Zaburi 58 – NEN & CCB

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Zaburi 58:1-11

Zaburi 58

Mungu Kuwaadhibu Waovu

Kwa mwimbishaji. Mtindo wa “Usiharibu!” Utenzi wa Daudi.

1Enyi watawala, je, kweli mwanena kwa haki?

Je, mnahukumu kwa unyofu miongoni mwa watu?

258:2 Za 74:20; Isa 10:1; Mt 15:19; Lk 6:38La, mioyoni mwenu mnatunga udhalimu,

na mikono yenu hupima jeuri duniani.

358:3 Za 51:5Waovu ni wapotovu tangu kuzaliwa kwao,

toka tumboni mwa mama zao

ni wakaidi na husema uongo.

458:4 Hes 21:6; Za 140:4Sumu yao ni kama sumu ya nyoka,

kama ile ya fira ambaye ameziba masikio yake,

558:5 Za 81:11; Mhu 10:1; Yer 8:17ambaye hatasikia sauti ya kutumbuiza ya mwaguzi,

hata kama mganga angecheza kwa ustadi kiasi gani.

658:6 Ay 4:10; Za 3:7Ee Mungu, yavunje meno katika vinywa vyao;

Ee Bwana, vunja meno makali ya hao simba!

758:7 Law 26:36; Ay 11:16; Za 11:2; 57:4; 64:3Na watoweke kama maji yapitayo kwa kasi,

wavutapo pinde zao, mishale yao na iwe butu.

858:8 Isa 13:7; Ay 3:16Kama konokono ayeyukavyo akitembea,

kama mtoto aliyezaliwa akiwa mfu,

wasilione jua.

958:9 Za 118:12; Mhu 7:6; Ay 7:10; Mit 10:25Kabla vyungu vyenu havijapata moto wa kuni za miiba,

zikiwa mbichi au kavu,

waovu watakuwa

wamefagiliwa mbali.

1058:10 Ay 22:19; Kum 32:42; 32:35; Yer 11:20; Mit 10:11; Rum 12:17-21; Za 18:47; 7:9; 91:8; 68:23; Ufu 18:20Wenye haki watafurahi waonapo wakilipizwa kisasi,

watakapochovya nyayo zao katika damu ya waovu.

1158:11 Mwa 4:12, 13; 15:1; Za 128:2; Lk 6:23; Ufu 2:23; Rum 2:6-11; 14:12; Ay 34:11; Mhu 5:8; Yer 32:19; Eze 7:27Ndipo wanadamu watasema,

“Hakika utulivu wa wenye haki bado una thawabu,

hakika kuna Mungu ahukumuye dunia.”

Chinese Contemporary Bible (Simplified)

诗篇 58:1-11

第 58 篇

祈求上帝惩罚恶人

大卫作的诗,交给乐长,调用“休要毁坏”。

1你们做官长的主持公道吗?

你们的审判公正吗?

2不,你们心中图谋不义,

你们在地上行凶作恶。

3恶人生下来就步入歧途,

一出母胎就离开正道,

谎话连篇。

4他们像喷出毒液的毒蛇,

又像耳聋的眼镜蛇,

5任法师的邪术再高超,

也听不见他的咒语。

6上帝啊,求你敲碎他们的牙齿;

耶和华啊,

求你拔掉这些猛狮的利齿。

7愿他们如流水逝去,

愿他们弯弓搭箭时箭头折断。

8愿他们像蜗牛一样溶为烂泥,

又如流产的胎儿不见天日。

9刹那间,

荆棘还没有把锅烧热的工夫,

上帝必除灭他们。

10义人必因恶人遭报而欢欣,

并用恶人的血洗脚。

11这样,人们必说:

“义人终有善报,

确实有一位审判天下的上帝。”