Philemon 1 – NIV & NEN

New International Version

Philemon 1:1-25

1Paul, a prisoner of Christ Jesus, and Timothy our brother,

To Philemon our dear friend and fellow worker— 2also to Apphia our sister and Archippus our fellow soldier—and to the church that meets in your home:

3Grace and peace to you1:3 The Greek is plural; also in verses 22 and 25; elsewhere in this letter “you” is singular. from God our Father and the Lord Jesus Christ.

Thanksgiving and Prayer

4I always thank my God as I remember you in my prayers, 5because I hear about your love for all his holy people and your faith in the Lord Jesus. 6I pray that your partnership with us in the faith may be effective in deepening your understanding of every good thing we share for the sake of Christ. 7Your love has given me great joy and encouragement, because you, brother, have refreshed the hearts of the Lord’s people.

Paul’s Plea for Onesimus

8Therefore, although in Christ I could be bold and order you to do what you ought to do, 9yet I prefer to appeal to you on the basis of love. It is as none other than Paul—an old man and now also a prisoner of Christ Jesus— 10that I appeal to you for my son Onesimus,1:10 Onesimus means useful. who became my son while I was in chains. 11Formerly he was useless to you, but now he has become useful both to you and to me.

12I am sending him—who is my very heart—back to you. 13I would have liked to keep him with me so that he could take your place in helping me while I am in chains for the gospel. 14But I did not want to do anything without your consent, so that any favor you do would not seem forced but would be voluntary. 15Perhaps the reason he was separated from you for a little while was that you might have him back forever— 16no longer as a slave, but better than a slave, as a dear brother. He is very dear to me but even dearer to you, both as a fellow man and as a brother in the Lord.

17So if you consider me a partner, welcome him as you would welcome me. 18If he has done you any wrong or owes you anything, charge it to me. 19I, Paul, am writing this with my own hand. I will pay it back—not to mention that you owe me your very self. 20I do wish, brother, that I may have some benefit from you in the Lord; refresh my heart in Christ. 21Confident of your obedience, I write to you, knowing that you will do even more than I ask.

22And one thing more: Prepare a guest room for me, because I hope to be restored to you in answer to your prayers.

23Epaphras, my fellow prisoner in Christ Jesus, sends you greetings. 24And so do Mark, Aristarchus, Demas and Luke, my fellow workers.

25The grace of the Lord Jesus Christ be with your spirit.

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Filemoni 1:1-25

11:1 Efe 3:1; 2Kor 1:1; Flp 2:25Paulo, mfungwa wa Kristo Yesu, pamoja na Timotheo ndugu yetu:

Kwa Filemoni rafiki yetu mpendwa na mtendakazi mwenzetu, 21:2 Kol 4:17; Flp 2:25; Rum 16:5kwa dada yetu mpendwa Afia, kwa Arkipo askari mwenzetu na kwa kanisa lile likutanalo nyumbani mwako:

31:3 Rum 1:7; Efe 1:2Neema iwe nanyi na amani itokayo kwa Mungu Baba yetu na Bwana Yesu Kristo.

Shukrani Na Maombi

41:4 Rum 1:8; 1:10; Efe 1:16; 1The 1:2; 2The 1:2Siku zote ninamshukuru Mungu ninapokukumbuka katika maombi yangu, 51:5 2Tim 2:22; Mdo 23:1; 1Tim 4:2; Gal 5:23kwa sababu ninasikia juu ya imani yako katika Bwana Yesu na upendo wako kwa watakatifu wote. 61:6 Flp 1:9, 11Naomba utiwe nguvu katika kuishuhudia imani yako, ili upate kuwa na ufahamu mkamilifu juu ya kila kitu chema tulicho nacho ndani ya Kristo. 71:7 2Kor 7:4, 13; 7:4, 13; 2Tim 1:16; Flm 20Upendo wako umenifurahisha mno na kunitia moyo, kwa sababu wewe ndugu, umeiburudisha mioyo ya watakatifu.

Maombi Ya Paulo Ya Kumtetea Onesimo

81:8 1The 2:6Hata hivyo, ingawa katika Kristo ningeweza kuwa na ujasiri na kukuagiza yale yakupasayo kutenda, 91:9 Efe 3:1; Flm 1, 23; 1Kor 1:10lakini ninakuomba kwa upendo, mimi Paulo, mzee na pia sasa nikiwa mfungwa wa Kristo Yesu, 101:10 1Kor 4:15; 1The 2:11nakuomba kwa ajili ya mwanangu Onesimo,1:10 Onesimo maana yake ni Wa manufaa. aliyefanyika mwanangu nilipokuwa kwenye minyororo. 11Mwanzoni alikuwa hakufai, lakini sasa anakufaa sana wewe na mimi pia.

12Namtuma kwako, yeye aliye moyo wangu hasa. 131:13 Flm 10; Mdo 21:33; 1Kor 16:17; Flp 2:20; Kol 4:9Ningependa nikae naye ili ashike nafasi yako ya kunisaidia wakati huu nikiwa kifungoni kwa ajili ya Injili. 141:14 2Kor 9:7; 1Pet 5:2Lakini sikutaka kufanya lolote bila idhini yako, ili wema wowote uufanyao usiwe wa lazima, bali wa hiari. 151:15 Mwa 45:5, 8Huenda sababu ya yeye kutengwa nawe kwa kitambo kidogo ni ili uwe naye daima. 161:16 Mt 23:8; Mdo 1:16Si kama mtumwa, bali bora kuliko mtumwa, kama ndugu mpendwa. Yeye ni mpendwa sana kwangu na hata kwako zaidi, yeye kama mwanadamu na kama ndugu katika Bwana.

171:17 2Kor 8:23Hivyo kama unanihesabu mimi kuwa mshirika wako, mkaribishe kama vile ungenikaribisha mimi mwenyewe. 181:18 Mwa 43:9Kama amekukosea lolote au kama unamdai chochote, nidai mimi. 191:19 1Kor 16:21; Gal 6:11; 2The 3:17Ni mimi Paulo, ninayeandika waraka huu kwa mkono wangu mwenyewe. Nitakulipa. Sitaji kwamba nakudai hata nafsi yako. 201:20 1Kor 16:18; Flm 7Ndugu yangu, natamani nipate faida kwako katika Bwana, uuburudishe moyo wangu katika Kristo. 211:21 2Kor 2:3; 1Kor 7:16Nikiwa na hakika ya utii wako, nakuandikia, nikijua kwamba utafanya hata zaidi ya yale ninayokuomba.

221:22 Flp 2:24; Ebr 13:19; Flp 1:19Jambo moja zaidi: Niandalie chumba cha wageni, kwa kuwa nataraji kurudishwa kwenu kama jibu la maombi yenu.

Salamu Za Mwisho Na Dua Ya Kuwatakia Heri

231:23 Kol 1:17Epafra, aliye mfungwa mwenzangu katika Kristo Yesu, anakusalimu. 241:24 Mdo 12:12; 19:29; 2Tim 4:10Vivyo hivyo Marko, Aristarko, Dema na Luka, watendakazi wenzangu wanakusalimu.

251:25 2Tim 4:22Neema ya Bwana Yesu Kristo iwe pamoja na roho zenu. Amen.