Neno: Bibilia Takatifu

Waebrania 1

Ukuu Wa Mwana Wa Mungu

1Hapo zamani Mungu alisema na baba zetu mara nyingi na kwa namna mbali mbali kwa kuwatumia manabii. Lakini katika siku hizi za mwisho, amesema na sisi kwa njia ya Mwanae, ambaye alim chagua kuwa mrithi wa vitu vyote. Na kwa njia ya Mwanae, Mungu aliumba ulimwengu. Yeye Mwana ni mng’ao wa utukufu wa Mungu na chapa halisi ya nafsi yake, naye huudumisha na kuuendeleza ulim wengu kwa neno lake lenye nguvu. Alipokwisha kuwapatia wanadamu utakaso wa dhambi, alikaa upande wa kulia wa Mungu Mwenyezi aliye juu. Kwa hiyo Mwana alikuwa mkuu zaidi kuliko malaika, kama ambavyo jina alilorithi kwa Mungu ni kuu kuliko jina la malaika ye yote.

Kwa maana ni malaika gani ambaye Mungu aliwahi kumwambia: “Wewe ni mwanangu; leo hii nimekuzaa”? Au tena: “Mimi nita kuwa Baba yake na yeye atakuwa Mwanangu”? Na tena Mungu ana pomleta mwanae, mzaliwa wa kwanza ulimwenguni, anasema: “Malaika wote wa Mungu wamwabudu yeye.” Anapozungumza juu ya malaika anasema: “Anawafanya malaika wake kuwa upepo, watumishi wake kuwa ndimi za moto.” Lakini kuhusu Mwana, anasema: “Kiti chako cha enzi, Wewe Mungu, kitadumu milele na milele, na haki takuwa fimbo ya ufalme wako. Umependa haki na kuchukia uovu. Kwa hiyo Mungu, Mungu wako, amekuchagua wewe na kukuweka juu ya wenzako kwa kukupaka mafuta ya furaha.” 10 Pia anasema: “Hapo mwanzo , Wewe Bwana, uliweka misingi ya ulimwengu, na mbingu ni kazi ya mikono yako. 11 Vyote vitaangamia lakini wewe unadumu; vyote vitachakaa kama nguo, nawe 12 utavikunja kama vazi na kuvibadilisha. Bali wewe hubadiliki, na miaka yako haitakwisha kamwe. ” 13 Lakini ni malaika gani amewahi kumwambia, “Keti kulia kwangu mpaka niwafanye adui zako kuwa kiti cha kuwekea miguu yako”? 14 Malaika ni nani basi? Wao ni roho wa utumishi waliotumwa kuwahudumia wale watakaopokea wokovu.

Chinese Contemporary Bible (Traditional)

希伯來書 1

劃時代的啟示

1在古代,上帝曾藉著先知以各種方式多次向我們的祖先說話; 在這世界的末期,祂又藉著自己的兒子親自向我們說話。上帝早已立祂承受萬物,並藉著祂創造了宇宙萬物。 祂正是上帝榮耀的光輝,是上帝本體的真像。祂用自己充滿能力的話語維繫萬物。祂洗淨了世人的罪之後,便坐在天上至高上帝的右邊。 祂既承受了比天使更高的名分,就遠超越天使。

上帝從未對任何一個天使說:

「你是我的兒子,我今日成為你父親。」

或說:

「我要作你的父親,你要作我的兒子。」

上帝差遣祂的長子到世上來時,說:

「上帝的天使都要敬拜祂。」

上帝提到天使的時候,也只是說:

「上帝使祂的天使成為風,使祂的僕役成為火焰。」

但論到祂的兒子,祂卻說:

「上帝啊,你的寶座永遠長存,
你以公義的杖執掌王權。
你喜愛公義,憎惡邪惡。
所以上帝,你的上帝,
用喜樂之油膏你,使你超過同伴。」

10 此外又說:

「主啊,太初你奠立大地的根基,
親手創造諸天。
11 天地都要消亡,但你永遠長存。
天地都會像衣服漸漸破舊,
12 你要像捲外衣一樣把天地捲起來。
天地將如衣服一樣被更換,
但你永遠不變,
你的年日永無窮盡。」

13 上帝從未對任何一個天使說:

「你坐在我的右邊,
等我使你的仇敵成為你的腳凳。」

14 天使豈不都是服役的靈嗎?他們奉差遣,豈不是去為那些將要承受救恩的人服務嗎?