2 Samuel 6 – NIRV & NEN

New International Reader’s Version

2 Samuel 6:1-23

David Brings the Ark to Jerusalem

1Again David brought together the best soldiers in Israel. The total number was 30,000. 2He and all his men went to Baalah in Judah. They wanted to bring the ark of God up to Jerusalem from there. The ark is named after the Lord. He is the Lord who rules over all. He sits on his throne between the cherubim that are on the ark. 3The ark of God was placed on a new cart. Then it was brought from Abinadab’s house, which was on a hill. Uzzah and Ahio were guiding the cart. They were the sons of Abinadab. 4The ark of God was on the cart. Ahio was walking in front of it. 5David was celebrating with all his might in front of the Lord. So was the whole community of Israel. All of them were playing castanets, harps, lyres, tambourines, rattles and cymbals.

6They came to the threshing floor of Nakon. The oxen nearly fell there. So Uzzah reached out and took hold of the ark of God. 7Then the Lord was very angry with Uzzah. That’s because what Uzzah did showed that he didn’t have any respect for the Lord. So God struck him down. He died there beside the ark of God.

8David was angry because the Lord’s great anger had broken out against Uzzah. That’s why the place is still called Perez Uzzah to this day.

9David was afraid of the Lord that day. He asked, “How can the ark of the Lord ever be brought to me?” 10He didn’t want to take the ark of the Lord to be with him in the City of David. Instead, he took it to the house of Obed-Edom. Obed-Edom was from Gath. 11The ark of the Lord remained in Obed-Edom’s house for three months. And the Lord blessed him and his whole family.

12King David was told, “The Lord has blessed the family of Obed-Edom. He has also blessed everything that belongs to him. That’s because the ark of God is in Obed-Edom’s house.” So David went down there to bring up the ark. With great joy he brought it up from the house of Obed-Edom. He took it to the City of David. 13Those carrying the ark of the Lord took six steps forward. Then David sacrificed a bull and a fat calf. 14David was wearing a sacred linen apron. He danced in front of the Lord with all his might. 15He did it while he was bringing up the ark of the Lord. The whole community of Israel helped him bring it up. They shouted. They blew trumpets.

16The ark of the Lord was brought into the City of David. Saul’s daughter Michal was watching from a window. She saw King David leaping and dancing in front of the Lord. That made her hate him in her heart.

17The ark of the Lord was brought into Jerusalem. It was put in its place in the tent David had set up for it. David sacrificed burnt offerings and friendship offerings to the Lord. 18After he finished sacrificing those offerings, he blessed the people in the name of the Lord who rules over all. 19He gave to each Israelite man and woman a loaf of bread. He also gave each one a date cake and a raisin cake. Then all the people went home.

20David returned home to bless his family. Saul’s daughter Michal came out to meet him. She said, “You are the king of Israel. You have really brought honor to yourself today, haven’t you? You have gone around half-naked right in front of the female slaves of your officials. You acted like a fool!”

21David said to Michal, “I did it to honor the Lord. He chose me instead of your father or anyone else in Saul’s family. The Lord appointed me ruler over his people Israel. I will celebrate to honor the Lord. 22And that’s not all. I will bring even less honor to myself. I will bring even more shame on myself. But those female slaves you spoke about will honor me.”

23Saul’s daughter Michal didn’t have any children as long as she lived.

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

2 Samweli 6:1-23

Sanduku La Mungu Laletwa Yerusalemu

(1 Nyakati 13:1-14; 15:25–16:6, 43)

16:1 Za 80:1; 1Nya 13:5Tena Daudi akakusanya watu 30,000 wa Israeli waliochaguliwa. 26:2 Yos 15:9; 1Sam 4:4; 7:1; Law 24:16; Kum 28:10; Isa 63:10; Za 99:1; 132:14; Mwa 3:24; Kut 25:22Yeye na watu wake wote wakatoka Baala ya Yuda6:2 Baala ya Yuda ni jina la Kiebrania; yaani Kiriath-Yearimu. kulipandisha Sanduku la Mungu kutoka huko, linaloitwa kwa Jina, naam, jina la Bwana Mwenye Nguvu Zote, ambaye anaketi katika kiti cha enzi kati ya makerubi walioko juu ya hilo Sanduku. 36:3 Hes 7:4-6; 1Sam 6:7; 2Sam 7:1Wakaweka hilo Sanduku la Mungu juu ya gari jipya la kukokotwa na kulileta kutoka nyumba ya Abinadabu, iliyokuwa juu ya kilima. Uza na Ahio, wana wa Abinadabu, walikuwa wakiongoza hilo gari jipya la kukokotwa 4likiwa na Sanduku la Mungu juu yake, naye Ahio alikuwa anatembea akiwa mbele yake. 56:5 Kut 15:20; Ezr 3:10; Neh 12:27; Za 105:5Daudi na nyumba yote ya Israeli walikuwa wanacheza mbele za Bwana kwa nguvu zao zote, kwa nyimbo, vinubi, zeze, matari, kayamba na matoazi.

66:6 Hes 4:15, 19-20; 1Nya 13:9Walipofika kwenye uwanja wa kupuria nafaka wa Nakoni, Uza akanyoosha mkono na kulishika Sanduku la Mungu kwa sababu maksai walijikwaa. 76:7 1Nya 15:13-15; Kut 19:23; 1Sam 5:6; 6:19; 25:32Hasira ya Bwana ikawaka dhidi ya Uza kwa sababu ya kitendo chake cha kukosa heshima, kwa hiyo Mungu akampiga akafia papo hapo kando ya Sanduku la Mungu.

86:8 Za 7:11; Mwa 38:29Ndipo Daudi akakasirika kwa sababu ghadhabu ya Bwana ilifurika dhidi ya Uza, hivyo hadi leo mahali hapo panaitwa Peres-Uza.

96:9 1Sam 6:20; Za 119:120; Hes 17:12-13; 1Sam 5:10-11; Lk 5:8Daudi akamwogopa Bwana siku ile, akasema, “Ni jinsi gani Sanduku la Bwana litakavyoweza kunijia?” 106:10 1Nya 15:18; 26:4-5; 13:13Hakuwa radhi kulichukua Sanduku la Bwana kwake katika Mji wa Daudi. Badala yake akalipeleka kwenye nyumba ya Obed-Edomu, Mgiti. 116:11 Mwa 30:27; 39:5; Mit 3:9-10; Isa 61:9Sanduku la Bwana likabaki katika nyumba ya Obed-Edomu, Mgiti, kwa miezi mitatu, naye Bwana akambariki pamoja na nyumba yake yote.

126:12 1Fal 8:1; 1Nya 15:25Kisha Mfalme Daudi akaambiwa, “Bwana ameibariki nyumba ya Obed-Edomu pamoja na kila alicho nacho, kwa sababu ya Sanduku la Mungu.” Basi Daudi akateremka na kulipandisha Sanduku la Mungu kutoka nyumba ya Obed-Edomu hadi Mji wa Daudi kwa shangwe. 136:13 1Fal 8:5, 62; Ezr 6:17; Hes 4:15; Yos 3:3; 1Nya 15:2, 15; 2Nya 5:6Wale waliokuwa wamebeba Sanduku la Bwana walipokuwa wametembea hatua sita, Daudi alitoa dhabihu fahali na ndama aliyenoneshwa. 146:14 Kut 19:6; 1Sam 2:18; Kut 15:20; Amu 11:34; 21:21; Za 30:11; 1Nya 15:27Daudi, akiwa amevaa kisibau cha kitani, alicheza mbele za Bwana kwa nguvu zake zote, 156:15 Yos 6:5; Za 47:5; 98:6wakati yeye na nyumba yote ya Israeli walipopandisha Sanduku la Bwana kwa shangwe na sauti za tarumbeta.

166:16 2Sam 5:7; 1Sam 18:27Ikawa Sanduku la Bwana lilipokuwa linaingia katika Mji wa Daudi, Mikali binti Sauli akachungulia dirishani. Naye alipomwona Mfalme Daudi akirukaruka na kucheza mbele za Bwana, akamdharau moyoni mwake.

176:17 1Fal 8:6; 1Nya 15:1; 2Nya 1:4; Law 1:1-17; 1Fal 8:62-64; Za 132:8Wakaleta Sanduku la Bwana na kuliweka mahali pake ndani ya hema ambalo Daudi alikuwa amelisimamisha kwa ajili yake, naye Daudi akatoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani mbele za Bwana. 186:18 1Fal 8:22; Kut 39:43Baada ya kumaliza kutoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani, Daudi akawabariki watu katika jina la Bwana Mwenye Nguvu Zote. 196:19 Hos 3:1; Kum 26:13; Neh 8:10Kisha akatoa mkate, andazi la tende na andazi la zabibu kavu kwa kila mtu katika mkutano wote wa Waisraeli, wanaume kwa wanawake. Nao watu wote wakaenda nyumbani kwao.

206:20 1Sam 19:24; Mhu 7:16; Isa 59:15; Amu 9:4Daudi aliporudi ili kuwabariki watu wa nyumbani mwake, Mikali binti Sauli akatoka nje kumlaki, akamwambia, “Tazama jinsi mfalme wa Israeli alivyojibainisha mwenyewe leo kwa kuvua mavazi yake machoni pa vijakazi wa watumishi wake, kama vile ambavyo mtu asiye na adabu angelifanya!”

216:21 1Sam 13:14; 15:28; 2Sam 5:2; 7:8; 1Nya 5:2; 17:7; Mik 5:2Daudi akamwambia Mikali, “Nilifanya hivyo mbele za Bwana ambaye alinichagua mimi badala ya baba yako au mwingine yeyote kutoka nyumba yake wakati aliponiweka niwe mtawala juu ya Israeli, watu wa Bwana. Kwa hiyo nitacheza mbele za Bwana. 22Nitakuwa asiye na heshima zaidi kuliko sasa, nami nitajishusha machoni pangu mwenyewe. Lakini kwa hawa vijakazi uliosema habari zao nitaheshimiwa.”

236:23 1Sam 15:35; Isa 22:14Naye Mikali binti Sauli hakuwa na watoto mpaka siku ya kufa kwake.