Zaburi 79
Maombi Kwa Ajili Ya Wokovu Wa Taifa
Zaburi ya Asafu.
179:1 Kut 34:9; Law 20:3; 2Fal 25:9; Neh 4:2; Isa 6:11; Yer 26:18Ee Mungu, mataifa yameuvamia urithi wako,
wamelinajisi Hekalu lako takatifu,
wameifanya Yerusalemu kuwa magofu.
279:2 Ufu 19:17-18; Kum 28:26; Yer 7:33Wametoa maiti za watumishi
kuwa chakula cha ndege wa angani
na nyama ya watakatifu wako
kwa wanyama wa nchi.
379:3 Ufu 11:9; Yer 25:33; 16:4Wamemwaga damu kama maji
kuzunguka Yerusalemu yote,
wala hakuna yeyote wa kuwazika.
479:4 Eze 5:14; Za 39:8; 44:13Tumekuwa kitu cha aibu kwa jirani zetu,
cha dharau na mzaha kwa wale wanaotuzunguka.
579:5 Za 74:10; 74:1; 85:5; Kum 29:20; Za 89:46; Sef 3:8; Eze 36:5Hata lini, Ee Bwana? Je, wewe utakasirika milele?
Wivu wako utawaka kama moto hadi lini?
679:6 Ufu 16:1; Za 2:5; 110:5; 14:4; 53:4; 147:20; 69:24; Yer 10:25; Isa 45:4Mwaga ghadhabu yako kwa mataifa yasiyokukubali,
juu ya falme za hao wasioliitia jina lako,
779:7 Isa 9:12; Yer 10:25kwa maana wamemrarua Yakobo
na kuharibu nchi ya makao yake.
879:8 Mwa 9:25; Yer 44:21; Za 116:6; 142:6Usituhesabie dhambi za baba zetu,
huruma yako na itujie hima,
kwa maana tu wahitaji mno.
979:9 2Nya 14:11; 25:11; 31:3; Yer 14:7; Yos 7:9Ee Mungu Mwokozi wetu, utusaidie,
kwa ajili ya utukufu wa jina lako;
tuokoe na kutusamehe dhambi zetu
kwa ajili ya jina lako.
1079:10 Za 42:3; 94:1; Ufu 6:10; Za 79:3Kwa nini mataifa waseme,
“Yuko wapi Mungu wenu?”
Mbele ya macho yetu,
dhihirisha kati ya mataifa
kwamba unalipiza kisasi damu iliyomwagwa
ya watumishi wako.
1179:11 Hes 14:17Kilio cha huzuni cha wafungwa kifike mbele zako;
kwa nguvu za mkono wako
hifadhi wale waliohukumiwa kufa.
1279:12 Isa 65:6; Yer 32:18; Mwa 4:15Walipize jirani zetu mara saba vifuani mwao
aibu walizovurumisha juu yako, Ee Bwana.
1379:13 Za 44:8; 74:1; Isa 43:21Ndipo sisi watu wako, kondoo wa malisho yako,
tutakusifu milele;
toka kizazi hadi kizazi
tutasimulia sifa zako.
第 79 篇
祈求上帝拯救
亞薩的詩。
1上帝啊,
外族人侵佔你的產業,
玷污你的聖殿,
使耶路撒冷淪為廢墟。
2他們把你僕人的屍體餵飛鳥,
把你忠心子民的屍體給野獸吃,
3使耶路撒冷周圍血流成河,
屍體無人埋葬。
4我們成了列國羞辱的對象,
周圍的人都嗤笑、譏諷我們。
5耶和華啊,你向我們發怒,
要到何時呢?
難道要到永遠嗎?
你的怒火要燒到何時呢?
6求你把烈怒撒向那些不承認你的列邦,
撒向那些不求告你的列國。
7因為他們吞噬了雅各,
摧毀了他的家園。
8求你不要向我們追討我們祖先的罪,
願你快快地憐憫我們,
因為我們已經落入絕望中。
9拯救我們的上帝啊,
求你為了自己榮耀的名而幫助我們,
為你名的緣故拯救我們,
赦免我們的罪。
10為何讓列邦說:
「他們的上帝在哪裡?」
求你讓我們親眼看見,
也讓列邦都知道,
你為自己被害的子民伸冤。
11求你垂聽被囚之人的哀歎,
求你用大能的臂膀留住死囚的性命。
12主啊,我們的鄰邦羞辱你,
求你以七倍的羞辱來報應他們。
13這樣,你的子民,你草場上的羊必永遠稱謝你,世代稱頌你。