivyo na Kristo. 12:13 Efe 2:18; Gal 3:28; Kol 3:11; Yn 7:37-38Kwa maana katika Roho mmoja wote tulibatizwa katika mwili mmoja, kama ni Wayahudi au Wayunani, kama ni watumwa au watu huru, nasi sote tulinyweshwa Roho mmoja.

12:14 1Kor 12:12, 20Basi mwili si kiungo kimoja, bali ni viungo vingi. Kama mguu ungesema, “Kwa kuwa mimi si mkono basi mimi si wa mwili,” hiyo isingefanya huo mguu usiwe sehemu ya mwili. Na kama sikio lingesema, “Kwa kuwa mimi si jicho, basi mimi si wa mwili,” hiyo isingefanya hilo sikio lisiwe sehemu ya mwili. Kama mwili wote ungelikuwa jicho, kusikia kungekuwa wapi? Au kama mwili wote ungelikuwa sikio, kunusa kungekuwa wapi? 12:18 1Kor 12:28; 12:11Lakini kama ilivyo, Mungu ameweka viungo katika mwili, kila kimoja kama alivyopenda. Kama vyote vingekuwa kiungo kimoja, mwili ungekuwa wapi? Kama ulivyo, una viungo vingi, lakini mwili ni mmoja.

Jicho haliwezi kuuambia mkono, “Sina haja nawe!” Wala kichwa hakiwezi kuiambia miguu, “Sina haja na ninyi!” Lakini badala yake, vile viungo vya mwili vinavyoonekana kuwa dhaifu, ndivyo ambavyo ni vya muhimu sana. Navyo vile viungo tunavyoviona havina heshima, ndivyo tunavipa heshima maalum. Vile viungo vya mwili ambavyo havina uzuri, tunavipa heshima ya pekee; wakati vile viungo vyenye uzuri havihitaji utunzaji wa pekee. Lakini Mungu ameviweka pamoja viungo vya mwili na akavipa heshima zaidi vile vilivyopungukiwa, ili pasiwe na mafarakano katika mwili, bali viungo vyote vihudumiane kwa usawa kila kimoja na mwenzake. Kama kiungo kimoja kikiumia, viungo vyote huumia pamoja nacho, kama kiungo kimoja kikipewa heshima, viungo vyote hufurahi pamoja nacho.

Read More of 1 Wakorintho 12