Neno: Bibilia Takatifu

Waefeso 1

1Kutoka kwa Paulo, mtume wa Kristo Yesu kwa mapenzi ya Mungu. Kwa watu wa Mungu walio waaminifu kwa Kristo Yesu. Nawa takieni neema ya Mungu na amani kutoka kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwana wetu Yesu Kristo. Asifiwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo ambaye ametu bariki sisi kwa kila baraka za kiroho zitokazo mbinguni tukiwa ndani ya Kristo. Mungu alituchagua sisi tuwe ndani ya Kristo hata kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu, ili tuwe watakatifu, watu wasio na lawama mbele zake. Kwa upendo wake, alipanga kabla ya mambo yote, kutufanya sisi kuwa watoto wake kwa njia ya Yesu Kristo kwa mapenzi yake mwenyewe; na hivyo apewe sifa kwa ajili ya neema yake tukufu ambayo tumepewa bure katika Mpendwa wake. Kutoka kwake, tunapata ukombozi kwa ajili ya damu yake, yaani, kusamehewa dhambi zetu; kulingana na wingi wa neema yake ambayo ametumiminia kwa wingi. Kwa maana ametufahamisha kwa hekima yote na ufahamu, siri ya mapenzi yake, kulingana na mpango aliokusudia kuukamilisha kwa njia ya Kristo. 10 Mpango huo ambao ungetekelezwa wakati ukitimia, ni kwamba Mungu ataviunganisha vitu vyote po pote vilipo, mbinguni na duniani, viwe kwake chini ya Kristo. 11 Tukiwa ndani ya Kristo, tulichaguliwa kama alivy opanga Mungu kwa makusudio yake yeye ambaye hufanya mambo yote kulingana na mapenzi yake. 12 Kwa njia hiyo, sisi ambao tulikuwa wa kwanza kumtegemea Kristo, tupate kuishi maisha yatakayoleta sifa kwa utukufu wake. 13 Ninyi pia mliingia ndani ya Kristo mliposikia neno la kweli, Injili ya wokovu wenu. Nanyi mmemwa mini, mkawekewa muhuri na Roho Mtakatifu ambaye mliahidiwa, 14 yeye ndiye dhamana ya urithi wetu mpaka hapo tutakapoupokea, kwa sifa ya utukufu wake. Shukrani Na Maombi

15 Hii ndio sababu nilipopata habari za imani yenu katika Bwana wetu Yesu, na juu ya upendo mlio nao kwa watu wa Mungu, 16 sijaacha kumshukuru Mungu kwa ajili yenu, na kuwakumbuka katika sala zangu. 17 Nazidi kumwomba Mungu wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba wa utukufu, awajalieni roho ya hekima na ya mafunuo mpate kumfahamu zaidi. 18 Ninaomba pia kwamba macho ya mioyo yenu yaangaziwe ili mpate kujua tumaini mliloitiwa, na mtambue utajiri wa urithi wa utukufu wake kwa watu wa Mungu; 19 na muu fahamu uweza wake usiopimika ambao ametupa sisi tunaoamini. Uweza huo ni sawa na ile nguvu kuu 20 ambayo aliitumia alipomfufua Kristo kutoka kwa wafu, akamweka akae mkono wake wa kulia katika enzi yake mbinguni. 21 Hapo alipo ni juu sana, kupita tawala na mamlaka zote na nguvu zote na milki, na kupita cheo cho chote kinachoweza kutolewa, si tu katika nyakati hizi, bali pia katika nyakati zijazo. 22 Na Mungu ameweka vitu vyote viwe chini ya mamlaka yake na akamteuwa awe mkuu wa vitu vyote kwa ajili ya kanisa, 23 ambalo ni mwili wake, nalo limejawa na yeye ambaye hujaza kila kitu kwa kila njia. Tumefanywa Kuwa Hai Ndani Ya Kristo

Chinese Contemporary Bible (Traditional)

以弗所書 1

1我是奉上帝旨意作基督耶穌使徒的保羅,寫信給以弗所忠於基督耶穌的眾聖徒。

願我們的父上帝和主耶穌基督賜給你們恩典和平安!

基督徒的屬靈恩福

讚美我們主耶穌基督的父上帝!祂在基督裡賜給了我們天上各樣屬靈的恩福。 早在創造世界以前,祂已經在基督裡揀選了我們,使我們在祂眼中成為聖潔無瑕的人。

上帝因為愛我們,就按照祂自己美好的旨意,預定我們藉著耶穌基督得到作祂兒女的名分。 我們讚美祂奇妙無比的恩典,這恩典是上帝藉著祂的愛子賜給我們的。 我們藉著祂愛子的血蒙救贖,過犯得到赦免,這都是出於祂的洪恩。 上帝用各種智慧和聰明把這恩典豐豐富富地賜給我們, 照著祂在基督裡所定的美好計劃叫我們知道祂旨意的奧祕, 10 等所定的時候一到,叫天地萬物一同歸在基督的名下。

11 我們也在基督裡被揀選成為祂的子民。這都是按自己旨意行萬事的上帝預先定下的計劃, 12 好讓我們這些首先在基督裡得到盼望的人都來頌讚祂的榮耀。

13 你們聽過真理之道,就是那使你們得救的福音,而且也信了基督。你們既然信祂,就領受了上帝應許賜下的聖靈為印記。 14 聖靈是我們領受產業的擔保,直到上帝的子民得到救贖,使祂的榮耀受到頌讚。

保羅的禱告

15 我聽到你們對主耶穌的信心和對眾聖徒的愛心後, 16 不斷地為你們感謝上帝,禱告的時候常常提到你們。 17 我求我們主耶穌基督的上帝——榮耀的父把賜智慧和啟示的靈給你們,好使你們更深地認識祂。 18 我也求上帝照亮你們心中的眼睛,使你們知道祂的呼召給你們帶來了何等的盼望,祂應許賜給眾聖徒的產業有何等豐富的榮耀, 19 並且祂在我們這些信的人身上所運行的能力是何等浩大。 20 上帝曾用這大能使基督從死裡復活,使基督在天上坐在自己右邊, 21 遠遠超越今生永世所有執政的、掌權的、有能力的、作主宰的和一切的權勢。 22 祂又使萬物降服在基督腳下,使基督為教會作萬物的元首。 23 教會是基督的身體,蘊涵著那無所不在、充滿萬物者的豐盛。