Neno: Bibilia Takatifu

2 Wakorintho 12

Maono Ya Paulo Na Mwiba Aliokuwa Nao

1Inanibidi nijisifu. Ingawa hakuna faida, nitawaeleza juu ya maono na mafunuo niliyopata kutoka kwa Bwana. Namfahamu mtu aliyekuwa ndani ya Kristo ambaye miaka kumi na minne iliyopita alijikuta katika mbingu ya tatu. Kama alikuwa katika mwili au katika roho mimi sijui, Mungu anajua. Na ninafahamu ya kuwa huyu mtu alijikuta yuko Paradiso, kama alikuwa katika mwili au katika roho mimi sijui, Mungu anajua. Naye alisikia mambo ambayo hayawezi kusimuliwa, ambayo mtu hawezi kuyatamka. Kwa niaba ya mtu huyu nitajisifu, lakini kwa ajili yangu mwenyewe sitajisifu isipokuwa kuhusu udhaifu wangu. Lakini ningependa kujisifu, sitakuwa mjinga kwa maana nitakuwa nasema kweli. Ila najizuia, ili mtu ye yote asije akaniona mimi kuwa bora zaidi kuliko ninavyoonekana katika yale ninayotenda na kusema.

Na ili nisijione bora kuliko nilivyo, kutokana na mafunuo haya makuu, nilipewa mwiba katika mwili wangu, mtumishi wa she tani, ili anitese. Nimemsihi Bwana mara tatu aniondolee mwiba huu. Lakini aliniambia, “Neema yangu inakutosha, kwa kuwa uwezo wangu unakamilika katika udhaifu.” Kwa hiyo nitajisifu kwa furaha zaidi kuhusu udhaifu wangu ili uwezo wa Kristo ukae juu yangu. 10 Basi, kwa ajili ya Kristo, naridhika na udhaifu, mat usi, taabu, mateso na maafa; kwa maana ninapokuwa mdhaifu ndipo nina nguvu.

Upendo Wa Paulo Kwa Wakorintho

11 Nimekuwa mjinga, lakini ninyi mmenilazimisha niwe hivyo. Kwa kuwa ninyi ndio ambao mngenisifu. Kwa sababu sikuwa wa chini kuliko hawa “mitume wakuu,” hata ingawa mimi si kitu. 12 Mambo yanayomtambulisha mtume wa kweli, yaani ishara, miujiza na maaj abu, yalifanywa miongoni mwenu kwa uvumilivu wote. 13 Je, kuna kitu ambacho hamkupewa sawa na wengine, isipokuwa mimi sikuwa mzigo kwenu? Nisameheni kwa kosa hili.

14 Na sasa niko tayari kuwatembelea kwa mara ya tatu, nami sitahitaji msaada wenu kwa sababu sitaki mnipe mali yenu, ninaowahitaji ni ninyi. Kwa kuwa si sawa watoto waweke akiba kwa ajili ya wazazi wao bali wazazi waweke akiba kwa ajili ya watoto wao. 15 Nitafurahi kutumia kila nilicho nacho hata mwili wangu pia, kwa ajili yenu. Je kama nawapenda zaidi, mtanipenda kidogo tu kwa sababu hiyo? 16 Hata kama mnakubali kwamba sikuwa mzigo kwenu, wengine watasema nilikuwa mjanja nikawanasa kwa hila. 17 Je, niliwahi kuwadanganya kupitia mmojawapo wa hao watu nil iowatuma kwenu? 18 Nilimsihi Tito aje kwenu nikamtuma ndugu mwingine waje pamoja. Je, Tito aliwatoza cho chote? Je, sisi sote hatukutenda kwa kuongozwa na Roho mmoja na kufuata njia moja?

19 Pengine mnafikiri wakati wote kwamba sisi tunajaribu kujitetea mbele yenu. Sisi tunajitetea mbele ya Mungu katika Kristo, na yote haya ni kwa nia ya kuwajenga ninyi, wapendwa wetu. 20 Kwa maana nina hofu kwamba nitakapokuja nitawakuta hamko kama ambavyo ningependa muwe, na ninyi mtakuta siko kama ambavyo mngependa niwe. Nina hofu kwamba kati yenu huenda kuna ugomvi, wivu, hasira, ubinafsi, uzushi, usengenyaji, majivuno na machafuko. 21 Nina hofu kuwa nitakapokuja tena Mungu wangu ata ninyenyekeza mbele yenu, na huenda nikaomboleza kuhusu wengi wenu ambao walitenda dhambi na hawajatubu na kuacha hayo matendo machafu, uasherati na ufisadi ambao walikuwa wakitenda.

New American Standard Bible

2 Corinthians 12

Paul’s Vision

1Boasting is necessary, though it is not profitable; but I will go on to visions and revelations [a]of the Lord. I know a man in Christ who fourteen years ago—whether in the body I do not know, or out of the body I do not know, God knows—such a man was caught up to the third heaven. And I know how such a man—whether in the body or apart from the body I do not know, God knows— was caught up into Paradise and heard inexpressible words, which a man is not permitted to speak. On behalf of such a man I will boast; but on my own behalf I will not boast, except in regard to my weaknesses. For if I do wish to boast I will not be foolish, for I will be speaking the truth; but I refrain from this, so that no one will credit me with more than he sees in me or hears from me.

A Thorn in the Flesh

Because of the surpassing greatness of the revelations, for this reason, to keep me from exalting myself, there was given me a thorn in the flesh, a messenger of Satan to [b]torment me—to keep me from exalting myself! Concerning this I implored the Lord three times that it might leave me. And He has said to me, “My grace is sufficient for you, for power is perfected in weakness.” Most gladly, therefore, I will rather boast [c]about my weaknesses, so that the power of Christ may dwell in me. 10 Therefore I am well content with weaknesses, with [d]insults, with distresses, with persecutions, with difficulties, for Christ’s sake; for when I am weak, then I am strong.

11 I have become foolish; you yourselves compelled me. Actually I should have been commended by you, for in no respect was I inferior to the [e]most eminent apostles, even though I am a nobody. 12 The [f]signs [g]of a true apostle were performed among you with all perseverance, by [h]signs and wonders and [i]miracles. 13 For in what respect were you treated as inferior to the rest of the churches, except that I myself did not become a burden to you? Forgive me this wrong!

14 Here for this third time I am ready to come to you, and I will not be a burden to you; for I do not seek what is yours, but you; for children are not responsible to save up for their parents, but parents for their children. 15 I will most gladly spend and be expended for your souls. If I love you more, am I to be loved less? 16 But be that as it may, I did not burden you myself; nevertheless, crafty fellow that I am, I took you in by deceit. 17 Certainly I have not taken advantage of you through any of those whom I have sent to you, have I? 18 I urged Titus to go, and I sent the brother with him. Titus did not take any advantage of you, did he? Did we not [j]conduct ourselves [k]in the same spirit and walk in the same steps?

19 All this time [l]you have been thinking that we are defending ourselves to you. Actually, it is in the sight of God that we have been speaking in Christ; and all for your upbuilding, beloved. 20 For I am afraid that perhaps when I come I may find you to be not what I wish and may be found by you to be not what you wish; that perhaps there will be strife, jealousy, angry tempers, disputes, slanders, gossip, arrogance, disturbances; 21 I am afraid that when I come again my God may humiliate me before you, and I may mourn over many of those who have sinned in the past and not repented of the impurity, [m]immorality and sensuality which they have practiced.

Notas al pie

 1. 2 Corinthians 12:1 Or from
 2. 2 Corinthians 12:7 Lit beat
 3. 2 Corinthians 12:9 Lit in
 4. 2 Corinthians 12:10 Or mistreatment
 5. 2 Corinthians 12:11 Or super-apostles
 6. 2 Corinthians 12:12 Or attesting miracles
 7. 2 Corinthians 12:12 Lit of the apostle
 8. 2 Corinthians 12:12 Or attesting miracles
 9. 2 Corinthians 12:12 Or works of power
 10. 2 Corinthians 12:18 Lit walk
 11. 2 Corinthians 12:18 Or by the same Spirit
 12. 2 Corinthians 12:19 Or have you been thinking...?
 13. 2 Corinthians 12:21 I.e. sexual immorality