Zaburi 27
Sala Ya Kusifu
Zaburi ya Daudi.
127:1 2Sam 22:29; Ay 13:5; Za 3:8; 9:9; 56:4, 11; 118:6; Kut 15:2Bwana ni nuru yangu na wokovu wangu,
nimwogope nani?
Bwana ni ngome ya uzima wangu,
nimhofu nani?
227:2 Za 9:3; 20:8; 37:24; Dan 11:19; Rum 11:11Waovu watakaposogea dhidi yangu
ili wanile nyama yangu,
adui zangu na watesi wangu watakaponishambulia,
watajikwaa na kuanguka.
327:3 Mwa 4:7; Za 3:6; Ay 4:6Hata jeshi linizunguke pande zote,
moyo wangu hautaogopa;
hata vita vitokee dhidi yangu,
hata hapo nitakuwa na ujasiri.
427:4 Lk 10:42; Za 23:6; 61:4Jambo moja ninamwomba Bwana,
hili ndilo ninalolitafuta:
niweze kukaa nyumbani mwa Bwana
siku zote za maisha yangu,
niutazame uzuri wa Bwana
na kumtafuta hekaluni mwake.
527:5 Ay 38:23; Za 12:7, 8; 40:2Kwa kuwa siku ya shida,
atanihifadhi salama katika maskani yake,
atanificha uvulini mwa hema yake
na kuniweka juu kwenye mwamba.
627:6 2Sam 22:49; Za 3:3; 33:2; 54:6; 18:48; 22:12; 92:1; 50:14; 107:22; 116:17; 147:7; Ezr 3:13; Ay 22:26; Kut 15:1; Efe 5:19Kisha kichwa changu kitainuliwa
juu ya adui zangu wanaonizunguka.
Katika maskani yake nitatoa dhabihu kwa kelele za shangwe;
nitamwimbia Bwana na kumsifu.
727:7 Za 4:1; 5:3; 18:6; 55:17; 119:149; 130:2; Isa 28:23Isikie sauti yangu nikuitapo, Ee Bwana,
unihurumie na unijibu.
827:8 1Nya 16:11Moyo wangu unasema kuhusu wewe,
“Utafute uso wake!”
Uso wako, Bwana “Nitautafuta.”
927:9 Za 2:5; 119:8; 18:46; 22:24; 37:28; Mwa 49:25; Kum 31:17; 33:29; 4:31; Isa 41:17; 62:12; Yer 14:9Usinifiche uso wako,
usimkatae mtumishi wako kwa hasira;
wewe umekuwa msaada wangu.
Usinikatae wala usiniache,
Ee Mungu Mwokozi wangu.
10Hata kama baba yangu na mama wakiniacha,
Bwana atanipokea.
1127:11 Ezr 8:21; Za 5:8; 72:4; 78:42; 106:10; Yer 21:12; Kut 33:13Nifundishe njia yako, Ee Bwana,
niongoze katika njia iliyonyooka
kwa sababu ya watesi wangu.
1227:12 Kum 19:16; Mt 26:60; Mdo 6:13; 1Kor 15:15Usiniachilie kwa nia za adui zangu,
kwa maana mashahidi wa uongo
wameinuka dhidi yangu,
wakipumua ujeuri.
1327:13 Kut 33:19; 2Nya 6:41; Za 33:6; 31:19; 145:7; Ay 18:13Nami bado nina tumaini hili:
nitauona wema wa Bwana
katika nchi ya walio hai.
1427:14 Efe 6:10; Amu 5:21; Kum 1:21; Sef 3:8; Hab 2:3; Za 33:20; 130:5, 6; Mdo 1:4; Isa 8:17; 30:18Mngojee Bwana,
uwe hodari na mwenye moyo mkuu,
nawe, umngojee Bwana.
第 27 篇
讚美的禱告
大衛的詩。
1耶和華是我的光,我的拯救,
我還怕誰?
耶和華是我的堡壘,
我還怕誰?
2當惡人來吞吃我,
仇敵來攻擊我時,
必失足跌倒。
3雖然大軍圍攻我,
我心中卻一無所懼;
雖然戰爭來臨,我仍滿懷信心。
4我曾向耶和華求一件事,
我還要求,就是能一生住在祂的殿中,
瞻仰祂的榮美,尋求祂的旨意。
5危難之時,祂保護我,
把我藏在祂的聖幕裡,
高高地安置在磐石上。
6我要昂首面對四圍的敵人,
我要在祂的聖幕裡歡呼獻祭,
歌頌讚美祂。
7耶和華啊,求你垂聽我的呼求,
求你恩待我,應允我。
8你說:「來尋求我!」
我心中回應:
「耶和華啊,我要尋求你。」
9別掩面不理我,
別憤然拒絕你的僕人,
你一向是我的幫助。
拯救我的上帝啊,
別離開我,別撇棄我。
10縱使父母離棄我,
耶和華也必收留我。
11耶和華啊,
求你指教我行你的道,
引導我走正路,遠離仇敵。
12求你不要讓仇敵抓到我,
遂其所願,
因為他們誣告我,恐嚇我。
13我深信今世必能看見耶和華的美善。
14要等候耶和華,
要堅定不移地等候耶和華。