Neno: Bibilia Takatifu

Ufunua wa Yohana 5

Hati Na Mwana-Kondoo

1Kisha nikaona katika mkono wa kulia wa yule aliyeketi kwe nye kile kiti cha enzi hati iliyoandikwa ndani na nje, ambayo ilikuwa imefungwa na mihuri saba. Tena nikamwona malaika mwenye nguvu akitangaza kwa sauti kuu, “Ni nani anayestahili kufungua hati hii na kuvunja mihuri yake?” Lakini hakupatikana mtu mbinguni, juu ya nchi, wala chini ya nchi aliyeweza kufungua hati hiyo, wala kuitazama. Nililia sana kwa sababu hakupatikana mtu aliyestahili kuifungua hati hiyo wala kuitazama. Kisha, mmoja wapo wa wale wazee akaniambia, “Usilie! Tazama, yule simba wa kabila la Yuda, wa ukoo wa Daudi, ameshinda. Yeye anaweza kufun gua hati hiyo na kuvunja mihuri yake saba.” Katikati ya kile kiti cha enzi na wale viumbe wanne na wale wazee, nikaona Mwana- Kondoo amesimama, akionekana kama amechinjwa. Alikuwa na pembe saba, na macho saba, ambayo ni wale roho saba wa Mungu waliotumwa ulimwenguni kote . Huyo Mwana-Kondoo akaenda, akaichukua ile hati kutoka kwenye mkono wa kulia wa yule aliyeketi kwenye kile kiti cha enzi. Alipokwisha kuichukua ile hati, wale viumbe wanne pamoja na wale wazee ishirini na wanne walianguka mbele ya yule Mwana-Kondoo. Kila mmoja wao alikuwa na kinubi, nao walikuwa wameshika mabakuli ya dhahabu yaliyojaa ubani , ambao ni maombi ya watu wa Mungu. Nao wakaimba wimbo mpya: “Wewe unastahili kuichukua hati na kuifungua mihuri yake. Kwa sababu wewe uliuawa na kwa damu yako ukamnunulia Mungu watu kutoka katika kila kabila na kila lugha; watu wa kila jamaa na kila taifa. 10 Umewafanya hawa wawe ufalme na makuhani wa kumtumikia Mungu wetu, na watata wala ulimwenguni.” 11 Kisha nikatazama, nikasikia sauti za mal aika wengi sana wakizunguka kile kiti cha enzi, pamoja na wale viumbe wanne na wale wazee ishirini na wanne. Idadi ya hao mal aika ilikuwa ni maelfu na maelfu na kumi elfu mara kumi elfu. 12 Nao waliimba kwa sauti kuu, “Mwana -Kondoo aliyeuawa anasta hili kupewa uweza na utajiri na hekima na nguvu na heshima, na utukufu na sifa!” 13 Kisha nikasikia kila kiumbe mbinguni na duniani, juu ya nchi na chini ya nchi, baharini na vyote vilivy omo baharini wakiimba, “Baraka na heshima na utukufu na uweza ni wake yeye aketiye juu ya kiti cha enzi; na kwa Mwana-Kondoo, hata milele na milele! 14 Na wale viumbe wenye uhai wanne wakasema, “Amina!” Na wale wazee wakaanguka kifudifudi wakaabudu.

King James Version

Revelation 5

1And I saw in the right hand of him that sat on the throne a book written within and on the backside, sealed with seven seals.

And I saw a strong angel proclaiming with a loud voice, Who is worthy to open the book, and to loose the seals thereof?

And no man in heaven, nor in earth, neither under the earth, was able to open the book, neither to look thereon.

And I wept much, because no man was found worthy to open and to read the book, neither to look thereon.

And one of the elders saith unto me, Weep not: behold, the Lion of the tribe of Judah, the Root of David, hath prevailed to open the book, and to loose the seven seals thereof.

And I beheld, and, lo, in the midst of the throne and of the four beasts, and in the midst of the elders, stood a Lamb as it had been slain, having seven horns and seven eyes, which are the seven Spirits of God sent forth into all the earth.

And he came and took the book out of the right hand of him that sat upon the throne.

And when he had taken the book, the four beasts and four and twenty elders fell down before the Lamb, having every one of them harps, and golden vials full of odours, which are the prayers of saints.

And they sung a new song, saying, Thou art worthy to take the book, and to open the seals thereof: for thou wast slain, and hast redeemed us to God by thy blood out of every kindred, and tongue, and people, and nation;

10 And hast made us unto our God kings and priests: and we shall reign on the earth.

11 And I beheld, and I heard the voice of many angels round about the throne and the beasts and the elders: and the number of them was ten thousand times ten thousand, and thousands of thousands;

12 Saying with a loud voice, Worthy is the Lamb that was slain to receive power, and riches, and wisdom, and strength, and honour, and glory, and blessing.

13 And every creature which is in heaven, and on the earth, and under the earth, and such as are in the sea, and all that are in them, heard I saying, Blessing, and honour, and glory, and power, be unto him that sitteth upon the throne, and unto the Lamb for ever and ever.

14 And the four beasts said, Amen. And the four and twenty elders fell down and worshipped him that liveth for ever and ever.