Zaburi 31 – NEN & CCB

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Zaburi 31:1-24

Zaburi 31

Maombi Na Sifa Kwa Kuokolewa Kutoka Kwa Adui

Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi.

131:1 Za 7:1; 5:8Ee Bwana, nimekukimbilia wewe,

usiache nikaaibika kamwe,

kwa haki yako uniokoe.

231:2 Za 6:4Nitegee sikio lako,

uje uniokoe haraka;

uwe kwangu mwamba wa kimbilio,

ngome imara ya kuniokoa.

331:3 Za 18:2; 23:3; Yer 14:7Kwa kuwa wewe ni mwamba wangu na ngome yangu,

uniongoze na kunilinda kwa ajili ya jina lako.

431:4 1Sam 28:9; Ay 18:10; Za 9:9Uniepushe na mtego niliotegewa,

maana wewe ndiwe kimbilio langu.

531:5 Lk 23:46; Ebr 6:18; Mdo 7:59; Isa 45:19; 65:16; 2Tim 1:12Ninaikabidhi roho yangu mikononi mwako,

unikomboe Ee Bwana, uliye Mungu wa kweli.

631:6 Kum 32:21; Za 4:5Ninawachukia wale wanaongʼangʼania sanamu batili;

mimi ninamtumaini Bwana.

731:7 Yn 10:27; Lk 22:44; Za 25:17Nitafurahia na kushangilia upendo wako,

kwa kuwa uliona mateso yangu

na ulijua maumivu ya nafsi yangu.

831:8 Za 18:19; Kum 32:30; 2Sam 22:20Hukunikabidhi kwa adui yangu

bali umeiweka miguu yangu mahali penye nafasi.

931:9 Za 4:1; 6:7; 63:1Ee Bwana unihurumie, kwa kuwa niko kwenye shida;

macho yangu yanafifia kwa huzuni,

nafsi yangu na mwili wangu kwa sikitiko.

1031:10 Za 6:6; 22:5; 32:4; 38:10; 73:26; 25:18; 6:2Maisha yangu yamedhoofika kwa majonzi,

naam, miaka yangu kwa kulia kwa maumivu makali;

nguvu zangu zinaisha kwa ajili ya mateso,

na mifupa yangu inachakaa.

1131:11 Kum 30:7; Za 3:7; 25:19; 102; 22:6; 38:11; 88:8Kwa sababu ya adui zangu wote,

nimedharauliwa kabisa na jirani zangu,

hata kwa rafiki zangu nimekuwa tisho,

wale wanionao barabarani hunikimbia.

1231:12 Za 28:1; 88:4Nimesahaulika miongoni mwao kama mtu aliyekufa,

nimekuwa kama chombo cha mfinyanzi kilichovunjika.

1331:13 Law 19:16; Isa 13:8; Za 50:20; 41:7; 56:6; 71:10; 83:3; Ay 18:11; Yer 6:25; 20:3, 10; 46:5; 49:5; Mao 2:22; Mwa 37:18; Mt 12:14; 27:1Kwa maana nimesikia maneno niliyosingiziwa na wengi;

vitisho viko pande zote;

kwa kuwa wamefanya mashauri dhidi yangu,

na kula njama kuniua.

1431:14 Za 4:5Lakini mimi ninakutumaini wewe peke yako, Ee Bwana;

nimesema, “Wewe ndiwe Mungu wangu.”

1531:15 Ay 14:5Siku za maisha yangu ziko mikononi mwako,

uniokoe mikononi mwa adui zangu

na wale wanifuatiao.

1631:16 Hes 6:25; Dan 9:17; Za 4:6; 6:4Mwangazie mtumishi wako uso wako,

uniokoe kwa ajili ya upendo wako usiokoma.

1731:17 Za 22:5; 94:17; 115:17; 25:2; 1Sam 2:9Usiniache niaibike, Ee Bwana,

kwa maana nimekulilia wewe,

bali waovu waaibishwe

na kunyamazishwa Kuzimu.

1831:18 Za 120:2; 12:3; Mit 10:18; 26:24; 1Sam 2:3; Yud 15Midomo yao isemayo uongo na inyamazishwe,

kwa maana kwa kiburi na dharau

wao husema kwa majivuno

dhidi ya wenye haki.

1931:19 Za 27:13; 23:5; Isa 64:4; 1Kor 2:9; Rum 11:22Tazama jinsi ulivyo mkuu wema wako,

uliowawekea akiba wakuchao,

ambao huwapa wale wakukimbiliao

machoni pa watu.

2031:20 Za 55:8; 27:5; 17:8; Mwa 37:18; Ay 5:21Unawahifadhi katika uvuli wa uwepo wako

kutokana na hila za wanadamu;

katika makao yako huwaweka salama

kutokana na ndimi za mashtaka.

2131:21 Za 28:6; 17:7; 1Sam 23:7Atukuzwe Bwana,

kwa kuwa amenionyesha upendo wake wa ajabu

nilipokuwa katika mji uliozingirwa.

2231:22 Za 116:11; 37:9; 88:5; 6:9; 66:19; 116:1; 145:19; Ay 6:9; 17:1; Isa 38:12Katika hofu yangu nilisema,

“Nimekatiliwa mbali na macho yako!”

Hata hivyo ulisikia kilio changu

ukanihurumia nilipokuita unisaidie.

2331:23 Za 4:3; 94:2; 18:25; Ufu 2:10; Kum 32:41; 1Pet 1:5Mpendeni Bwana ninyi watakatifu wake wote!

Bwana huwahifadhi waaminifu,

lakini wenye kiburi huwalipiza kikamilifu.

2431:24 Za 27:14Kuweni hodari na mjipe moyo,

ninyi nyote mnaomtumaini Bwana.

Chinese Contemporary Bible (Simplified)

诗篇 31:1-24

第 31 篇

信靠上帝的祷告

大卫的诗,交给乐长。

1耶和华啊,我寻求你的庇护,

求你让我永不蒙羞;

你是公义的,求你拯救我。

2求你侧耳听我的呼求,

快来救我,作我坚固的避难所,

作拯救我的堡垒。

3你是我的磐石,我的堡垒,

求你为了自己的名而引导我,带领我。

4你是我的避难所,

求你救我脱离人们为我设下的陷阱。

5我将灵魂交托给你。

信实的上帝耶和华啊,

你必救赎我。

6我憎恨拜假神的人,

我信靠耶和华。

7你已经看见我的困苦,

知道我心中的愁烦,

你的恩慈使我欢喜快乐。

8你没有将我交给仇敌,

而是领我到宽阔之地。

9耶和华啊,我落在苦难之中,

求你怜悯我,

我双眼哭肿,身心疲惫。

10我的生命被愁苦吞噬,

岁月被哀伤耗尽,

力量因罪恶而消逝,

我成了枯骨一堆。

11仇敌羞辱我,

邻居厌弃我,

朋友害怕我,

路人纷纷躲避我。

12我就像已死之人,被人遗忘;

又像破碎的陶器,被人丢弃。

13我听见许多人毁谤我,

惊恐笼罩着我。

他们图谋不轨,

谋害我的性命。

14然而,耶和华啊,

我依然信靠你;

我说:“你是我的上帝。”

15我的时日都掌握在你手中,

求你救我脱离仇敌和追逼我的人。

16求你笑颜垂顾仆人,

施慈爱拯救我。

17耶和华啊,我曾向你呼求,

求你不要叫我蒙羞。

求你使恶人蒙羞,

寂然无声地躺在阴间。

18愿你堵住撒谎之人的口,

他们骄傲自大,

狂妄地攻击义人。

19你的恩惠何其大——为敬畏你的人而预备,

在世人面前赐给投靠你的人。

20你把他们藏在你那里,

使他们得到庇护,

免遭世人暗算。

你使他们在你的居所安然无恙,

免受恶言恶语的攻击。

21耶和华当受称颂!

因为我被困城中时,

祂以奇妙的爱待我。

22我曾惊恐地说:

“你丢弃了我!”

其实你听了我的呼求。

23耶和华忠心的子民啊,

你们要爱祂。

祂保护忠心的人,

严惩骄傲的人。

24凡仰望耶和华的人啊,

要刚强壮胆!