Neno: Bibilia Takatifu

1 Yohana 1

Neno La Uzima

1Tunawaandikieni kuhusu kile ambacho kimekuwapo tangu mwanzo, ambacho tumekisikia na kukiona kwa macho yetu; ambacho tumekigusa kwa mikono yetu; yaani Neno la uzima. Uzima huo uli tokea, nasi tumeuona na tunaushuhudia, na tunawatangazieni uzima wa milele uliokuwa kwa Baba, nao ukadhihirishwa kwetu. Tunawa tangazia hicho tulichokiona na kukisikia ili nanyi pia mpate kushirikiana nasi. Na ushirika tulio nao ni wetu na Baba na Mwa nae Yesu Kristo. Tunawaandikieni mambo haya ili furaha yetu ikamilike.

Kutembea Nuruni

Huu ndio ujumbe tuliousikia kutoka kwake, ambao tunawatan gazia: Mungu ni nuru na ndani yake hamna giza kamwe. Tukisema tuna ushirika naye huku tunaendelea kuishi gizani tunasema uongo, wala hatutendi yaliyo ya kweli. Bali tukiishi nuruni, kama yeye alivyo nuru, tunakuwa na ushirika sisi kwa sisi na damu ya Mwanae Yesu, inatutakasa dhambi zote. Tukisema kwamba hatuna dhambi tunajidanganya wenyewe wala kweli haimo ndani yetu. Tukiziungama dhambi zetu, yeye ni mwa minifu na wa haki na atatusamehe dhambi zetu na kututakasa na uovu wote. 10 Tukisema hatujatenda dhambi tunamfanya yeye kuwa mwongo, na neno lake halimo ndani yetu.

Chinese Contemporary Bible (Simplified)

约翰一书 1

生命之道

1论到从太初就已经存在的生命之道,我们曾经耳闻目睹,亲眼看过,亲手摸过。 这生命曾显现过,我们看见了,现在做见证,向你们传扬这原本与父同在、曾向我们显现的永恒生命。 我们把所见所闻传给你们,使你们可以与我们相交。诚然,我们是与父和祂儿子耶稣基督相交。 我们将这些话写给你们,是要让大家都充满喜乐。

要活在光中

我们从耶稣那里听见、现在传给你们的信息就是:上帝是光,在祂里面毫无黑暗。 如果我们说与祂相交,却仍过着黑暗的生活,就是撒谎,没有遵行真理。 如果我们生活在光明之中,像上帝在光明中一样,就能够彼此相交,上帝儿子耶稣的血能洗净我们一切的罪。

如果我们说自己没有罪,便是自欺,真理就不在我们心中。 如果我们承认自己的罪,上帝是信实公义的,必赦免我们的罪,洗净我们一切的不义。 10 我们如果说自己没有犯过罪,就是把上帝看作说谎的,祂的道也不在我们心中。