Zekaria 6 – NEN & NIVUK

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Zekaria 6:1-15

Maono Ya Nane: Magari Manne Ya Vita

16:1 2Fal 2:12Nikatazama juu tena: nikaona mbele yangu magari manne ya vita yakija kutoka kati ya milima miwili, milima ya shaba! 26:2 Ufu 6:5; Zek 1:8Gari la kwanza lilivutwa na farasi wekundu, la pili lilivutwa na farasi weusi, 36:3 Ufu 6:2la tatu lilivutwa na farasi weupe na gari la nne lilivutwa na farasi wa madoadoa ya kijivu, wote wenye nguvu. 46:4 Zek 5:10Nikamuuliza malaika aliyekuwa akizungumza nami, “Hawa ni nani bwana wangu?”

56:5 Eze 37:9; Mt 24:31; Yos 3:11; Za 68:17; Ebr 1:7; 1:7, 14; Dan 7:10; Lk 1:19Malaika akanijibu, “Hizi ni roho nne za mbinguni zisimamazo mbele ya uwepo wa Bwana wa dunia yote, zinatoka kwenda kufanya kazi yake. 66:6 Yer 1:14Gari linalovutwa na farasi weusi linaelekea katika nchi ya kaskazini, la farasi weupe linaelekea magharibi na la farasi wa madoadoa ya kijivu linaelekea kusini.”

76:7 Isa 43:6; Mwa 13:17Wakati hao farasi wenye nguvu walipokuwa wakitoka, walikuwa wakijitahidi kwenda duniani kote. Akasema, “Nenda duniani kote!” Kwa hiyo wakaenda duniani kote.

86:8 Mhu 10:4; Eze 5:13; 24:13; Zek 1:10Kisha akaniita, “Tazama, wale wanaokwenda kuelekea nchi ya kaskazini wamepumzisha Roho yangu katika nchi ya kaskazini.”

Taji Kwa Ajili Ya Yoshua

9Neno la Bwana likanijia kusema: 106:10 Ezr 2:1; 7:14-16; Yer 28:6“Chukua fedha na dhahabu kutoka kwa watu waliohamishwa, yaani Heldai, Tobia na Yedaya ambao wamefika kutoka Babeli. Siku iyo hiyo nenda nyumbani kwa Yosia mwana wa Sefania. 116:11 Kut 28:36; Za 21:3; 1Nya 6:15; Ezr 2:2; 3:2; Zek 3:1Chukua fedha na dhahabu utengeneze taji, nawe uiweke kichwani mwa kuhani mkuu Yoshua, mwana wa Yehosadaki. 126:12 Isa 4:2; Eze 17:22; Ezr 3:8-10; Zek 4:6-9; Isa 9:6; Mik 5:5; Yer 23:5; 33:15; Zek 13:7; Mk 15:39; Lk 1:78; Yn 1:45; Za 80:15-17; Efe 2:20; Ebr 2:9Umwambie, hili ndilo asemalo Bwana Mwenye Nguvu Zote: ‘Huyu ndiye mtu ambaye jina lake ni Tawi, naye atachipua kutoka mahali pake na kujenga Hekalu la Bwana. 136:13 Za 110:4; 21:5Ni yeye atakayejenga Hekalu la Bwana, naye atavikwa utukufu na ataketi kumiliki katika kiti cha enzi naye atakuwa kuhani katika kiti chake cha enzi. Hapo patakuwa amani kati ya hao wawili.’ 146:14 Kut 28:12; Mk 14:9Taji itatolewa kwa Heldai, Tobia, Yedaya na Heni mwana wa Sefania kama kumbukumbu ndani ya Hekalu la Bwana. 156:15 Efe 2:13; Isa 60:10; Zek 2:9-11; Isa 58:12; Yer 7:23Wale walio mbali sana watakuja na kusaidia kulijenga Hekalu la Bwana, nanyi mtajua ya kwamba Bwana Mwenye Nguvu Zote amenituma kwenu. Hili litatokea ikiwa mtamtii Bwana Mungu wenu kwa bidii.”

New International Version – UK

Zechariah 6:1-15

Four chariots

1I looked up again, and there before me were four chariots coming out from between two mountains – mountains of bronze. 2The first chariot had red horses, the second black, 3the third white, and the fourth dappled – all of them powerful. 4I asked the angel who was speaking to me, ‘What are these, my lord?’

5The angel answered me, ‘These are the four spirits6:5 Or winds of heaven, going out from standing in the presence of the Lord of the whole world. 6The one with the black horses is going towards the north country, the one with the white horses towards the west,6:6 Or horses after them and the one with the dappled horses towards the south.’

7When the powerful horses went out, they were straining to go throughout the earth. And he said, ‘Go throughout the earth!’ So they went throughout the earth.

8Then he called to me, ‘Look, those going towards the north country have given my Spirit6:8 Or spirit rest in the land of the north.’

A crown for Joshua

9The word of the Lord came to me: 10‘Take silver and gold from the exiles Heldai, Tobijah and Jedaiah, who have arrived from Babylon. Go the same day to the house of Josiah son of Zephaniah. 11Take the silver and gold and make a crown, and set it on the head of the high priest, Joshua son of Jozadak.6:11 Hebrew Jehozadak, a variant of Jozadak 12Tell him this is what the Lord Almighty says: “Here is the man whose name is the Branch, and he will branch out from his place and build the temple of the Lord. 13It is he who will build the temple of the Lord, and he will be clothed with majesty and will sit and rule on his throne. And he6:13 Or there will be a priest on his throne. And there will be harmony between the two.” 14The crown will be given to Heldai,6:14 Syriac; Hebrew Helem Tobijah, Jedaiah and Hen6:14 Or and the gracious one, the son of Zephaniah as a memorial in the temple of the Lord. 15Those who are far away will come and help to build the temple of the Lord, and you will know that the Lord Almighty has sent me to you. This will happen if you diligently obey the Lord your God.’