New International Version

Ephesians 5:1-33

1Follow God’s example, therefore, as dearly loved children 2and walk in the way of love, just as Christ loved us and gave himself up for us as a fragrant offering and sacrifice to God.

3But among you there must not be even a hint of sexual immorality, or of any kind of impurity, or of greed, because these are improper for God’s holy people. 4Nor should there be obscenity, foolish talk or coarse joking, which are out of place, but rather thanksgiving. 5For of this you can be sure: No immoral, impure or greedy person—such a person is an idolater—has any inheritance in the kingdom of Christ and of God.5:5 Or kingdom of the Messiah and God 6Let no one deceive you with empty words, for because of such things God’s wrath comes on those who are disobedient. 7Therefore do not be partners with them.

8For you were once darkness, but now you are light in the Lord. Live as children of light 9(for the fruit of the light consists in all goodness, righteousness and truth) 10and find out what pleases the Lord. 11Have nothing to do with the fruitless deeds of darkness, but rather expose them. 12It is shameful even to mention what the disobedient do in secret. 13But everything exposed by the light becomes visible—and everything that is illuminated becomes a light. 14This is why it is said:

“Wake up, sleeper,

rise from the dead,

and Christ will shine on you.”

15Be very careful, then, how you live—not as unwise but as wise, 16making the most of every opportunity, because the days are evil. 17Therefore do not be foolish, but understand what the Lord’s will is. 18Do not get drunk on wine, which leads to debauchery. Instead, be filled with the Spirit, 19speaking to one another with psalms, hymns, and songs from the Spirit. Sing and make music from your heart to the Lord, 20always giving thanks to God the Father for everything, in the name of our Lord Jesus Christ.

Instructions for Christian Households

21Submit to one another out of reverence for Christ.

22Wives, submit yourselves to your own husbands as you do to the Lord. 23For the husband is the head of the wife as Christ is the head of the church, his body, of which he is the Savior. 24Now as the church submits to Christ, so also wives should submit to their husbands in everything.

25Husbands, love your wives, just as Christ loved the church and gave himself up for her 26to make her holy, cleansing5:26 Or having cleansed her by the washing with water through the word, 27and to present her to himself as a radiant church, without stain or wrinkle or any other blemish, but holy and blameless. 28In this same way, husbands ought to love their wives as their own bodies. He who loves his wife loves himself. 29After all, no one ever hated their own body, but they feed and care for their body, just as Christ does the church— 30for we are members of his body. 31“For this reason a man will leave his father and mother and be united to his wife, and the two will become one flesh.”5:31 Gen. 2:24 32This is a profound mystery—but I am talking about Christ and the church. 33However, each one of you also must love his wife as he loves himself, and the wife must respect her husband.

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Waefeso 5:1-33

Kuenenda Nuruni

15:1 Lk 6:36; Mt 5:45; 8; Lk 6:26; Efe 4:32Kwa hiyo, mfuateni Mungu kama watoto wapendwao, 25:2 Gal 1:4; 2Kor 6:15; Ebr 7:27mkiishi maisha ya upendo, kama vile Kristo alivyotupenda sisi akajitoa kwa ajili yetu kuwa sadaka yenye harufu nzuri na dhabihu kwa Mungu.

35:3 Kol 3:5; 1Kor 6:18; Efe 4:29Lakini uasherati, usitajwe miongoni mwenu, wala uchafu wa aina yoyote, wala tamaa, kwa sababu mambo haya hayastahili miongoni mwa watakatifu. 45:4 Mt 12:35; Efe 4:29; Rum 1:28; Kol 3:8Wala pasiwepo mazungumzo machafu ya aibu, au maneno ya upuzi au mzaha, ambayo hayafai, badala yake mshukuruni Mungu. 55:5 Kol 3:5; 1Kor 6:9Kwa habari ya mambo haya mjue hakika kwamba: Msherati, wala mtu mwovu, wala mwenye tamaa mbaya, mtu kama huyo ni mwabudu sanamu, kamwe hataurithi Ufalme wa Kristo na wa Mungu. 65:6 Rum 1:18; Kol 2:4, 8; Yer 29:8; Mt 24:4; Kol 2:4, 8, 18; 2The 2:3; Rum 1:1Mtu yeyote na asiwadanganye kwa maneno matupu, kwa kuwa hasira ya Mungu huwaka kwa sababu ya mambo kama haya juu ya wale wasiomtii. 7Kwa hiyo, msishirikiane nao.

85:8 Efe 2:2; Yn 8:12Kwa maana zamani ninyi mlikuwa giza, lakini sasa ninyi ni nuru katika Bwana. Enendeni kama watoto wa nuru 95:9 Gal 5:22; Mt 7:16-20; Rum 15:14(kwa kuwa tunda la nuru hupatikana katika wema wote, haki na kweli), 105:10 1Tim 5:4; Rum 12:2; Flp 1:10; 1The 5:21; 1Tim 2:3nanyi tafuteni yale yanayompendeza Bwana. 115:11 Rum 13:12; 2Kor 6:14; Yn 16:8Msishiriki matendo ya giza yasiyofaa, bali yafichueni. 125:12 Rum 1:24, 26; Efe 5:3Kwa maana ni aibu hata kutaja mambo yale ambayo wasiotii wanayafanya sirini. 135:13 Yn 3:20, 21Lakini kila kitu kilichowekwa nuruni, huonekana, 145:14 Rum 13:11; Yn 5:25; Isa 60:1kwa kuwa nuru ndiyo hufanya kila kitu kionekane. Hii ndiyo sababu imesemekana:

“Amka, wewe uliyelala,

ufufuke kutoka kwa wafu,

naye Kristo atakuangazia.”

15Kwa hiyo angalieni sana jinsi mnavyoenenda, si kama watu wasio na hekima, bali kama wenye hekima, 165:16 Kol 4:5; Efe 6:13mkiukomboa wakati, kwa sababu nyakati hizi ni za uovu. 175:17 Rum 12:2; Kol 1:9Kwa hiyo msiwe wajinga, bali mpate kujua nini mapenzi ya Bwana. 185:18 Isa 28:7; Lk 1:15Pia msilewe kwa mvinyo, ambamo ndani yake mna upotovu, bali mjazwe Roho. 195:19 Za 27:6Msemezane ninyi kwa ninyi kwa zaburi, nyimbo na tenzi za rohoni, mkimwimbia na kumsifu Bwana mioyoni mwenu, 205:20 Ay 1:21siku zote mkimshukuru Mungu Baba kwa kila jambo katika Jina la Bwana wetu Yesu Kristo.

215:21 Gal 5:13; 1Pet 5:5; Flp 2:3Nyenyekeaneni ninyi kwa ninyi kwa heshima kwa ajili ya Kristo.

Mafundisho Kuhusu Wake Na Waume

225:22 Mwa 3:16; Tit 2:5; Efe 6:5Ninyi wake, watiini waume zenu kama kumtii Bwana. 235:23 1Kor 11:3; Efe 1:22Kwa maana mume ni kichwa cha mkewe kama vile Kristo alivyo kichwa cha Kanisa, ambalo ni mwili wake, naye Kristo ni Mwokozi wake. 245:24 Kol 3:20; Tit 2:9Basi, kama vile Kanisa linavyomtii Kristo, vivyo hivyo na wake nao imewapasa kuwatii waume zao kwa kila jambo.

255:25 Kol 3:19Ninyi waume, wapendeni wake zenu, kama vile Kristo alivyolipenda Kanisa akajitoa kwa ajili yake 265:26 Mdo 22:16kusudi alifanye takatifu, akilitakasa kwa kuliosha kwa maji katika Neno lake, 275:27 Efe 1:4; Kol 1:22apate kujiletea Kanisa tukufu lisilo na doa wala kunyanzi au waa lolote, bali takatifu na lisilo na hatia. 28Vivyo hivyo imewapasa waume kuwapenda wake zao kama miili yao wenyewe. Ampendaye mkewe hujipenda mwenyewe. 29Hakuna mtu anayeuchukia mwili wake mwenyewe, bali huulisha na kuutunza vizuri, kama Kristo anavyolitunza Kanisa lake. 305:30 1Kor 12:27Sisi tu viungo vya mwili wake. 315:31 Mwa 2:24; Mt 19:5“Kwa sababu hii, mwanaume atamwacha baba yake na mama yake, naye ataambatana na mkewe, na hao wawili watakuwa mwili mmoja.” 32Siri hii ni kubwa, bali mimi nanena kuhusu Kristo na Kanisa. 33Hata hivyo, kila mmoja wenu ampende mkewe kama anavyoipenda nafsi yake mwenyewe, naye mke lazima amheshimu mumewe.