1 Nyakati 1:1-54, 1 Nyakati 2:1-17 NEN

1 Nyakati 1:1-54

Kumbukumbu Za Historia Kuanzia Adamu Hadi Abrahamu

(Mwanzo 5:1-32; 10:1-32; 11:10-26)

Adamu Hadi Wana Wa Noa

1:1 Mwa 5:1-32; Lk 3:36-38Adamu, Sethi, Enoshi, 1:2 Mwa 5:9; 5:12; 5:15Kenani, Mahalaleli, Yaredi, 1:3 Mwa 5:18; Yud 14; Mwa 5:21; 5:25; 5:29Enoki, Methusela, Lameki, Noa.

1:4 Mwa 6:10; 10:1; 5:32Wana wa Noa walikuwa:

Shemu, Hamu na Yafethi.

Wana Wa Yafethi

Wana wa Yafethi walikuwa:

Gomeri, Magogu, Madai, Yavani, Tubali, Mesheki na Tirasi.

Wana wa Gomeri walikuwa:

Ashkenazi, Rifathi na Togarma.

Wana wa Yavani walikuwa:

Elisha, Tarshishi, Kitimu na Rodanimu.

Wana Wa Hamu

1:8 Mwa 16:10Wana wa Hamu walikuwa:

Kushi, Misraimu,1:8 Yaani Misri. Putu na Kanaani.

Wana wa Kushi walikuwa:

Seba, Havila, Sabta, Raama na Sabteka.

Wana wa Raama walikuwa:

Sheba na Dedani.

1:10 Mwa 10:8, 13Kushi akamzaa

Nimrodi, ambaye alikua akawa mtu shujaa katika nchi.

Misraimu akawazaa:

Waludi, Waanami, Walehabi, Wanaftuhi, 1:12 Mwa 10:14; Kum 2:23; Yer 47:4; Amo 9:7Wapathrusi, Wakasluhi (hao ndio asili ya Wafilisti) na Wakaftori.

Wana wa Kanaani walikuwa:

Sidoni, mzaliwa wake wa kwanza, na Hethi, Wayebusi, Waamori, Wagirgashi, Wahivi, Waariki, Wasini, Waarvadi, Wasemari na Wahamathi.

Wana Wa Shemu

1:17 Mwa 9:23-26; 10:22; 11:10Wana wa Shemu walikuwa:

Elamu, Ashuru, Arfaksadi, Ludi na Aramu.

Wana wa Aramu walikuwa:

Usi, Huli, Getheri na Mesheki.

Arfaksadi akamzaa Shela,

Shela akamzaa Eberi.

Eberi alipata wana wawili:

Mmoja wao aliitwa Pelegi,1:19 Pelegi maana yake Mgawanyiko. kwa kuwa wakati wake dunia iligawanyika; nduguye aliitwa Yoktani.

Wana wa Yoktani walikuwa:

Almodadi, Shelefu, Hasarmawethi, Yera, Hadoramu, Uzali, Dikla, Obali, Abimaeli, Sheba, Ofiri, Havila na Yobabu. Wote hawa walikuwa wana wa Yoktani.

1:24 Mwa 10:21-29; Lk 3:34-36Wana wa Shemu walikuwa Arfaksadi, Shela,

1:25 Mwa 11:15; Hes 24:24; Lk 3:35Eberi, Pelegi, Reu,

Serugi, Nahori, Tera,

1:27 Mwa 17:5; 2Nya 20:7; Isa 41:8; 51:2; Rum 4:16Tera akamzaa Abramu (yaani, Abrahamu).

Jamaa Ya Abrahamu

1:28 Mwa 21:2-3; 16:11, 15Abrahamu alikuwa na wana wawili:

Isaki na Ishmaeli.

Wazao Wa Hagari

(Mwanzo 25:12-16)

1:29 Mwa 25:13-26Hawa ndio waliokuwa wazao wa Hagari:

Nebayothi mzaliwa wa kwanza wa Ishmaeli, Kedari, Adbeeli, Mibsamu, Mishma, Duma, Masa, Hadadi, Tema, Yeturi, Nafishi na Kedema. Hao ndio wana wa Ishmaeli.

Wazao Wa Ketura

1:32 Mwa 22:24; 10:7Wana waliozaliwa na Ketura suria wa Abrahamu walikuwa:

Zimrani, Yokshani, Medani, Midiani, Ishbaki na Shua.

Wana wa Yokshani walikuwa:

Sheba na Dedani.

Wana wa Midiani walikuwa:

Efa, Eferi, Hanoki, Abida na Eldaa.

Wote hao walikuwa wa uzao wa Ketura.

Wazao Wa Sara

1:34 Lk 3:34; Mwa 21:2-3; Mdo 7:8; Mwa 18:5; 25:25-26Abrahamu alikuwa baba wa Isaki.

Wana wa Isaki walikuwa:

Esau na Israeli.

Wana Wa Esau

(Mwanzo 36:1-19)

1:35 Mwa 36:19; 36:4; Kum 2:22; Rum 9:13; Ebr 12:16; Mal 1:2-3Wana wa Esau walikuwa:

Elifazi, Reueli, Yeushi, Yalamu na Kora.

1:36 Kut 17:14; Mwa 36:11Wana wa Elifazi walikuwa:

Temani, Omari, Sefo, Gatamu na Kenazi;

Elifazi kwa Timna akamzaa Amaleki.

1:37 Mwa 36:17Wana wa Reueli walikuwa:

Nahathi, Zera, Shama na Miza.

Watu Wa Seiri Waliokuwa Edomu

(Mwanzo 36:20-30)

1:38 Mwa 36:20Wana wa Seiri walikuwa:

Lotani, Shobali, Sibeoni, Ana, Dishoni, Eseri na Dishani.

1:39 Mwa 36:22Wana wa Lotani walikuwa wawili:

Hori na Homamu. Lotani alikuwa na dada yake aliyeitwa Timna.

1:40 Mwa 36:2Wana wa Shobali walikuwa:

Alvani,1:40 Maandishi ya Kiebrania yanamwita Alian. Manahathi, Ebali, Shefo na Onamu.

Wana wa Sibeoni walikuwa:

Aiya na Ana.

1:41 Mwa 36:25-26Mwana wa Ana alikuwa:

Dishoni.

Nao wana wa Dishoni walikuwa:

Hemdani, Eshbani, Ithrani na Kerani.

Wana wa Eseri walikuwa:

Bilhani, Zaavani na Akani.

Wana wa Dishani walikuwa:

Usi na Arani.

Watawala Wa Edomu

(Mwanzo 36:31-43)

1:43 Mwa 36:31; 49:10Hawa ndio wafalme waliotawala Edomu kabla hajatawala mfalme yeyote wa Waisraeli:

Bela mwana wa Beori, ambaye mji wake ni Dinhaba.

Bela alipofariki, Yobabu mwana wa Zera kutoka Bosra akawa mfalme baada yake.

1:45 Mwa 36:11Yobabu alipofariki, Hushamu kutoka nchi ya Watemani akawa mfalme baada yake.

1:46 1Fal 11:14Hushamu alipofariki, Hadadi mwana wa Bedadi, aliyeshinda Midiani katika nchi ya Moabu, akawa mfalme baada yake. Mji wake uliitwa Avithi.

Hadadi alipofariki, Samla kutoka Masreka akawa mfalme baada yake.

1:48 Mwa 36:37Samla alipofariki, Shauli kutoka Rehobothi ngʼambo ya Mto Frati, akawa mfalme baada yake.

Shauli alipofariki, Baal-Hanani mwana wa Akbori akawa mfalme baada yake.

1:50 Mwa 36:39Baal-Hanani alipofariki, Hadadi akawa mfalme baada yake. Mji wake uliitwa Pau, na mkewe aliitwa Mehetabeli binti Matredi, binti Me-Zahabu. 1:51 Mwa 36:40; Kut 15:15Naye Hadadi pia akafa.

Wakuu wa Edomu walikuwa:

Timna, Alva, Yethethi, Oholibama, Ela, Pinoni, Kenazi, Temani, Mibsari, Magdieli na Iramu. Hao ndio wakuu wa makabila ya Edomu.

Read More of 1 Nyakati 1

1 Nyakati 2:1-17

Wana Wa Israeli

2:1 Mwa 32:28; 35:10; Kut 32:13; Hes 1:5-15; 13:4-15; Mwa 29:32; 1Fal 18:31Hawa ndio waliokuwa wana wa Israeli:

Reubeni, Simeoni, Lawi, Yuda, Isakari, Zabuloni, Dani, Yosefu, Benyamini, Naftali, Gadi na Asheri.

Yuda

Hadi Wana Wa Hesroni

2:3 Mwa 29:35; 38:2; Hes 26:19Wana wa Yuda walikuwa:

Eri, Onani na Shela. Hawa watatu walizaliwa kwake na mkewe Mkanaani, binti wa Shua. Eri, mzaliwa wa kwanza wa Yuda, alikuwa mwovu machoni pa Bwana, kwa hiyo Bwana alimuua. 2:4 Mwa 38:11-30; 11:31; 38:29Tamari, mkwewe Yuda, alimzalia wana wawili: Peresi na Zera. Yuda alikuwa na jumla ya wana watano.

2:5 Mwa 46:12; Hes 26:21; Rut 4:18Wana wa Peresi walikuwa:

Hesroni na Hamuli.

2:6 1Fal 4:31Wana wa Zera walikuwa:

Zimri, Ethani, Hemani, Kalkoli na Dara. Jumla ya wana wa Zera walikuwa watano.

2:7 Yos 7:1; 6:18; 1Nya 4:1Mwana wa Karmi alikuwa:

Akari,2:7 Akari maana yake Taabisha; pia anaitwa Akani (Yos 6:1-26; 22:20). ambaye alileta taabu kwa Waisraeli kwa kukiuka onyo la kutokuchukua vitu vilivyokuwa vimewekwa wakfu.

Mwana wa Ethani alikuwa:

Azariya.

2:9 Hes 26:21Wana wa Hesroni walikuwa:

Yerameeli, Ramu na Kalebu.

Kuanzia Ramu Mwana Wa Hesroni

2:10 Lk 3:32-33; Kut 6:23; Hes 1:7; Rut 4:19Ramu alimzaa

Aminadabu, na Aminadabu akamzaa Nashoni, kiongozi wa kabila la Yuda. Nashoni akamzaa Salmoni, Salmoni akamzaa Boazi, 2:12 Rut 2:1; 4:17Boazi akamzaa Obedi, Obedi akamzaa Yese.

2:13 Rut 4:17; Isa 16:6Yese akawazaa

Eliabu mwanawe wa kwanza; wa pili Abinadabu, wa tatu Shimea,2:13 Au: Shima, maana yake Sifa njema (pia 1Sam 16:9; 17:13). wa nne Nethaneli, wa tano Radai, wa sita Osemu, na wa saba Daudi. 2:16 1Sam 26:6; 2Sam 2:18; 2:13Dada zao walikuwa Seruya na Abigaili. Wana wa Seruya walikuwa watatu: Abishai, Yoabu na Asaheli. 2:17 2Sam 17:25Abigaili alikuwa mama yake Amasa, ambaye baba yake alikuwa Yetheri, Mwishmaeli.

Read More of 1 Nyakati 2