Proverbs 8 – NIRV & NEN

New International Reader’s Version

Proverbs 8:1-36

Wisdom Calls Out

1Doesn’t wisdom call out?

Doesn’t understanding raise her voice?

2At the highest point along the way,

she takes her place where the paths meet.

3Beside the gate leading into the city,

she cries out at the entrance. She says,

4“People, I call out to you.

I raise my voice to all human beings.

5You who are childish, get some good sense.

You who are foolish, set your hearts on getting it.

6Listen! I have things to say that you can depend on.

I open my lips to speak what is right.

7My mouth speaks what is true.

My lips hate evil.

8All the words of my mouth are honest.

None of them is twisted or sinful.

9To those who have understanding, all my words are right.

To those who have found knowledge, they are true.

10Choose my teaching instead of silver.

Choose knowledge rather than fine gold.

11Wisdom is worth more than rubies.

Nothing you want can compare with her.

12“I, wisdom, live together with understanding.

I have knowledge and good sense.

13To have respect for the Lord is to hate evil.

I hate pride and bragging.

I hate evil ways and twisted words.

14I have good sense and give good advice.

I have understanding and power.

15By me kings rule.

Leaders make laws that are fair.

16By me princes and nobles govern.

It is by me that anyone rules on earth.

17I love those who love me.

Those who look for me find me.

18With me are riches and honor.

With me are lasting wealth and success.

19My fruit is better than fine gold.

My gifts are better than the finest silver.

20I walk in ways that are honest.

I take paths that are right.

21I leave riches to those who love me.

I give them more than they have room for.

22“The Lord created me as the first of his works,

before his acts of long ago.

23I was formed a long, long time ago.

I was formed at the very beginning, when the world was created.

24Before there were any oceans, I was born.

It was before there were springs flowing with water.

25Before the mountains were settled in place, I was born.

Before there were any hills, I was born.

26It happened before the Lord made the world and its fields.

It was before he made the dust of the earth.

27I was there when he set the heavens in place.

When he marked out the place where the sky meets the sea, I was there.

28That was when he put the clouds above.

It was when he fixed the ocean springs in place.

29It was when he set limits for the sea

so that the waters had to obey his command.

When the Lord marked out the foundations of the earth, I was there.

30I was constantly at his side.

I was filled with delight day after day.

I was always happy to be with him.

31His whole world filled me with joy.

I took delight in all human beings.

32“My children, listen to me.

Blessed are those who keep my ways.

33Listen to my teaching and be wise.

Don’t turn away from it.

34Blessed are those who listen to me.

They watch every day at my doors.

They wait beside my doorway.

35Those who find me find life.

They receive blessing from the Lord.

36But those who don’t find me harm only themselves.

Everyone who hates me loves death.”

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Mithali 8:1-36

Wito Wa Hekima

18:1 Mit 1:20; 9:3; Ay 28:12; 1Kor 1:24Je, hekima haitani?

Je, ufahamu hapazi sauti?

2Juu ya miinuko karibu na njia,

penye njia panda, ndipo asimamapo;

38:3 Ay 29:7; Mit 7:6-13kando ya malango yaelekeayo mjini,

kwenye maingilio, hulia kwa sauti kubwa, akisema:

48:4 Isa 42:2“Ni ninyi wanaume, ninaowaita;

ninapaza sauti yangu kwa wanadamu wote.

58:5 Mit 1:22; 1:4Ninyi ambao ni wajinga, pateni akili;

ninyi mlio wapumbavu, pateni ufahamu.

68:6 Za 49:3; Mt 2:6, 7; Kol 1:26Sikilizeni, kwa maana nina mambo muhimu ya kusema;

ninafungua midomo yangu kusema lililo sawa.

78:7 Za 37:30; Yn 8:14; Rum 15:8Kinywa changu husema lililo kweli,

kwa maana midomo yangu huchukia uovu.

8Maneno yote ya kinywa changu ni haki;

hakuna mojawapo lililopotoka wala ukaidi.

9Kwa wenye kupambanua yote ni sahihi;

hayana kasoro kwa wale wenye maarifa.

108:10 Za 19:10; Mit 3:14-15Chagua mafundisho yangu badala ya fedha,

maarifa badala ya dhahabu safi,

118:11 Ay 28:15-19; Mit 3:13-15kwa maana hekima ina thamani kuliko marijani

na hakuna chochote unachohitaji kinacholingana naye.

128:12 Mit 1:4“Mimi hekima, nakaa pamoja na busara;

ninamiliki maarifa na busara.

138:13 Kut 20:20; Yer 44:4; Zek 8:17; Mit 16:6Kumcha Bwana ni kuchukia uovu;

ninachukia kiburi na majivuno,

tabia mbaya na mazungumzo potovu.

148:14 Mhu 7:19; Ay 9:4Ushauri na hukumu sahihi ni vyangu;

nina ufahamu na nina nguvu.

158:15 Dan 2:21; Mt 28:18; Rum 13:1Kwa msaada wangu wafalme hutawala

na watawala hutunga sheria zilizo za haki,

168:16 2Nya 1:10; Mit 29:4kwa msaada wangu wakuu hutawala,

na wenye vyeo wote watawalao dunia.

178:17 Za 91:14; Yn 14:21-24; 1Sam 2:30; Yak 1:5Nawapenda wale wanipendao,

na wale wanitafutao kwa bidii wataniona.

188:18 Mt 6:33; 1Fal 3:13; Kum 8:18; Mit 3:16Utajiri na heshima viko kwangu,

utajiri udumuo na mafanikio.

198:19 Mit 3:13-14; 10:20Tunda langu ni bora kuliko dhahabu safi;

kile nitoacho hupita fedha iliyo bora.

20Natembea katika njia ya unyofu

katika mapito ya haki,

218:21 Mit 15:6; 24:4nawapa utajiri wale wanipendao

na kuzijaza hazina zao.

228:22 Mit 3:19; Yn 1:1Bwana aliniumba mwanzoni mwa kazi yake,

kabla ya matendo yake ya zamani;

238:23 Mwa 1:26; Za 2:6; Mik 5:2; Yn 17:24niliteuliwa tangu milele,

tangu mwanzoni, kabla ya dunia kuumbwa.

248:24 Mwa 7:11Wakati hazijakuwepo bahari, nilikwishazaliwa,

wakati hazijakuwepo chemchemi zilizojaa maji;

258:25 Ay 15:7kabla milima haijawekwa mahali pake,

kabla vilima havijakuwepo, nilikwishazaliwa,

268:26 Za 90:2kabla hajaumba dunia wala mashamba yake

au vumbi lolote la dunia.

278:27 Ay 26:7; Mit 3:19Nilikuwepo alipoziweka mbingu mahali pake,

wakati alichora mstari wa upeo wa macho

juu ya uso wa kilindi,

288:28 Ay 36:29; Mwa 1:7; Ay 9:8; 26:10wakati aliweka mawingu juu

na kuziweka imara chemchemi za bahari,

298:29 Ay 38:8-10; 1Sam 2:8wakati aliiwekea bahari mpaka wake

ili maji yasivunje agizo lake,

na wakati aliweka misingi ya dunia.

30Wakati huo nilikuwa fundi stadi kando yake.

Nilijazwa na furaha siku baada ya siku,

nikifurahi daima mbele zake,

318:31 Ay 28:25-27; Yn 1:1-4nikifurahi katika dunia yake yote

nami nikiwafurahia wanadamu.

328:32 Lk 11:28; 2Sam 22:22; Za 119:1-2“Basi sasa wanangu, nisikilizeni;

heri wale wanaozishika njia zangu.

33Sikilizeni mafundisho yangu mwe na hekima;

msiyapuuze.

348:34 1Fal 10:8; Mit 3:13-18; Flp 3:8-9Heri mtu yule anisikilizaye mimi,

akisubiri siku zote malangoni mwangu,

akingoja kwenye vizingiti vya mlango wangu.

358:35 Yn 3:16, 36; Flp 3:8, 9; Mit 13:18; 9:6; Yn 5:39-40Kwa maana yeyote anipataye mimi amepata uzima

na kujipatia kibali kutoka kwa Bwana.

368:36 Isa 3:9; Yer 40:2Lakini yeyote ashindwaye kunipata

hujiumiza mwenyewe;

na wote wanichukiao mimi hupenda mauti.”