Zaburi 78 – NEN & BPH

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Zaburi 78:1-72

Zaburi 78

Mungu Na Watu Wake

Utenzi wa Asafu.

178:1 Kut 19:5; Kum 32:29; Isa 51:4; 55:3Enyi watu wangu, sikieni mafundisho yangu,

sikilizeni maneno ya kinywa changu.

278:2 Za 49:4; Mt 13:35Nitafungua kinywa changu kwa mafumbo,

nitazungumza mambo yaliyofichika, mambo ya kale:

378:3 Za 44:1; Amu 6:13yale ambayo tuliyasikia na kuyajua,

yale ambayo baba zetu walituambia.

478:4 Kut 12:26; Yos 4:6, 7; Kum 4:9; 11:19; 32:7; Za 71:18; 26:7; 71:17Hatutayaficha kwa watoto wao;

tutakiambia kizazi kijacho

matendo yastahiliyo sifa ya Bwana,

uweza wake, na maajabu aliyoyafanya.

578:5 Za 19:7; 81:5; 147:19Aliagiza amri kwa Yakobo

na akaweka sheria katika Israeli,

ambazo aliwaamuru baba zetu

wawafundishe watoto wao,

678:6 Za 22:31; 102:18ili kizazi kijacho kizijue,

pamoja na watoto ambao watazaliwa,

nao pia wapate kuwaeleza watoto wao.

778:7 Kum 6:12; 5:29Ndipo wangeweka tumaini lao kwa Mungu,

nao wasingesahau matendo yake,

bali wangalizishika amri zake.

878:8 2Nya 30:7; Kut 32:9; 23:21; Kum 21:18; Isa 30:9; 65:2Ili wasifanane na baba zao,

waliokuwa kizazi cha ukaidi na uasi,

ambao roho zao hazikuwa na uaminifu kwake,

ambao roho zao hazikumwamini.

978:9 Za 78:57; 1Nya 12:2; Hos 7:16; Amu 20:39Watu wa Efraimu, ingawa walijifunga pinde,

walikimbia siku ya vita.

1078:10 Yos 7:10; 2Fal 17:15; Kut 16:28; Yer 11:8Hawakulishika agano la Mungu

na walikataa kuishi kwa sheria yake.

1178:11 Za 106:13; Isa 17:10; Yer 2:32Walisahau aliyokuwa ameyatenda,

maajabu aliyokuwa amewaonyesha.

1278:12 Neh 9:17; Za 106:22; Kut 11:9; Hes 13:22; Mwa 32:3; Isa 19:11Alitenda miujiza machoni mwa baba zao,

huko Soani, katika nchi ya Misri.

1378:13 Kut 14:21, 22; 15:8; Za 66:6; 136:13Aliigawanya bahari akawapitisha,

alifanya maji yasimame imara kama ukuta.

1478:14 Kut 13:21; Za 105:39Aliwaongoza kwa wingu mchana

na kwa nuru kutoka kwenye moto usiku kucha.

1578:15 Hes 20:11; 1Kor 10:4; Kut 17; 6; Za 105:41; Isa 41:18Alipasua miamba jangwani

na akawapa maji tele kama bahari,

1678:16 Kum 9:21alitoa vijito kutoka kwenye jabali lililochongoka,

akayafanya maji yatiririke kama mito.

1778:17 Za 78:32Lakini waliendelea kutenda dhambi dhidi yake,

wakiasi jangwani dhidi ya Aliye Juu Sana.

1878:18 Kut 15:24; 17:2; 1Kor 10:9; Hes 11:4Kwa makusudi walimjaribu Mungu,

wakidai vyakula walivyovitamani.

1978:19 Hes 11:4; 21:5Walinena dhidi ya Mungu, wakisema,

“Je, Mungu aweza kuandaa meza jangwani?

2078:20 Hes 20:11; Kut 17:6Alipopiga mwamba, maji yalitoka kwa nguvu,

vijito vikatiririka maji mengi.

Lakini je, aweza kutupa chakula pia?

Je, anaweza kuwapa watu wake nyama?”

2178:21 Hes 11:1Bwana alipowasikia, alikasirika sana,

moto wake ukawa dhidi ya Yakobo,

na ghadhabu yake ikawaka dhidi ya Israeli,

2278:22 Kum 1:32; Ebr 3:19; 3:10kwa kuwa hawakumwamini Mungu,

wala kuutumainia ukombozi wake.

2378:23 Mwa 7:11; Kum 28:12; 2Fal 7:2Hata hivyo alitoa amri kwa anga zilizo juu

na kufungua milango ya mbingu,

2478:24 Kut 16:4; Yn 6:31; Neh 9:15, 20; 1Kor 10:3akawanyeshea mana ili watu wale;

aliwapa nafaka ya mbinguni.

25Watu walikula mkate wa malaika,

akawatumia chakula chote ambacho wangeliweza kula.

2678:26 Hes 11:31Aliachia upepo wa mashariki kutoka kwenye mbingu

na kuuongoza upepo wa kusini kwa uwezo wake.

2778:27 Kut 16:13; Hes 11:31Aliwanyeshea nyama kama mavumbi,

ndege warukao kama mchanga wa pwani.

28Aliwafanya washuke ndani ya kambi yao,

kuzunguka mahema yao yote.

2978:29 Hes 11:20Walikula na kusaza,

kwa maana alikuwa amewapa kile walichotamani.

3078:30 Hes 11:33Kabla hawajamaliza kula walichokitamani,

hata kilipokuwa kingali bado vinywani mwao,

3178:31 Isa 10:16hasira ya Mungu ikawaka juu yao,

akawaua wale waliokuwa na nguvu zaidi miongoni mwao,

akiwaangusha vijana wa Israeli.

3278:32 Za 78:11, 17, 22Licha ya haya yote, waliendelea kutenda dhambi,

licha ya maajabu yake, hawakuamini.

3378:33 Hes 14:29, 35Kwa hiyo akamaliza siku zao katika ubatili

na miaka yao katika vitisho.

3478:34 Kum 4:29; Hos 5:15; Hes 5:15Kila mara Mungu alipowaua baadhi yao,

waliosalia walimtafuta,

walimgeukia tena kwa shauku.

3578:35 Mwa 49:24; Kum 9:26Walikumbuka kwamba Mungu alikuwa Mwamba wao,

kwamba Mungu Aliye Juu Sana alikuwa Mkombozi wao.

3678:36 Eze 33:31Lakini walimdanganya kwa vinywa vyao,

wakisema uongo kwa ndimi zao,

3778:37 Za 78:8; Mdo 8:21mioyo yao haikuwa thabiti kwake,

wala hawakuwa waaminifu katika agano lake.

3878:38 Kut 34:6; Neh 9:17; Za 25:11; 85:2; 86:15; 1Fal 21:29; Isa 1:25; 27:9; 48:9, 10; 30:18; Mik 7:18; Rum 2:4; Dan 11:35Hata hivyo alikuwa na huruma,

alisamehe maovu yao

na hakuwaangamiza.

Mara kwa mara alizuia hasira yake,

wala hakuchochea ghadhabu yake yote.

3978:39 Mwa 6:3; Isa 29:5; Ay 7:7; Yak 4:14; Yn 3:6Alikumbuka kwamba wao walikuwa nyama tu,

upepo upitao ambao haurudi.

4078:40 Kut 23:21; Za 95:8; 106:14; Efe 4:30Mara ngapi walimwasi jangwani

na kumhuzunisha nyikani!

4178:41 Kut 17:2; 2Fal 19:22; Za 71:22; 89:18Walimjaribu Mungu mara kwa mara,

wakamkasirisha yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli.

4278:42 Amu 3:7; Neh 9:17; Za 27:11Hawakukumbuka uwezo wake,

siku aliyowakomboa kutoka kwa mtesi,

4378:43 Kut 10:1; 3:20siku aliyoonyesha ishara zake za ajabu huko Misri,

maajabu yake huko Soani.

4478:44 Kut 7:20, 21; Za 105:29; 78:45Aligeuza mito yao kuwa damu,

hawakuweza kunywa maji kutoka vijito vyao.

4578:45 Kut 8:2, 6, 24; Za 105Aliwapelekea makundi ya mainzi yakawala,

na vyura wakawaharibu.

4678:46 Nah 3:15; Kut 10:13Aliruhusu tunutu kuharibu mimea yao,

mazao yao kwa nzige.

4778:47 Za 105:32; 147:17; Kut 9:23Aliharibu mizabibu yao kwa mvua ya mawe

na mikuyu yao kwa mvua iliyochangamana na theluji.

4878:48 Kut 9:25Aliwaachia mifugo yao mvua ya mawe,

akayapiga makundi ya wanyama wao kwa radi.

4978:49 Kut 15:7; Mwa 19:13; 1Kor 10:10; Rum 2:8Aliwafungulia hasira yake kali,

ghadhabu yake, hasira na uadui,

na kundi la malaika wa kuharibu.

50Aliitengenezea njia hasira yake,

hakuwaepusha na kifo,

bali aliwaachia tauni.

5178:51 Mwa 9:12; Kut 12:12; Za 135:8; 105:23; 106:22Aliwapiga wazaliwa wote wa kwanza wa Misri,

matunda ya kwanza ya ujana katika mahema ya Hamu.

5278:52 Ay 21:11; Za 28:9; 77:20Lakini aliwatoa watu wake kama kundi,

akawaongoza kama kondoo kupitia jangwani.

5378:53 Kut 14:28; 15:7; Za 106:10Aliwaongoza salama, wala hawakuogopa,

bali bahari iliwameza adui zao.

5478:54 Kut 15:17; Za 44:3Hivyo akawaleta hadi kwenye mpaka wa nchi yake takatifu,

hadi nchi ya vilima ambayo mkono wake wa kuume ulikuwa umeitwaa.

5578:55 Za 44:2; Kum 1:38; Yos 13:7; Mdo 13:19Aliyafukuza mataifa mbele yao,

na kuwagawia nchi zao kama urithi,

aliwakalisha makabila ya Israeli katika makao yao.

56Lakini wao walimjaribu Mungu,

na kuasi dhidi ya Yeye Aliye Juu Sana,

wala hawakuzishika sheria zake.

5778:57 2Nya 30:7; Za 78:9; Eze 20:27; Hos 7:16Kama baba zao, hawakuwa thabiti wala waaminifu,

wakawa wasioweza kutegemewa

kama upinde wenye kasoro.

5878:58 Amu 2:12; Law 26:30; Kut 20:4; Kum 12:2; 5:8; 32:21; Hes 33:51Wakamkasirisha Mungu kwa mahali pao pa juu pa kuabudia miungu,

wakachochea wivu wake kwa sanamu zao.

5978:59 Za 55:19; Law 26:28; Hes 32:14; Kum 32:19; Ebr 4:13Wakati Mungu alipowasikia, alikasirika sana,

akamkataa Israeli kabisa.

6078:60 Yos 18:1; Eze 8:6; 1Sam 4:11; Yer 7:12Akaiacha hema ya Shilo,

hema aliyokuwa ameiweka katikati ya wanadamu.

6178:61 Amu 18:30; 1Sam 4:12; Za 132:8; 1Sam 4:17Akalipeleka Sanduku la nguvu zake utumwani,

utukufu wake mikononi mwa adui.

6278:62 Kum 28:25; 1Sam 10:1Aliachia watu wake wauawe kwa upanga,

akaukasirikia sana urithi wake.

6378:63 1Fal 4:32; Yer 7:32; 16:9; 25:10; Hes 11:1Moto uliwaangamiza vijana wao,

na wanawali wao hawakuimbiwa nyimbo za arusi,

6478:64 Ay 27:15; 1Sam 4:17makuhani wao waliuawa kwa upanga,

wala wajane wao hawakuweza kulia.

6578:65 Za 44:23; Isa 42:13Ndipo Bwana alipoamka kama vile kuamka usingizini,

kama vile mtu aamkavyo kutoka kwenye bumbuazi la mvinyo.

6678:66 1Sam 5:6Aliwapiga na kuwashinda adui zake,

akawatia katika aibu ya milele.

6778:67 Yer 7:15; Hos 9:13; 12:1Ndipo alipozikataa hema za Yosefu,

hakulichagua kabila la Efraimu,

6878:68 Hes 1:7; Kut 15:17; Za 68:16; 108:8lakini alilichagua kabila la Yuda,

Mlima Sayuni, ambao aliupenda.

6978:69 Za 15:1; 1Fal 6:1Alijenga patakatifu pake kama vilele,

kama dunia ambayo aliimarisha milele.

7078:70 1Sam 16:1Akamchagua Daudi mtumishi wake

na kumtoa kwenye mazizi ya kondoo.

7178:71 Mwa 37:2; Za 28:9; 2Sam 5:2; 1Nya 11:2; Mik 5:2-4; Zek 11:4Kutoka kuchunga kondoo alimleta

kuwa mchungaji wa watu wake Yakobo,

wa Israeli urithi wake.

7278:72 1Fal 9:4; Mwa 17:1Naye Daudi aliwachunga kwa uadilifu wa moyo,

kwa mikono ya ustadi aliwaongoza.

Bibelen på hverdagsdansk

Salmernes Bog 78:1-72

Israels Gud—historiens Gud

1En visdomssang af Asaf.

Mit folk, lyt til min belæring,

hør nøje efter, hvad jeg siger.

2Jeg vil tale i billeder,

fortælle om det, der har været skjult fra verdens begyndelse.

3Det er vore forfædres historier,

som er fortalt gennem mange generationer.

4Vi vil fortælle dem til vore børn,

som igen skal give dem videre til nye generationer.

De skal også høre om Herrens magt,

om de forunderlige ting, han har gjort.

5Han gav sine love til Jakobs slægt,

åbenbarede sin vilje for sit folk, Israel.

Han befalede vore forfædre

at undervise deres børn derom,

6så den næste generation ville vide besked,

så selv de børn, som endnu ikke var født,

til sin tid kunne belære deres børn,

7for at hvert slægtled må have tillid til Gud,

huske hans vældige gerninger

og adlyde hans befalinger,

8så de ikke bliver som deres forfædre,

der var stædige og oprørske,

som ikke vendte deres hjerte til Gud,

men var troløse og ulydige mod ham.

9Efraims krigere var udrustet med buer,

men flygtede alligevel i kampens hede.

10De overholdt ikke pagten med Gud,

og de nægtede at følge hans lov.

11De glemte, hvad Gud havde gjort,

alle de store undere, han havde udført.

12Han gjorde mirakler for deres forfædre,

da de kom fra Zoans slette i Egypten.

13Han delte havet og førte dem igennem,

vandet stod som en vold på begge sider.

14Om dagen ledte han dem ved en sky,

om natten var der en søjle af ild.

15Han kløvede ørkenens klipper

og skaffede masser af vand.

16En kilde sprang frem fra klippen,

så vandet flød som en flod.

17Men de fortsatte deres oprør mod Gud,

de vakte den Almægtiges vrede i ørkenen.

18De provokerede Gud med vilje,

forlangte deres egyptiske livretter.

19De fornærmede Gud ved at sige:

„Kan Gud dække bord i ørkenen?

20Han slog ganske vist på klippen,

så vandet strømmede ud.

Men kan han give os brød?

Kan han skaffe kød til sit folk?”

21Da Gud hørte det, blev han vred.

Hans vrede blussede op imod Israel,

22for de havde ikke tillid til deres Gud.

De troede ikke på, at han kunne tage sig af dem.

23Men han gav befaling til skyerne

og åbnede himlens sluser.

24Han lod det regne ned over dem med manna,

han gav dem brød fra himlen at spise.

25Han gav dem englemad,

så de havde rigeligt at spise.

26Han lod østenvinden fare hen over himlen,

styrede søndenvinden med sin mægtige hånd,

27lod kød hagle ned over dem,

fugle så talrige som sandkornene på stranden.

28Han lod dem falde ned midt i lejren,

de lå rundt omkring imellem teltene.

29Folket spiste sig overmætte,

Gud tilfredsstillede deres grådighed.

30Men mens de endnu havde munden fuld,

blev deres grådighed straffet.

31De blev ramt af Herrens vrede,

han dræbte deres stærkeste mænd,

gjorde det af med de bedste krigere.

32Alligevel blev de ved med at synde,

til trods for hans mægtige undere.

33Derfor dræbte han folk i deres bedste alder,

de blev alle grebet af rædsel.

34Når han dræbte en stor del af dem,

søgte resten tilbage til ham.

De angrede og vendte sig igen til Gud.

35Så huskede de, at Gud var deres redning,

den almægtige Gud var deres befrier.

36Men de dyrkede kun Gud med deres ord,

deres lovprisning var ikke andet end løgn.

37Deres hjerter var langt fra Gud,

de holdt ikke fast ved hans pagt.

38Alligevel var Gud barmhjertig,

han tilgav deres synd og udslettede dem ikke.

Ofte holdt han sin vrede tilbage,

lod ikke sit raseri få frit løb.

39Han vidste jo, at de kun var mennesker,

de var som et vindpust, der farer forbi.

40Hvor ofte gjorde de ikke oprør i ørkenen?

De vakte hans vrede og voldte ham sorg.

41De provokerede deres Gud gang på gang,

de var ulydige mod Israels Herre.

42De glemte hans underfulde kraft,

som befriede dem fra fjendens tyranni.

43De glemte, hvordan han sendte plager over egypterne,

gjorde mægtige undere på Zoans slette.

44Han forvandlede floderne til blod,

så vandet ikke kunne drikkes.

45Han sendte insekter, som stak dem,

et mylder af frøer, som ødelagde deres land.

46Han gav deres afgrøde til græshopperne,

hele deres høst blev ædt op.

47Han ødelagde deres vinstokke med hagl,

deres figentræer med den iskolde regn.

48Deres kvæg bukkede under for haglene,

deres får blev ramt af lynene.

49Han udøste sin vrede over dem,

sendte ødelæggelsen ind over dem.

50Han gav sin vrede frit løb

og sparede ikke egypternes liv,

men gjorde dem til ofre for de mange plager.

51Han dræbte alle Egyptens førstefødte,

symbolet på hver eneste families frugtbarhed.

52Men han førte sit eget folk i frihed,

ledte dem som en fåreflok gennem ørkenen.

53Han ledte dem frem i sikkerhed,

mens deres fjender blev begravet i havet.

54Han førte dem til det forjættede land,

det bjergland, han havde lovet at give dem.

55Han drev folkeslag bort foran dem,

han uddelte landet til dem ved lodkastning,

så Israels stammer kunne bosætte sig der.

56Men de trodsede igen den almægtige Gud,

de adlød ikke hans befalinger.

57De var troløse som deres forfædre og vendte sig bort,

de svigtede deres Gud som en bue, der er skæv.

58De krænkede ham med deres afgudsbilleder,

æggede ham med deres offerhøje.

59Gud så deres opførsel og blev meget vred,

han følte en stærk lede ved sit folk.

60Han forlod sin helligdom i Shilo,

hvor han havde lovet at bo blandt sit folk.

61Han tillod, at arken blev taget som bytte,

overgav symbolet på sin herlighed til fjenden.

62Han lod mange blive dræbt i krig,

for han var vred på sit udvalgte folk.

63De tapre krigere døde i deres ungdom,

de unge piger havde ingen at gifte sig med.

64Præsterne blev myrdet af fjendens soldater,

enkerne fik ikke lov at synge klagesange.

65Da rejste Herren sig som af søvne,

som en rasende kriger, der har fået for meget at drikke.

66Han drev fjenderne på flugt,

voldte dem et nederlag, der aldrig blev glemt.

67Men han forkastede Efraims krigere,

de der var efterkommere af Josef.

68I stedet valgte han Judas stamme,

og besluttede sig for Zions bjerg.

69Dér byggede han sin prægtige helligdom

på et fundament, som varer til evig tid.

70Han udvalgte sin tjener David,

som ikke var andet end en fårehyrde.

71Han fjernede ham fra faderens får

og gjorde ham til konge i Israel,

til hyrde for sit udvalgte folk.

72David blev en god og retfærdig konge,

han ledte folket med kyndig hånd.