Zaburi 28 – NEN & CCB

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Zaburi 28:1-9

Zaburi 28

Kuomba Msaada

Zaburi ya Daudi.

128:1 Kum 1:45; Es 4:14; Ay 33:18Ninakuita wewe, Ee Bwana, Mwamba wangu;

usiwe kwangu kama kiziwi.

Kwa sababu ukinyamaza

nitafanana na walioshuka shimoni.

228:2 Za 17:1; 61:1; 5:7; 11:4; 116:1; 63:4; 130:2; 142:1; 143:1; 141:2; Mao 2:19; Ezr 9:5; 1Tim 2:8Sikia kilio changu unihurumie

ninapokuita kwa ajili ya msaada,

niinuapo mikono yangu kuelekea

Patakatifu pa Patakatifu pako.

328:3 Za 12:2; 26:4; 55:21; Yer 9:8Usiniburute pamoja na waovu,

pamoja na hao watendao mabaya,

ambao huzungumza na jirani zao maneno mazuri,

lakini mioyoni mwao wameficha chuki.

428:4 Za 62:12; 2Tim 4:14; Mao 3:64; Ufu 18:6; 22:12Walipe sawasawa na matendo yao,

sawasawa na matendo yao maovu;

walipe sawasawa na kazi za mikono yao,

uwalipe wanavyostahili.

528:5 Isa 5:12Kwa kuwa hawaheshimu kazi za Bwana,

na yale ambayo mikono yake imetenda,

atawabomoa na kamwe

hatawajenga tena.

628:6 Mwa 24:27; Efe 1:3; 2Kor 1:3; 1Pet 1:3Bwana asifiwe,

kwa maana amesikia kilio changu

nikimwomba anihurumie.

728:7 Za 144:9; 13:5; 16:9; 33:3; 40:3; 69:30; 149:1; 18:1; 112:7; Isa 26:3; Kum 16:15Bwana ni nguvu zangu na ngao yangu,

moyo wangu umemtumaini yeye,

nami nimesaidiwa.

Moyo wangu unarukaruka kwa furaha

nami nitamshukuru kwa wimbo.

828:8 Za 18:1; 27:1; 20:6; Kut 15:2; Hab 3:13Bwana ni nguvu ya watu wake,

ngome ya wokovu kwa mpakwa mafuta wake.

928:9 Za 78:52, 71; 80:1; 106:47; 118:25; 23:1; 1Nya 6:35; 11:2; Kut 34:9; Isa 40:11; 46:3; 63:9; Eze 34:12; Yer 31:10; Mik 7:14; Kum 1:31; 32:11Waokoe watu wako na uubariki urithi wako;

uwe mchungaji wao na uwabebe milele.

Chinese Contemporary Bible (Simplified)

诗篇 28:1-9

第 28 篇

祈求上帝帮助

大卫的诗。

1耶和华啊,我呼求你;

我的磐石啊,别不理我。

你若默然不语,

我必绝望而死。

2我向你呼求,

向你的至圣所举手祷告时,

求你垂听。

3求你不要把我与奸恶人一同责罚,

他们对邻居口蜜腹剑。

4求你使他们罪有应得,

按他们的恶行,

按他们手上的罪恶报应他们。

5他们既然毫不在意耶和华的作为和祂的创造,

祂必永远毁灭他们。

6耶和华当受称颂!

因为祂听了我的恳求。

7祂是我的力量,我的盾牌,

我信靠祂,就得帮助。

我的心欢喜雀跃,

我要歌唱赞美祂。

8耶和华是祂子民的力量,

是祂膏立者得救的堡垒。

9耶和华啊,

求你拯救你的子民,

赐福给你拣选的人,

如牧人般照顾他们,

永远扶持他们。