New International Version

Zechariah 9:1-17

Judgment on Israel’s Enemies

1A prophecy:

The word of the Lord is against the land of Hadrak

and will come to rest on Damascus—

for the eyes of all people and all the tribes of Israel

are on the Lord9:1 Or Damascus. / For the eye of the Lord is on all people, / as well as on the tribes of Israel,

2and on Hamath too, which borders on it,

and on Tyre and Sidon, though they are very skillful.

3Tyre has built herself a stronghold;

she has heaped up silver like dust,

and gold like the dirt of the streets.

4But the Lord will take away her possessions

and destroy her power on the sea,

and she will be consumed by fire.

5Ashkelon will see it and fear;

Gaza will writhe in agony,

and Ekron too, for her hope will wither.

Gaza will lose her king

and Ashkelon will be deserted.

6A mongrel people will occupy Ashdod,

and I will put an end to the pride of the Philistines.

7I will take the blood from their mouths,

the forbidden food from between their teeth.

Those who are left will belong to our God

and become a clan in Judah,

and Ekron will be like the Jebusites.

8But I will encamp at my temple

to guard it against marauding forces.

Never again will an oppressor overrun my people,

for now I am keeping watch.

The Coming of Zion’s King

9Rejoice greatly, Daughter Zion!

Shout, Daughter Jerusalem!

See, your king comes to you,

righteous and victorious,

lowly and riding on a donkey,

on a colt, the foal of a donkey.

10I will take away the chariots from Ephraim

and the warhorses from Jerusalem,

and the battle bow will be broken.

He will proclaim peace to the nations.

His rule will extend from sea to sea

and from the River9:10 That is, the Euphrates to the ends of the earth.

11As for you, because of the blood of my covenant with you,

I will free your prisoners from the waterless pit.

12Return to your fortress, you prisoners of hope;

even now I announce that I will restore twice as much to you.

13I will bend Judah as I bend my bow

and fill it with Ephraim.

I will rouse your sons, Zion,

against your sons, Greece,

and make you like a warrior’s sword.

The Lord Will Appear

14Then the Lord will appear over them;

his arrow will flash like lightning.

The Sovereign Lord will sound the trumpet;

he will march in the storms of the south,

15and the Lord Almighty will shield them.

They will destroy

and overcome with slingstones.

They will drink and roar as with wine;

they will be full like a bowl

used for sprinkling9:15 Or bowl, / like the corners of the altar.

16The Lord their God will save his people on that day

as a shepherd saves his flock.

They will sparkle in his land

like jewels in a crown.

17How attractive and beautiful they will be!

Grain will make the young men thrive,

and new wine the young women.

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Zekaria 9:1-17

Hukumu Juu Ya Adui Za Israeli

1Neno:

9:1 Isa 17:1; Amo 1:5; Za 145:15Neno la Bwana liko kinyume na nchi ya Hadraki

na Dameski itakuwa mahali pa kupumzika,

kwa kuwa macho ya watu na ya kabila zote

za Israeli yako kwa Bwana,

29:2 Yer 49:23; Eze 28:1-19; Mwa 10:15; Amo 1:9; Oba 1:20pia juu ya Hamathi inayopakana nayo,

juu ya Tiro na Sidoni,

ingawa wana ujuzi mwingi sana.

39:3 Ay 27:16; Eze 28:4Tiro amejijengea ngome imara,

amelundika fedha kama mavumbi

na dhahabu kama taka za mitaani.

49:4 Isa 23:1, 11; Yer 25:22; Eze 26:3-5; 27:32-36; 28:18Lakini Bwana atamwondolea mali zake

na kuuangamiza uwezo wake wa baharini,

naye atateketezwa kwa moto.

59:5 Yer 47:5; Sef 2:5; Mdo 8:26Ashkeloni ataona hili na kuogopa;

Gaza atagaagaa kwa maumivu makali,

pia Ekroni, kwa sababu

matumaini yake yatanyauka.

Gaza atampoteza mfalme wake

na Ashkeloni ataachwa pweke.

69:6 Isa 14:30Wageni watakalia mji wa Ashdodi,

nami nitakatilia mbali kiburi cha Wafilisti.

79:7 Ay 25:2; Yoe 3:4; Sef 2:4; Yer 47:1Nitaondoa damu vinywani mwao,

chakula kile walichokatazwa kati ya meno yao.

Mabaki yao yatakuwa mali ya Mungu wetu,

nao watakuwa viongozi katika Yuda,

naye Ekroni atakuwa kama Wayebusi.

89:8 Isa 26:1; 52:1; 54:14; Zek 14:21; Yoe 3:17; Kum 33:27; Za 34:7; Kut 3:7Lakini nitailinda nyumba yangu

dhidi ya majeshi ya wanyangʼanyi.

Kamwe mdhalimu hatashambulia watu wangu tena,

kwa maana sasa ninawachunga.

Kuja Kwa Mfalme Wa Sayuni

99:9 Isa 62:11; 9:6-7; 43:3-11; 1Fal 1:39; Za 24:7; 149:2; Mik 4:8; Yer 23:5-6; Sef 3:14-15; Zek 2:10; Mwa 49:11; Mt 21:5; 1Fal 1:33; Yn 12:15; 1:49; Lk 19:38; Mdo 22:14; 1Pet 3:18Shangilia sana, ee Binti Sayuni!

Piga kelele, Binti Yerusalemu!

Tazama, Mfalme wako anakuja kwako,

ni mwenye haki, naye ana wokovu,

ni mpole, naye amepanda punda,

mwana-punda, mtoto wa punda.

109:10 Mik 4:3; 5:10; Hos 1:7; 2:18; Zek 10:4; Isa 2:4; Za 72:8; Isa 11:10; Efe 2:14; Kol 1:20-21; Za 2:8; Isa 9:6-7; Mik 5:4; Ufu 11:15Nitaondoa magari ya vita kutoka Efraimu

na farasi wa vita kutoka Yerusalemu,

nao upinde wa vita utavunjwa.

Atatangaza amani kwa mataifa.

Utawala wake utaenea kutoka bahari hadi bahari,

na kutoka Mto Frati hadi mwisho wa dunia.

119:11 Kut 24:8; Mt 26:28; Lk 22:20; Isa 10:4; 42:7; Yer 38:6; Isa 61:1Kwako wewe, kwa sababu ya damu ya Agano langu nawe,

nitawaacha huru wafungwa wako

watoke kwenye shimo lisilo na maji.

129:12 Yoe 3:16; Isa 40:2; Kum 21:17Rudieni ngome yenu, enyi wafungwa wa tumaini;

hata sasa ninatangaza kwamba

nitawarejesheeni maradufu.

139:13 2Sam 22:25; Isa 49:2; Yoe 3:6; Yer 51:20Nitampinda Yuda kama nipindavyo upinde wangu,

nitamfanya Efraimu mshale wangu.

Nitawainua wana wako, ee Sayuni,

dhidi ya wana wako, ee Uyunani,

na kukufanya kama upanga wa shujaa wa vita.

Bwana Atatokea

14Kisha Bwana atawatokea;

mshale wake utamulika

kama umeme wa radi.

Bwana Mwenyezi atapiga tarumbeta,

naye atatembea katika tufani za kusini,

159:15 Isa 31:5; 37:35; Zek 12:8; 10:7; 14:3, 20; Kut 27:2; Law 4:25na Bwana Mwenye Nguvu Zote atawalinda.

Wataangamiza na kushinda

kwa mawe ya kutupa kwa kombeo.

Watakunywa na kunguruma kama waliolewa mvinyo;

watajaa kama bakuli linalotumika kunyunyizia

kwenye pembe za madhabahu.

169:16 Isa 10:20; Yer 31:11; Eze 37:23; Mal 3:17; Isa 11:12Bwana Mungu wao atawaokoa siku hiyo

kama kundi la watu wake.

Watangʼara katika nchi yake

kama vito vya thamani kwenye taji.

17Jinsi gani watavutia na kuwa wazuri!

Nafaka itawastawisha vijana wanaume,

nayo divai mpya vijana wanawake.