Acts 24 – NIRV & NEN

New International Reader’s Version

Acts 24:1-27

Paul’s Trial in Front of Felix

1Five days later Ananias the high priest went down to Caesarea. Some elders and a lawyer named Tertullus went with him. They brought their charges against Paul to the governor. 2So Paul was called in. Tertullus began to bring the charges against Paul. He said to Felix, “We have enjoyed a long time of peace while you have been ruling. You are a wise leader. You have made this a better nation. 3Most excellent Felix, we gladly admit this everywhere and in every way. And we are very thankful. 4I don’t want to bother you. But would you be kind enough to listen to us for a short time?

5“We have found that Paul is a troublemaker. This man stirs up trouble among Jews all over the world. He is a leader of those who follow Jesus of Nazareth. 6-7He even tried to make our temple impure. So we arrested him. 8Question him yourself. Then you will learn the truth about all these charges we are bringing against him.”

9The other Jews said the same thing. They agreed that the charges were true.

10The governor motioned for Paul to speak. Paul said, “I know that you have been a judge over this nation for quite a few years. So I am glad to explain my actions to you. 11About 12 days ago I went up to Jerusalem to worship. You can easily check on this. 12Those bringing charges against me did not find me arguing with anyone at the temple. I wasn’t stirring up a crowd in the synagogues or anywhere else in the city. 13They can’t prove to you any of the charges they are making against me. 14It is true that I worship the God of our people. I am a follower of the Way of Jesus. Those bringing charges against me call it a cult. I believe everything that is in keeping with the Law. I believe everything that is in keeping with what is written in the Prophets. 15I have the same hope in God that these men themselves have. I believe that both the godly and the ungodly will rise from the dead. 16So I always try not to do anything wrong in the eyes of God or in the eyes of people.

17“I was away for several years. Then I came to Jerusalem to bring my people gifts for those who were poor. I also came to offer sacrifices. 18They found me doing this in the temple courtyard. I had already been made pure and ‘clean’ in the usual way. There was no crowd with me. I didn’t stir up any trouble. 19But there are some other Jews who should be here in front of you. They are from Asia Minor. They should bring charges if they have anything against me. 20Let the Jews who are here tell you what crime I am guilty of. After all, I was put on trial by the Sanhedrin. 21Perhaps they blame me for what I said when I was on trial. I shouted, ‘I believe that people will rise from the dead. That is why I am on trial here today.’ ”

22Felix knew all about the Way of Jesus. So he put off the trial for the time being. “Lysias the commanding officer will come,” he said. “Then I will decide your case.” 23He ordered the commander to keep Paul under guard. He told him to give Paul some freedom. He also told him to allow Paul’s friends to take care of his needs.

24Several days later Felix came with his wife Drusilla. She was a Jew. Felix sent for Paul and listened to him speak about faith in Christ Jesus. 25Paul talked about how to live a godly life. He talked about how people should control themselves. He also talked about the time when God will judge everyone. Then Felix became afraid. “That’s enough for now!” he said. “You may leave. When I find the time, I will send for you.” 26He was hoping that Paul would offer him some money to let him go. So he often sent for Paul and talked with him.

27Two years passed. Porcius Festus took the place of Felix. But Felix wanted to do the Jews a favor. So he left Paul in prison.

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Matendo 24:1-27

Mbele Ya Feliksi Huko Kaisaria

124:1 Mdo 23:2; 23:30-35; 23:24Baada ya siku tano, kuhani mkuu Anania akashuka akiwa amefuatana na baadhi ya wazee pamoja na mwanasheria mmoja aitwaye Tertulo, nao wakaleta mashtaka yao dhidi ya Paulo mbele ya mtawala. 224:2 Lk 1:3; Mdo 23:26Paulo alipoitwa aingie ndani, Tertulo akaanza kutoa mashtaka akisema, “Mtukufu Feliksi, kwa muda mrefu tumefurahia amani na matengenezo mengi mazuri yamefanywa kwa ajili ya watu hawa kwa sababu ya upeo wako wa kuona mambo ya mbele. 324:3 Lk 1:3; Mdo 23:26; 26:25Wakati wote na kila mahali, kwa namna yoyote, mtukufu sana Feliksi, tumeyapokea mambo haya yote kwa shukrani nyingi. 4Lakini nisije nikakuchosha zaidi, ningekuomba kwa hisani yako utusikilize kwa kifupi.

524:5 Mdo 16:20; 17:6; 21:28; Mk 1:24; Mdo 28:22“Tumemwona mtu huyu kuwa ni msumbufu, anayechochea ghasia miongoni mwa Wayahudi duniani pote. Yeye ndiye kiongozi wa dhehebu la Wanazarayo, 624:6 Mdo 21:28na hata amejaribu kulinajisi Hekalu, hivyo tukamkamata; [tukataka kumhukumu kufuatana na sheria zetu. 7Lakini jemadari Lisia alitujia na nguvu nyingi, akamwondoa mikononi mwetu, 8akiwaamuru washtaki wake waje mbele yako: ili] kwa kumchunguza wewe mwenyewe unaweza kujua kutoka kwake mambo yote tunayomshtaki kwayo.”

924:9 1The 2:16Pia wale Wayahudi wakaunga mkono wakithibitisha kuwa mashtaka yote haya ni kweli.

Paulo Ajitetea Mbele Ya Feliksi

1024:10 Mdo 23:24Mtawala Feliksi alipompungia Paulo mkono ili ajitetee, yeye akajibu, “Najua kwamba wewe umekuwa hakimu katika taifa hili kwa miaka mingi, hivyo natoa utetezi wangu kwa furaha. 1124:11 Mdo 21:27Unaweza kuhakikisha kwa urahisi kuwa hazijapita zaidi ya siku kumi na mbili tangu nilipopanda kwenda Yerusalemu kuabudu. 1224:12 Mdo 25:8; 28:17Hawa wanaonishtaki hawakunikuta nikibishana na mtu yeyote Hekaluni au kuchochea umati wa watu katika sinagogi au mahali pengine popote mjini. 1324:13 Mdo 25:7Wala hawawezi kabisa kukuthibitishia mashtaka haya wanayonishtaki kwayo. 1424:14 Mdo 3:13; 9:2; 26:6, 22; 28:23Lakini, ninakubali kwamba mimi namwabudu Mungu wa baba zetu, mfuasi wa Njia, ile ambayo wao wanaiita dhehebu. Ninaamini kila kitu kinachokubaliana na Sheria na kile kilichoandikwa katika Manabii, 1524:15 Mdo 23:6; 28:20; Dan 12:12; Mt 25:46nami ninalo tumaini kwa Mungu, ambalo hata wao wenyewe wanalikubali kwamba kutakuwa na ufufuo wa wafu, kwa wenye haki na wasio na haki. 1624:16 Mdo 23:1Kwa hiyo ninajitahidi siku zote kuwa na dhamiri safi mbele za Mungu na mbele za wanadamu.

1724:17 Mdo 11:29, 30; Rum 15:25-28, 31; 1Kor 16:1-4, 15; 2Kor 8:1-4; Gal 2:10“Basi, baada ya kutokuwepo kwa miaka mingi nilikuja Yerusalemu ili kuwaletea watu wangu msaada kwa ajili ya maskini na kutoa dhabihu. 1824:18 Mdo 21:26Nilikuwa nimeshatakaswa kwa taratibu za kiibada waliponikuta Hekaluni nikifanya mambo haya. Hapakuwa na umati wa watu, pamoja nami wala aliyehusika kwenye fujo yoyote. 1924:19 Mdo 23:30Lakini kulikuwa na baadhi ya Wayahudi kutoka Asia, ambao wangelazimika wawepo hapa mbele yako ili watoe mashtaka kama wanalo jambo lolote dhidi yangu. 20Au, watu hawa walioko hapa waseme ni uhalifu gani walioniona nao waliponisimamisha mbele ya baraza, 2124:21 Mdo 23:6isipokuwa ni kuhusu jambo hili moja nililopiga kelele mbele yao kwamba, ‘Mimi nashtakiwa mbele yenu leo kwa sababu ya ufufuo wa wafu.’ ”

2224:22 Mdo 9:2; 24:7Basi Feliksi ambaye alikuwa anafahamu vizuri habari za Njia ile, akaahirisha shauri lile kwa maelezo yake akisema, “Wakati jemadari Lisia atakapoteremka huku, nitaamua shauri lako.” 2324:23 Mdo 23:35; 28:16; 23:16; 27:3Ndipo akaamuru kiongozi wa askari amweke chini ya ulinzi lakini ampe uhuru na kuwaruhusu rafiki zake wamhudumie.

2424:24 Mdo 20:21Baada ya siku kadhaa, Feliksi alikuja pamoja na Drusila mkewe, ambaye alikuwa Myahudi. Alituma aitiwe Paulo, naye akamsikiliza alipokuwa akinena juu ya imani katika Kristo Yesu. 2524:25 Gal 5:23; 1Pet 4:7; Mdo 10:42Naye Paulo alipokuwa akinena juu ya haki, kuwa na kiasi na juu ya hukumu ijayo, Feliksi aliingiwa na hofu na kusema, “Hiyo yatosha sasa! Waweza kuondoka. Nitakapokuwa na wasaa nitakuita.” 26Wakati huo Feliksi alitazamia kwamba Paulo angempa rushwa. Hivyo akawa anamwita mara kwa mara na kuzungumza naye.

2724:27 Mdo 25:1, 4, 9, 14; 12:3; 25:9; 23:35; 25:14Baada ya miaka miwili kupita, Porkio Festo akaingia kwenye utawala mahali pa Feliksi, lakini kwa kuwa Feliksi alitaka kuwapendeza Wayahudi, akamwacha Paulo gerezani.