Zaburi 135 – NEN & CCBT

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Zaburi 135:1-21

Zaburi 135

Wimbo Wa Sifa Kwa Mungu

1135:1 Neh 7:73Msifuni Bwana.

Lisifuni jina la Bwana,

msifuni, enyi watumishi wa Bwana,

2135:2 1Nya 15:2; Lk 2:37; Za 116:19ninyi ambao mnatumika ndani ya nyumba ya Bwana,

katika nyua za nyumba ya Mungu wetu.

3135:3 1Nya 16:34; Za 119:68; 68:4; 92:1; 147:1Msifuni Bwana, kwa kuwa Bwana ni mwema,

liimbieni sifa jina lake, kwa maana hilo lapendeza.

4135:4 Kut 19:5; Kum 7:6, 7; 10:15; Mal 3:17; Tit 2:14Kwa maana Bwana amemchagua Yakobo kuwa wake mwenyewe,

Israeli kuwa mali yake ya thamani.

5135:5 Za 48:1; 145:3; Kut 12:12; 1Nya 16:25; Ay 21:22Ninajua ya kuwa Bwana ni mkuu,

kwamba Bwana wetu ni mkuu kuliko miungu yote.

6135:6 Za 115:3; Dan 4:35; Mt 6:10Bwana hufanya lolote apendalo,

mbinguni na duniani,

katika bahari na vilindi vyake vyote.

7135:7 Ay 5:10; Za 68:6; Isa 30:23; Amo 4:13; Yer 10:13; 51:16; Yoe 2:23; Zek 10:1; Kum 28:12; Mwa 2:6; Ay 28:25; 38:22Hufanya mawingu kupanda kutoka miisho ya dunia;

hupeleka umeme wa radi pamoja na mvua

na huleta upepo kutoka ghala zake.

8135:8 Kut 4:23; 12:12Alimuua mzaliwa wa kwanza wa Misri,

mzaliwa wa kwanza wa wanadamu na wanyama.

9135:9 Kut 7:9; Za 136:10-15Alipeleka ishara zake na maajabu katikati yako, ee Misri,

dhidi ya Farao na watumishi wake wote.

10135:10 Hes 21:21-25; Yos 24:8-11; Za 44:2; 78:55; 136:17-21Aliyapiga mataifa mengi,

na akaua wafalme wenye nguvu:

11135:11 Hes 21:21, 26, 33; Yos 12:7-24Mfalme Sihoni na Waamori,

Ogu mfalme wa Bashani

na wafalme wote wa Kanaani:

12135:12 Kum 29:8akatoa nchi yao kuwa urithi,

urithi kwa watu wake Israeli.

13135:13 Kut 3:15; Za 102:12Ee Bwana, jina lako ladumu milele,

kumbukumbu za fahari zako, Ee Bwana, kwa vizazi vyote.

14135:14 1Sam 24:15; Ebr 10:30; Kum 32:36Maana Bwana atawathibitisha watu wake,

na kuwahurumia watumishi wake.

15135:15 Ufu 9:20; Isa 2:8; 31:7; 37:19; 40:19; Yer 1:16; 10:5; Za 96:5Sanamu za mataifa ni fedha na dhahabu,

zilizotengenezwa kwa mikono ya wanadamu.

16135:16 1Fal 18:26Zina vinywa, lakini haziwezi kusema,

zina macho, lakini haziwezi kuona;

17135:17 Yer 10:14; Hab 2:19zina masikio, lakini haziwezi kusikia,

wala hakuna pumzi katika vinywa vyao.

18Wale wanaozitengeneza watafanana nazo,

vivyo hivyo wale wote wanaozitumainia.

19135:19 Za 22:23Ee nyumba ya Israeli, msifuni Bwana;

ee nyumba ya Aroni, msifuni Bwana;

20ee nyumba ya Lawi, msifuni Bwana;

ninyi mnaomcha, msifuni Bwana.

21135:21 Za 128:5; 134:3; 1Fal 8:13; 2Nya 6:2Msifuni Bwana kutoka Sayuni,

msifuni yeye aishiye Yerusalemu.

Msifuni Bwana.

Chinese Contemporary Bible (Traditional)

詩篇 135:1-21

第 135 篇

讚美之歌

(平行經文:詩篇115·4-11

1-2你們要讚美耶和華!

讚美祂的名!

耶和華的僕人啊,

在耶和華的殿中,

在我們上帝的院宇中事奉的人啊,

你們要讚美祂!

3你們要讚美耶和華,

因為祂是美善的;

你們要歌頌祂的名,

因為祂的名美好無比。

4祂揀選雅各做祂的子民,

揀選以色列作祂的產業。

5我知道耶和華偉大,

我們的主超越一切神明。

6耶和華在天上、地下、海洋、

深淵按自己的旨意行事。

7祂使雲霧從地極上升,

發出電光,帶來雨水,

從祂的倉庫帶出風來。

8祂擊殺了埃及人的長子和頭胎的牲畜。

9祂在埃及行神蹟奇事,

懲罰法老和他的一切臣僕。

10祂毀滅列國,

殺戮強大的君王:

11亞摩利西宏巴珊迦南所有的君王。

12祂把這些國家的土地賜給祂的以色列子民,

作為他們的產業。

13耶和華啊,

你的名永遠長存,

你的威名傳到萬代。

14因為耶和華必為祂的子民伸冤,

憐憫祂的僕人。

15外族人的神像是人用金銀造的。

16它們有口不能說,有眼不能看,

17有耳不能聽,口中毫無氣息。

18那些製造它們、信靠它們的人也會和它們一樣。

19以色列人啊,

你們要稱頌耶和華!

亞倫的子孫啊,

你們要稱頌耶和華!

20利未的子孫啊,

你們要稱頌耶和華!

你們敬畏耶和華的人都要稱頌祂!135·15-20 平行經文:詩篇115·4-11

21要讚美錫安的耶和華,

讚美住在耶路撒冷的耶和華。

你們要讚美耶和華!