Zaburi 136 – Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu) NEN

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Zaburi 136:1-26

Zaburi 136

Wimbo Wa Kumshukuru Mungu

1136:1 Za 105:1; 100:5; 145:9; 118:1-4; 106:1; Ezr 3:11; Hes 2:26; 1:7; 2Nya 5:13; Yer 33:11Mshukuruni Bwana, kwa kuwa ni mwema.

Fadhili zake zadumu milele.

2136:2 Za 105:1; Kum 10:17; Kut 18:11Mshukuruni Mungu wa miungu.

Fadhili zake zadumu milele.

3136:3 Za 105:1; Kum 10:17; 1Tim 6:15Mshukuruni Bwana wa mabwana:

Fadhili zake zadumu milele.

4136:4 Kut 3:20; Ay 9:10Kwake yeye pekee atendaye maajabu makuu,

Fadhili zake zadumu milele.

5136:5 Mit 3:19; Yer 51:15; Mwa 1:1Ambaye kwa ufahamu wake aliziumba mbingu,

Fadhili zake zadumu milele.

6136:6 Mwa 1:1; 1:6; Isa 42:5; Yer 10:12; 33:2Ambaye aliitandaza dunia juu ya maji,

Fadhili zake zadumu milele.

7136:7 Mwa 1:14, 16; Za 74:16; Yak 1:17Ambaye aliumba mianga mikubwa,

Fadhili zake zadumu milele.

8136:8 Mwa 1:16Jua litawale mchana,

Fadhili zake zadumu milele.

9Mwezi na nyota vitawale usiku,

Fadhili zake zadumu milele.

10136:10 Kut 4:23; 12:12Kwake yeye aliyemuua mzaliwa wa kwanza wa Misri,

Fadhili zake zadumu milele.

11136:11 Kut 6:6; 13:3; Za 105:43Na kuwatoa Israeli katikati yao,

Fadhili zake zadumu milele.

12136:12 Kut 3:20; Kum 5:15; 9:29Kwa mkono wenye nguvu ulionyooshwa,

Fadhili zake zadumu milele.

13136:13 Za 78:13Kwake yeye aliyeigawa Bahari ya Shamu,

Fadhili zake zadumu milele.

14136:14 Kut 14:22; Za 106:9Na kuwapitisha Israeli katikati yake,

Fadhili zake zadumu milele.

15136:15 Kut 14:27Lakini alimfagia Farao na jeshi lake katika Bahari ya Shamu,

Fadhili zake zadumu milele.

16136:16 Kut 13:18; Za 78:52Kwake yeye aliyewaongoza watu wake katika jangwa,

Fadhili zake zadumu milele.

17136:17 Hes 21:23-25; Yos 24:8-11; Za 78:55; 135:9-12Ambaye aliwapiga wafalme wenye nguvu,

Fadhili zake zadumu milele.

18136:18 Kum 29:7; Yos 12:7-24Naye aliwaua wafalme wenye nguvu,

Fadhili zake zadumu milele.

19136:19 Hes 21:21-25Sihoni mfalme wa Waamori,

Fadhili zake zadumu milele.

20136:20 Hes 21:33-35Ogu mfalme wa Bashani,

Fadhili zake zadumu milele.

21136:21 Kum 1:38; Yos 12:1; 14:1Akatoa nchi yao kuwa urithi,

Fadhili zake zadumu milele.

22136:22 Kum 29:8; Za 78:55; Isa 20:3; 41:8; 42:19; 43:10; 44:1, 21; 45:4; 49:5-7Urithi kwa Israeli mtumishi wake,

Fadhili zake zadumu milele.

23136:23 Za 78:29; 103:14; 115:12Aliyetukumbuka katika unyonge wetu,

Fadhili zake zadumu milele.

24136:24 Yos 10:14; Neh 9:28; Kum 6:19Alituweka huru toka adui zetu,

Fadhili zake zadumu milele.

25136:25 Mwa 1:30; Mit 6:26Ambaye humpa chakula kila kiumbe.

Fadhili zake zadumu milele.

26136:26 Za 105:1; 115:3; Ezr 3:11Mshukuruni Mungu wa mbinguni,

Fadhili zake zadumu milele.