Zaburi 63
Shauku Kwa Ajili Ya Uwepo Wa Mungu
Zaburi ya Daudi. Wakati alipokuwa katika Jangwa la Yuda.
163:1 Za 42:2; 84:2; 143:6Ee Mungu, wewe ni Mungu wangu,
nakutafuta kwa moyo wote;
nafsi yangu inakuonea kiu,
mwili wangu unakuonea wewe shauku,
katika nchi kame na iliyochoka
mahali ambapo hapana maji.
263:2 Za 15:1; 27:4; 68:24; Kut 16:7; 1Nya 16:11Nimekuona katika mahali patakatifu
na kuuona uwezo wako na utukufu wako.
363:3 Isa 30:13; Yn 3:16; Za 36:7; 69:16; 106:45; 109:21Kwa sababu upendo wako ni bora kuliko uhai,
midomo yangu itakuadhimisha.
463:4 Za 28:3; 104:33; 146:2; Isa 38:20; 1Tim 2:8Nitakusifu siku zote za maisha yangu,
na kwa jina lako nitainua mikono yangu.
563:5 Za 17:15; 36:8; Mt 5:6; Isa 25:6Nafsi yangu itatoshelezwa
kama kwa wingi wa vyakula;
kwa midomo iimbayo
kinywa changu kitakusifu wewe.
663:6 Kum 6:4-9; Za 119:148; 16:7; 140:5; Mt 14:25Kitandani mwangu ninakukumbuka wewe,
ninawaza juu yako makesha yote ya usiku.
763:7 Za 27:9; 118:7; Rum 2:12; Isa 26:9Kwa sababu wewe ndiwe msaada wangu,
chini ya uvuli wa mbawa zako naimba.
863:8 Hes 32:12; Hos 6:3; Isa 26:9; Za 41:12Nafsi yangu inaambatana nawe,
mkono wako wa kuume hunishika.
963:9 Za 40:14; 55:15; 71:20; 95:4; 139:15Wale wanaotafuta uhai wangu wataharibiwa,
watakwenda chini kwenye vilindi vya dunia.
1063:10 Yer 18:21; Eze 35:5; Amo 1:11; Mao 5:18Watatolewa wafe kwa upanga,
nao watakuwa chakula cha mbweha.
1163:11 Sef 1:5; Isa 19:18; 45:23; 65:16; Ay 5:16; Rum 3:19Bali mfalme atafurahi katika Mungu,
wale wote waapao kwa jina la Mungu watamsifu,
bali vinywa vya waongo vitanyamazishwa.
Salmo 63
Salmo de David, cuando estaba en el desierto de Judá.
1Oh Dios, tú eres mi Dios;
yo te busco intensamente.
Mi alma tiene sed de ti;
todo mi ser te anhela,
cual tierra seca, extenuada y sedienta.
2Te he visto en el santuario
y he contemplado tu poder y tu gloria.
3Tu amor es mejor que la vida;
por eso mis labios te alabarán.
4Te bendeciré mientras viva,
y alzando mis manos te invocaré.
5Mi alma quedará satisfecha
como de un suculento banquete,
y con labios jubilosos
te alabará mi boca.
6En mi lecho me acuerdo de ti;
pienso en ti toda la noche.
7A la sombra de tus alas cantaré,
porque tú eres mi ayuda.
8Mi alma se aferra a ti;
tu mano derecha me sostiene.
9Los que buscan mi muerte serán destruidos;
bajarán a las profundidades de la tierra.
10Serán entregados a la espada
y acabarán devorados por los chacales.
11El rey se regocijará en Dios;
todos los que invocan a Dios lo alabarán,
pero los mentirosos serán silenciados.