Zaburi 91 – Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu) NEN

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Zaburi 91:1-16

Zaburi 91

Mungu Mlinzi Wetu

191:1 Kut 33:2; Isa 49:2; Mao 4:20; Za 63:7Yeye akaaye mahali pa salama pake Yeye Aliye Juu Sana,

atadumu katika uvuli wake Mwenyezi.91:1 Mwenyezi hapa ina maana ya Shaddai kwa Kiebrania.

291:2 Za 9:9; 91:9; 2Sam 22:2, 3Nitasema kumhusu Bwana, “Yeye ndiye kimbilio langu na ngome yangu,

Mungu wangu, ambaye ninamtumaini.”

391:3 Za 124:7; Mit 6:5; 1Fal 8:37Hakika yeye ataniokoa na mtego wa mwindaji,

na maradhi ya kuambukiza ya kuua.

491:4 Za 61:4; 17:8; 35:2; Rum 2:12; Kum 32:10; Isa 27:3; 31:5; Zek 12:8Atakufunika kwa manyoya yake,

chini ya mbawa zake utapata kimbilio,

uaminifu wake utakuwa ngao na kinga yako.

591:5 Ay 5:21; 5:19; Mit 3:23; Isa 43:2Hutaogopa vitisho vya usiku,

wala mshale urukao mchana,

6wala maradhi ya kuambukiza

yanayonyemelea gizani,

wala tauni iharibuyo adhuhuri.

7Ijapo watu elfu wataangukia kando yako,

kumi elfu mkono wako wa kuume,

lakini haitakukaribia wewe.

891:8 Za 37:34; 58:10; Mal 1:5Utatazama tu kwa macho yako

na kuona adhabu ya waovu.

9Kama ukimfanya Aliye Juu Sana kuwa makao yako:

naam, Bwana ambaye ni kimbilio langu,

1091:10 Mit 1:33; 12:21; 2The 3:3; 2Pet 2:9basi hakuna madhara yatakayokupata wewe,

hakuna maafa yataikaribia hema yako.

1191:11 Mwa 32:1; Ebr 1:14; Lk 4:10; Za 34:7; Mt 4:6Kwa kuwa atawaagiza malaika zake kwa ajili yako,

wakulinde katika njia zako zote.

1291:12 Lk 1:10, 11; Ay 5:23; Mt 4:6; Za 37:24Mikononi mwao watakuinua,

ili usijikwae mguu wako kwenye jiwe.

1391:13 Dan 6:22; Lk 10:19Utawakanyaga simba na nyoka wakali,

simba mkubwa na nyoka utawaponda kwa miguu.

1491:14 1Sam 2:30; Yn 12:26; Ay 22:27; Za 18:3; Yer 33:3; Zek 13:9; Ebr 5:7Bwana asema, “Kwa kuwa ananipenda, nitamwokoa;

nitamlinda, kwa kuwa analikiri Jina langu.

1591:15 Za 43:2; 1Sam 2:30Ataniita, nami nitamjibu;

nitakuwa pamoja naye katika taabu,

nitamwokoa na kumheshimu.

1691:16 Kum 6:2; Za 21:4; 50:23Kwa siku nyingi nitamshibisha

na kumwonyesha wokovu wangu.”