Exodus 28 – NIVUK & NEN

New International Version – UK

Exodus 28:1-43

The priestly garments

1‘Let Aaron your brother be brought to you from among the Israelites, with his sons Nadab and Abihu, Eleazar and Ithamar, so that they may serve me as priests. 2Make sacred garments for your brother Aaron to give him dignity and honour. 3Tell all the skilled workers to whom I have given wisdom in such matters that they are to make garments for Aaron, for his consecration, so that he may serve me as priest. 4These are the garments they are to make: a breastpiece, an ephod, a robe, a woven tunic, a turban and a sash. They are to make these sacred garments for your brother Aaron and his sons, so that they may serve me as priests. 5Make them use gold, and blue, purple and scarlet yarn, and fine linen.

The ephod

6‘Make the ephod of gold, and of blue, purple and scarlet yarn, and of finely twisted linen – the work of skilled hands. 7It is to have two shoulder pieces attached to two of its corners, so that it can be fastened. 8Its skilfully woven waistband is to be like it – of one piece with the ephod and made with gold, and with blue, purple and scarlet yarn, and with finely twisted linen.

9‘Take two onyx stones and engrave on them the names of the sons of Israel 10in the order of their birth – six names on one stone and the remaining six on the other. 11Engrave the names of the sons of Israel on the two stones the way a gem cutter engraves a seal. Then mount the stones in gold filigree settings 12and fasten them on the shoulder pieces of the ephod as memorial stones for the sons of Israel. Aaron is to bear the names on his shoulders as a memorial before the Lord. 13Make gold filigree settings 14and two braided chains of pure gold, like a rope, and attach the chains to the settings.

The breastpiece

15‘Fashion a breastpiece for making decisions – the work of skilled hands. Make it like the ephod: of gold, and of blue, purple and scarlet yarn, and of finely twisted linen. 16It is to be square – a span28:16 That is, about 23 centimetres long and a span wide – and folded double. 17Then mount four rows of precious stones on it. The first row shall be carnelian, chrysolite and beryl; 18the second row shall be turquoise, lapis lazuli and emerald; 19the third row shall be jacinth, agate and amethyst; 20the fourth row shall be topaz, onyx and jasper.28:20 The precise identification of some of these precious stones is uncertain. Mount them in gold filigree settings. 21There are to be twelve stones, one for each of the names of the sons of Israel, each engraved like a seal with the name of one of the twelve tribes.

22‘For the breastpiece make braided chains of pure gold, like a rope. 23Make two gold rings for it and fasten them to two corners of the breastpiece. 24Fasten the two gold chains to the rings at the corners of the breastpiece, 25and the other ends of the chains to the two settings, attaching them to the shoulder pieces of the ephod at the front. 26Make two gold rings and attach them to the other two corners of the breastpiece on the inside edge next to the ephod. 27Make two more gold rings and attach them to the bottom of the shoulder pieces on the front of the ephod, close to the seam just above the waistband of the ephod. 28The rings of the breastpiece are to be tied to the rings of the ephod with blue cord, connecting it to the waistband, so that the breastpiece will not swing out from the ephod.

29‘Whenever Aaron enters the Holy Place, he will bear the names of the sons of Israel over his heart on the breastpiece of decision as a continuing memorial before the Lord. 30Also put the Urim and the Thummim in the breastpiece, so they may be over Aaron’s heart whenever he enters the presence of the Lord. Thus Aaron will always bear the means of making decisions for the Israelites over his heart before the Lord.

Other priestly garments

31‘Make the robe of the ephod entirely of blue cloth, 32with an opening for the head in its centre. There shall be a woven edge like a collar28:32 The meaning of the Hebrew for this word is uncertain. around this opening, so that it will not tear. 33Make pomegranates of blue, purple and scarlet yarn around the hem of the robe, with gold bells between them. 34The gold bells and the pomegranates are to alternate round the hem of the robe. 35Aaron must wear it when he ministers. The sound of the bells will be heard when he enters the Holy Place before the Lord and when he comes out, so that he will not die.

36‘Make a plate of pure gold and engrave on it as on a seal:

Holy to the Lord.

37Fasten a blue cord to it to attach it to the turban; it is to be on the front of the turban. 38It will be on Aaron’s forehead, and he will bear the guilt involved in the sacred gifts the Israelites consecrate, whatever their gifts may be. It will be on Aaron’s forehead continually so that they will be acceptable to the Lord.

39‘Weave the tunic of fine linen and make the turban of fine linen. The sash is to be the work of an embroiderer. 40Make tunics, sashes and caps for Aaron’s sons to give them dignity and honour. 41After you put these clothes on your brother Aaron and his sons, anoint and ordain them. Consecrate them so they may serve me as priests.

42‘Make linen undergarments as a covering for the body, reaching from the waist to the thigh. 43Aaron and his sons must wear them whenever they enter the tent of meeting or approach the altar to minister in the Holy Place, so that they will not incur guilt and die.

‘This is to be a lasting ordinance for Aaron and his descendants.

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Kutoka 28:1-43

Mavazi Ya Kikuhani

(Kutoka 39:1-7)

128:1 Law 8:30; Za 99:9; Ebr 5; 4; Kut 6:23; 24:9; Law 8:2; 21:1; Hes 18:1-7; Kum 18:5; 1Sam 2:28; Ebr 5:1“Mtwae Aroni ndugu yako aliyeletwa kwako kutoka miongoni mwa Waisraeli, pamoja na wanawe Nadabu, Abihu, Eleazari na Ithamari, ili wanitumikie katika kazi ya ukuhani. 228:2 Kut 29:5; 31:10; 35:19; Law 8:7-9; 16:32; Hes 20:26-28Mshonee Aroni ndugu yako mavazi matakatifu ili yampe ukuu na heshima. 328:3 Kut 31:6; 35:10, 25, 35; 36:1; 31:3; Kum 34:9; Isa 11:2Waambie mafundi stadi wote niliowapa hekima katika shughuli hiyo wamtengenezee Aroni mavazi hayo, ili awekwe wakfu, anitumikie katika kazi ya ukuhani. 428:4 Kut 25:7; Law 10:5Haya ndiyo mavazi watakayoshona: kifuko cha kifuani, kisibau, kanzu, joho lililorembwa, kilemba na mshipi. Mavazi haya yatashonwa kwa ajili ya ndugu yako Aroni na wanawe ili wanitumikie katika kazi ya ukuhani. 528:5 Kut 25:4-7; 25:4-7Waambie watumie dhahabu na nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, na za rangi nyekundu pamoja na kitani safi.

Kisibau

628:6 Kut 39:2; Law 8:7“Tengeneza kisibau cha dhahabu, na nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, za rangi nyekundu na kitani safi iliyosokotwa, kazi ya fundi stadi. 7Kitakuwa na vipande viwili vya mabegani vilivyoshikizwa kwenye pembe zake mbili ili kufungia kisibau. 828:8 Kut 29:5Mshipi wa kiunoni uliofumwa kwa ustadi utafanana nacho: utakuwa kitu kimoja na hicho kisibau, nao utengenezwe kwa dhahabu na nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, na nyekundu na kwa kitani iliyosokotwa vizuri.

928:9 Wim 8:6; Isa 44:16; Hag 2:23“Chukua vito viwili vya shohamu, na uchore juu yake majina ya wana wa Israeli 10kufuatana na walivyozaliwa: majina sita katika kito kimoja, na mengine sita katika kito kingine. 11Yachore majina ya wana wa Israeli juu ya vito hivyo viwili kama vile sonara anavyochonga muhuri. Kisha uvitie vito hivyo katika vijalizo vya dhahabu, 1228:12 Kum 33:12; Ay 31:36; Kut 30:16; Hes 10:10; 31:54; Yos 4:7; Zek 6:14; Kut 39:7; Mwa 9:12-17; Kut 12:14; Mk 14:9; Mdo 10:4; 1Kor 11:24, 25na uvifungie juu ya vipande vya mabega ya kisibau yawe kama vito vya ukumbusho kwa wana wa Israeli. Aroni atavaa majina hayo mabegani mwake kama kumbukumbu mbele za Bwana. 13Tengeneza vijalizo vya dhahabu 14na mikufu miwili ya dhahabu safi iliyosokotwa kama kamba, na uifunge mikufu hiyo kwenye vijalizo.

Kifuko Cha Kifuani

(Kutoka 39:8-21)

1528:15 Kut 25:7; 39:8; Law 8:8; Isa 59:17; 1The 5:7; Efe 6:14“Fanyiza kifuko cha kifuani kwa ajili ya kufanya maamuzi, kazi ya fundi stadi. Kitengeneze kama kile kisibau: cha dhahabu, na nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, na za rangi nyekundu, cha kitani safi iliyosokotwa. 16Kitakuwa cha mraba, chenye urefu wa shibiri moja28:16 Shibiri moja ni sawa na sentimita 22. na upana wa shibiri moja, na kikunjwe mara mbili. 1728:17 Eze 28:13; Ufu 21:19-20; Kut 30:10; Mal 3:17Kisha weka safu nne za vito vya thamani juu yake. Safu ya kwanza itakuwa na akiki, yakuti manjano na zabarajadi; 18katika safu ya pili itakuwa na almasi, yakuti samawi na zumaridi; 19safu ya tatu itakuwa na hiakintho, akiki nyekundu na amethisto; 2028:20 Eze 1:16; 10:9; Dan 10:6na safu ya nne itakuwa na krisolitho, shohamu na yaspi. Yote yatiwe kwenye vijalizo vya dhahabu. 2128:21 Yos 4:8; Ufu 21:12; Hes 1:5; 2:3; Ufu 7:4-8; 21:12Patakuwa na vito kumi na viwili, kila kimoja kwa jina mojawapo la wana wa Israeli, kila kimoja kichorwe kama muhuri kikiwa na jina mojawapo la yale makabila kumi na mawili.

22“Kwa ajili ya kile kifuko cha kifuani, tengeneza mikufu ya dhahabu safi, iliyosokotwa kama kamba. 23Tengeneza pete mbili za dhahabu kwa ajili yake, uzifungie kwenye pembe mbili za hicho kifuko cha kifuani. 24Funga ile mikufu miwili ya dhahabu kwenye hizo pete zilizo katika pembe za hicho kifuko cha kifuani, 25nazo zile ncha nyingine za mkufu zifunge kwenye vile vijalizo viwili, na uzishikamanishe na vile vipande vya mabega vya kile kisibau upande wa mbele. 26Tengeneza pete mbili za dhahabu, uzishikamanishe kwenye pembe mbili za chini, upande wa ndani wa kifuko cha kifuani karibu na kisibau. 27Tengeneza pete nyingine mbili za dhahabu, na uzishikamanishe sehemu ya chini ya vipande vya mabega upande wa mbele wa kile kisibau, karibu na pindo juu kidogo ya mshipi wa kiunoni wa kisibau. 28Pete za kifuko cha kifuani zitafungwa kwenye pete zile za kisibau kwa kamba ya buluu, ziunganishwe na ule mshipi wa kiunoni, ili kifuko cha kifuani kisisogee kutoka kwenye kile kisibau.

2928:29 Wim 8:6; Isa 49:15, 16; Ebr 9:24“Wakati wowote Aroni aingiapo Mahali Patakatifu, atakuwa na yale majina ya wana wa Israeli moyoni mwake juu ya kile kifuko cha kifuani cha uamuzi kama kumbukumbu ya kudumu mbele za Bwana. 3028:30 Law 8:8; Hes 27:21; Kum 33:8; 1Sam 28:6; Ezr 2:63; Neh 7:65Pia weka Urimu na Thumimu28:30 Urimu na Thumimu maana yake ni Nuru na Kweli; vifaa hivi viliwekwa kwenye kifuko cha juu cha kisibau cha kuhani mkuu ili kujua mapenzi ya Mungu kwenye mambo ya kutatanisha. ndani ya kifuko cha kifuani, yawe juu ya moyo wa Aroni kila mara aingiapo mbele za Bwana. Kwa hiyo siku zote Aroni atakuwa na uwezo kufanya maamuzi kwa ajili ya wana wa Israeli mbele za Bwana.

Mavazi Mengine Ya Kikuhani

(Kutoka 39:22-31)

3128:31 Kut 39:22; Law 8:7; 2Sam 6:14; Hos 3:4“Shona joho la kisibau lote kwa kitambaa cha rangi ya buluu tupu, 32na katikati uweke nafasi ya kuingizia kichwa. Kutakuwa na utepe uliofumwa, unaofanana na ukosi kuizunguka nafasi hiyo, ili isichanike. 3328:33 Hes 13:23; 1Sam 14:2; 1Fal 7:18; Wim 4:3; Yer 52:22; Yoe 1:12; Hag 2:19Tengeneza makomamanga ya nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, na za rangi nyekundu kuzunguka pindo la hilo joho, na uweke pia vikengele vya dhahabu kati ya hayo makomamanga. 34Hivyo vikengele vya dhahabu na makomamanga vitapishana kuzunguka upindo wa joho lile. 35Ni lazima Aroni alivae anapofanya huduma. Sauti ya hivyo vikengele itasikika anapoingia na kutoka Mahali Patakatifu mbele za Bwana, ili asije akafa.

3628:36 Kut 29:6; Law 8:9; Zek 14:20; Kut 39:30; 1Nya 16:29; Za 29:2; 93:5; Ebr 4:15; 7:26“Tengeneza bamba la dhahabu safi na uchore juu yake maneno haya kama vile muhuri huchorwa: Mtakatifu kwa Bwana. 37Lifunge hilo bamba kwa kamba ya buluu kwenye kilemba, nalo ni lazima liwe mbele ya kilemba. 3828:38 Law 5:1; 10:17; 16:22; 22:9, 16; Hes 18:1; Isa 53:5-11; Eze 4:4-6; Ebr 9:28; 1Pet 2:24; Mwa 32:20; Law 22:20, 27; 23:11; Isa 56:7Aroni alivae bamba hilo kwenye paji la uso wake, naye atachukua hatia kuhusu sadaka takatifu za Waisraeli wanazoweka wakfu, sadaka za aina yoyote. Litakuwa kwenye paji la uso wa Aroni daima ili zikubalike kwa Bwana.

3928:39 Kut 29:6; Law 16:4; Eze 24:17-23; 44:18“Fuma koti la kitani safi na ufanye kilemba cha kitani safi. Mshipi uwe ni kazi ya mtarizi. 4028:40 Kut 29:8-9; 39:41; 40:14; Law 8:13; Eze 44:17Watengenezee wana wa Aroni makoti, mishipi na kofia, ili kuwapa ukuu na heshima. 4128:41 Kut 40:13; 29:7; Law 6:20; 10:7; 21:12; Hes 35:25; Kut 29:7-9; 30:30; 40:15; Law 4:3; 6:22; 8:1-36; Hes 3:3; Ebr 7:28Baada ya kumvika Aroni ndugu yako pamoja na wanawe nguo hizi, watie mafuta na kuwabariki. Waweke wakfu ili wanitumikie katika kazi ya ukuhani.

4228:42 Law 6:10; 16:4, 23; Eze 44:18“Watengenezee nguo za ndani za kitani zitakazofunika mwili, kutoka kiunoni hadi mapajani. 4328:43 Kut 27:21; 30:20-21; Law 16:13; 22:9; Hes 1:51; 4:15-20; 18:22Aroni na wanawe ni lazima wavae haya kila wanapoingia katika Hema la Kukutania au wanaposogelea madhabahu wakati wa kutoa huduma katika Mahali Patakatifu, ili wasije wakafanya kosa wakafa.

“Haya yawe maagizo ya kudumu kwa Aroni na vizazi vyake.