Genesis 43 – NIVUK & NEN

New International Version – UK

Genesis 43:1-34

The second journey to Egypt

1Now the famine was still severe in the land. 2So when they had eaten all the grain they had brought from Egypt, their father said to them, ‘Go back and buy us a little more food.’

3But Judah said to him, ‘The man warned us solemnly, “You will not see my face again unless your brother is with you.” 4If you will send our brother along with us, we will go down and buy food for you. 5But if you will not send him, we will not go down, because the man said to us, “You will not see my face again unless your brother is with you.” ’

6Israel asked, ‘Why did you bring this trouble on me by telling the man you had another brother?’

7They replied, ‘The man questioned us closely about ourselves and our family. “Is your father still living?” he asked us. “Do you have another brother?” We simply answered his questions. How were we to know he would say, “Bring your brother down here”?’

8Then Judah said to Israel his father, ‘Send the boy along with me and we will go at once, so that we and you and our children may live and not die. 9I myself will guarantee his safety; you can hold me personally responsible for him. If I do not bring him back to you and set him here before you, I will bear the blame before you all my life. 10As it is, if we had not delayed, we could have gone and returned twice.’

11Then their father Israel said to them, ‘If it must be, then do this: put some of the best products of the land in your bags and take them down to the man as a gift – a little balm and a little honey, some spices and myrrh, some pistachio nuts and almonds. 12Take double the amount of silver with you, for you must return the silver that was put back into the mouths of your sacks. Perhaps it was a mistake. 13Take your brother also and go back to the man at once. 14And may God Almighty43:14 Hebrew El-Shaddai grant you mercy before the man so that he will let your other brother and Benjamin come back with you. As for me, if I am bereaved, I am bereaved.’

15So the men took the gifts and double the amount of silver, and Benjamin also. They hurried down to Egypt and presented themselves to Joseph. 16When Joseph saw Benjamin with them, he said to the steward of his house, ‘Take these men to my house, slaughter an animal and prepare a meal; they are to eat with me at noon.’

17The man did as Joseph told him and took the men to Joseph’s house. 18Now the men were frightened when they were taken to his house. They thought, ‘We were brought here because of the silver that was put back into our sacks the first time. He wants to attack us and overpower us and seize us as slaves and take our donkeys.’

19So they went up to Joseph’s steward and spoke to him at the entrance to the house. 20‘We beg your pardon, our lord,’ they said, ‘we came down here the first time to buy food. 21But at the place where we stopped for the night we opened our sacks and each of us found his silver – the exact weight – in the mouth of his sack. So we have brought it back with us. 22We have also brought additional silver with us to buy food. We don’t know who put our silver in our sacks.’

23‘It’s all right,’ he said. ‘Don’t be afraid. Your God, the God of your father, has given you treasure in your sacks; I received your silver.’ Then he brought Simeon out to them.

24The steward took the men into Joseph’s house, gave them water to wash their feet and provided fodder for their donkeys. 25They prepared their gifts for Joseph’s arrival at noon, because they had heard that they were to eat there.

26When Joseph came home, they presented to him the gifts they had brought into the house, and they bowed down before him to the ground. 27He asked them how they were, and then he said, ‘How is your aged father you told me about? Is he still living?’

28They replied, ‘Your servant our father is still alive and well.’ And they bowed down, prostrating themselves before him.

29As he looked about and saw his brother Benjamin, his own mother’s son, he asked, ‘Is this your youngest brother, the one you told me about?’ And he said, ‘God be gracious to you, my son.’ 30Deeply moved at the sight of his brother, Joseph hurried out and looked for a place to weep. He went into his private room and wept there.

31After he had washed his face, he came out and, controlling himself, said, ‘Serve the food.’

32They served him by himself, the brothers by themselves, and the Egyptians who ate with him by themselves, because Egyptians could not eat with Hebrews, for that is detestable to Egyptians. 33The men had been seated before him in the order of their ages, from the firstborn to the youngest; and they looked at each other in astonishment. 34When portions were served to them from Joseph’s table, Benjamin’s portion was five times as much as anyone else’s. So they feasted and drank freely with him.

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Mwanzo 43:1-34

Safari Ya Pili Ya Kwenda Misri

143:1 Mwa 12:10Wakati huu njaa ilikuwa bado ni kali mno katika nchi. 2Hivyo wakati walikuwa wamemaliza kula nafaka yote waliyoileta kutoka Misri, Yakobo baba yao akawaambia, “Rudini Misri mkatununulie chakula kingine zaidi.”

343:3 Mwa 42:15Lakini Yuda akamwambia, “Mtu yule alituonya kwa msisitizo, ‘Hamtauona uso wangu tena mpaka mje na ndugu yenu.’ 4Kama utakubali ndugu yetu aende pamoja nasi, tutakwenda kuwanunulia chakula. 543:5 2Sam 3:13Lakini ikiwa hutamruhusu aende, hatutakwenda, kwa sababu mtu yule alituambia, ‘Hamtauona uso wangu tena mpaka mje pamoja na ndugu yenu.’ ”

643:6 Mwa 34:30Israeli akauliza, “Kwa nini mkaniletea taabu hii kwa kumwambia yule mtu mlikuwa na ndugu mwingine?”

743:7 Mwa 42:13Wakamjibu, “Yule mtu alituhoji kwa undani sana habari zetu na za jamaa yetu. Alituuliza, ‘Je, baba yenu bado yungali hai? Je mnaye ndugu mwingine?’ Sisi tulimjibu maswali yake tu. Tungewezaje kujua kwamba angesema, ‘Mleteni mdogo wenu hapa’?”

8Ndipo Yuda akamwambia baba yake Israeli, “Mtume kijana pamoja nami, nasi tutaondoka mara, ili sisi na wewe pamoja na watoto wetu tuweze kuishi, wala tusife. 943:9 Mwa 42:37; Flm 18-19Mimi mwenyewe nitakuhakikishia usalama wake, mimi mwenyewe nitawajibika kumrudisha. Ikiwa sitamrudisha kwako na kumweka mbele yako, nitakuwa mwenye lawama mbele yako maisha yangu yote. 1043:10 Mwa 45:9Hakika, kama hatukuchelewa kuondoka, tungekuwa tumekwenda na kurudi mara mbili.”

1143:11 Mwa 37:25Basi baba yao Israeli akawaambia, “Kama ni lazima iwe hivyo, basi fanyeni hivi: Wekeni baadhi ya mazao bora ya nchi katika mifuko yenu na mpelekeeni yule mtu kama zawadi, zeri kidogo, asali kidogo, vikolezo, manemane, kungu na lozi. 1243:12 Mwa 42:25Chukueni fedha mara mbili, kwa kuwa mtazirudisha zile fedha zilizowekwa midomoni mwa magunia yenu. Labda ziliwekwa kwa makosa. 13Mchukueni ndugu yenu pia mrudi kwa huyo mtu mara moja. 1443:14 Kum 13:17Naye Mungu Mwenyezi43:14 Mungu Mwenyezi hapa ni jina la Kiebrania, El-Shaddai (yaani Mungu Mwenye utoshelevu wote). awajalieni rehema mbele ya huyo mtu ili apate kumwachia yule ndugu yenu na Benyamini mweze kurudi pamoja. Kwangu mimi kama nikufiwa nimefiwa.”

15Basi hao watu wakazichukua zile zawadi na zile fedha mara mbili pamoja na Benyamini. Wakafanya haraka kwenda Misri na walipofika wakajionyesha kwa Yosefu. 1643:16 Mwa 44:1, 4, 12Yosefu alipomwona Benyamini pamoja nao, akamwambia msimamizi wa nyumba yake, “Wachukue watu hawa nyumbani kwangu, mchinje mnyama na kuandalia chakula kwa kuwa watakula chakula cha mchana pamoja nami.”

1743:17 Mwa 43:16Yule Msimamizi akafanya kama Yosefu alivyomwambia na akawachukua wale watu nyumbani kwa Yosefu. 1843:18 Mwa 44:14Basi watu hao wakaogopa walipopelekwa nyumbani kwa Yosefu. Wakafikiri, “Tumeletwa hapa kwa ajili ya zile fedha zilizorudishwa katika magunia yetu mara ile ya kwanza. Anataka kutushambulia na kutushinda, atuchukue sisi kama watumwa, na atwae hawa punda zetu.”

19Hivyo wakamwendea msimamizi wa nyumba wa Yosefu na kuzungumza naye kwenye ingilio la nyumbani. 2043:20 Mwa 42:3Wakasema, “Tafadhali bwana, tulikuja hapa mara ya kwanza kununua chakula. 2143:21 Mwa 43:15Lakini mahali pale tulipotua wakati wa jioni tulifungua magunia yetu, na kila mmoja wetu akakuta fedha zake, kwenye mdomo wa gunia lake kiasi kile kile tulicholeta. Kwa hiyo tumezirudisha. 22Pia tumeleta fedha nyingine kwa ajili ya kununulia chakula. Hatujui ni nani aliziweka fedha hizo katika magunia yetu.”

23Akawaambia, “Vema, msiogope. Mungu wenu, Mungu wa baba yenu, amewapa ninyi hazina katika magunia yenu; mimi nilipokea fedha yenu.” Ndipo akawaletea Simeoni.

2443:24 Mwa 43:16; 18:4Msimamizi akawapeleka wale watu katika nyumba ya Yosefu, akawapa maji ya kunawa miguu na kuwapa punda wao majani. 2543:25 Mwa 32:13Wakaandaa zawadi zao ili wampe Yosefu wakati atakapofika adhuhuri, kwa kuwa walikuwa wamesikia kwamba watakula chakula huko.

2643:26 Mt 2:11Yosefu alipokuja nyumbani, walimkabidhi zile zawadi walizokuwa nazo, ambazo walikuwa wamezileta mle nyumbani, nao wakamsujudia hadi nchi. 2743:27 Mwa 37:3Akawauliza kuhusu hali yao, kisha akawaambia, “Yule baba yenu mzee mliyeniambia habari zake, yu hali gani? Je, bado yu hai?”

2843:28 Mwa 37:7Wakamjibu, “Mtumishi wako baba yetu bado anaishi na ni mzima.” Kisha wakainama chini kumpa heshima.

2943:29 Mwa 42:13Alipotazama na kumwona Benyamini ndugu yake, mwana wa mama yake hasa, akauliza, “Je, huyu ndiye ndugu yenu wa mwisho, ambaye mlinieleza habari zake?” Ndipo akasema, “Mungu na akufadhili, mwanangu.” 30Akiwa ameguswa sana kwa kumwona ndugu yake, Yosefu akatoka nje kwa haraka na kutafuta mahali pa kulilia. Akaingia kwenye chumba chake cha pekee na kulilia humo.

31Baada ya kunawa uso wake, akatoka nje na huku akijizuia akasema, “Pakueni chakula.”

3243:32 Mwa 46:34Wakampakulia Yosefu peke yake, ndugu zake peke yao na Wamisri waliokula pamoja naye peke yao, kwa sababu Wamisri wasingeweza kula pamoja na Waebrania, kwa maana ilikuwa ni chukizo kwa Wamisri. 33Watu hao walikuwa wameketi mbele yake kwa mfuatano wa umri wao, kuanzia mzaliwa wa kwanza hadi mzaliwa wa mwisho, wakatazamana wao kwa wao kwa mshangao. 3443:34 Mwa 37:3Wakati walipelekewa sehemu ya chakula kutoka mezani mwa Yosefu, sehemu ya Benyamini ilikuwa mara tano zaidi ya sehemu ya wale wengine. Kwa hiyo wakanywa na kufurahi pamoja naye.