Zaburi 77 – Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu) NEN

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Zaburi 77:1-20

Zaburi 77

Matendo Makuu Ya Mungu Yanakumbukwa

Kwa mwimbishaji. Mtindo wa Yeduthuni. Zaburi ya Asafu.

177:1 1Fal 8:52Nilimlilia Mungu ili anisaidie,

nilimlilia Mungu ili anisikie.

277:2 Mwa 37:35; 32:7; 2Sam 22:7; Za 118:5; 6:6; 22:2; 88:1; 50:15; Kut 9:29; Ay 11:13; Mt 2:18; Isa 26:9Nilipokuwa katika taabu, nilimtafuta Bwana,

usiku nilinyoosha mikono bila kuchoka

na nafsi yangu ilikataa kufarijika.

377:3 Za 6:6; 78:35; Kut 2:23; Yer 45:3; 6:2Ee Mungu, nilikukumbuka wewe, nikalia kwa huzuni;

nikatafakari, roho yangu ikadhoofika.

477:4 Za 39:2Ulizuia macho yangu kufumba;

nilikuwa nasumbuka, nikashindwa kusema.

577:5 Kum 32:7; Isa 51:9; Za 44:1; 143:5; Mhu 7:16Nilitafakari juu ya siku zilizopita,

miaka mingi iliyopita,

6nilikumbuka nilivyoimba nyimbo usiku.

Moyo wangu ulitafakari

na roho yangu ikauliza:

777:7 Za 85:1; 102:13; 106:4; 1Nya 28:9“Je, Bwana atakataa milele?

Je, hatatenda mema tena?

877:8 Za 6:4; 90:14; 2Pet 3:9; Isa 27:11; Yn 2:4; Hes 23:19; Yer 15:18; Rum 9:6Je, upendo wake usio na mwisho umetoweka milele?

Je, ahadi yake imekoma nyakati zote?

977:9 Za 25:6; 40:11; 51:1; Isa 49:15Je, Mungu amesahau kuwa na huruma?

Je, katika hasira amezuia huruma yake?”

1077:10 Ay 42:3; Za 31:22; Yer 10:19; Kut 15:6Ndipo nikawaza, “Huu ndio udhaifu wangu:

lakini nitakumbuka

miaka ya mkono wa kuume

wa Aliye Juu Sana.”

1177:11 Neh 9:17; 1Nya 16:12; Za 28:5; Isa 5:14Nitayakumbuka matendo ya Bwana;

naam, nitaikumbuka miujiza yako ya zamani.

1277:12 Mwa 24:63; Za 143:5Nitazitafakari kazi zako zote

na kuyawaza matendo yako makuu.

1377:13 Za 73:17; 71:19; 86:8; Kut 15:11Ee Mungu, njia zako ni takatifu.

Ni mungu yupi aliye mkuu kama Mungu wetu?

1477:14 Kut 3:20; 34:10Wewe ndiwe Mungu utendaye miujiza,

umeonyesha uwezo wako katikati ya mataifa.

1577:15 Kut 6:6Kwa mkono wako wenye nguvu umewakomboa watu wako,

uzao wa Yakobo na Yosefu.

1677:16 Kut 14:21, 28; Isa 50:2; Hab 3:8, 10; Yos 3:15, 16; Za 114:4Maji yalikuona, Ee Mungu,

maji yalikuona yakakimbia,

vilindi vilitetemeka.

1777:17 Amu 5:4; Kut 9:23; Za 29:3; Kum 32:23Mawingu yalimwaga maji,

mbingu zikatoa ngurumo kwa radi,

mishale yako ikametameta huku na huko.

1877:18 Za 55:8; 2Sam 22:13; Amu 5:4Ngurumo yako ilisikika katika upepo wa kisulisuli,

umeme wako wa radi ukaangaza dunia,

nchi ikatetemeka na kutikisika.

1977:19 Hab 3:15; Kut 14:28; 14:22; Ay 9:8; 37:23Njia yako ilipita baharini,

mapito yako kwenye maji makuu,

ingawa nyayo zako hazikuonekana.

2077:20 Kut 4:16; 13:21; Za 78:52; Isa 63:11; Hes 33:1Uliongoza watu wako kama kundi

kwa mkono wa Mose na Aroni.