Psalms 22 – NIV & NEN

New International Version

Psalms 22:1-31

Psalm 22In Hebrew texts 22:1-31 is numbered 22:2-32.

For the director of music. To the tune of “The Doe of the Morning.” A psalm of David.

1My God, my God, why have you forsaken me?

Why are you so far from saving me,

so far from my cries of anguish?

2My God, I cry out by day, but you do not answer,

by night, but I find no rest.22:2 Or night, and am not silent

3Yet you are enthroned as the Holy One;

you are the one Israel praises.22:3 Or Yet you are holy, / enthroned on the praises of Israel

4In you our ancestors put their trust;

they trusted and you delivered them.

5To you they cried out and were saved;

in you they trusted and were not put to shame.

6But I am a worm and not a man,

scorned by everyone, despised by the people.

7All who see me mock me;

they hurl insults, shaking their heads.

8“He trusts in the Lord,” they say,

“let the Lord rescue him.

Let him deliver him,

since he delights in him.”

9Yet you brought me out of the womb;

you made me trust in you, even at my mother’s breast.

10From birth I was cast on you;

from my mother’s womb you have been my God.

11Do not be far from me,

for trouble is near

and there is no one to help.

12Many bulls surround me;

strong bulls of Bashan encircle me.

13Roaring lions that tear their prey

open their mouths wide against me.

14I am poured out like water,

and all my bones are out of joint.

My heart has turned to wax;

it has melted within me.

15My mouth22:15 Probable reading of the original Hebrew text; Masoretic Text strength is dried up like a potsherd,

and my tongue sticks to the roof of my mouth;

you lay me in the dust of death.

16Dogs surround me,

a pack of villains encircles me;

they pierce22:16 Dead Sea Scrolls and some manuscripts of the Masoretic Text, Septuagint and Syriac; most manuscripts of the Masoretic Text me, / like a lion my hands and my feet.

17All my bones are on display;

people stare and gloat over me.

18They divide my clothes among them

and cast lots for my garment.

19But you, Lord, do not be far from me.

You are my strength; come quickly to help me.

20Deliver me from the sword,

my precious life from the power of the dogs.

21Rescue me from the mouth of the lions;

save me from the horns of the wild oxen.

22I will declare your name to my people;

in the assembly I will praise you.

23You who fear the Lord, praise him!

All you descendants of Jacob, honor him!

Revere him, all you descendants of Israel!

24For he has not despised or scorned

the suffering of the afflicted one;

he has not hidden his face from him

but has listened to his cry for help.

25From you comes the theme of my praise in the great assembly;

before those who fear you22:25 Hebrew him I will fulfill my vows.

26The poor will eat and be satisfied;

those who seek the Lord will praise him—

may your hearts live forever!

27All the ends of the earth

will remember and turn to the Lord,

and all the families of the nations

will bow down before him,

28for dominion belongs to the Lord

and he rules over the nations.

29All the rich of the earth will feast and worship;

all who go down to the dust will kneel before him—

those who cannot keep themselves alive.

30Posterity will serve him;

future generations will be told about the Lord.

31They will proclaim his righteousness,

declaring to a people yet unborn:

He has done it!

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Zaburi 22:1-31

Zaburi 22

Kilio Cha Uchungu Na Wimbo Wa Sifa

Kwa mwimbishaji. Mtindo wa utenzi wa “Kulungu wa Alfajiri.” Zaburi ya Daudi.

122:1 Za 9:10; 10:1; Mt 27:46; Ay 3:24; 6:15; Mk 15:34; Ebr 5:7Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?

Kwa nini uko mbali hivyo kuniokoa?

Mbali hivyo na maneno ya kuugua kwangu?

222:2 Ay 19:7; Za 42:3; 88:1Ee Mungu wangu, ninalia mchana, lakini hunijibu,

hata usiku, sinyamazi.

322:3 2Fal 19:22; Za 71:22; 148:14; Mk 1:24; Ufu 4:8; Kut 15:2; Isa 6:3Hata hivyo umesimikwa katika kiti cha enzi kama Uliye Mtakatifu;

wewe ni sifa ya Israeli.22:3 Tafsiri zingine zinasema: uketiye juu ya sifa za Israeli.

422:4 Za 78:53; 107:6Kwako wewe baba zetu waliweka tumaini lao,

walikutumaini nawe ukawaokoa.

522:5 1Nya 5:20; Rum 9:33; Za 25:3; 31:17; 71:1; 2Nya 13:18; Isa 8:17; 25:9; 26:3; 30:18; 49:23Walikulilia wewe na ukawaokoa,

walikutegemea wewe nao hawakuaibika.

622:6 Ay 4:19; Mt 16:21; Mal 2:9; Isa 60:14; 49:7; 53:3; Za 119:141; 64:8; 109:25; 69:19; 2Sam 12:14Mimi ni mnyoo wala si mwanadamu,

wanaume wamenibeza, na watu wamenidharau.

722:7 Mt 9:24; 27:41; Mk 15:20, 29, 31, 32; Lk 16:14; 23:36, 39; Mt 27:39, 44; Ay 17:2; Za 35:16; 69:12; 74:18Wote wanionao hunidhihaki,

hunivurumishia matusi, wakitikisa vichwa vyao:

822:8 Za 91:14; 3:2; 2Sam 22:20; Mt 3:17; 27:43Husema, “Anamtegemea Bwana,

basi Bwana na amwokoe.

Amkomboe basi, kwa maana

anapendezwa naye.”

922:9 Ay 10:18; Hes 1:7; Za 71:6; 78:7Hata hivyo ulinitoa tumboni,

ukanifanya nikutegemee,

hata nilipokuwa ninanyonya

matiti ya mama yangu.

1022:10 Za 71:6; Isa 46:3; 49:1Nimekabidhiwa kwako tangu kuzaliwa,

toka tumboni mwa mama yangu

umekuwa Mungu wangu.

1122:11 Za 10:1, 14; 2Fal 14:26; Isa 41:28Usiwe mbali nami,

kwa maana shida iko karibu

na hakuna wa kunisaidia.

1222:12 Za 69:30; 17:9; 27:6; 49:5; 109:3; 140:9; Kum 32:14; Isa 2:3; Eze 27:6; 39:18; Amo 4:1Mafahali wengi wamenizunguka,

mafahali wa Bashani wenye nguvu

wamenizingira.

1322:13 Eze 22:25; Sef 3:3; Mwa 49:9; 1Pet 5:8; Mao 3:6; Za 35:21Simba wangurumao wanaorarua mawindo

yao hupanua vinywa vyao dhidi yangu.

1422:14 Za 6:2Nimemiminwa kama maji,

mifupa yangu yote imetoka katika viungo vyake.

Moyo wangu umegeuka kuwa nta,

umeyeyuka ndani yangu.

1522:15 Isa 45:9; Yn 19:28; Za 137:6; 104:29; Mao 4:4; Ay 7:21; Eze 3:26Nguvu zangu zimekauka kama kigae,

ulimi wangu umegandamana

na kaakaa la kinywa changu,

kwa sababu umenilaza

katika mavumbi ya kifo.

1622:16 Flp 3:2; Isa 51:9; 53:5; Mit 17:22; Zek 12:10; Yn 20:25Mbwa wamenizunguka,

kundi la watu waovu limenizingira,

wametoboa mikono yangu na miguu yangu.

1722:17 Lk 23:35; Mik 7:8; Za 25:2; 30:1; 35:19; 38:16; Mao 2:17Naweza kuhesabu mifupa yangu yote,

watu wananikodolea macho na kunisimanga.

1822:18 Law 16:8; Yn 19:24; Mt 27:35; Mk 9:12; 15:24; Lk 23:34Wanagawana nguo zangu wao kwa wao,

na vazi langu wanalipigia kura.

1922:19 Za 18:1; 38:22; 70:5; 14:1; 40:13Lakini wewe, Ee Bwana,

usiwe mbali.

Ee Nguvu yangu,

uje haraka unisaidie.

2022:20 Ay 5:20; Za 141:1; 40:13Okoa maisha yangu na upanga,

uhai wangu wa thamani kutoka nguvu za mbwa.

2122:21 Ay 4:10, 12; Ebr 2:12; Hes 23:22; Za 22:13; 68:26; 40:9, 10; 35:18; 2Tim 4:17Niokoe kutoka kinywani mwa simba,

niokoe kutoka pembe za mafahali mwitu.

2222:22 Za 26:12; 35:18; 40:9, 10; 68:26; Ebr 2:12; Yn 20:17Nitalitangaza jina lako kwa ndugu zangu,

katika kusanyiko nitakusifu wewe.

2322:23 Yer 3:17; Za 66:8; 33:2, 8; 103:1; 86:12; 106:1; 50:15; 113:1; 117:1; 135:19; Isa 24:15; 25:3; 49:23; 60:9; Kum 14:23Ninyi ambao mnamcha Bwana, msifuni!

Ninyi nyote wazao wote wa Yakobo, mheshimuni yeye!

Mcheni yeye, ninyi wazao wote wa Israeli!

2422:24 Ebr 5:7; Za 9:12; 102:17; 13:1; 27:9; 69:17; 102:2; 143:7; Ay 24:12; 36:5Kwa maana hakupuuza wala kudharau

mateso ya aliyeonewa;

hakumficha uso wake

bali alisikiliza kilio chake ili amsaidie.

2522:25 Za 26:12; 35:18; 40:9; 82:1; Hes 30:2Kwako wewe hutoka kiini cha sifa zangu katika kusanyiko kubwa,

nitatimiza nadhiri zangu mbele ya wale wakuchao wewe.

2622:26 Za 107:9; 40:16Maskini watakula na kushiba,

wale wamtafutao Bwana watamsifu:

mioyo yenu na iishi milele!

2722:27 Za 2:8; 86:9; 102:22; Dan 7:27; Mik 4:1Miisho yote ya dunia itakumbuka

na kumgeukia Bwana,

nazo jamaa zote za mataifa

watasujudu mbele zake,

2822:28 Za 47:7; Zek 14:9; Mt 6:13kwa maana ufalme ni wa Bwana

naye hutawala juu ya mataifa.

2922:29 Za 45:12; 89:48; 95:6; 96:9; 99:5; Isa 26:19; 27:13; 49:7; 66:23; Zek 14:16Matajiri wote wa dunia watasherehekea na kuabudu.

Wote waendao mavumbini

watapiga magoti mbele yake,

wote ambao hawawezi

kudumisha uhai wao.

3022:30 Isa 53:10; 54:3; 61:9; 66:22; Za 102:18Wazao wa baadaye watamtumikia yeye;

vizazi vijavyo vitajulishwa habari za Bwana.

3122:31 Za 5:8; 71:18; 78:6; 40:9; 102:18; Lk 18:31; 24:44Watatangaza haki yake kwa watu

ambao hawajazaliwa bado,

kwa maana yeye ametenda hili.