Zaburi 88 – Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu) NEN

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Zaburi 88:1-18

Zaburi 88

Kilio Kwa Ajili Ya Kuomba Msaada

Wimbo. Zaburi ya wana wa Kora. Kwa mwimbishaji. Mtindo wa mahalathi leanothi. Utenzi wa Hemani Mwezrahi.

188:1 Za 51:14; 3:4; 22:2; Lk 18:7Ee Bwana, Mungu uniokoaye,

nimelia mbele zako usiku na mchana.

2Maombi yangu yafike mbele zako,

utegee kilio changu sikio lako.

388:3 Ay 33:22; Isa 38:10; Za 6:3; 25:17; 107:18Kwa maana nafsi yangu imejaa taabu,

na maisha yangu yanakaribia kaburi.88:3 Kaburi hapa maana yake ni Kuzimu, kwa Kiebrania ni Sheol.

488:4 Za 31:12; 18:1Nimehesabiwa miongoni mwa wale waendao shimoni,

niko kama mtu asiye na nguvu.

588:5 Za 31:22Nimetengwa pamoja na wafu,

kama waliochinjwa walalao kaburini,

ambao huwakumbuki tena,

ambao wamekatiliwa mbali na uangalizi wako.

688:6 Za 30:1; 69:15; Mao 3:55; Yon 2:3Umenitupa katika shimo lenye kina kirefu sana,

katika vina vya giza nene.

788:7 Za 7:11; 42:7Ghadhabu yako imekuwa nzito juu yangu,

umenigharikisha kwa mawimbi yako yote.

888:8 Ay 3:23; 19:13; Za 31:11; Yer 32:2; 33:1Umenitenga na rafiki zangu wa karibu

na kunifanya chukizo kwao.

Nimezuiliwa, wala siwezi kutoroka;

988:9 Za 38:10; 5:2; 143:6; Ay 11:13nuru ya macho yangu

imefifia kwa ajili ya huzuni.

Ee Bwana, ninakuita kila siku,

ninakunyooshea wewe mikono yangu.

1088:10 Za 6:5Je, wewe huwaonyesha wafu maajabu yako?

Je, wale waliokufa huinuka na kukusifu?

1188:11 Za 30:9Je, upendo wako hutangazwa kaburini,

uaminifu wako katika Uharibifu?88:11 Yaani Abadon.

1288:12 Ay 10:21; 31:12; Mhu 8:10Je, maajabu yako hujulikana mahali pa giza,

au matendo yako ya haki katika nchi ya usahaulifu?

1388:13 Za 30:2; 5:3; 55:17; 119:147Lakini ninakulilia wewe, Ee Bwana, unisaidie;

asubuhi maombi yangu huja mbele zako.

1488:14 Za 43:2; 13:1Ee Bwana, kwa nini unanikataa

na kunificha uso wako?

1588:15 Dan 9:26; Za 9:12; 129:1; Yer 22:21; Eze 16:22; Hos 2:15; Isa 53:8; Ay 6:4; 18:11; 2Kor 4:8Tangu ujana wangu nimeteseka, nikakaribia kifo;

nimepatwa na hofu zako, nami nimekata tamaa.

1688:16 Za 7:11; Ay 6:4Ghadhabu yako imepita juu yangu;

hofu zako zimeniangamiza.

1788:17 Za 124:4Mchana kutwa zinanizunguka kama mafuriko;

zimenimeza kabisa.

1888:18 Za 88:8; 38:11; Ay 19:13Umeniondolea marafiki na wapendwa wangu;

giza limekuwa ndilo rafiki yangu wa karibu kuliko wote.