Matouš 1 – SNC & NEN

Slovo na cestu

Matouš 1:1-25

Ježíšův rodokmen

1Ježíšův rodokmen sahá přes Davida až k Abrahamovi.

2Abraham – Izák

Izák – Jákob

3Jákob – Juda (a bratři)

Juda – Peres a Zerach (matka Támar)

Peres – Chesrón

Chesrón – Rám

4Rám – Amínadab

Amínadab – Nachšón

Nachšón – Salmón

5Salmón – Bóaz (matka: Rachab)

Bóaz – Obéd (matka: Rút)

Obéd – Jišaj

6Jišaj – David (král)

David – Šalomoun (matka: Batšeba).

7Šalomoun – Rechabeám

Rechabeám – Abijám

Abijám – Ása

8Ása – Jóšafat

Jóšafat – Jóram

Jóram – Uzijáš

9Uzijáš – Jótam

Jótam – Achaz

Achaz – Chizkijáš

10Chizkijáš – Menaše

Menaše – Ámon

Ámon – Jóšijáš

11Jóšijáš – Jechoniáš

12Jekonjáš a jeho bratři.

Babylónské zajetí –

Jekonjáš – Šealtíel

Šealtíel – Zerubábel

13Zerubábel – Abiud

Abiud – Eljakim

Eljakim – Azór

14Azór – Sádok

Sádok – Achim

Achim – Eliud

15Eliud – Eleazar

Eleazar – Mattan

Mattan – Jákob

16Jákob – Josef

Josef (muž Marie)

JEŽÍŠ KRISTUS (narozen z Marie).

Rodokmen uzavírá Josef, manžel Marie, které se narodil Ježíš – Boží Syn.

17Od praotce Abrahama k Davidovi je to čtrnáct generací, dále čtrnáct generací od Davida po babylónské zajetí a od zajetí v Babylóně až ke Kristu také čtrnáct.

Anděl se zjevuje Josefovi

18S narozením Ježíše Krista to bylo takto: Ježíšova matka Marie byla zasnoubena s Josefem. Dříve, než se vzali, se však ukázalo, že bude matkou. 19Josef byl ohleduplný muž a nechtěl Marii vystavit veřejné hanbě, proto se rozhodl, že se s ní rozejde. 20Když o tom uvažoval, ukázal se mu ve snu Boží posel a řekl: „Josefe, Davidův synu, neboj se vzít si Marii. Co v ní bylo počato, je z Ducha svatého. 21Porodí syna a dáš mu jméno Ježíš. On vysvobodí svůj lid z moci zla. 22Těmito událostmi se splní předpověď proroka Izajáše: 23‚Slyšte! Panna bude těhotná a porodí syna. Budete mu říkat Immanuel, to znamená: Bůh je s námi.‘ “

24Když se Josef probudil, udělal vše tak, jak mu přikázal Boží posel, a oženil se s Marií. 25Ale nežil s ní manželsky až do doby, kdy se jí narodil syn, kterému dal jméno Ježíš.

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Mathayo 1:1-25

Kumbukumbu Za Ukoo Wa Yesu Kristo

(Luka 3:23-38)

11:1 Rum 1:3; Mwa 22:18; Lk 3:23-38Habari za ukoo wa Yesu Kristo mwana wa Daudi, mwana wa Abrahamu:

21:2 Mwa 21:3, 12; 25:26; 29:35; 49:10Abrahamu akamzaa Isaki,

Isaki akamzaa Yakobo,

Yakobo akawazaa Yuda na ndugu zake,

31:3 Mwa 38:27-30; 1Nya 2:5, 9; Rut 4:18-22; 1Nya 2:10-12Yuda akawazaa Peresi na Zera, ambao mama yao alikuwa Tamari,

Peresi akamzaa Hesroni,

Hesroni akamzaa Aramu,

4Aramu akamzaa Aminadabu,

Aminadabu akamzaa Nashoni,

Nashoni akamzaa Salmoni,

51:5 Rut 4:13-17; Ebr 11:31Salmoni akamzaa Boazi, na mama yake Boazi alikuwa Rahabu,

Boazi akamzaa Obedi, ambaye mama yake alikuwa Ruthu,

Obedi akamzaa Yese,

61:6 1Sam 16:1; 17:12; 2Sam 12:24Yese akamzaa Daudi ambaye alikuwa mfalme.

Daudi akamzaa Solomoni, ambaye mama yake ni yule aliyekuwa mke wa Uria.

71:7 1Nya 3:10-14Solomoni akamzaa Rehoboamu,

Rehoboamu akamzaa Abiya,

Abiya akamzaa Asa,

8Asa akamzaa Yehoshafati,

Yehoshafati akamzaa Yoramu,1:8 Yoramu ndiye Yehoramu, maana yake ni Yehova yu juu.

Yoramu akamzaa Uzia,

9Uzia akamzaa Yothamu,

Yothamu akamzaa Ahazi,

Ahazi akamzaa Hezekia,

101:10 2Fal 20:21; 1Nya 3:13Hezekia akamzaa Manase,

Manase akamzaa Amoni,

Amoni akamzaa Yosia,

111:11 Dan 1:1-2; 2Fal 24:14-16; Yer 27:20; 40:1wakati wa uhamisho wa Babeli, Yosia alimzaa Yekonia na ndugu zake.

121:12 1Nya 3:17-19; Ezr 3:2Baada ya uhamisho wa Babeli:

Yekonia alimzaa Shealtieli,

Shealtieli akamzaa Zerubabeli,

13Zerubabeli akamzaa Abiudi,

Abiudi akamzaa Eliakimu,

Eliakimu akamzaa Azori,

14Azori akamzaa Sadoki,

Sadoki akamzaa Akimu,

Akimu akamzaa Eliudi,

15Eliudi akamzaa Eleazari,

Eleazari akamzaa Matani,

Matani akamzaa Yakobo,

161:16 Lk 1:27; Mt 27:17naye Yakobo akamzaa Yosefu ambaye alikuwa mumewe Maria, mama yake Yesu, aitwaye Kristo.1:16 Kristo maana yake ni Masiya, yaani Aliyetiwa mafuta.

17Hivyo, kulikuwepo na jumla ya vizazi kumi na vinne tangu Abrahamu mpaka Daudi, vizazi kumi na vinne tangu Daudi hadi wakati wa uhamisho kwenda utumwani Babeli, na vizazi kumi na vinne tangu wakati wa uhamisho kwenda utumwani Babeli hadi Kristo.

Kuzaliwa Kwa Yesu Kristo

(Luka 2:1-7)

181:18 Lk 1:35Basi Kuzaliwa kwake Yesu Kristo kulikuwa hivi: Maria mama yake alikuwa ameposwa na Yosefu, lakini kabla hawajakutana kimwili, Maria alionekana kuwa na mimba kwa uweza wa Roho Mtakatifu. 191:19 Kum 24:1Kwa kuwa Yosefu, mwanaume aliyekuwa amemposa alikuwa mtu mwadilifu, hakutaka kumwaibisha Maria hadharani, aliazimu kumwacha kwa siri.

201:20 Lk 1:35Lakini mara alipoazimu kufanya jambo hili, malaika wa Bwana akamtokea katika ndoto na kusema, “Yosefu mwana wa Daudi, usiogope kumchukua Maria awe mke wako, kwa maana mimba aliyo nayo ni kwa uweza wa Roho Mtakatifu. 211:21 Lk 1:31; Za 130:8; Tit 2:14Naye atamzaa mwana, nawe utamwita Jina lake Yesu,1:21 Yesu ni Iesous kwa Kiyunani, na kwa Kiebrania ni Yoshua au Yeshua. Maana yake ni Yehova ni wokovu. kwa maana yeye ndiye atakayewaokoa watu wake kutoka dhambi zao.”

221:22 Mt 22:15; 17:23; 4:14; Lk 4:21; 21:22; Yn 13:18; 19:24Haya yote yalitukia ili litimie lile Bwana alilokuwa amenena kupitia nabii, akisema: 231:23 Isa 7:14; 8:8-10“Tazama, bikira atachukua mimba, naye atamzaa mwana, nao watamwita Jina lake Imanueli”: maana yake, “Mungu pamoja nasi.”

241:24 Mdo 5:19Yosefu alipoamka kutoka usingizini, akafanya kama vile alivyoagizwa na malaika wa Bwana, akamchukua Maria kuwa mke wake. 251:25 Lk 1:31; 2:7; 2:1; 2:4-7; 1:5Lakini hawakukutana kimwili mpaka Maria alipojifungua mwanawe kifungua mimba akamwita Jina lake Yesu.