John 7 – NIRV & NEN

New International Reader’s Version

John 7:1-53

Jesus Goes to the Feast of Booths

1After this, Jesus went around in Galilee. He didn’t want to travel around in Judea. That was because the Jewish leaders there were looking for a way to kill him. 2The Jewish Feast of Booths was near. 3Jesus’ brothers said to him, “Leave Galilee and go to Judea. Then your disciples there will see the works that you do. 4No one who wants to be well known does things in secret. Since you are doing these things, show yourself to the world.” 5Even Jesus’ own brothers did not believe in him.

6So Jesus told them, “The time for me to show who I really am is not here yet. For you, any time would be the right time. 7The people of the world can’t hate you. But they hate me. This is because I am a witness that their works are evil. 8You go to the feast. I am not going up to this feast. This is because my time has not yet fully come.” 9After he said this, he stayed in Galilee.

10But when his brothers had left for the feast, he went also. But he went secretly, not openly. 11At the feast the Jewish leaders were watching for Jesus. They were asking, “Where is he?”

12Many people in the crowd were whispering about him. Some said, “He is a good man.”

Others replied, “No. He fools the people.” 13But no one would say anything about him openly. They were afraid of the leaders.

Jesus Teaches at the Feast

14Jesus did nothing until halfway through the feast. Then he went up to the temple courtyard and began to teach. 15The Jews there were amazed. They asked, “How did this man learn so much without being taught?”

16Jesus answered, “What I teach is not my own. It comes from the one who sent me. 17Here is how someone can find out whether my teaching comes from God or from me. That person must choose to do what God wants them to do. 18Whoever speaks on their own does it to get personal honor. But someone who works for the honor of the one who sent him is truthful. Nothing about him is false. 19Didn’t Moses give you the law? But not one of you obeys the law. Why are you trying to kill me?”

20“You are controlled by demons,” the crowd answered. “Who is trying to kill you?”

21Jesus said to them, “I did one miracle, and you are all amazed. 22Moses gave you circumcision, and so you circumcise a child on the Sabbath day. But circumcision did not really come from Moses. It came from Abraham. 23You circumcise a boy on the Sabbath day. You think that if you do, you won’t break the law of Moses. Then why are you angry with me? I healed a man’s entire body on the Sabbath day! 24Stop judging only by what you see. Judge in the right way.”

People Don’t Agree About Who Jesus Is

25Then some of the people of Jerusalem began asking questions. They said, “Isn’t this the man some people are trying to kill? 26Here he is! He is speaking openly. They aren’t saying a word to him. Have the authorities really decided that he is the Messiah? 27But we know where this man is from. When the Messiah comes, no one will know where he is from.”

28Jesus was still teaching in the temple courtyard. He cried out, “Yes, you know me. And you know where I am from. I am not here on my own authority. The one who sent me is true. You do not know him. 29But I know him. I am from him, and he sent me.”

30When he said this, they tried to arrest him. But no one laid a hand on him. The time for him to show who he really was had not yet come. 31Still, many people in the crowd believed in him. They said, “How will it be when the Messiah comes? Will he do more signs than this man?”

32The Pharisees heard the crowd whispering things like this about him. Then the chief priests and the Pharisees sent temple guards to arrest him.

33Jesus said, “I am with you for only a short time. Then I will go to the one who sent me. 34You will look for me, but you won’t find me. You can’t come where I am going.”

35The Jews said to one another, “Where does this man plan to go? Does he think we can’t find him? Will he go where our people live scattered among the Greeks? Will he go there to teach the Greeks? 36What did he mean when he said, ‘You will look for me, but you won’t find me’? And what did he mean when he said, ‘You can’t come where I am going’?”

37It was the last and most important day of the feast. Jesus stood up and spoke in a loud voice. He said, “Let anyone who is thirsty come to me and drink. 38Does anyone believe in me? Then, just as Scripture says, rivers of living water will flow from inside them.” 39When he said this, he meant the Holy Spirit. Those who believed in Jesus would receive the Spirit later. Up to that time, the Spirit had not been given. This was because Jesus had not yet received glory.

40The people heard his words. Some of them said, “This man must be the Prophet we’ve been expecting.”

41Others said, “He is the Messiah.”

Still others asked, “How can the Messiah come from Galilee? 42Doesn’t Scripture say that the Messiah will come from the family line of David? Doesn’t it say that he will come from Bethlehem, the town where David lived?” 43So the people did not agree about who Jesus was. 44Some wanted to arrest him. But no one laid a hand on him.

The Jewish Leaders Do Not Believe

45Finally the temple guards went back to the chief priests and the Pharisees. They asked the guards, “Why didn’t you bring him in?”

46“No one ever spoke the way this man does,” the guards replied.

47“You mean he has fooled you also?” the Pharisees asked. 48“Have any of the rulers or Pharisees believed in him? 49No! But this mob knows nothing about the law. There is a curse on them.”

50Then Nicodemus, a Pharisee, spoke. He was the one who had gone to Jesus earlier. He asked, 51“Does our law find a man guilty without hearing him first? Doesn’t it want to find out what he is doing?”

52They replied, “Are you from Galilee too? Look into it. You will find that a prophet does not come out of Galilee.”

53Then they all went home.

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Yohana 7:1-53

Kutokuamini Kwa Ndugu Zake Yesu

17:1 Yn 1:19; 5:18; Mt 12:18Baada ya mambo haya, Yesu alikwenda sehemu mbalimbali za Galilaya. Hakutaka kwenda Uyahudi kwa sababu Wayahudi huko walitaka kumuua. 27:2 Law 23:34; Kum 16:16Sikukuu ya Vibanda ya Wayahudi ilikuwa imekaribia. 37:3 Mt 12:46Hivyo ndugu zake Yesu wakamwambia, “Ondoka hapa uende Uyahudi ili wanafunzi Wako wapate kuona miujiza unayofanya. 4Mtu anayetaka kujulikana hafanyi mambo yake kwa siri. Kama unafanya mambo haya, jionyeshe kwa ulimwengu.” 57:5 Za 69:8; Mk 3:21Hata ndugu zake mwenyewe hawakumwamini.

67:6 Mt 26:18Yesu akawaambia, “Wakati wangu bado haujawadia, lakini wakati wenu upo siku zote. 77:7 Yn 3:19-20; 15:18-19Ulimwengu hauwezi kuwachukia ninyi, lakini unanichukia mimi kwa sababu ninawashuhudia kwamba matendo yao ni maovu. 87:8 Yn 7:6; Mt 26:18; Yn 8:30Ninyi nendeni kwenye Sikukuu, lakini mimi sitahudhuria Sikukuu hii kwa sababu wakati wangu haujawadia.” 9Akiisha kusema hayo, akabaki Galilaya.

Yesu Kwenye Sikukuu Ya Vibanda

10Lakini ndugu zake walipokwisha kuondoka kwenda kwenye Sikukuu, yeye pia alikwenda lakini kwa siri. 117:11 Yn 11:56Wayahudi walikuwa wakimtafuta huko kwenye Sikukuu na kuulizana, “Yuko wapi huyu mtu?”

127:12 Yn 9:16; 10:19; Mt 21:46; Lk 7:16; Yn 6:14Kulikuwa na minongʼono iliyoenea kumhusu Yesu katika umati wa watu, wakati wengine wakisema, “Ni mtu mwema.”

Wengine walikuwa wakisema, “La, yeye anawadanganya watu.” 137:13 Yn 19:38; 20:19Lakini hakuna mtu yeyote aliyemsema waziwazi kumhusu kwa sababu ya kuwaogopa Wayahudi.

Yesu Afundisha Kwenye Sikukuu

147:14 Mt 26:55Ilipokaribia katikati ya Sikukuu, Yesu alipanda kwenda Hekaluni na kuanza kufundisha. 157:15 Mdo 26:24; Mt 13:54Wayahudi wakastaajabia mafundisho yake wakasema, “Mtu huyu amepataje kujua mambo haya bila kufundishwa?”

167:16 Yn 3:11; 14:24Ndipo Yesu akawajibu, “Mafundisho yangu si yangu mwenyewe, bali yanatoka kwake yeye aliyenituma. 177:17 Za 25:14; Yn 8:23Mtu yeyote akipenda kufanya mapenzi ya Mungu, atajua kama mafundisho yangu yanatoka kwa Mungu au ninasema kwa ajili yangu mwenyewe. 187:18 Yn 5:41; 8:50-54Wale wanenao kwa ajili yao wenyewe hufanya hivyo kwa kutaka utukufu wao wenyewe. Lakini yeye atafutaye utukufu wa yule aliyemtuma ni wa kweli, wala hakuna uongo ndani yake. 197:19 Kum 32:46; Mt 12:14Je, Mose hakuwapa ninyi sheria? Lakini hakuna hata mmoja wenu anayeishika hiyo sheria. Kwa nini mnataka kuniua?”

207:20 Mk 3:22; Yn 10:20Ule umati wa watu ukamjibu, “Wewe una pepo mchafu! Ni nani anayetaka kukuua?”

217:21 Yn 5:16Yesu akawajibu, “Nimefanya muujiza mmoja na nyote mkastaajabu. 227:22 Law 12:3; Mwa 17:10-14Lakini kwa kuwa Mose aliwaamuru tohara (ingawa kwa kweli haikutoka kwa Mose bali kwa baba zenu wakuu), mnamtahiri mtoto hata siku ya Sabato. 237:23 Yn 5:8Ikiwa mtoto aweza kutahiriwa siku ya Sabato kusudi sheria ya Mose isivunjwe, kwa nini mnanikasirikia kwa kumponya mtu mwili wake wote siku ya Sabato? 247:24 1Sam 16:7; 2Nya 10:7; Yn 8:15Acheni kuhukumu mambo kwa jinsi mnavyoona tu, bali hukumuni kwa haki.”

Je, Yesu Ndiye Kristo?

257:25 Yn 7:19Ndipo baadhi ya watu wa Yerusalemu wakawa wanasema, “Tazameni, huyu si yule mtu wanayetaka kumuua? 267:26 Yn 7:48; 4:29Mbona yuko hapa anazungumza hadharani na wala hawamwambii neno lolote? Je, inawezekana viongozi wanafahamu kuwa huyu ndiye Kristo?7:26 Kristo maana yake ni Masiya, yaani Aliyetiwa mafuta. 277:27 Mt 13:55; Lk 4:22Tunafahamu huyu mtu anakotoka, lakini Kristo atakapokuja, hakuna yeyote atakayejua atokako.”

287:28 Yn 8:14, 26, 42Ndipo Yesu, akaendelea kufundisha Hekaluni, akisema, “Ninyi mnanifahamu na kujua nitokako. Mimi sikuja kwa ajili yangu mwenyewe, bali yeye aliyenituma ni wa kweli na ninyi hammjui. 297:29 Mt 11:27Mimi namjua kwa kuwa nimetoka kwake, naye ndiye alinituma.”

307:30 Yn 10:39Ndipo wakatafuta kumkamata, lakini hakuna mtu yeyote aliyethubutu kumshika kwa sababu saa yake ilikuwa bado haijawadia. 317:31 Yn 11:45; 12:11, 42; 2:11Nao watu wengi wakamwamini, wakasema, “Je, Kristo atakapokuja, atafanya miujiza mikuu zaidi kuliko aliyoifanya mtu huyu?”

Walinzi Wanatumwa Kumkamata Yesu

32Mafarisayo wakasikia watu wakinongʼona mambo kama hayo kuhusu Yesu, ndipo wao pamoja na viongozi wa makuhani wakatuma walinzi wa Hekalu waende kumkamata.

337:33 Yn 16:5, 10, 17, 28Yesu akasema, “Mimi bado niko pamoja nanyi kwa kitambo kidogo, kisha nitarudi kwake yeye aliyenituma. 347:34 Yn 8:21; 13:33Mtanitafuta lakini hamtaniona, nami niliko ninyi hamwezi kuja.”

357:35 Yak 1:1; Mdo 17:4; 1Pet 1:1Wayahudi wakaulizana wao kwa wao, “Huyu mtu anataka kwenda wapi ambako hatuwezi kumfuata? Je, anataka kwenda kwa Wayunani ambako baadhi ya watu wetu wametawanyikia, akawafundishe Wayunani? 367:36 Yn 7:34Yeye ana maana gani anaposema, ‘Mtanitafuta lakini hamtaniona,’ na, ‘nami niliko ninyi hamwezi kuja’?”

Mito Ya Maji Ya Uzima

377:37 Law 23:36; Isa 55:1; Ufu 22:17Siku ile ya mwisho ya Sikukuu, siku ile kuu, wakati Yesu akiwa amesimama huko, akapaza sauti yake akasema, “Kama mtu yeyote anaona kiu na aje kwangu anywe. 387:38 Isa 58:1; Yn 4:10Yeyote aniaminiye mimi, kama Maandiko yasemavyo, vijito vya maji ya uzima vitatiririka ndani mwake.” 397:39 Yoe 2:28; Mdo 2:17, 33; Yn 20:22; 12:23; 13:31-32Yesu aliposema haya alimaanisha Roho Mtakatifu ambaye wote waliomwamini wangempokea, kwani mpaka wakati huo, Roho alikuwa hajatolewa, kwa kuwa Yesu alikuwa bado hajatukuzwa.

Mgawanyiko Miongoni Mwa Watu

407:40 Mt 2:11; Yn 1:21Waliposikia maneno hayo, baadhi ya watu miongoni mwa ule umati wakasema, “Hakika huyu ndiye yule Nabii.”

417:41 Yn 7:52; 1:21Wengine wakasema, “Huyu ndiye Kristo!”

Lakini wengine wakauliza, “Je, Kristo kwao ni Galilaya? 427:42 Mt 1:1; Mik 5:2; Mt 2:5-6Je, Maandiko hayasemi kwamba Kristo atakuja kutoka jamaa ya Daudi na kutoka Bethlehemu, mji alioishi Daudi?” 437:43 Yn 9:16; 10:9Kwa hiyo watu wakagawanyika kwa ajili ya Yesu. 447:44 Yn 7:30Baadhi yao walitaka kumkamata, lakini hakuna aliyethubutu kumgusa.

Kutokuamini Kwa Viongozi Wa Wayahudi

457:45 Yn 7:32Hatimaye wale walinzi wa Hekalu wakarudi kwa viongozi wa makuhani na Mafarisayo waliokuwa wamewatuma ili kumkamata Yesu, wakaulizwa, “Mbona hamkumkamata?”

467:46 Mt 7:28Wale walinzi wakajibu, “Kamwe hajanena mtu yeyote kama yeye anenavyo.”

477:47 Yn 7:12Mafarisayo wakajibu, “Je, nanyi pia mmedanganyika? 487:48 Yn 12:42Je, kuna kiongozi yeyote au mmoja wa Mafarisayo ambaye amemwamini? 49Lakini huu umati wa watu wasiojua Sheria ya Mose, wamelaaniwa.”

507:50 Yn 3:1Ndipo Nikodemo, yule aliyekuwa amemwendea Yesu siku moja usiku, ambaye alikuwa mmoja wao akauliza, 517:51 Kum 1:16, 17; 19:15“Je, sheria zetu zinaturuhusu kumhukumu mtu kabla ya kumsikiliza na kufahamu alilotenda?”

527:52 Yn 1:46; 7:41Wakamjibu, “Je, wewe pia unatoka Galilaya? Chunguza nawe utaona kwamba hakuna nabii atokae Galilaya!” [ 53Kisha wakaondoka, kila mtu akarudi nyumbani kwake.