Zaburi 80
Maombi Kwa Ajili Ya Kuponywa Kwa Taifa
Kwa mwimbishaji. Mtindo wa “Yungiyungi za Agano.” Zaburi ya Asafu.
180:1 Kut 25:22; 1Sam 4:4; Za 77:20; 89:1; Kum 33:2Ee Mchungaji wa Israeli tusikie,
wewe umwongozaye Yosefu kama kundi;
wewe uketiye katika kiti cha enzi
katikati ya makerubi, angaza
280:2 Hes 2:18-24; Za 35:23; 54:1; 71:2; 109:26; 116:4; 119:94mbele ya Efraimu, Benyamini na Manase.
Uamshe nguvu zako,
uje utuokoe.
380:3 Za 71:20; 85:4; Yer 31:18; Mao 5:21; Hes 6:25; Za 80:7, 19; 1Fal 18:37Ee Mungu, uturejeshe,
utuangazie uso wako,
ili tuweze kuokolewa.
480:4 Za 74:10; Kum 29:20Ee Bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote,
hata lini hasira yako itawaka na kufoka moshi
dhidi ya maombi ya watu wako?
580:5 Ay 3:24; Isa 30:20Umewalisha kwa mkate wa machozi,
umewafanya wanywe machozi bakuli tele.
680:6 Za 79:4Tumekuwa chanzo cha ugomvi kwa jirani zetu,
na adui zetu wanatudhihaki.
780:7 Za 80:3Ee Mungu Mwenye Nguvu Zote, uturejeshe;
utuangazie uso wako,
nasi tuweze kuokolewa.
880:8 Isa 5:1-2, 7; Yer 2:21; Mt 21:33-41; Kut 15:17; 23:28-30; Yos 13:6; Mdo 7:45; Eze 15:6Ulileta mzabibu kutoka Misri,
ukawafukuza mataifa, ukaupanda.
9Uliandaa shamba kwa ajili yake,
mizizi ikawa imara, ukajaza nchi.
10Milima ilifunikwa kwa kivuli chake,
matawi yake yakafunika mierezi mikubwa.
1180:11 Kut 23:31; Za 72:8Matawi yake yalienea mpaka Baharini,80:11 Huenda inamaanisha Bahari ya Mediterania.
machipukizi yake mpaka kwenye Mto.80:11 Yaani Mto Frati.
1280:12 Isa 5:5; 30:13; Za 89:40; Yer 39:8Mbona umebomoa kuta zake
ili wote wapitao karibu
wazichume zabibu zake?
1380:13 Yer 5:6Nguruwe mwitu wanauharibu
na wanyama wa kondeni hujilisha humo.
1480:14 Kum 26:15; Zek 1:12, 16, 17; Isa 63:15Turudie, Ee Mungu Mwenye Nguvu Zote!
Tazama chini kutoka mbinguni na uone!
Linda mzabibu huu,
1580:15 Isa 49:5mche ulioupanda kwa mkono wako wa kuume,
mwana uliyemlea
kwa ajili yako mwenyewe.
1680:16 Za 79:1; Kum 28:20Mzabibu wako umekatwa, umechomwa moto,
unapowakemea, watu wako huangamia.
1780:17 Ay 25:6; Za 89:21; 110:1; Kut 4:22; Dan 7:13, 14; Yn 5:21-27Mkono wako na utulie juu ya mtu aliyeko mkono wako wa kuume,
mwana wa mtu uliyemlea kwa ajili yako mwenyewe.
1880:18 Za 85:6; Isa 57:15; Hos 6:2Ndipo hatutakuacha tena,
utuhuishe, nasi tutaliitia jina lako.
1980:19 Hes 6:25; Za 27:4, 9Ee Bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote, uturejeshe;
utuangazie uso wako,
ili tuweze kuokolewa.
第 80 篇
为国家复兴祈求
亚萨的诗,交给乐长,调用“作证的百合花”。
1-2以色列的牧者啊,
你像照顾羊群一样带领约瑟的子孙,
求你垂听我们的祈祷。
坐在基路伯天使之上的耶和华啊,
求你向以法莲、便雅悯和玛拿西发出光辉,
求你施展大能来拯救我们。
3上帝啊,求你复兴我们,
用你脸上的荣光照耀我们,
使我们得救。
4万军之上帝耶和华啊,
你因你子民的祷告而发怒,
要到何时呢?
5你使我们以泪洗面,
以哀伤果腹,
6又使我们成为邻国争夺的对象,
仇敌都嘲笑我们。
7万军之上帝啊,
求你复兴我们,
用你脸上的荣光照耀我们,
使我们得救。
8你从埃及带出一棵葡萄树,
赶走外族人,把它栽种起来。
9你为它开垦土地,
它就扎根生长,布满这片土地。
10它的树荫遮盖群山,
枝子遮蔽香柏树。
11它的枝条延伸到地中海,
嫩枝伸展到幼发拉底河。
12你为何拆毁了它的篱笆,
让路人随意摘取葡萄呢?
13林中的野猪蹂躏它,
野兽吞吃它。
14万军之上帝啊,
求你回来,
求你在天上垂顾我们这棵葡萄树,
15这棵你亲手栽种和培育的葡萄树。
16这树被砍倒,被焚烧,
愿你发怒毁灭仇敌。
17求你扶持你所拣选的人,你为自己所养育的人。
18我们必不再背弃你,
求你复兴我们,
我们必敬拜你。
19万军之上帝耶和华啊,
求你复兴我们,
用你脸上的荣光照耀我们,
使我们得救。